menuz

Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ujuehicho ndicho unacho mtendea YESUKRISTO !


Jiulize unawatendea nini ?,  watu mbalimbali unaowajua au usio wajua hicho ndicho unamtendea MUNGU!.

Haipingiki kuwa kuna kwenda mbinguni kama umemkubali YESU au kwenda kwenye moto wa milele kama umemkataa baada ya kifo.

Imeandikwa “32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”-mathayo 25:33-46.
Anaposema nilikuwa uchi mkanivisha nilikuwa na njaa mkanilisha  na kadhalika,Hayo yote ni matendo ya upendo na Hii  inamaanisha kuwa Upendo wa kweli ndio utamfanya mtu aweze kwenda mbinguni,

Jiulize unamtendea nini  jirani yako,nduguyo,rafiki yako,hata adui wako ?,Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ndicho hicho unamtendea YESUKRISTO.

Imeandikwa “40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”-Mathayo 25:40

Je kuna baadhi ya watu unawadharau ?, Jua unamdharau YESUKRISTO au kunabaadhi ya watu unawaona sii kitu yaani wewe uko juu yao jua unamshusha YESU.

Imeandikwa “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”- Mathayo 18:3

Waweza jiuliza inamaanisha nini ?
Watoto hawatunzi chuki,hawa hesabu mabaya ya mtu, watoto ni wepesi wa kusahau mabaya waliotendewa ,hawahesabu hata mazuri waliowatendea watu . . . .hizi ni baadhi tuu ya  tabia ambazo wanazo watoto ambazo MUNGU pia anataka tuwe nazo ilituu kuweza kumpenza YEYE.

Tunatakiwa tuwe na upendo wa kweli ,upendo wa vitendo kutoka moyoni.Imeandikwa "Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu" Wakolosai 3:14

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!