menuz

MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA


Kuna vita kubwa kuacha tabia mbaya ambazo  hazimpendezi MUNGU.Tabia mbaya ambazo zimejiwekea mazoea katika maisha yetu mpaka zinakuwa na nguvu kana kwamba ni sehemu ya maisha yetu.

Imeandikwa “ Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohon i ”-1 Wakorintho 2:14

Watu wengi wanaokoka na kuanza maisha ya wokovu huku bado zile tabia zao zamani kabla hawajaokoa zinawafuatilia na kuwasumbua sumbua.

Mfano: labda mtu alikuwa mlevi sana kabla ya kuokoka basi  baada ya kuokoka anaweza kuwa anajikuta mara kwa mara anajaribiwa kurudia ile tabia ya kulewa.

Baadhi ya tabia sugu kwa watu wengi ambazo zinamchukiza MUNGU ni
ü  Ulevi

ü  Kusema uongo
ü  Kutukana matusi
ü  Kuangalia picha za uchi
ü  Kupiga punyeto/kujichua
ü  Uzinzi
ü  Uvivu
ü  Hasira
ü  Na n.k



Hakika kuna dawa ya kuacha tabia mbaya iliyokithiri yaani “addiction” na dawa pekee inayoweza kutatua ni uwepo wa MUNGU ambao huondoa kiu ya mambo machafu na kuweka kiu ya kutafuta mambo ya Rohoni zaidi.









Unapokuta mtu ameacha kwa kujilazimisha na kujizuia kimwili labda ilikuwa ni tabia ya kuvuta sigara na akaamua kuacha kwa kujilazimisha pasipo msaada wa MUNGU huyo anawezekana 

anaonekana kimwili kama ameacha lakini kiroho bado ile tabia anayo na ndio maana  mara nyingi anaweza jikuta akilala huwa anaota anavuta sigara pia watu kama hao hawakai sana wakiwa wameziacha tabia hizo bali si muda utasikia amezirudia tena na akizirudia anakuwa na kiu kubwa zaidi ya awali.

Imeandikwa “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.” -Warumi 2:14

Ukweli ni kwamba uwepo wa MUNGU pekee ndio anaweza kukufutia kiu ya mazoea ya kutenda tabia mbaya.
Je huo udhihirisho wa MUNGU au uwepo wa MUNGU unapatikana vipi  ?.
Uwepo wa MUNGU unapatikana kwa kumuomba MUNGU mara kwa mara kwa kuwa uwepo huo huondoa kiu ya dhambi kabisa.

MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA
Kila mtu anatabia fulani inayomsumbua ambayo anatamani imtoke ili azidi kuwa safi mbele za MUNGU na kuweza kumwabudu MUNGU katika roho na kweli,Yamkini  tabia ambayo wewe inakusumbua ni madawa ya kulevya,ulevi,uzinzi,pornography,kusengenya,kutukana,au kuhukumu watu.

Haya ni mambo unayotakiwa kuyafanya ili uondokane na tabia hizo :-
1.Kabla hujaitenda lazimisha kutaka uwepo wa MUNGU.
Pindi unapojisikia hamu ya kutenda ile tabia mbaya inayokusumbua labda ni kuvuta sigara,madawa ya kulevya au ni uzinzi ,

Basi wewe  jitahidi kabla ya kufanya hiyo tabia inayokusumbua  jitafutie sehemu ya siri labda ni chumbani na uombe kidogo tuu na ndipo utakapo shangaa kwa kuwa ukitoka utajikuta huna hamu tena ya kutenda ile tabia mbaya.

Mfano: Kunywa pombe, kuvuta sigara, kutumia madawa ya kulevya yaani tabia yoyote ambayo ni mbaya  badala ya kukimbilia kuitenda hiyi tabia ,Jiambie kama utani kuwa ngoja nika Sali kwanza ndipo nitakuja kifanya hiyo tabia mbaya hapo wewe nenda chumbani kwako sirini uombe MUNGU

uwepo huo unakufanya uisikie vizuri sauti ya MUNGU kupitia Roho mtakatifu.

Kila tabia mbaya yaani,uzinzi,uasherati ,tamaa mbaya,kuvuta sigara, madawa, kukasirika, kutukana, kunywa pombe, kusema uongo, 

kujichua au kupiga punyeto . . . . . . . . .tabia zote mbaya huwa zinapewa nguvu na roho za giza yaani mapepo ilizifanye kazi katika maisha yetu kwa hiyo unapokaribia uwepo wa MUNGU kwa njia ya maombi ya mara kwa mara baasi hayo mapepo yanayoleta  kiu ya kuendelea na tabia mbaya yanakimbia.

Na unapokuwa mbali na uwepo wa MUNGU basi mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukuharibu kwa kukupa kiu na hamu kubwa ya kurudia ile tabia fulani mbaya uliyoiacha.


2.Mara kwa mara unahitajika kumuomba MUNGU juu ya tabia mbaya uliyo nayo  hata kama ulishamuomba.

Imeandikwa “ombeni bila kukoma;Ukweli” 1 Wathesalonike 5:17 .




Usiogope kuomba hata mara kumi(10) kwa siku juu ya tabia ikusumbuayo kwani ukweli ni kuwa mwanzoni nguvu hiyo inakuwa inafanania na chaji katika simu  ,kwa kuwa uwepo huo wa MUNGUunweza  kupungua na unaweza ungezaka ,

Uwepo huo unapopungua sana ndipo hujikuta unatamani kufanya na kuzirudia zile tabia mbaya za zamani ,hapo  ukurudi kumuomba MUGU tena kuhusu hiyo hiyo tabia na uwepo wa MUNGU unajichaji na kuongezeka kwako kukuondolea ile kiu ya dhambi.

Hatutakiwi kuacha kuomba kwa ajili ya tabia mbaya zitusumbuazo kwa kuwa tunapoomba MUNGU hushusha wingu lake ambao ndio uwepo na kwa huo unafukuza kila pepo wanaoleta kiu za kutenda zile tabia mbaya katika maisha yako.

 “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.. .” Yakobo 5:16
3.Jitenge na mazingira yaliyo rafiki na tabia unayoikataa

Jitenge na mazingira ambayo yanaurafiki na tabia unayoipinga :Mfano labda unatumia madawa ya kulevya na umeamua  sasa unabidi uachane na kundi la marafiki wa aina hiyo kwa kutokaa karibu na mazingira yao.

Jiondoe kwenye mazungumzo na watu ambao wanakufanya ukumbuke ile tabia ambayo huipendi.Imeandikwa “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” 1 Wakorintho 15:33.

Jitahidi kukaa karibu na watu wanaokupa moyo wa kuiacha ile tabia mbaya na sio kukaa karibu na wanaokuchukia na kukucheka kwa uamuzi wako wa kuacha hiyo tabia mbaya.

4.Kiri na sema mara kwa mara kile tuu unachokipenda kitokee na sio unachokitenda.

Siku zote sema mimi nitaacha hii tabia mbaya inayonisumbua labda ya kuvuta sigara,ulevi nitaacha umalaya,nitaacha kuangalia picha za uchi(pornography),nitaacha kupiga punyeto(kujichua/ masturbation), 

kiwe chochote we sema tuu hata kama bado unaendelea na tabia hiyo tabia mbaya wewe endelea kusema tuu hata kama unasema huku ukiwa huna uhakika kama itakuwa rahisi hivyo.

Kuna nguvu kubwa katika vinywa vyetu  ingawa haionekani kwa macho.“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”-Mithali 18:21

Kuwa na hali ya kuongea kile unachotaka kitokee na sio kile unachokitenda ,kwa kuwa waweza kuwa unapenda sana uache hiyo tabia mbaya lakini unashindwa kujisemea kuwa nitaiacha kwa kuwa bado kila iitwapo leo unaitenda.

Imeandikwa  “Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila .”- Zaburi 34:13
Kwa kinywa chako kinaumba kitu katika ulimwengu wa kiroho ambao huja kutokea katika ulimwengu wa kimwili.Kwa hiyo ukiwa mara kwa mara bila kuchoka unajisemea nitaiacha tuu tabia mbaya niliyo nayo”,au kuna siku nitakuja kuacha milele hii tabia mbaya kwa msaada wa MUNGU,Kweli utashangaa siku utaacha kabisa na itakuwa shuhuda kubwa sana .imeandikwa“. . . . . . . . . . . . . . . .. . . . . . . . ; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.”-  Zaburi 45:1

“Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. “- Mithali 15:2

5.Usikate tamaa kumrudia MUNGU pale unapoanguka mara kwa mara.
Usije kata tamaa  kumuomba msamaha MUNGU mara kwa mara pale unapoanguka katika hiyo tabia mbaya.

MUNGU anapenda watu wote ila anachukia dhambi,kwa hiyo usione aibu kumwendea MUNGU kuomba msamaha kila unapoirudia ile tabia mbaya ambayo huipendi .



Kwa kuto kukata tamaa kwako  juu ya kumuomba msamaha MUNGU kila unapoitenda hiyo tabia yako mbaya,

Yeye MUNGU hutuma uwezo wake kwa neema yake ukusaidie kuacha hiyo tabia kwa kuwa anajua kuwa ukiacha hiyo tabia mbaya utaweza kumtumikia vyema na kwa ujasiri zaidi.

MUNGU hajali kuwa umeirudia ile tabia yako mbaya mara ngapi ,bali anajali umenyanyuka nakumrudia MUNGU kila ulipo itenda hiyo dhambi inayotokana na tabia yako.

Imeandikwa “ Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; . . . . . . . . . . .” Mithali 24:16.

Kitu cha muhimu ni kwamba kila unapoanguka nakuirudia tabia yako mbaya hapo hapo rudi kwake MUNGU na kutubu kwa ajili ya hicho ulichotenda naye atakusamehe na kukupa nguvu ya kuacha hiyo tabia mbaya.     




JINSI YA KUSALI NA KUOMBA MUNGU !


Hatua saba(7) unazopitia pindi uombapo.
Ni vizuri kujua namna ya kusali na kuomba MUNGU kwa kuwa sala na maombi ndio funguo kuu kwa mkristo kupokea kutoka kwa BWANA.

Imeandikwa “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”- Wafilipi 4:6


Sio maombi ilimradi maombi ,bali ni maombi ambayo MUNGU anajibu.





Hatuendi tuu kuomba kile tunachotaka bila utaratibu na tukapata bali kuna hatua za kumuomba MUNGU na kwa utaratibu utaowezesha kuomba MUNGU sawa sawa na kupokea kutoka kwake.


Vitu vya kuzingatia kabla hujaanza maombi ni:-

       1.Unatakiwa uwe na neno la MUNGU linalothibitisha  ombi lako kwa MUNGU.
Kabla hata ya kuanza kuomba jaribu kutafuta neno la MUNGU ambalo litathibitisha ombi unalolipeleka kwa BWANA.


Mfano: “unataka kumuomba MUNGU upate nyumba/ mtaji / fedha au upate utajiri” basi muendee MUNGU ukiwa na mstari kama ilivyoandikwa


2 Wakorintho 8:9 -Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

Ukamuomba MUNGU kwa hoja kuwa umeasema ulifanyika masikini ili sisi tuwe matajiri ,leo naomba ule utajiri ambao kwa huo wewe ulifanyika kuwa masikini”


 Au waweza kutumia huu mstari Kumbukumbu la torati 15:4 “Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)”

Nawe ukamuomba MUNGU kwa hoja ukimueleza kuwa “MUNGU wangu ni ahadi yako toka awali kuwa utanibarikia mimi na hapatakuwepo masikini kati ya wale wanaokuabudu nakuomba uniondolee huu umasikini nilionao”.

Kuna maneno ya MUNGU mengi mengi waweza kuyatumia  tofauti na hayo ambayo unaweza kuyatumia kuthibitisha ombi lako kwa MUNGU kwa kuwa neno la MUNGU lina pumzi hai ya MUNGU.

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;”-2 Timotheo 3:16.

MUNGU anaangalia neno lake ili alitimize,nawe watakiwa umkumbushe neno  lake linaloshawishi kuwa ombi lako. 

Imeandikwa  Maana mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.- Ezekieli 12:25

Tena Imeandikwa “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.”- Mathayo 6:7 .

            2.  Mahali unapotumia kuomba MUNGU
Unapotaka kuomba maombi yako binafsi chagua mahali pazuri patulivu uweze kuomba pasipo usumbufu .

Imeandikwa “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” -Mathayo 6:6




Kama katika sehemu unayokaa kuna kelele na vurugu ,basi waweza kufungulia redio za injili kwa sauti kipindi wewe unasali,au simu yako au redio ikiimba nyimbo za injili huku wewe ukisali. 


Hapo utakuwa umeepuka kelele zitazokuhamisha kwenye uwepo wa MUNGU.

         3.  Kumbuka kutumia jina la YESU pindi uombapo
Zingatia kuomba kwa MUNGU kupitia jina la YESU.Imeandikwa “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.” -Yohana 14:13.

Usiombe kupitia jina lolote bali katika jina la YESU ndilo tulilopewa lenye nguvu na mamlaka pekee ya kufanya upokee chochote unachoomba kutoka kwa BWANA.

Kuna hatua kwa hatua unapotaka kusali au kumuomba MUNGU.
Sio kwa kukariri sala bali Ili maombi yako yafike kwa MUNGU na kupata majibu vyema  basi ni lazima uombe kwa mtiririko na kwa mpangilio unaotakiwa.

Imeandikwa “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi”-Mathayo 6:7.

Kwa hiyo kuna utaratibu wa kuomba vyema na sio kuongea maneno tuu pasipo maana yoyote wala mpangilio.

Hatua saba(7) na mtiririko unaotakiwa kwenda nao unapotaka kuomba nazo ni :-         

1.KUMSIFU/KUMSHUKURU
Unapoanza kusali anza kwa kumsifu MUNGU kwa kukupa uhai/uzima /afya na hata mshukuru kwa kukupa nafasi ya kusali pia.Mtambulishe MUNGU unayemuomba kwa kuwa kuna miungu wengi ,tena mtambulishe kwa majiina ukimaanisha 

Mfano:wewe ambaye NIKO ambaye NIKO ,MUNGU aliye hai,MUNGU wa miungu ,MUNGU wa israel,MUNGU wa isaka ,yakobo,ibrahim.

Imeandikwa “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” -1 Wathesalonike 5:18 .

MUNGU anastahili kusifiwa na wenye dhambi na wasio na dhambi.MUNGU anastahili kusifiwa hata kama uanaona hajakusaidia kitu kwa kuwa yeye MUNGU hutuchagulia kilicho bora kuliko tufikiriavyo.

Huku ukijinyenyekeza na kuona MUNGU ndiye yeye pekee unayemtegemea kupata msaada kutoka kwake.

2.KUTUBU DHAMBI ZAKO ZOTE.
Hatua ya pili ni kutubu dhambi zako zote ulizowahi kuzifanya kama unazikumbuka unataja moja baada ya ingine.Omba msamaha hata kama unajihisi au unajiona kuwa wewe ni mtakatifu,Tubu kwa ajili ya dhambi unazozijua na zile usizojua !



Imeandikwa “Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo”-Yohana 9:31


“15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.”-Isaya 1:15

Hiyo inamaana maombi ya mwenye dhambi ni kelele kwa MUNGU na hayasikilizwi bali mtu anapotubu kwa kumaanisha kuacha hayo maovu basi naye MUNGU husamehe!. “9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”-1 Yohana 1:9

Unapoomba msamaha basi kumbuka kusamehe watu waliokukosea kwa kuwa MUNGU hata kusamehe mpaka usamehe waliokukosea.

Imeandikwa “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” -Mathayo 6:14 .Ukiomba msamaha utakuwa unanafasi kama mtoto wa MUNGU kusikiwa ombi lako KWAKE.

3.KUMSHUKURU/KUMSIFU MUNGU.
Hatua ya tatu ni kumshukuru na kumsifu  MUNGU kwa kukupa msamaha wa dhambi kukupa nafasi nzuri kama mtoto wa MUNGU.

Imeandikwa“na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;”- Waefeso 5:20

Hapa unamshukuru kwa kuwa amekusamehe pale ulipo muomba msamehe, na una msifu kwa kuwa amekupa msamaha na nafasi nzuri yakukusikiliza kwa lolote umuombalo.




4.KUOMBA OMBI LAKO SASA
Imeandikwa “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”-1 Yohana 5:14

Hatua ya nne ni  kuomba ombi lako kabisa,Hapa unaweza ukaambatanisha maombi matatu  kwa imani huku ukiongozwa na Roho wa MUNGU.Kwa kuwa tayari unakuwa na nguvu za MUNGU.


Imeandikwa “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”- Yohana 16:24.

Peleka ombi lako kwa MUNGU huku ukiwa na mstari au neno la MUNGU linalothibitisha kupata ombi lako.

Mfano:Unataka umuombe MUNGU akuponye na magonjwa  basi waweza tumia mstari usemao kutoka  Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Kwa hiyo unapomuomba MUNGU  unaenda na hoja kuu ukimwambia “Eee BWANA kwa kupigwa kwako YESU sisi tumepona nakuomba niondolee magonjwa haya!”

Katika hatua hii ya nne(4) una mamlaka ya YESU tena waweza hata kuamuru mapepo na nguvu za giza au kufunga kila kazi za shetani za uharibifu na ikafanikiwa.

5.KUSHUKURU NA KUMSIFU MUNGU.
Hatua ya tano(5) ya maombi yako unatakiwa umshukuru MUNGU na kumsifu kwa kuwa MUNGU wetu hupenda kusifiwa na kushukuriwa hivyo unapaswa kumsifu na kumshukuru  MUNGU

 kwa ajili ya maombi yote uliyoyapeleka kana kwamba umepata kile ulichoomba ingawa bado katika mwili huoni kitu.
Imeandikwa “Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele”- Zaburi 136:26

6.KUJITABIRIA NA KUKIRI USHINDI KABLA YA KUTUKIA
Hatua ya sita (6) ya maombi yako  ni ya kujitabiria na kukiri ushindi kabla hujauona.Kiri kwa kusema yote kwa furaha kama umeshayapata kabisa.Imeandikwa “Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”- Mathayo 12:37.




Wewe mwenyewe ni nabii wa maisha yako mwenyewe.







Imeandikwa “28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; ”-Yoeli 2:28

Mfano:Ulikuwa unamuomba MUNGU upate mpenyo wa kibiashara au akutoe kwenye umasikini basi anza kukiri na kujitabiria kwa kusema asante MUNGU kwa kuwa utanifanya niwe tajiri wa aina yake ,najiona nikisaidia watu wasiojiweza, leo BWANA amenikubalia ombi langu nitakuwa na fedha nyingi zisizo za kawaida.

Jitabiri makubwa kadiri uwezavyo huku ukiamini kila unachojitabiria na kukikiri .Usiogope kujitabiria mambo makubwa kwa kuwa si wewe ambaye unaenda kuyafanya bali ni MUNGU mwenyewe.

7.KUSHUKURU  NA KUMSIFU MUNGU
Mshukuru MUNGU kwa sadaka ya fedha ya kuifanya kazi ya BWANA.
Hatua ya saba(7) ni kumshukuru na kumsifu MUNGU kwa kukuwezesha kufanya maombi vyema teka mwanzo mpaka mwisho.Mshukuru MUNGU kwa ROHO wake mtakatifu aliyekusaidia kusali ipasavyo!.


Kama yalikuwa ni maombi ya mfululizo yaani maombi ya kitu fulani labda ulikuwa kwa muda mrefu unaombea nchi,labda familia,labda ndoa yako au chochote kilichokuwa kina kusumbua kwa muda mrefu ,ikiwezekana nenda kanisani au katika watu wenye matatizo na kutolea sadaka ya kumshukuru.


Imeandikwa “Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako”- Zaburi 50:14

Kwa kutoa sadaka ya shukurani kwa ajili ya lile jambo ulilomuomba MUNGU kwa imani.

Itakuwa vyema zaidi kwa kuwa kwa sadaka hiyo utakuwa umeweka kumbukumbu kwa MUNGU na hatasahau kulijibu  ombi lako kamwe.