Neno: “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni,
Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8
Theme:umoja ni asili ya
MUNGU
Kama watumishi wa BWANA
sisi tunatakiwa kumuiga MUNGU katika utendaji wa kazi yake kwa kuwa wamoja
kuineza kweli yake YESUKRISTO.
MUNGU
ametuumba kwa mfano wake hata katika utendaji wetu kwa kuwa YEYE ni mwenye
umoja ,
“Mimi na Baba tu umoja.” Yohana 10:30.
basi nasi pia tumeumbwa
tutende kazi katika umoja huo huo siku zetu zote.
Kama watumishi wa MUNGU hatuna umoja tutakosa
ujasiri wa kufaidi karama mbalimbali ambazo MUNGU ametujalia,
Kwa kuwa MUNGU
ametoa karama mbalimbali,kama ilivyo andikwa “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali,
kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
“Warumi 12:6.
Kuna mtu mwingine ana
karama ya unabii, mwingine kufundisha na kadhalika .
Lakini kama watumishi
wa BWANA hatuna umoja yule mtumishi ambaye
hana karama ya unabii na anahitaji unabii atakosa ujasiri wa kuhitaji huduma ya
huyu mtumishi ambaye amepewa na MUNGU karama ya unabii,
Vivyo hivyo huyu
mtumishi mwenye karama ya unabii akihitaji mafundisho atashindwa kupata kwa
kuwa hana umoja katika YESUKRISTO.
Sisi tu wa moja.Na kama
tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja
yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!