menuz

MAONO JUU YA SIKU ZA MWISHO, KANISA, UNYAKUO, MBINGU NA KUZIMU na Othusitse Mmusi.

Maono aliyoonyeshwa na Bwana, ndugu Othusitsie Mmusi kutoka Botswana kuhusiana na Siku za mwisho, Mateso ya majaribu, Dunia katika vita, Uchumi utavyoanguka, Malango ya kuzimu yamefunguliwa, Mashambulizi ya kiroho, Hali ya kanisa, utayari wa unyakuo, mbingu na kuzimu.Maonyo makuu kutoka kwa Bwana ili wote wenye masikio wasikie ili wajiandae wenyewe.

Jumapili ya mwezi wa 8,tarehe 30 mwaka 2015 mida ya saa 9 usiku.Nilikuwa kitandani mwangu na ghafla macho yangu ya kiroho yakafunguka Nikaona nje ya paa la nyumba wakati nipo ndani ya nyumba, nikaona nyota na anga.Ghafla nikawa nje ya mwili,nikasafiri katikakatika anga kwa mwendo mkubwa.Nikaona nyota na anga.

MATESO YA MAJARIBU KWA WAKRISTO
Bwana MUNGU akaanza kunionyesha mateso ya siku za mwisho kwa waKristo, Nikawaona waKristo wamekamatwa, wanapelekwa jela, Nikawaona wachungaji wamekamatwa, Nikaonyeshwa kwenye gazeti na majina ya wachungaji na makanisa waliofungwa.Nikaona watu wamekaa chini wakipanga nani anayefuta kufungwa.Haya yalikuwa yakionekana sehemu mbali mbali duniani,Hasa mashariki na kati.Nilionyeshwa wanawake, watoto na waume wakiuwawa kwa njia mbalimbali, wakikatwa, roli lililojaa watu waliotekwa,watu walikuwa wakilia na kuogopa wengine walikuwa wakikimbia kujaribu kujificha na hao watesi.ilikuwa inaumiza sana.Bwana akasema nami, “Hii ni ishara ya ujio WANGU u karibu”.
Mathayo 24:9-“Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”
Mathayo 24:33-“33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.”

VITABU VYA KIKRISTO, MAKANISA NA FACEBOOK PEJI
Bwana MUNGU akanionyesha stoo ya vitabu vya kiKristo Nikaangalia katika mashelfu na vitabu vingi na vilivyoandikwa na waKristo lakini vyote vinahusu “Furahia maisha”, “Mafanikio katika maisha”, “Funguo za utajiri”.Nikaangalia karibu vitabu vyote vilikuwa vina masomo hayo ya kufanana.Nikauliza tafadhali naweza  kupata kitabu kinachohusu Kuzimu ,Mbinguni au Unyakuo.Nikashangaa sana katika stoo kubwa yenye vitabu vingi sana vya kikristo nikaletewa kitabu pekee kimoja tuu nacho ni kidogo sana ndicho pekee kinachohusu mambo ya kuzimu na mbinguni.

Bwana MUNGU akanichukua na kunionyesha majina ya makanisa tofauti tofauti na waanzilishi wake.Katika hayo nikaonyeshwa ujumbe mkuu na unahubiriwa mara kwa mara katika hayo yote makanisa ni ujumbe unaohusu “Mafanikio katika maisha”.Nikaonyeshwa kanisa moja lilikuwa dogo sana ndilo lilikuwa linajali kuwa andaa watu wake kwa ajili ya ujio wake Bwana YESUKRISTO.
Uwiano wa makanisa yaliokuwa yanahubiri bibilia kikamilifu na kuweka msisitizo kuhusiana na mambo ya milele, ilikuwa ni kama 1:20 kama hesabu ya makanisa yote ya ile orodha.
Ndipo Bwana akafungua kioo, Nikaona Fesibuku peji(Facebook page) nyingi sana, Na nyingi zake zilikuwa zikijikita kufundisha watu kuishi vyema,kufurahia sasa maisha, kupokea baraka na fedha, Baada ya hayo nikaona peji (page) iliyojikita kufundisha watu nini kinachofuata baada ya haya maisha,kuzimu, unyakuo, mbinguni na utakatifu.

Nikaangalia watu walio (like) hiyo peji(page) niliona majina ya marafiki zangu wawili tu,na hao wengine nilikuwa siwa fahamu.Nilishangaa kwa nini peji(page) zenye ujumbe wa maana zina watu wachache ukilinganisha na zingine.Na kwanini wakristo wachache sana ninao wafahamu walio like peji hizo.

Bwana akaniambia “Mwanangu, Hii ni hali ya kanisa LANGU, Hii inakuonyesha watu wangu wengi wasivyokuwa tayari kwa ujio WANGU.Wengi wanasumbikia vitu vidogo badala ya kusumbukia kunipendza MIMI.Watu wangu wachache sana ndio wako tayari kwa unyakuo WANGU,Kama ndio ningekuja sasa ,wachache ndio wangenyakuliwa, Waonye sasa, Muda ni mfupi sana sana.”

2 Timotheo 4:1-4 “1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
 2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;”
 4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.”

YOHANA MBATIZAJI, UNYAKUO, MTAZAMO WA MBINGUNI NA KUZIMU.
Jumatatu, mwezi huo huo,31,2015.Asubuhi Bwana akafungua macho yangu ,Nilikuwa nimesafiri kwenye dunia ndipo likaja jangwa, Nikamuona mtu ambaye inaonekana kama anaishi hapo katika hiyo nchi.Alikuwa ana mavazi yaliyotengenezewa na ngozi ya mnyama na manyoya.Nywele zake zilikuwa ndefu,Naye alikuwa akipaza sauti katika jangwa kama vile akihubiri,Bwana akafanya nielewe kuwa alikuwa ni Yohana mbatizaji, Nikaona watu wengi wanamjia ili kusikia ujumbe wake.

Bwana akaniambia, Ninatuma wahubiri ambao watakuwa kama Yohana mbatizaji na wataandaa njia kwa ajili ya kuja kwake BWANA, Hao wahubiri wataohubiri TOBA na kufanya watu WANGU wawe tayari kwa ujio WANGU”.
Malaki 3:1 “1 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.”
Mathayo 3:1-6 “1 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
 2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
 3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
 4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
 5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;
 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.”

JE, UNYAKUO TAYARI ?
Bwana MUNGU akanichukua na kunionyesha siku hizi hizi duniani, nikiwa nimesimama na viumbe vya kimbingu na nilipo inua macho yangu juu ,Niliona jambo la ajabu nikaona upinde mkubwa , wingu linalong`aa na utukufu wa MUNGU ulikuwa unang`aa.Nikaona mianga myeupe inatembea  tembea kwenye mawingu na niliweza kusikia sauti kutoka huko,Nayo ilikuwa inakuwa kila sekunde ndipo nikajua hili ni wingu la kupokea ujio wa YESUKRISTO.Nikajua muda wowote tokea sasa unyakuo unaweza tokea hivyo vitu katika anga vikazidi kukua na kuongezeka hasa anga la mashariki.Nikaangalia duniani, nikaona watu wengi, wakristo, nao walikuwa hawaoni lolote walikuwa wakiendelea na shughuli zao wako bize kila siku na shughuli zao za siku kwa siku wako huru hata kutenda dhambi kama siku nyingine.Kwa wao ni siku kama siku zingine.Nilijua kuwa muda wowote unyakuo utatokea.

Bwana akaniambia “Mwanangu,angalia, hawakeshi wala kuomba,Sio wakeshaji kwa ajili ya ujio WANGU,Wako kwenye usingizi wa kiroho pamoja na dunia, Hawajui ishara hata ishara zangu za ujio Wangu,Hawajui si muda nachukua KANISA”
Mwili wangu ukawa mwepesi kwa uzito nikajisikia kama nimebadilishwa, Nikajiona mwepesi kwa uzito, mwili unaweza ukawa kwenye hewa na kuja chini, kama vile putolinalo nyanyuliwa na upepo  na kushushwa chini tena,Nilikuwa naenda juu na chini kama vile kuna kitu kinataka kutokea.
-Luka 21:36 “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
-Ufunuo 22:7 “Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.”
MBINGU
Mara nikapelekwa mbinguni, Kitu cha kwanza nilichokiona kilikuwa ni paradise hali ya hewa ya mule ilikuwa nzuri sana yenye amani kutoelezeka.Kulikuwa na mianga kila kona,niliona maeneo makubwa na mashamba yanayoonyesha ni vigumu kuona mwisho wake.Niliziona bustani nzuri na zenye kupambwa kwa maua na chemi chem za maji, Nikaona mwanga wa dhahabu unaongaa kwenye bustani, niliona miti ya mapori iko sawa sawa.Nikaona wanyama wenye nguvu na afya, Nikaona ndege wa kila aina ,vitu vya mbinguni vya shangaza kupita kawaida nilibaki kujisemea “wow”, “vizuri sana” “utukufu”.nikasikia furaha na amani isiyo ya kawaida katika roho yangu.

Nikaja kwenye mji wa Mbinguni , Nikaona mitaa ya dhahabu ,nikaona majumba,jumba la kwanza nililoliona lilikuwa kubwa sana na zuri mno lililochukua eneo kubwa ,nilijua kwa ufunuo litakuwa na vyumba vya kulala mia, vifaavilivyotumiwa kujengea nyumba hiyo havijawahi onekana hapa duniani. Lilikuwa likiwaka waka,lenye rangi mbali mbali na refu , Nyumba ingine ilikuwa kubwa kuliko ya kwanza niliyoiona, na yatatu niliyoiona ilikuwa kubwa kuliko ya pili.Zote zilitengenezwa kwa malighafi za mbinguni.Bwana akaniambia: “Hao ni watumishi Wangu walionitumikia kwa uaminifu duniani,Pia kuna majengo makubwa zaidi ya hayo”.
Bwana akaniambia; “Nitakuchukua wewe muda mwingine na kukuonyesha jumba la Ibrahim na Paulo”.Nikajua majengo yao yatakuwa makubwa sana kulingana na vile Bwana alivyo nieleza na kutokana na uaminifu wao na kazi kubwa walioifanya kwa MUNGU imewapa majumba makubwa mbinguni.
Bwana akaniambia “Kuwa mtii na mwaminifu katika kufanya kile nilichokuitia kukifanya”
-Yohana 14:1-3 “1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”
-1 Wakorintho 4:1-2 “1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
 2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.”
Niliona sehemu, ambako kila kitu kilikuwa kinang`aa dhahabu, Mwanga wa dhahabu wa uwepo wa udhihirisho Wake, Maua pia yalionekana ya dhahabu.Sikutumia muda mwingi hapo.
Mji wote wa mbinguni ulikuwa unamwanga,rangi nzuri,uzuri na uhai.Nilikuwa nikipiga kwa sauti msifu MUNGU!,msifu MUNGU !,Pia vitu vingi vilijitokeza kipindi ambacho nilichokuwa naenda kwa spidi ya mawazo,Nakuwa mara moja katika sehemu MUNGU aliyotaka mimi niwe.
MTAZAMO WA KUZIMU
Mara nikajikuta nje ya mbingu ,nkapelekwa sehemu za chini za dunia ,nikaona Kuzimu, kulikuwa na giza la kutisha lililo samba,mapepo wa kila aina, watu walikuwa wakiteseka na moto na wakilia na kupiga kelele kwa uchungu , “awf !, awf !” na kuomboleza kwa roho zao kupotea.
VIPAO MBELE VYA MILELE
Mara nikatolewa nikawa ninakuja.Nilikuwa nina paa kwa spidi isiyo ya kawaida dunia nzima ,nikiona mataifa mbali mbali, wakila tamaduni,watu wa rangi zote.Nikasikia sauti kutoka kwa MUNGU mbinguni ikisema “Nenda na uwaambie watu wadunia kuwa umeiona mbingu na kuzimu.Nenda na uwaambie hao,kuwa umeona viumbe mbinguni na umeona mapepo ya kutisha Kuzimu pia,Nenda na uwaambie wanatakiwa wajiandae kwa ujio WANGU,Waambie nimetuma ujumbe huu,Waambie nitathibitisha pindi mtumishi WANGU atapohubiri ujumbe huu,Waambie saa hii, nnaweka thamani zaidi kuhubiri kuhusu utakatifu na ujio wangu kuliko mafanikio”.
- Zaburi 9:17 “Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.”
- 1 Petro 1:13-16“Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
 16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
- 1 Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”
Ghafla nikaoka katika maono.Nilishangazwa na kuanza kuongozwa kwa kile nilichokiona na kupitia.

MALANGO YA KUZIMU, roho ZA GIZA, SAUTI YA BWANA YESUKRISTO.
Jumamosi,Mwezi wa 9, tarehe 19,2015 saa kumi na moja(11) asubuhi.Macho yangu ya rohoni yalifunguliwa kwa uwazi ,Na kuangalia chini  nikaona malango ya kuzimu, Mara nikaona kundi la roho za giza zilikuwa zikitoka kwa kasi ,nilipoangalia kwa karibu ,nikagundua mapepo ya kila aina wengine wapo kama viumbe warukao na mbwa.Nao walikuwa wakipanda kuja duniani.
Ndipo nikasikia kwa sauti ya YESUKRISTO ikiongea wazi wazi kutoka mbinguni ikiongea kwa sauti kubwa setensi hiz tano.
1.    “MALANGO YA KUZIMU YAKO WAZI,
2.    LAKINI HAWATAWEZA KUSHINDA,
3.    WATU WENGI WATAANGUKA
4.    NA WATU WENGI WENGINE WATAINUKA
5.    LAKINI ATAKAYEVUMILIA MPAKA MWISHO ATAOKOLEWA”
Ghafla nilipokuwa nikaona kitu kilichonishtua nikaona wachungaji wengi wakubwa na maarufu, baadhi wakianguka katika dhambi , na hawakutubu na hakuna anayejua na wengi kushindwa kuingia mbinguni.
Ilikuwa ni mchanganyiko ,wa mbio tofauti tofauti, niliweza kerejesha kwa kiasi tu kumbukumbu yake.Zile roho zilizokuwa zinatoka kuzimu , nyingi zake zilikuwa ni roho zinazoleta kuhamasisha dhambi za uasherati,uzinzi na kila aina ya matamanio, ndiyo maana watu wengi walianguka.Nilikuwa nikiruka karibia na mwisho, kulikuwa na kila aina ya mapepo duniani,kwa kutongoza, na kufanya kila aina ya uovu.
Nakumbuka nililia nikisema “Bwana YESU, niokoe niokoe mimi kutoka kwenye huu mtego wa shetani, tafadhali, tafadhali  nisaidie kuwa mwaminifumpaka mwisho”.Nilikuwa katika machozi nikiomba,kuona jinsi gani shetani anawaharibu watu.Niliangalia maisha yangu kama nacheza na movi,sasa mpaka karibia mwisho, kutembea na Bwana,Na ilipofika mwisho ,maono yalinyanyuliwa juu kwa haraka.Nilitetemeka kutokana na kilichoko duniani na kuhusu wakristo wengi ambao wanaanguka na kushindwa kuingia mbinguni ,hata wale wachungaji wakubwa na maarufu sana.
Niliwahi rudi nyuma na kuacha wokovu kipindi nilipokuwa kijana,Bwana alinionyesha sehemu na kunipa nafasi ingine.
Katika hizi siku za mwisho tunatakiwa kila siku kuwa na ushirika mkubwa na MUNGU,Tunatakiwa kusoma neno la MUNGU,kufunga na kuomba, Tunatakiwa tuwe na marafiki/makundi mazuri, hatutakiwi kukosa kusanyiko la wapendwa (Kanisa na Ushirika).
“21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”-Mathayo 7:21-23
- “8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8

VITA YA TATU(III) YA DUNIA, GIZA NA KUANGUKA KWA UCHUMI
Jumatatu ya mwezi septemba,21,2015.Asubuhi mishale ya saa mbili.Nilionyeshwa kuna wanajeshi wengi sana wakiwa kutoka nchi mbali mbali wakiwa na gwanda tofauti tofauti kulingana na mpangilio wa nchi zao.Wakiwa tayari kwa vita,Marekani na walioungana nao,China na walioungana nao,Kulikuwa na bunduki nyingi sana, wanajeshi wa miguu,Silaha za kila aina.Inaonekana vita ya dunia ya tatu(3) ikiwekwa tayari kuanza.
Niliona giza la ajabu lililofunika ardhi,anga,na umemeulikuwa haupo kwa baadhi ya maeneo,Watu wengi wakaenda kujificha katika makanisa ili wapate ulinzi.Niliona Nikaona sehemu watu wakiwa maelfu ya watu, vijana, watotot na wakubwa ,wako wakiwa wakimbizi katika nchi zao wenyewe.

Niliona uchumi ulioshuka , kuwa mbaya na watu wakishindwa kutoa fedha kwenye ATM.Katika maono hayo hali iliyo karibu sana na kujua mapema mapema tarumbeta italia, kanisa litanyakuliwa na dunia ikaachwa katika dhiki kuu.Ghafla nikatoka katika maono hayo.

-“ 25 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;
26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.
27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
28 Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.”-Luka 25-28
SHARE KWA WENGINE 

4 comments:

  1. Hello there! I could have sworn I've been to this website
    before but after reading through some of the post I realized it's new to me.
    Anyhow, I'm definitely glad I found it and I'll
    be bookmarking and checking back frequently!

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe mtumishi,endelea kuwahimiza watu kuhusu toba

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!