##### IELEWE OFISI YA KINABII #####
Huduma
ya kinabii ni moja kati ya huduma tano(5) ambazo MUNGU ameziweka katika kanisa
lake.Imeandikwa “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii,
wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na
masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.”-1 Wakorintho 12:28.
Kuna manabii wengi sana mpaka sasa na huduma zao
zimeenea sana duniani kwa mafanikio makubwa sana!.Lakini bado watu wengi
hawazielewi huduma hizo, kwa namna moja au nyingine.
Watu
wengi hawaelewi manabii gani ni wauongo na manabii wa aina gani ni manabii wa
ukweli ?,Watu wengi hawana ufahamu kuhusu huduma za kinabii ?
Hawa ndio manabii wa uongo!.
Neno
la MUNGU linaeleza wazi kabisa kuwa kutatokea manabii wa uongo na akafahamisha
ni namna gani unaweza kuwatambua!.Imeandikwa “Jihadharini na manabii wa uongo,
watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu
wakali.”-Mathayo 7:15
Namna ya kuwatambua manabii wa
uongo
Imeandikwa “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho,
kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea
duniani”-1
Yohana 4:1.
MUNGU anatuambia tusiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwa kuwa
kuna weza kuwa na manabii waongo humo humo. Mtu anaweza kupima na kujaribu roho
kuwa ni nabii wa ukweli au wa uongo kwa kutumia neno la MUNGU na kwa maombi.
Imeandikwa “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu
katika miiba, au tini katika mibaruti?
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa
matunda mabaya.
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu
kuzaa matunda mazuri.”-Mathayo 7:16-18
Wewe ukiona mtu wanamuita watu ni nabii na unataka
kumtambua kuwa kama ni nabii wa kweli au wa uongo, wewe angalia matunda yake
yaani tabia zake na matokeo ya tabia zake.
Matunda ni tabia, Wote tunajua mtu hawezi kuwa ni
Nabii au mtumishi wa MUNGU huku akiwa amejaa tabia mbaya kama vile
uongo,uzinzi,rushwa,chuki,kupenda fedha,uuaji,hasira,chuki,majivuno na
kadhalika.
Tabia
au matunda yanayoendana na Nabii wa kweli ni
upendo,furaha,uvumilivu,utuwema,amani na watu wote !.
...............Nabii wa uongo VS Nabii wa kweli...................
1.Nabii wa uongo huongozwa na roho wa giza katika kutenda
kazi hivyo manabii hao hawawezi kuona
shida kutenda uovu wa aina yeyote kwa kuwa roho za giza ndio furaha yao.
Wakati
Nabii wa kweli huongozwa na ROHO wa MUNGU katika kutenda
kazi hivyo manabii hao mar azote hujihadhari na kutenda uovu kwa kuwa ROHO wa
MUNGU hapendi na hawezi kuendana na uovu.
Imeandikwa “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”- Yohana 10:10
2.Nabii wa uongo anatabiri vyovyote na inaweza itokee au
isitokee !.
Wakati
Kila anachotabiri Nabii wa kweli ni lazima kitokee kwa kuwa huonyeshwa na
MUNGU mwenyewe na MUNGU hawezi kukosea kwa kuwa anajua mwisho kabla ya mwanzo.
Imeandikwa “Atakaponena nabii kwa jina la
Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai
amelinena huyo nabii, usimwogope”-Kumbukumbu la Torati 18:22
3.Furaha kubwa ya Nabii wa
uongo ni
kupata watu wengi ili apate umaarufu na fedha nyingi zaidi kwa njia ya sadaka
bila kujali watu hao wanampendeza MUNGU au la!.
Wakati
Furaha
kubwa ya Nabii wa ukweli ni kupata watu wengi ambao
atawafundisha kuzishika amri za YESU na kuona wanaishi katika mapenzi ya MUNGU
maisha yao yote hata kama hapati kiasi chochote cha fedha.
4. Nabii wa uongo hujali sana wale wenye
fedha na mali ,pia kutojali sana watu wasio na fedha wenye shida yaani
wajane,yatima nk
Wakati
Nabii
wa ukweli hujali
wote na hutumia nguvu zake,fedha zake kwa hali yeyote kuwasaidia wenye shida
,wajane,yatima na wanyonge.
5.Nabii wa uongo
hutumia ishara,miujiza na maajabu ya uongo kuwavuta watu wengi kwake na
sio kwa YESU.
Wakati
Nabii wa kweli
hutumia ishara,miujiza ya kweli kuwavuta watu wengi kwa YESU.
Ofisi ya kinabii na silaha zake !.......
Silaha kubwa katika
ofisi ya kinabii ni MANENO.Kuna neno la
kinabii kupitia mafunuo na Neno la MUNGU
kupitia bibilia.Watu wengi hawaifahamu utendaji wa kinabii na huduma hiyo
kiujumla hasa kutokana na uendeshwaji wake hutegemea mafunuo kutoka kwa MUNGU
sio wanadamu!.
Nabii ni mtu ambaye
anakuwa na karama ya unabii yaani utabiri.Imeandikwa “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.”- 1 Wakorintho 12:4
Nabii anakuwa na ROHO
yule yule mtakatifu lakini ROHO huyo
huachilia karama ya unabii na utabiri ndani yake.Watu wengi ambao leo tunawaita
manabii hawakujijua kipindi wanakuwa kama
wao watakuwa manabii.
Watu hao huanza kuota ndoto zenye
kutokea ,kuona maono wazi wazi mchana kabisa na kwa kuonyeshwa huko husema kile wanachokiona na kubadilisha maisha ya
watu kwa kuwageuza ili wamfuate YESU.
Kazi ya kinabii muda
mwingine inakuwa ni kazi yenye mzigo mzito kwa upande mwingine kwa kuwa inahitaji
nabii awe muombaji sana kwa kuwa ROHO mtakatifu hujifunua kwa mafunuo na maono
kwa nabii baada ya kuomba sana.
Hivyo
nabii wa kweli na mwenye kuipenda kazi hiyo anatakiwa awe ni mtu wa maombi sana
kwa kuwa atavyoomba sana ndivyo MUNGU humuonyesha mambo mengi sana kwa ajili ya
watu wake!.
Nyanja tatu(3) ambazo nabii anaweza kuzigusa pindi
atumiwapo na MUNGU.
i.Unabii wa
undani (Insight prophecy)
Mungu anaweza
kumtumia nabii na kumuonyesha chanzo cha shida yako na Nabii akakwambia hata kama hakuwa anaishi siku hizo
ulizopata hayo matatizo.
Mfano
katika biblia MUSA alikuwa nabii wa BWANA na ndiye aliyeandika kitabu cha
mwanzo ambacho ni unabii wa undani kwani
aliandika habari za mwazo kuwa MUNGU aliziumba mbingu huku kiukweli yeye
hakuwepo kipindi hicho.
Lakini MUNGU alimjulisha nabii MUSA kuhusu mwanzo
utadhani naye alikuwepo siku hizo na hivyo ndivyo MUNGU huwatumia mnabii katika
unabii wa undani.
ii.Unabii
wa mbele(Foresight prophecy)
Unabii
unaoongelea mambo ya mbele yaani utabiri wa siku zijazo kuhusiana na
chochote.Mfano katika bibilia ni kwamba MUNGU ameshamuonyesha Manabii DANIEL,ISAYA,EZEKIEL
kuhusu siku za mwisho wa dunia utakuwaje
”-
Hivyo ndivyo MUNGU anavyoweza kumtumia Nabii kwa
kumuonyesha vitu vitakavyotokea siku za mbele yetu!.
iii.Unabii
wa kuzidi siri(Oversight prophecy)
Imeandikwa “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi
wake manabii siri yake”-.
Amosi 3:7
MUNGU anaweza kumtumia nabii kwa kumuonesha siri zake juu ya yajayo au
hata juu ya mambo ya waumini wake !.
Makosa makuu manne(4) yanayofanyika katika huduma
nyingi za kinabii .
Kweli kuna manabii wa ukweli wengi sana lakini mara
nyingi kumekuwa na mapungufu makubwa katika huduma hizo na yanakomaa sana ingawa
makosa hayo yalianza kidogo kidogo.
Baadhi ya makosa hayo katika huduma hizo za
kinabii ni yafuatayo:-
1.Kuwa na mafundisho haba ya NENO la
MUNGU hasa kwa wale walio wachanga kiroho.
Imeandikwa“…… naye Neno alikuwa Mungu”-Yohana 1:1.Neno la MUNGU ni MUNGU mwenyewe pia ni sauti ya MUNGU
kwa watoto wake.
Huduma nyingi zinazo anza za kinabii zimekuwa na mafundisho haba ya
NENO la MUNGU kwa sababu ya unabii, ishara na miujiza hivyo kufanya watu wengi
ambao ni wachanga kiroho kudumaa na kubaki kumtegemea nabii kwa kila jambo hata
kwa yale ambayo wao wenyewe wangeweza kuyafanya.
Neno ndiye MUNGU mwenyewe kwa hiyo kama halisisitizwi kukaa ndani ya
watu.Hao watu watakuwa watu wakupenda miujiza na ishara na unabii lakini
hawamjui MUNGU na ndiyo maana baadhi yao wakipatwa na jaribu kidogo tuu huanguka
kabisa.
Utawala
wa kanisa ukiwa mzuri utaunda mashemasi ,wachungaji wasaidizi na wengineo kwa
ajili ya kufundisha hawa watu ambao ni wapya katika wokovu.
Mfano unakuta mtu alikuwa
muislam na baada ya kutabiriwa na nabii na kufunguliwa kutoka kwenye matatizo
yanayomkabili basi naye akaamua aokoke lakini baada ya kuokoka anatakiwa apatiwe
mtu ambaye atamfundisha masomo ya awali ili azidi kukulia wokovu, kitu
ambacho hakitendeki katika huduma nyingi za kinabii zinazo anza.
Imeandikwa “Nikwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili
wa Kristo ujengwe”-
Waefeso 4:12
Mungu aliweka huduma hizi kwa ajili ya kujenga watoto wake hata wao
pia waweze kujitegemea na kukua kiroho huku wakimjua MUNGU lakini watamjua vipi
kama hawasisitiziwi kulishika neno la MUNGU.
2.Kutegemeza waumini kwa Nabii badala ya YESUKRISTO.
Kosa kubwa ambalo huduma nyingi zinazo anza za
kinabii hutendeka ni hili la kuwategemeza waumini kwa Nabii kana kwamba yeye
ndiye anayetenda badala ya YESUKRISTO.
Badala
ya kutumia miujiza kama chambo cha kuvuta watu ili kuwafundisha kweli ya
YESU.Kumekuwa na makosa kuwa huduma nyingi za kinabii kuwa sehemu ya kushangaa
miujiza sana badala ya kumjua YESU kiasi kwamba kama miujiza haipo basi watu
nao hawakai tena kanisani.
3.Kutojali kujengea waumini misingi mizuri ya kukua
kiroho kwa kuijua kweli.
Waumini wamefundishwa kama jambo baya likiwapata basi
moja kwa moja wampigie simu Nabii nasio Waombe kwa YESU msaada.
Waumini wameshawekewa msingi kuwa majibu yao yote yamatatizo
yao watayapata kutoka kwa Nabii na sio kwa YESU kupitia nabii.
Kosa
ambalo hufanya waumini kuwa wategemezi na kudumaa katika uchanga wa kiroho maisha
yao yote.Kwa kuwa hawajawahi jengewa misingi imara ya kiroho misingi ya kufunga
,kuomba na kusoma neno la MUNGU.
4.Kuiba utukufu wa MUNGU na kujivuna kwa sababu ya upako.
Kutokana
na miujiza na ishara zinazo onekana na kutendwa na nguvu ya YESU kupitia
manabii zake basi baadhi ya hao manabii hujikuta wakijaribiwa kujivuna na kuiba
utukufu wa MUNGU.
Imekuwa
kama kawaida kwa kosa hili kwa baadhi ya manabii ambao huiba utukufu wa MUNGU
kwa kujitukuza .Manabii hutumiwa na MUNGU kufanya ishara hizo nao hujaribiwa
kujiweka katika nafasi ya kuutengeneza miujiza hio.
Mfano:Mtu
alikuwa anaumwa na haoni na MUNGU anamtumia nabii wake kumponya huyo mtu
Basi Nabii hujikuta
akisema “alikuja akiwa anaumwa macho nami nimemponya” kitu ambacho ni
kosa kubwa kuwa alitakiwa kusema “MUNGU amenitumia kumponya mtu huyu”.
Umuhimu
wa nabii katika maisha yako.
Kuna
baadhi ya watu hawajui umuhimu wa manabii lakini kiukweli nabii ni mtu muhimu
sana kwa kuwa ndiye sauti ya MUNGU kwa watu wake.
Baadhi ya vitu
vitavyokuonyesha umuhimu wa manabii navyo ni baadhi yake ni:-
ü
MUNGU
hujenga na kuunganisha familia zilizo tengana kwa kumtumia NABII
ü MUNGU huwatumia manabii kuwatia
moyo mitume katika kujenga kanisa “Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi
waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa
Israeli.”- Ezra 5:1
ü MUNGU hutumia manabii kuwaweka
madarakani watawala ambao MUNGU amewapenda waongoze. “Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka
nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na
maneno ya Bwana.”- 1 Samweli 15:1
ü MUNGU hutumia manabii zake kuonya
watu na matukio yajayo. “27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka
Yerusalemu hata Antiokia. 28
Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa
uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima,
nayo ikatukia katika siku za Klaudio.”-Matendo ya Mitume 11:27-28
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!