Duniani tuko kwa muda mfupi sana kitu
ambacho watu wengi hatupendi kukisikia ingawa ni kweli, Imeandikwa “Mwanadamu siku zake zi kama
majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.”-Zaburi 103:15 .
Na ndani ya hiyo miaka michache tunayoishi
hapa duniani kwa ujumla imejaa shida na dhiki. Imeandikwa “Mwanadamu aliyezaliwa na
mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.”-Ayubu 14:1
Mtu anazaliwa anahangaika anasoma
anajenga majumba ,anaoa/kuolewa anazaa watoto ,anakuwa hata nakila fahari
yoyote lakini mwishowe anakufa.
Baada ya mtu kufa kuna machaguo
mawili (2) ama kuishi milele katika moto wa milele kama ulimkataa YESU hapa
duniani au kuishi na BWANA YESU kwa amani na furaha milele endapo ulipokuwa
duniani ulimkubali YESU.
Imeandikwa “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake
wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele,
aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.”-Mathayo 25:41
Hakuna njia yoyote tofauti na njia ya YESUKRISTO
ili kwenda mbinguni(makazi ya milele na ya raha baada ya kifo hapa
duniani).Imeandikwa “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa
Baba, ila kwa njia ya mimi.”- Yohana 14:6.
Kama umekusudia kuishi milele na
kutokuangamia na moto wa milele katika siku za mwisho baasi wewe chagua leo
kumfuata YESU na uachane na njia tofauti ambazo zinadai eti utaenda mbinguni
pasipo kumtambua YESU kama MUNGU na kama njia pekee.
Ukweli ambao waweza kuufanyia uchunguzi: YESUKRISTO anajithibitisha mpaka leo kwa
kutenda miujiza ya kuponya watu,kufufua watu, hata kutoa mapepo kupitia
watumishi wake mbalimbali waliomkubali katika makanisa mbalimbali.
YESUKRISTO ni mkweli kabisa kwa
kuwa YESU amezungumza ukweli kuwa duniani kuna dhiki na kweli tunaiona dhiki.Imeandikwa
“
. . . . . . . Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda
ulimwengu.”-Yohana 16:33.
Hakuna ambapo YESU anasema kuwa
mbinguni kuna dhiki ,lakini anatushauri
tumchague YEYE ili tufurahie pamoja naye mbinguni tusije angamia kwa kuzifuata
njia tofauti na YEYE.Imeandikwa “Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu
yenu ni kubwa mbinguni . . . . . . . . . .”-Mathayo 5:12.
Imeandikwa “Amin, amin, nawaambia, Mtu
akilishika neno langu, hataona mauti milele.”- Yohana 8:51. Kuna mauti
ya kwanza ambayo kila mtu itampata na baada ya hapo kuna mauti ya pili ambayo
ni ya hukumu kutoka kwa MUNGU mwenyewe.Kwahiyo kwa walio mfuata YESU hiyo mauti
ya pili haitawapata.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!