Faida zitokanazo na
vita yako
Mtu
anapopitia vita kali au magumu katika maisha yake na akamtegemea Mungu katika
muda wote wa vita yake, Kuna faida zitokanazo na vita yake hujitengeneza ndani
yake.
Kuna faida
nyingi sana za vita yako moja wapo ni njia ya kutangaza injili ya Bwana, fikiria
pale watu wanapoona ulivyokuwa na matatizo makubwa sana na Bwana akakupigania
ukashinda kabisa.
Watu wanamjua Mungu wa kweli kupitia wewe kwa kuwa wameona
jinsi alivyokuokoa.
i.Bwana anakufundisha vita
Faida moja
wapo kubwa ambayo mtu anaweza kuipata ni kufundishwa vita na Bwana.Bwana
anakufundisha vita mpaka uweze kupambana na kupata ushindi.Imeandikwa “Na
ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu
kupigana. ” Zaburi 144:1
Unapopitia
vita Mungu anakuwa anakuandaa kwa kusudi alilokuwekea kulifanya hapa duniani.Bwana
anakufundisha vita kwa namna ya rohoni, anakuongoza nakukutia nguvu kuelewa
namna ya kutumia silaha za rohoni. Imeandikwa “Maana ingawa tunaenenda katika
mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;”2 wakorintho10:3
Imeandikwa.
“Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.”
Zaburi 18:34 .Mtu anapopitia mambo magumu,vita kubwa kwenye maisha yake
naye Bwana humfundisha vita hata aweze kusimama mpaka ushindi unapotokea katika
hayo ayapitiayo.
Mtu ambaye
kawaida yake ni mtu wa kujikweza. Wakati wa vita na mambo magumu yatakapomfika
naye Bwana atamfundisha kujishusha.Imeandikwa “Bwana
hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.” 1 Samweli
2:7.
Mungu
hufundisha pasipo hata mtu mwenyewe kujua kuwa ni Mungu ndiye amfundishaye, kwa
mfano watu wengi huanza kufunga na kuomba sana pale vita inapokabili maisha yao.
Watu wengi
hukumbuka kuutafuta uso wa Bwana pale tuu wanapopitia vita katika maisha yao.
Imeandikwa “Kulikuwa na
njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta
uso wa Bwana. . . . . . . . . . . .” 2
Samweli 21:1
Imeandikwa “Awafunge
masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima.” Zaburi 105:22.
Bwana hufundisha watu wake hekima ya kuvumilia, hekima
ya kusema na watesi wako na hata hekima ya kupenda wale wote waliokuumiza
kipindi cha vita yako.
Imeandikwa “Tazama, Mungu
hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye?”Ayubu 36:22.Mambo magumu yanapotokea,vita
inapojiinua katika maisha yetu ujue kuna jambo ambalo Mungu anataka
kutufundisha kupitia vita hiyo.
Mungu
hutufundisha mambo makuu na hayo mambo makuu atufundishayo hutufanya kugeuka na
kuwa watu tofauti yaani watu wenye kumuheshimu Mungu ili aweze kutenda kazi
pamoja nasi.
Imeandikwa “Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la
shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi
nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.” Yeremia 15:20
Kwa hiyo
faida inayotokana na vita yako ni kufundishwa na Bwana vita.Mungu humtengenezea mtu uwezo wa kusimama vyema kwa
kuwa humfundisha namna ya kushinda vita yake.“Ananifundisha mikono yangu vita;
Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”2 Samweli 22:35.
ii.Mungu anatukuzwa kupitia
vita
yako
Mungu
hutukuzwa kupitia vita yako.Pale ambapo ulikuwa una matatizo, ulipokuwa
unakabiliwa na vita kubwa ya kusemwa vibaya katika maisha yako ndipo hapo hapo
Mungu hujitwalia utukufu.
Watu
wanapoona ulikuwa na vita kubwa na wakaona jinsi Mungu alivyokushindia, hapo Mungu anatukuzwa
kweli kweli.
Mungu kutukuzwa ni moja ya
faida kubwa zitokanazo na vita yako.
Mungu alijitwalia utukufu katika vita iliyokuwa ikimkabili
shadraka,meshaki na Abednego.
Imeandikwa “Nebukadreza
akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego;
aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza
neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala
kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.”Danieli 3:28
Bwana Mungu
hupenda kutukuzwa kupitia vita yetu.Imeandikwa“Nami, tazama, nitaifanya mioyo
ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu
kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.
Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokwisha kujipatia
utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi zake.” Kutoka 14:17-18
Mungu
hujitwalia utukufu katika vita au magumu tuyapitiayo katika maisha yetu.Mungu
ni Mungu wa utukufu.Imeandikwa “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye
nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”. Zaburi 24:8.Yeye Mungu hupenda
kutukuzwa kupitia vita tuipitiayo katika maisha yetu.
Mungu
alitukuzwa kupitia vita iliyokuwa ikimkabili Danieli pale alipookolewa na Bwana
kwenye tundu la simba.Imeandikwa “Mimi naweka
amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa
mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na
ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.”
Danieli 6:26
iii.Kuinuliwa na Mungu katika
kiwango usichotarajia
Faida nyingine ambayo hutokana na vita
yako ni Mungu kukuinua kutoka pale ambapo upo kwenda kwenye kiwango cha
kipekee, kiwango usichokitarajia.
Imeandikwa “Ndipo Farao
akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa,
akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao” mwanzo 41:14.
Vita iliyompata Yusufu ilimuachia faida
ya kuinuliwa na Mungu kutoka kuwa mfungwa gerezani mpaka kuwa waziri
mkuu.Imeandikwa “Farao akamwambia
Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya
muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu
; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa
dhahabu shingoni mwake.
Akampandisha
katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake,
Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.” mwanzo 41:41-43.
Faida iliyotokana na vita iliyompata Danieli ni
kuinuliwa na Bwana kutoka kwenye hatari yakuuwawa na mfalme hadi kuwa mkubwa wa nchi.Imeandikwa “Basi
ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu
wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe.” Daniel 2:13.
“Basi mfalme
akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu
ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa
Babeli.” Danieli 2:48
Vita
iliyowapata shadraka ,Meshaki na Abednego iliwaachia faida ya Bwana kuwainua
kutoka kutaka kuuwawa mpaka kuwa wasimamizi wa wilaya.Imeandikwa“Kisha
mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.”
Danieli 3:30
Hakuna mtu
yeyote aliyewahi kupitia magumu, kupitia vita huku akimtegemea Bwana katika
vita yake naye Bwana alipomshindia akabakia kwenye ngazi ile ile.Kuinuliwa ni
faida kubwa itokanayo na vita unayopitia.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!