menuz

SIRI YA KUWA NA NGUVU KUBWA YA MUNGU

SIRI YA KUWA NA NGUVU KUBWA YA MUNGU
Imeandikwa"Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka."-Mathayo 11:12 .
MUNGU hajaishiwa nguvu za kutenda miujiza bali sisi kama wakristo hatuja amua kuchukua nafasi zetu ili kutembea na nguvu ya MUNGU.

Uhusiano mkubwa na MUNGU huleta nguvu kubwa ya MUNGU katika maisha yetu.
Watu wote kwenye biblia ambao walikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU walikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.

Imeandikwa "Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako."-Zaburi 119:164
Huyu ni mtumishi wa MUNGU Daudi anatueleza uhusiano wake na MUNGU ulivyo mkubwa na MUNGU wake anasema yeye kila siku anamsifu MUNGU mara saba.Hayo ni mahusiano makubwa sana na MUNGU.

Hakuna asiyejua nguvu ya MUNGU juu ya Daudi iliyo muangusha Goliath na kuwa ogopesha wafilisti, lakini kumbe siri ya Daudi kutembea na nguvu kubwa ya MUNGU ni uhusiano mkubwa aliokuwa nao na MUNGU uhusiano wa kumsifu MUNGU mara saba kila siku.
Imeandikwa". . . . . . .  akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo."-Danieli 6:10
Hapa tunaonauhusiano wa Daudi na MUNGU ulivyokuwa mkubwa,kwa kusali mara tatu si kila siku na sio kwa sababu ya matatizo lakini ndio ilikuwa kawaida yake kusali mara tatu kwa siku.

Danieli alikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU kiasi kwamba simba wenye njaa kali hawakuweza kumla wala kumdhuru ,lakini siri yake  ya kuwa na nguvu kubwa ya MUNGU kiasi hiko ni kwa kuwa alikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.Uhusiano wa kumuomba MUNGU kila siku mara  tatu na kumshukuru.

Hao ni baadhi tuu ya watumishi wa MUNGU lakini ukichunguza utakuta watumishi wote wenye nguvu za MUNGU walikuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU.

ukisoma kwa habari ya Nabii Eliya alikuwa ni mtu wa maombi sana maombi ya bidii-Yakobo 5:17 .Ukisoma habari za YESU japo alikuwa ni MUNGU lakini alituonyesha mfano wa kuishi na kuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU kwa kukesha mara kwa mara kwa kuomba.

Imeandikwa"Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa."Matendo ya mitume 3:1 Hata wanafunzi wa YESU walishafundishwa namna ya kujitengenezea uhusiano mkubwa na MUNGU na ndiyo sababu walikuwa na nguvu kubwa ya MUNGU maishani mwao.

Kama kweli unataka kuwa mkristo ambaye si wakawaida basi wewe jijengee leo tabia za kuanzisha mahusiano makubwa na MUNGU ,sio jumapili kwa jumapili ndio unasali au ndio unasoma biblia . 

Jijengee tabia ya kutoenda kazini pasipo kusoma neno la MUNGU na kulitafakari, Jijengee tabia ya kufanya maombi ya maisha yako wewe binafsi kila siku kwa muda wa kutosha kila siku ,hata kama huna matatizo wewe ya kuombea wewe waombee wengine katika familia yako yenye matatizo au watu wanaokuzunguka hata ombea nchi.

Kama unasali tuu pale unapopatwa na tatizo bado hauna uhusiano mkubwa na MUNGU!,
Kama unamsifu MUNGU jumapili mpaka jumapili  bado huna uhusiano mkubwa na MUNGU.
Kama unasoma biblia jumapili kwa jumapili yaani hauna muda wa kujisomea mwenyewe biblia ,wewe bado una uhusiano mdogo na MUNGU.

MUNGU hataki umuombe siku moja tuu, hataki umsifu kwa muda kidogo tuu, hataki usome neno lake jumapili kwa jumapili tuu,
 bali anataka umuombe kila siku,umsifu kila siku na usome neno lake na kulitafakari kila siku na kwa muda wa kutosha huku ukitii maagizo yake.

Angalizo:
usishangae kuona miujiza na mambo makuu utapo anza kuwa na uhusiano mkubwa na MUNGU,usishangae kuanza kuona maono ya MUNGU wazi wazi-live, au kuombea mgonjwa na akawa huru papo hapo, hata kuwa na nguvu ya ajabu usiyotarajia pindi utapojitengenezea mahusiano makubwa na MUNGU.

7 comments:

  1. Mimi haron wachira kutoka eldoret Kenya ninatembea na nguvu za mungu tena mniombee nataka ushirika na YESU KRISTO zaidi na zaidi katika jina la YESU KRISTO

    ReplyDelete
  2. Ameni Asante saana

    ReplyDelete
  3. Uko sawa Barikiwa sana Kwa mafundisho haya

    ReplyDelete
  4. Mimi niombee niweze kuwa na nguvu kubwa mungu

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!