Zaidi ametupa kujua ishara zitazotokea katika nyakati
hizoo tuu na sio muda au siku kamili ya
kuja kwake duniani tena !!.
Imeandikwa “32 Walakini habari ya siku ile na saa ile
hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. 33 Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui
wakati ule utakapokuwapo.”- Marko 13:32-33.
YESU anatupenda sana kwa kuwa pamoja na kutotaja muda wala
nyakati za ujio wake lakini ameeleza mbinu ya kufanya ili tusije aibika pindi
atakapokuja mbinu yenyewe ni kukesha, kuwa macho kiroho.
Hakuna
binu tofauti na hii kama wewe uu msafiri kuelekea mbinguni hii ndio pekee
mbinu.
Imeandikwa “Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala
saa”-mathayo 25:13.Unaweza kujua mambo yajayo mengi sana hata kujua
siku zako kwa idadi yake ulizopewa hapa duniani lakini hakuna mtu yeyote wakujua
muda au saa kamili ya kuja kwake YESU .
Siri na mbinu kuu ya kumsubiri YESUKRISTO nikukesha yaani kuwa
macho kiroho masaa yote kwa kuwa hatujui saa wala muda.Imeandikwa “Kesheni
basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”-mathayo 24:42.
Imeandikwa “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na
kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”-ufunuo
16:15.
Sababu ya kukesha yaani kuwa macho kiroho ni kwa kuwa hatujui na
hakuna anayejua muda wala saa pia atakuja kama mwivi.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!