menuz

Kitu cha thamani unachopoteza pindi uangaliapo picha za ngono(porn)

Kwanini inanibidi nichukue gharama zote kuacha kuangalia picha za ngono(porno) ? .
Kazi ya shetani ni kuhamasisha watu kutenda dhambi sana kwa kuwa mwisho wa dhambi ni mauti na kazi ya MUNGU ni kuhamasisha watu kutenda mema zaidi kwa kuwa mwisho wa mema ni uzima wa milele.


Kuna vitu vya thamani na vikubwa sana unavipoteza pindi tuu unapoangalia picha za ngono/porno. Mikanda hiyo ya ngono imekuwa na majina tofauti tofauti kama vile pilau,picha za bluu,mijengo na mengineyo.


Nini kinatokea pale tunapoangalia picha za uchi/ngono?,Jibu ni tunaamsha tamaa za mwili na tunakwenda kinyume na MUNGU kwa kutokukubali kuongozwa na ROHO wa MUNGU bali tunakuwa tumekubali kuutii miili yetu.




 Imeandikwa “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” -Mathayo 5:28
Kwa hiyo mtu yeyote anapoangalia picha za ngono/uchi anakuwa amezini moja kwa moja bila kujijua.Kwa hiyo vitu anavyovikosa baada ya kuangalia picha za ngono/porno ni:-

1.Unakosa ROHO mtakatifu
Mtu anapoangalia mikanda ya ngono(kutenda dhambi) basi ROHO mtakatifu wa MUNGU anaondoka katikati yake.
ROHO mtakatifu kazi yake ni kumpa ulinzi ,kumuongoza na kumfunulia mambo ya sirini ya siku zijazo.

2.Unakosa uwepo wa MUNGU
Unapoangalia mikanda ya ngono unakosa nguvu ya MUNGU inayoweza kukuletea msaada katika maisha ya kawaida pasipo wewe kujua.
Mfano :malaika wa MUNGU wanaokulinda kila mara wanaacha kukulinda pale mtu anapoangalia mikanda ya ngono(atendapo dhambi).

3.Unakosa uhusiano na MUNGU
Unapoangalia picha za ngono uhusiano unapovunjika na MUNGU maana yake jina lako linakuwa halipo katika kitabu cha uzima wa milele kwa hiyo unakuwa haupo katika majina ya wataokwenda mbinguni.

HAKUNA FAIDA YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO(PORN).
Wimbi la picha za uchi na mikanda ya ngono/porno katika mitandao ni wimbi la kazi za shetani kwa kuwa yeye hupenda watu wafanye dhambi zaidi ili kwa kuwa mwisho wa dhambi ni mauti.


Watu wengi wamekuwa wakiangalia picha za ngono/porno kupitia mitandao mbalimbali na blog bila kujua hasara za kuangalia picha hizo katika maisha yao ya kiroho na kimwili pia.


Imeandikwa “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu”-Waefeso 5:3

 1.Kuangalia mikanda ya ngono/porno kuna leta laana.
Imeandikwa wenye macho yajaayo uzinzi, . . . . . . . . . . . . .  mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;” -2 Petro 2:14
Kuna laana inajitengeneza pale mtu anapojizoesha kuangalia picha za ngono.




Imeandikwa “Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa;” -Ezekieli 16:36

 Imeandikwa “basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote.”- Ezekieli 16:37

Kwa hiyo sii vyema kuziangalia picha hizo za ngono zinazochochea kutokea laana ambazo zitaziba kuonekana kwa baraka katika maisha yetu.

2.Picha za ngono(porno) zina athiri mtazamo hasa katika kufikiri yaani mawazo

Mawazo mabaya huwa yanamtawala mara zote mtu aangaliae picha za ngono Imeandikwa “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;”-Mathayo 15:19

Mtu ambaye amezoea kuangalia picha za ngono(porn) kila anapoona watu wengine mitaani yeye anawaona au anaweza anza wawazia/imagine wakiwa uchi na kuwaona wakiwa uchi  hata kama amevaa nguo yeye atawafikiria/imagine wanavyokuaga uchi huwa wanakuaje.



Mtazamo utabadilika kwa kuona ni vyema kuangalia picha za ngono kuliko kuwa na mwenzi wako.

Inafanya watu wengi wanaoangalia picha za ngono(porn) kutoridhika pale wanapofanya mapenzi na wake au waume zao kwa kuwa walitazamia kupata kulingania na kile walichokuwa wakikiona katika mikanda ya ngono.

Mfano :Mikanda ya ngono inapoonyesha mwanaume mmoja anawaingilia kingono wanawake wanne(4). Basiii hiyo hali inaathiri huyo anaye tazama kwa kuwa naye atatamani apate wanawake wengi kiasi hicho ili kufaidi kama alivyoona katika mikanda hiyo.

3.Kuangalia picha za ngono(porno) kuna gharimu muda na hata kukupotezea muelekeo.
Imeandikwa “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.Tuukomboe wakati”- Wakolosai 4:5


Duniani tupo kwa muda kidogo tuu na kila mtu amepewa lengo na kusudi la kuwepo hapa duniani.


Pia ametupa muda wa kutimiza hayo makusudi sasa unapokuta mtu anaopenda sana kuangalia picha hizi za ngono anaweza jikuta muda wake mwingi ukitumika kuangalia picha za ngono/porno katika blog na website badala ya kulenga kile ambacho ni lengo lake kuwepo duniani kwalo.

Imeandikwa “mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”- Waefeso 5:16

4.Unakuwa mtumwa wa kuangalia picha za ngono(pornography/porn).


Ukweli usiopingika ni huu kuwa kwa kadri unavyozidi kuangalia picha za ngono(porn) ndivyo hivyo unapakuwa na kiu kubwa ya kuangalia picha za ngono(porn) tena na tena.


Hatutakiwi tuwe watumwa wa kuangalia picha za uchi bali tuwe vijana wenye msimamo katika kutimiza kazi au kusudi  la MUNGU alilotuwekea hapa duniani huku tukiukomboa wakati.

5.Kuangalia picha za ngono(porn) kunaalika roho chafu.
Mtu anapoangalia picha za uchi anajikuta taratibu anavutwa kufanya vitu vingine kama vile labda awali alikuwa hana tabia za uzinzi basi baada ya kuwa anaangalia hizi picha za uchi basi anaanza uzinzi,au umalaya .


Kuangalia picha za ngono(porn) kunaalika roho ya uzinzi,umalaya,ushoga,roho ya kupiga punyeto hata uvivu.


Njia za kuacha kuangalia picha au mikanda ya ngono/porno
Imeandikwa “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”- Warumi 8:14
Kama watoto wa MUNGU hatutakiwi kuongozwa na mwili bali na ROHO wa MUNGU na ROHO wa MUNGU hupingana na matendo ya mwili.

Imeandikwa “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,”-Wagalatia 5:19
Hatutakiwi kujiendekeza kufanya matendo ya mwili kwa kuwa matendo ya mwili hatutaweza kuyatimiza kamwe na mwisho wa matendo ya mwili ni kifo/mauti.

Pima mwenyewe Baada ya kuangalia hizo picha za ngono umepata nini?, na umekosa nini ?, 

Ukisha tathimini ndipo uchukue gharama kubwa ya kuamua kuacha kuangalia picha hizo za ngono kwa maombi na kwa neno la MUNGU.

Usijiulize kwa nini unapenda kuangalia picha za ngono(porno) bali penda kujua nini kinachokufanya uangalie picha hizo.

Mipaka yetu kama watoto wa MUNGU kwa kuwa tuu hekalu la ROHO mtakatifu.

1.Hatuufuati mwili bali tunafuata ROHO wa MUNGU aliye ndani yetu.
“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;” -1 Wakorintho 6:19
Ili tuwe watu wakubwa wa kiroho hatutakiwi kuufuata mwili kwa kuwa sisi sii mali yetu wenyewe bali ya MUNGU.Hivyo basi inatubidi tuishi kama yeye MUNGU aliyetuumba anavyopenda sisi kuishi.

Imeandikwa “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.” -Wagalatia 5:13

2.Kuwaza kwetu na kuwe na mipaka katika ROHO mtakatifu.
 Ili tuache kuangalia picha za ngono inabidi tujifunze kuwa za sawa sawa na ROHO wa MUNGU apendavyo na sio kuwaza mambo ambayo ROHO wa MUNGU hatayapenda .

Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”- Wakolosai 3:5

3.Ujana wako usiwe kigezo cha kukufanya  uende kinyume na taratibu za MUNGU

MUNGU anatuonya kama wanawe kuwa ujana wetu isiwe ni kisingizio au kigezo chochote chakutufanya kuwaka tamaa aua kuishi maisha ya kutenda dhambi bali tuwe mfano na kielelezo na wenye msimamo katika kuacha kuangalia picha za ngono.
 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”- 2 Timotheo 2:22

4.Vita vikubwa vimo ndani yetu na sio nje ya mwili
Imeandikwa  “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?” -Yakobo 4:1
Vita vipo vikubwa hasa pale unapotaka kuacha kuangalia picha za ngono sasa hapo unatakiwa ujiwekee msimamo katika kutenda mazuri ya kila namna ili kukuwezesha kuacha kuangalia picha za ngono.

Dunia inapita na pia kuna taji kubwa la kukabidhiwa kama mtoto wa MUNGU baada ya kuishi duniani.


“Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” -1 Yohana 2:17


No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!