Maombi ya kushinda vita yako
Ndugu kabla
ya kufanya maombi haya yatakayo kuwezesha kushinda vita yako, yatakayo
kutenganisha na wanao onewa, maombi yatakayo rudisha kile ambacho adui(shetani)
amekiiba maishani mwako.
Ili kuomba
vizuri maombi haya ya kushinda vita yako ni lazima uwe una YESU, kwa kuwa wale
waliokuwa na YESU ndiyo pekee waliopewa mamlaka na nguvu za katika kuharibu kazi
za ibilisi (shetani).
Ni jambo jema
zaidi kuwa na YESUKRISTO ili atawale na aongoze maisha yako katika kusudi la
mema yake aliokuwekea katika dunia hii na kukupa kuishi milele hata baada ya
kufa kwako. Imeandikwa “YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na
uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;”
Yohana 11:25
Mpendwa kuna
njia moja tuu ya kwenda mbinguni, kuna njia moja tuu ya kuishi milele nayo ni
kumkubali Yesukristo katika maisha yako. Imeandikwa “YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli,
na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana 14:6
Kumkubali
YESUKRISTO katika maisha yako ni kukubali kuishi kama yeye apendavyo yaani
kutenda yale yoote akuagizayo kupitia neno lake.Imeandikwa “wale ambao kwa saburi katika
kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa
milele;” Warumi 2:7.
Mwanzo wa kumpokea YESU
Omba sala
hii fupi kwa imani iwe mwanzo kumpokea YESU, Kwa kumpokea YESU atakuongoza
kushinda kila gumu unalopitia, kila aina ya vita katika maisha yako
atakuwezesha kuishinda.
Mbali na
kukushindia katika Vita yako na magumu upitiayo, YESU atakuokoa na hukumu ya
moto wa milele na kukuweka katika uzima wa milele. “Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.
Omba
sala hii fupi kwa imani
“ MUNGU uliyeniumba mimi na vyote
vilivyomo humu duniani na mbinguni nakutukuza, pia ninakushukuru kwa upendo
wako mkuu katika maisha yangu,
Nimeamua leo nikufuate wewe BWANA MUNGU
uliyeniumba katika jina la YESU, nakuomba unisamehe maovu yangu yote katika
jina la YESU, nakuomba unipe neema yako ya kuishi katika njia ikupendezayo wewe
YESU mpaka siku ya mwisho wa maisha yangu.Asante YESU kwa kuniokoa leo hata
milele.”
Wewe sasa
umeshakuwa kiumbe kipya kwa kuwa umempokea KRISTO kwa sala fupi hiyo kama neno
lake lisemavyo “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale
yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 2 Wakorintho 5:17.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!