Laura
wamna(lala) ni mtoto wa miaka kumi na miwili (12), kutoka nchini
indonesia.Tangu akiwa mtoto mdogo sana alikuwa anatamani sana akutane naye YESUKRISTO
ana kwa ana.
Laura
wamna anafahamika kwa jina lingine ambalo ni LALA sehemu moja akishuhudia
alisema “ROHO wa MUNGU alinijia akanichukua mimi katika roho kukutana na
YESUKRISTO”.Anaeleza jinsi ilivyokuwa
mpaka alivyochukuliwa na YESUKRISTO, alichokiona ni ukweli hakuna
kilichopungua au kuongezwa.Tafadhali
unaposoma ushuhuda huu omba ROHO mtakatifu akupe hekima yake na uelewa hata
kabla hujasoma ushuhuda huu.
YESUKRISTO ALIVYONICHUKUA KUNINIONYESHA
MBINGUNI
·
YESUKRISTO alivyomtembelea LALA siku ya kwanza:Ilikuwa ni kipindi cha kusifu na kuabudu mikono
yangu illikuwa imeinuliwa juu yenyewe, na nikamwambia mama yangu: “Mama, siwezi
kushusha mikono yangu chini,na ilikuwa imeendelea kuinuliwa juu.Nikawaona
malaika wengi ndani ya kile chumba, na ghafla nikaona mwanga mkali sana na
unapotoka mwanga ule, kulikuwa na sauti ya BWANA ikisema nami.
Bwana
YESUKRISTO aeleza juu ya kifo cha kaka wa LALA:BWANA akasema kutakuwa na kifo cha ndugu yangu wa
karibu sana akazidi kusema akaniambia “Nenda kamwambie kaka yako wa karibu, mwambie
anatakiwa anirudie MIMI , Kwa kuwa bado nina REHEMA kwa ajili yake, Kwa sababu
maisha yake aliyokuwa akiyaishi yalikuwa mbali NAMI.” Kaka yangu
alikuwa ana matatizo na alikuwa mzigomkubwa katika familia yetu.
·
YESUKRISTO alivyonitembelea siku ya pili:
Siku
ya pili BWANA YESU aliniambia “utafaulu mitihani yako tena kwa daraja
zuri”.Kipindi ambacho mimi na mama tulikuwa tunaabudu MUNGU, Ghafla
malaika akaja akaitwa roho yangu tukaenda naye juu mpaka juu ya mbwamba naye
malaika kanionyesha baadhi ya miji nayo ni Nabire,
Serui, Biak, Manokwari.Malaika akaongea nami akisema “MUNGU kakwambia uende usimame
katika hiyo miji na uhubiri ujumbe wa BWANA
,wanatakiwa WATUBU kwa sababu “HAKUNA
MUDA YESUKRISTO AKUJA HARAKA
SANA””.Nilimuuliza yule malaika wewe ni nani ?,Malaika akanijibu “mimi naitwa
Gabriel”, Malaika wa BWANA .Ndipo aliponirudisha roho yangu kwenye
mwili wangu.
·
Mauti ilivyozunguka watu:Tarehe 2o machi ,Nilipokuwa katika safari ya kutoka
mji wa Abe to Entrop, Nikafikamji wa Kotaraja nilikuwa kwemye taxi ambapo malaika
akanichukua tukaenda juu ya jiji la Jayapura.
Malaika
akaniambia “angalia”, Nilipotazama nikaona watu wengi wamesimama, Wamezaa nguo
nyeusi zilizo wafunika kutoka kichwani mpaka miguuni na macho yao ni meusi na
kuna moto ndani yao.
Niliwaona
kila mahali hospitalini ,pembezoni mwa barabara,katikati mwa mitaa, masokoni,
majumbani walikuwa kila sehemu.Niliona mikononi wameshika rato kubwa,Nikamuuliza
malaika “hawa ni wakina nani?”, Akanijibu hao ni “malaika wa mauti”.
Tulipokuwa
tunaruka kiroho juu ya mji wa Entrope, “Niliona makundi ya vijana wadogo wakinywa
pombe mitaani, nilijawa na huzuni kwa sababu mauti ilikuwa imewazunguka kila
sehemu”.
Malaika
akaniambia “Lala, kama kuna kitu kimetokea na hauwi huru nacho., unaweza itia
majina mawili nayo ni damu ya YESUKRISTO na kwa jina la YESUKRISTO kwa sababu
jina hili lina nguvu sana.”.
Malaika
kanichukua tukapaa juu ya mawingu nami nikazidi kuona dunia chini ikiwa ndogo
na ndogo sana.Tulivyokuwa tunazidi kwenda
juu kuna sehemu tulipita ilikuwa nyembamba yenye giza na yakutisha.
Niliogopa
lakini malaika alinishikilia tukafika nikaona mwanga na ilikuwa mbinguni, Mimi
na malaika tulifika getini kulikuwa na malaika walinzi wawili mbele ya geti la
mbinguni, Geti la mbinguni limepambwa kwa lulu nzuri za kung`aa ndipo
lilipofunguka na wote wawili tukaingia tukawa tunatembea katika bustani.
Kulikuwa
kuna mlango uliofunguka na ndani nikaona meza ndefu imepangwa vizuri inaonyesha
kwamba si muda kutakuwa na sherehe(Ushirika mtakatifu/Holy communion), Kuna
malaika waliosimama nyuma ya kila kiti, kila malaika ana tarumbeta mkononi
mwake.Inaonekana kama vile wanaenda kupiga tarumbeta mapema.
Nikaendelea
kutembea na katika bustani niliona miti mizuri sana,matunda mbali mbali mazuri,
nikaona maua mazuri sana, Malaika Gabriel akaja akaniambaia “muda
wako wakukaa hapa umeisha unabidi urudi” nami nikamjibu “ninafuraha na amani kukaa hapa sipendi
kurudi”.Ghafla sauti ikatoka kutoka kwenye kiti cha Enzi ambako
kulikuwa na mwanga na utukufu ikisikika “Lala ,unatakiwa urudi sasa”.Malaika
Gabriel kanisindikiza akanirudisha.
Kutoka juu naliangalia na kuiona ile taxi nyekundu niliyekuwa nimeipanda
mwanzo ,ilikuwa ikienda ofisi ya serikali ya mji wa Entrope.Malaika akairudisha
roho yangu kwenye mwili wangu nikaamka nikasema “Halleluya!”.
Abiria
ambao walikuwa pamoja nami kwenye hiyo taxi walishangaa na kupigwa na butwaa,
Wakiniuliza “Dada, je ni mzima ?”.Nilishangazwa
sana kwa sababu nilijikuta nikining`inia kwenye bega la abiria mmoja, naye
alikinichuwa na mafuta kwenye pua kwa kuwa walidhania nimezimia.Nalisimamisha
taxi pale nilipofika nyumbani.
Ilipofika
saa11 usiku nilipokuwa nimelala, Malaika akanijia kunipeleka kwa Bwana,
Tukaingia katika geti la mbinguni, Na nikaona mtu amesimama naye amevaa kamba
ndefu nyeupe.Akanionyesha mikono yake kwangu, Nami nikatembea kufika karibu
naye, nikajua kuwa ni YESUKRISTO akanichukua tukatembea wote mbinguni.Mbinguni
ni pazuri sana na kuna kila aina ya maua ambayo sijawahi yaona duniani.
Kila
kitu kipo pale , moyo wangu ulifarijika sana na kuwa na amani isiyokuwa ya
kawaida,kuna miti ya vivuli,itoayo matunda na kwa uwazi kabisa kulikuwa kuna
mto.Bwana YESUKRISTO akaniambia “Lala, utajaribu kuweka miguu yako kwenye
maji ?,”Nami nikaichovya kwenye maji.YESUKRISTO kaniambia tena “unaweza
kunywa maji haya”.
Nilipokunywa
yale maji nikajisikia amani katika moyo isiyokuwa ya kawaida.YESUKRISTO
aniambia “waweza kuzamisha hata kichwa chako humu kwenye maji na bado ukawa
unauwezo wa kuhema ndani mwa maji haya”.
Alichokisema YESUKRISTO kilikuwa ni kweli kabisa.Kulikuwa na samaki
wengi wakiogelea karibu yangu, Nikamwambia YESUKRISTO “Nilipokuwa duniani sikuweza kukamata samaki kwa kuwa kule samaki wanakimbia
ukitaka kuwakamata ”.YESUKRISTO akaniambia “Samaki wa huku wanaweza kuongea
na wewe, Lala !”.
Baada
ya muda nikamuuliza YESUKRISTO “Wawezaje
kuona dhambi wanazozitenda watu dunia
nzima na huku dunia ni kubwa sana, waona je?”.YESUKRISTO kaniambia “njoo
pamoja nami huku.”nikaenda akanionyesha kuna kioo kikubwa na nikaona
dunia kuwa ni ndogo.
Nikaweza
kuona watu wanaofanya dhambi nilishangazwa kuomuona mtu ninayemjua nikamwambia
YESUKRISTO , “Bwana, naweza kuona yote
chini” mama na baba walikuwa wamelala kitandani.Naye YESUKRISTO akanijibu “Ndio,
na kuna malaika amesimama katika chumba chako.”
Mimi
na Bwana YESUKRISTO tukatembea tena, kulikuwa na chumba ambacho malaika
wawili(2) walikuwa wamesimama hapo nje.Kulikuwa na kitabu kikubwa mezani, na
nikamuuliza Bwana, “MUNGU, kitabu cha
aina gani hiki ?”, YESUKRISTO akanijibu,
“Hiki ni kitabu cha uzima”,Nikamuuliza
tena “naweza kuona ndani yake ?”,
Bwana YESUKRISTO kaniambia “Ndio, unaweza”.
Na
hao malaika wawili (2) walikuwa wako tayari kufungua kile kitabu kurasa baada
ya kurasa, Kwenye ukurasa wa kwanza nikaona
moja ya majina ya familia ninayoijua, Nikaona tena kuna jina la kaka
yangu nikamwambia YESUKRISTO “Bwana, hili ni jina la kaka yangu” na
Bwana akajibu “Ndio, ninayajua maisha yake na sasa yupo humu akimsifu Bwana”.
Malaika
akanifungulia ukurasa unaofuata nikaona jina la mtu ninayemjua tena nikamwambia
YESUKRISTO “Huyu ni mjomba wangu”.Naye
Bwana akanijibu “Ndio , yuko hapa ” .Nikamkumbatia YESUKRISTO huku nikilia.
Tukaendelea
kutembea na YESUKRISTO kwenye bustani nikaona watu wawili(2) wakinijia mmoja
anaonekana kama anamiaka 18 au 19 hivii,na mwingine kama ana miaka miwili(2)
akanikimbilia akanikumbatia nikaona kama amenipita kwa kuwa tulikuwa wote
katika roho.
Huyu
aliye mkubwa wa kama miaka 18 au 19 alikuwa anafanana na mama yangu yaani
walikuwa kama mapacha na mama yangu kwa jinsi alivyofanana naye, Ndipo nikakumbuka kuwa mama aliwahi niambia
ana kaka yake ambaye alikufa nilivyokuwa mdogo sana,Nikwa nimemjua atakua ndiye
nao wote wakaenda katika vyumba vyao.
Nikaona
maua mazuri nikawa namuuliza Bwana , “Je
naweza kuchuma ua hili ?,ningependa kumpa mama yangu kwa kuwa mama yangu
anapenda maua” .YESUKRISTO akanijibu “Muda haujafika bado wa wewe kuchukua maua
na matunda kutoka sehemu hii mwanangu !”.
Tukawa
tunaendelea kutembea na YESUKRISTO nikaona nyumba ambayo mlango wake uko wazi,
nikamuuliza YESUKRISTO kama naweza ingia humo,Bwana akanijibu “ndio
,waweza kuingia”.
Nilipofika
mbele ya mlango wa nyumba, sikuingia ndani kwa sababu nilikuwa nashangaa sakafu
ya dhahabu.Nikamwambia Bwana “MUNGU waooh
!!!, ..chini pazuri sana hivi, duniani dhahabu ni ghali sana”. Naye
YESUKRISTO alikuwa akibasamu na akasema “Hii ni nyumba yako ,na kuna baadhi ya
nyumba zinazofanana na hii.”
Nikamuuliza
YESUKRISTO “Bwana ninaweza kwenda nyumba
ingine ?”.Bwana akanijibu “ nyumba ambazo milango imefungwa , ni za
watu wengine”.YESUKRISTO akaniambia “Nifuate mimi”.
YESUKRISTO
ALIVYONIPELEKA KOUNA KUZIMU.
Bwana
YESUKRISTO alinishika wote tukaenda njia pana.Nikaanza kuhisi harufu mbaya kwa
kadiri tunavyozidi kwenda nikajisikia hewa inakuwa ya moto.Kwa mbali nikaona
pepo lenye miguu mitatu amebeba mikuki mitatu iliyoshikana na alipo muona YESUKRISTO
akampigia magoti.
Tukaendelea
kwenda mimi na Bwana YESUKRISTO huku akiniruhusu niangalie kwa undani zaidi
ambako kuna watu walikuwa wakiteswa na shetani.Shetani alikuwa akiwatesa mpaka
miili yao inabaki kuwa vipande vipande lakini hawafi.
·
WAZINZI:
Nikaona
kitabu juu yake kimeandikwa “uzinzi”.Nikaona
watu uchi wakiwa kwenye moto.Walipomuona YESUKRISTO wakaanza kumuita “Baba,
Baba” lakini YESUKRISTO hakuwatazama.
·
Watumishi wa
MUNGU:
Nilivyozidi kuangalia nikagundua kuna watumishi wa
MUNGU.Ndipo nikamuuliza YESUKRISTO, “Bwana
!, Kwa nini kuna mtumishi wa MUNGU hapa kuzimu ?”.YESUKRISTO kanijibu
kuniambia “Nilimchagua yeye lakini haku utoa ujumbe wangu”.
Ndipo yule
mtumishi alipomuona YESUKRISTO akamwambia “Baba
Baba, tafadhali niondoe hapa japo kwa dakika moja, nataka kutubu”.Bwana
akamjibu “umechelewa ,akasema sasa namtumia binti huyu akinionyeshea kidole “mimi(lala)”
kama mmoja wa watumishi wangu”.
Nikaona watu wengi wakiteswa, YESUKRISTO akaniambia
mimi “hawa
watu hawakuwa waaminifu kutoa fungu la kumi(zaka)”.
Nikaona
kundi kubwa la vijana wadogo ambao walikuwa wanacheza muziki kwenye misumari,
Kama muziki huo wa rock ukisikika basi wao wanatakiwa kuruka kwa haraka zaidi
na hawakuruhusiwa kusimama hata muda kidogo.Kama wakisimama, shetani anakuja
kuwatesa sana.
Ndipo
tukarudi tukatoka kwenye njia pana na kuingia mbinguni.Tulivyofika mbinguni ,
Bwana YESUKRISTO kaniambia, “Lala, Yote uliyoyaona ukawaambie watu
wangu”.Bwana YESUKRISTO akanichukua na akasema, “Lala, umesalimisha maisha yako
Kwangu, unatakiwa ubatizwe mwezi machi 25 na mtumishi wangu Ronald, naweka
amana kwake ili uweze kuandika kitabu chako”.
YESUKRISTO
kamuangalia malaika Gabrieli na Gabrieli kapiga magoti kuabdu chini ya miguu ya
Bwana YESUKRISTO.YESUKRISTO kamwambia malaika Gabrieli “Mrudishe mnangu.”
Gabrieli
akanichukua na akatembea nami nje ya geti nikamwuona malaika mwingine akawa
anaongea na Gabrieli kwa lugha ambayo nilikuwa siielewi, lakini Gabrieli
alinionyeshea mimi na kuangalia kweye kiti cha enzi cha Baba MUNGU ,alikuwa malaika
maiko naye YESUKRISTO akatutazama ,malaika maiko akapiga magoti na kumruhusu
Gabrieli na mimi tuendelee na safari yetu.
Tulipokuwa
niani tunarudi ,Gabrieli alniuliza “Ulikuwa unaongea nini na Baba?” .Na
nikamjibu , “Kuna vitu vingi ambavyo YESUKRISTO ameongea nami”.Nikamuuliza
malaika Gabrieli “Unafanya nini mbinguni
?”.Malaika akanijibu “Ni mlinzi wa Bwana YESUKRISTO, Chochote
ambacho Bwana YESUKRISTO ananiagiza kukifanya ndipo nakifanya chote”.
Tulipokuwa
tumefika karibu na nyumbani takatembea nikaona malaika wa vifo wamesimama
pembezoni mwa barabara kushoto na kulia.Nilipofika nikaona mbele ya nyumba kuna
malaika wa mlinzi wa BWANA.
Malaika
wa kifo alikuwa anatamani sana kuingia nyumbani lakini hakuweza kwa sababu
kulikuwa na malaika wawili(2) walinzi wa Bwana walikuwa nyumbani kwetu.Malaika
wa mauti alitaka kuingia mara ya pili akatupwa nje ,akaanguka na kupotea kama
vumbi.
Gabrieli
kanisindikiza mpaka kwenye chumbani kwangu ndipo roho yangu ikarejea na kuingia
katika mwili wangu nami nikarejea katika shughuli zangu za kawaida.
Alhamisi ,Machi 22.Tulikuwa na ibada nyumbani na baadhi ya watu
wakanisani kwetu, Ndipo malaika Gabrieli alipokuja kunichukua kunipeleka kwa
YESUKRISTO.YESUKRISTO alinionyesha mji ninaotakiwa kwenda.Aliniambia nikatoe
ujumbe wake kwenye kanisa la Katoliki lililopo Wamena.
Ijumaa.machi 23.Malaika akaja kunichukua kunipeleka kwa Bwana.YESUKRISTO katoa ujumbe
maalumu kwa kanisa lililopo kijijini “Harapan” na akasema “Kaliambie kanisa
,wasiwewanachelewa sana ibada.Kwa wale ambao mara zote wanachelewa hao
hawatakuwa sehemu ya ufalme wa MUNGU.
Ibada
inapoanza hatakiwi yeyote kubakia nje ya
kanisa akazidi kuniambaia waambie wamama wenye watoto ambao bado ni wachanga
wanatakiwa kukaa ndani ya kanisa ili kusikiliza NENO la MUNGU.Asiwepo wakukaa
nje hata kama kanisa limejaa wanaweza kukaa chini wasikilize NENO LANGU sio
shida, kila mtu aheshimu NENO LANGU.
Siku
hiyo hiyo tuliomaliza “maombi ya kufunga”,Nikatoa ujumbe wa Bwana YESUKRISTO
kwa walimu wa shule ya jumapili(Sunday school) ,nikaanza kurudi nyumbani kutoka
kanisani.
Malaika
wa Bwana akanijia njiani na kuniambia “asante lala umeutoa ujumbe wa Bwana kwa
walimu wa shule ya jumapili”.Akaongea nami “Jumaili utoe ujumbe kwa waumini kanisani.Utatakiwa
kutoa ujumbe si kwa kanisa tuu na familia, lakini pia unatakiwa utoe ujumbe kwa
dini zingine pia wadudha,uisilam, uhindizim na kadhaliaka.
Wao
pia wanatakiwa kupokea wokovu, toa ujumbe mapema kwa kadiri uwezavyo kwa sababu
nitakuchukua kukupeleka katika miji mingine.”(yohana 14,6).
Ilivyofika
saa moja jioni ,Malaika wa Bwana akaja kunichukua na kunipeleka kwa Bwana,
Bwana YESUKRISTO akasema nami “Lala ,haraka, haraka ,haraka kimbia na
uwaambie watu wangu ,Muda wangu umekaribia kuisha!” .
Na Bwana
YESUKRISTO akanionyesha ,muda wa mbinguni .Nikaona mkono mfupi umeonyeshea
kwenye namba na mkono mrefu uko karibu nao sana ingawa sikuweza kuona namba
katika saa.
Bwana
YESUKRISTO kaniambia, “Lala, kimbia karaka nautume ujumbe kwa watu
wangu,Muda wangu umekaribia kuisha”.YESUKRISTO kaniambia tena “Lala,
hakuna malaika aliwahi kuona muda mbinguni.Nakuruhusu wewe kuona muda wa
mbinguni ili uende kutoa kwa haraka ujumbe wangu”.
Majira ya saa 2:30:-Malaika kanijia na kunichukua kwenda kwa Bwana ,Bwana
YESUKRISTO tena akanionyesha jinsi muda wa mbinguni ulivyobaki mfupi sana.Bwana
YESUKRISTO kaniambia “Waambie watu wa darasani kwako, walimu
wako, majirani zako na yeyote yule unatekutana naye.Waambie watubu na kunirudia
mimi.”
Jumamosi, mach 24-saa 7;-Nilikuwa na mama na shangazi yangu.Tulikuwa katika
nyumba ya familia ya Wilson Sentani.Kipindi shangazi yangu alipokuwa akiomba
kwa ajili ya familia ya Wilson, na nilipolala chumbani nikamuona malaika kaja,
Niliweza kumuona malaika kwa sababu roho yangu ilikuwa nje ya mwili na kukaa
kwenye kitanda.
Nikamwita
malaika kuingia katika chumba lakini malaika alikuwa amesimama nje ya chumba na
nikamwita tena ,na malaika akanijibu “siwezi kuingia chumbani, (akamnyooshea
kidole shangazi yangu),mtumishi anapoongea na Baba ,hivyo nimi nasubiri
mpakaamalize kusoma aseme ameni”.Shangazi yangu alivyo maliza kuomba
naye akaja.
Alinichukua
na kunipeleka kwa YESUKRISTO naye Bwana akanipa ujumbe wakuja kuwaambia watu,
siku ingine mnamo saa 6 usiku ,Nilikuwa nikijiona mwili wangu mzito sana , kwa
sababu malaika alitaka kuja kunichukua , lakini mama yangu alizidi kuniambia
niandae nguo zangu tayari kwa ajili ya ibada ya kesho.
Nilipokuwa
nimelala, malaika akaja na kunichukua kwenda kwa Bwana.Bwana YESUKRISTO akaniambia “Lala, mwambie mama yako awe
anakuruhusu ulale pindi unapojisikia mwili wako mzito sana, kwa sababu kuna
jambo muhimu sana ambalo nataka kusema nawe.”
Akanihakikisha
mara ya pili,YESUKRISTO akasema “Lala, kwa nini ?umesahau kutoa ujumbe
niliokuambia uutoe,Unatakiwa ukumbuke kila nilichokwambia na uwaambie watu”.Nikasema
“Bwana, tafadhali nisamehe mimi” naye
Bwana YESUKRISTO akajibu “Nitarejesha kila kitu utavyoshuhudia”.
Jumapili, Machi 25, wakati wa asubuhi.-Kwa rehema za Bwana YESUKRISTO, Nilisimama na kutoa
ushuhuda wote wa ujumbe wa Bwana YESUKRISTO kwenye kanisa la Barachiel.Baada ya
kumaliza kuutoa ushuhuda,Nilijikuta nimebatizwa (kufa na kufufuka na YESKRISTO)
na baada ya ibada kulikuwa kuna kikao cha kufanya uamsho.
Nami
nilitakiwa kushiriki katika huduma hiyo ya uamsho nikamuona malaika kaja
kunichukua kunipelaka kwake YESUKRISTO ,Bwana akaniambia “Waambie watumishi wangu waende
katika huduma hiyo ya uamsho nami nitashuka na kuingilia kati kuleta
usuluhisho”.
Kipindi
bado nipo katika nyumba ya mchungaji ,Bwana alinionyesha shimo kubwa ambalo
lilikuwa refu na lenye giza.Nikaona watu wengi wakivutwa kwenda kwenye hilo
shimo,Nao walikuwa wakijitahidi kujizuia lakini wakishindwa na kuanguka mpaka
kwenye shimo hilo.
Machi
26;Malaika kaja kunichukua tukaenda mpaka kwa Bwana YESUKRISTO naye Bwana
kaniambia “Nitakutumia wewe kama mtumishi wangu mpaka nitakapo kuja, Kazi zote na
majukumu yote nakupa wewe, hayajaisha bado, lakini nitazidi kukutumia wewe
mpaka nitakapo kuja.”
Saa
sita malaika kaja kunichukua kunipeleka kwa Bwana,Tena Bwana YESUKRISTO
akanionyesha shimo kubwa lenye giza.YESUKRISTO akaongea nami “Shimo
unaloliona ni sehemu kwa ajili ya wasio
waaminifu nao wataenda kwa mika mitatu na nusu( mika 3.5) miaka ya dhiki
kuu(Ufunuo 13), Na huku kwa walio waamoinifu kwangu nitawachukua mpaka sehemu
niliyo waandalia, mbali na macho ya joka.”
YESUKRISTO
kaniambia “Lala, usipingane na mama yako, tena usiende kinyume na amri yangu ya
5,unatakiwa uwaheshimu mama yako na baba yako.”
Nilipomsikia
akisema hivyo Bwana nilijisikia mwenye hatia na nikalia.Nikamuona YESUKRISTO
akilia na akionekana mwenye huzuni. Niliona machozi yakitoka kwenye macho
Yake.Bwana YESUKRISTO kaniambia “Lala usilie , ninataka unisikie na utii
amri yangu ya tano(5)(uheshimu wazazi wako) hivyo uweze kuishi maisha marefu na
yenye baraka.
Nataka
nikutumie wewe kiajabu na kwa kushangaza futa miziki ya kidunia kutoka kwenye
simu yako” .(yakobo 4:4).Akaniambia unatakiwa uwe mtaratibu na mkimya hata ukiwa
shuleni,YESUKRISTO akaniambia “nitawezaje kukupa ujumbe kama wewe
haujatulia mwenyewe.”
Nami
nikamjibu “Bwana , siwezi kwa kuwa
marafiki wanakuja na kunisumbua na hata kutakua nikacheze nao,Vipi kama nisipo
enda shule si ndio itakua vyema ?”,Naye akajibu “Hapana, unatakiwa uende shule”.
Machi
27-04:30,Siku niliyokuwa na mtihani shuleni, Malaika alinichukua mpaka kwa
Bwana YESUKRISTO naye akaniambia “ HAKUNA MUDA ZAIDI, unatakiwa uwape watu
ujumbe wangu haraka sana”.
Katika
ibada ya kuabudu jumapili , kama kawaida
malaika alinichukua mpaka kwa Bwana YESUKRISTO. Niliona YESU amesimama mbele ya
geti akinisubiri mimi na nilipofika,YESUKRISTO kaniambia “Unatakiwa uende kule ile sehemu
ya wamena mara moja na uwape ujumbe wangu, kuwa wanatakiwa WATUBU kwa sababu
muda umekwisha.Unatakiwa uende Wamena”.
Bwana
alikuwa akiongea huku uso wake ukiwa wenye huzuni na wenye kusinyaa huku
akilia, Machozi yake yakidondoka pale kwenye meza ya kioo ambayo anaweza kuona
kila kitu ambacho watu wanakifanya.
Nikamuuliza
“ Bwana kwanini walia ?” .Hakunijibu
swali langu na huku machozi yakizidi kumtoka nakudondoka kwenye meza nami
nikayafuta machozi na kamba nyeupe nilioivaa, kila nilivyokuwa mbinguni
nilikuwa mara zote navaa kamba nyeupe ambayo sijawi ivaa popote duniani.
Ndipo Bwana akaniambia huku machozi yakimtoka “Lala,
waambie watu wangu haraka ,wanatakiwa warudi kwangu haraka, Muda umekwisha
kabisa .”Bwana YESUKRISTO kasema tena, “Sitamani mtu yeyote apotee,
lakini wote wakae katika ufalme wangu”.
MUNGU unaposoma ujumbe huu pia mshirikishe na
mwingine (share),
Badilika na uanze kuishi kama MUNGU atakavyo hapo
ndipo utakapo okoa maisha yako.
Ushuhuda wa Laura Wamna(LALA), dada wa miaka kumi
na mbili (12) kutuka Indonesia.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!