Toka ndoa ya kwanza ,yaani ile aliyeifungisha na kuianzisha
MUNGU mwenyewe ilikuwa inasababu za kutosha kuvunjika kama adam na hawa
asingejua kuwa hawana ukamilifu.
Imeandikwa"Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi
mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali
pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke,
akamleta kwa Adamu.
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na
nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika
mwanamume.”-Mwanzo 2:21-23
Hapo tunaona MUNGU mwenyewe anamtafutia adam mke toka
ubavuni mwake yaani mke kutoka kwa BWANA.
Lakini ndoa yao ilikuwa inasababu za
kutosha kuvunjika ,kwa kuwa Hawa alifanya makosa na kudanganywa na nyoka
mpaka akala tunda ambalo aliamriwa asile na MUNGU hata kumkosesha mumewe adam
kwa kumpa naye ale tunda hilo.
Imeandikwa" Adamu akasema, Huyo mwanamke
uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.Bwana
Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, . . . . .
. " –Mwanzo 3:12-13
Ndoa za leo ambazo mwanamke au mwanaume akifanya kosa moja anapata
talaka,au anapigwa, anaachika au anateswa na kusemwa na mumewe au mkewe vibaya jifunzeni kuwa hakuna ndoa iliyokuwa kamilifu ila kila mwanandoa anachukulia udhaifu wa mwenziye.
Adam alikuwa na sababu ya kuachana na hawa kwa kuwa hawa ndio
aliyesababisha machungu ya kulaaniwa na MUNGU lakini kwa kuwa alijua na kutambua kuwa yeye si mkamilifu na anamapungufu
hivyo alimchukulia kwa hayo mkewe.Kwa wanandoa waleo na wanaoingia kwenye
ndoa hivi karibuni yapasa kujua kuwa hakuna aliyemkamilifu hata yule atokaye kwa MUNGU (mke mwema/mume
mwema).
Ndoa ya Sara na Ibrahim ilikuwa na utasa kwa muda mrefu hata uliwafanya wao wenyewe kukata tamaa,hiyo ingeweza kuwa ni sababu au kigezo cha ibrahimu kuachana na Sara kwa kuwa alikuwa hazai. Lakini hakuachana naye kwa kuwa alikuwa akijua kuwa hakuna aliye mkamilifu kila mtu anamapungufu.
Sasa kuna wanandoa wanaachana kisa tuu mwanamke au mwanaume ni tasa ,Imeandikwa“Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto”- Mwanzo 11:30. Ibrahimu hakumuacha mkewe wala hakuchukua kama sababu ya kumuacha mkewe Sara.
Hakuna popote duniani ndoa isiyopitia misukosuko ,toka agano la kale mpaka leo agano jipya hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto ila tuu inatofautiana namna ya kuzikabili changamoto hizo kwa kuwa wengine hukabili changamoto hizo kwa kuachana na ndoa zao,wengine huvumilia na kuzishinda.
Imeandikwa “Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?”- Mwanzo 30:2. tena Imeandikwa “Naye Raheli alipoona ya kuwa
hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo,
Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.”- Mwanzo 30:1
Si kwa yakobo bali hata Raheli alikuwa yuko radhi hata kuachana na ndoa hiyo,hataalikuwa yuko tayari hata kufa kwa matatizo aliyokuwa nayo yakutukuwa na mtoto na aibu aliyokuwa anakabiliana nayo kipindi hicho,lakini alivumilia na kuikabiliana na hiyo changamoto iliyo tendganisha ndoa yake.
Hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto ,kama changamoo yakupata mtoto huna basi itakuwepo kuwa na mume /mke mkali ,utakuwa na changamoto ya kuwa na mume/mke asiye eleweka kazi yake ni kuleta hasara tuu.
Imeandikwa “.Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa.
Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.” Mwanzo 25:20-22
Kuna mtazamo tofauti kwa dunia ya sasa pale watu wanapo oa au kuolewa wanahisi kama wakiolewa na mume sahihi wa maisha yao au mke sahihi ambao Bwana amewatengea kwa ajili ya maisha yao hawatapata kuona kikwazo chochote hawatapata shida kitu ambacho si kweli.
Kila wanandoa unaowaona wanasababu kubwa kabisa ya kuachana na ndoa zao ila haachi kwa kwa kuwa wanatambua ya kuwa hakuna aliye mkamilifu.
Imeandikwa
“Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.”- Waamuzi 13:2
Kama hakuna aliyemkamilifu baasi hakuna ndoa ambayo itakuwa ni kamilifu yaani hakuna anayemkosea mwenziye ,bali wanavumilia huku wakijua hakuna aliyemkamilifu.
Ndugu ukiona ndoa ni mbayaa labda kwa sababu ya mwanaume au mwanamke na unatamani ndoa ya mwingine au uolewe /kuoa mke au mume mwingine ,ujue wazi kuwa unayeitamni inamatatizo kama kawaida labda tuu yametofautiana tuu kwa jinsi anavyo yachukulia.
Kwanzia leo kaaa chunguza utagundua hata wale wanao sherehekea ndoa zao kuwa zimeduumu kwa miaka mingi utagundua kuna shida ziliwahi wakumba na zilikuwa ni sababu tosha za kuachana kwao ila wakazivumilia na wakazishinda .
Ukichunguza hata ukiweza wauliza we waulize wao wanao sherehekea miaka mingi ya ndoa zao utagundua kuna ukweli kabisa mume au mke alikuwa anatabia ya kutoka nje ya ndoa lakini mume au mke alimuonya alimvumilia akijua yeye pia si mkamilifu.
Anza kwa uzuri kutazama changamoto katika ndoa yako na kuzitatua na sio kukimbilia kuachana kwa kuwa kila ndoa hapa duniani inasababu za kutosha kuvunjika lakini kwa ajili ya kutambua hata ikivunjika hakuna aliye mkamilifu hiyo pekee husababisha kuvumiliana katika ndoa bila kujali mapungufu makubwa aliyonayo mume wake au mke wake.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!