menuz

Omba maombi ya kushinda vita yako



Omba maombi ya kushinda vita yako

Imeandikwa mamlaka “Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi” Luka 9:1. Kwa kuwa umeokoka umepokea nguvu na uwezo juu ya kila nguvu za giza.Waweza kuomba kwa imani sasa:-
“Mungu Baba Nakaribia kwenye kiti cha rehema katika jina la YESU, pale walipo makerubi kwa damu ya Mwana kondoo, mahali ilipo utukufu maana imeandikwa katika Isaya 40:5 “Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja;. .  . . . .  . ”.
Utukufu wa Bwana ukafunuliwe kutoka kwenye kiti cha rehema, kwa maana imeandikwa katika Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;ndio maana Bwana tuna kuja kwenye kiti chako cha rehema mahali ambapo makerubi wamekitia uvuli kiti cha rehema.
Imeandikwa katika 2 samweli 22:10-11 “Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.”
Mungu akaziungamanisha mbingu akaruka juu ya mbingu na dunia ikajaa utukufu wake ,akapanda juu ya kerubi, na dunia ikajaa utukufu wake, imeandikwa katika “Hagai 2:9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.”
Utukufu wa mwisho wa dunia hii utakuwa mkuu kuliko wa kwanza, ziinamishe mbingu bwana na dunia ikajae utukufu wako, ukapande juu ya kerubi.

Nasi Bwana tunakuja kwenye kiti cha rehema kwa damu ya mwanakondoo, ziinamishe mbingu Bwana nawe ukashuke  na ukapande juu ya kerubi ,dunia ikajae utukufu wako, Bwana ziinamishe mbingu ukapande juu ya kerubi , dunia ikajae utukufu wako.

Mungu wa utukufu uliomtokea baba yetu ibrahimu katika huru wa kalidayo. Imeandikwa katika 2 Samweli 22:10 “Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.” Utukufu wako ukajae dunia yote katika jina la Yesu, aliziinamisha mbingu akashuka.akapanda juu ya kerubi akaruka.
Katika jina la YESU ninasimama kinyume na kila roho za uharibifu.kwa mamlaka ya damu ya mwanakondoo katika jina la YESU.

Naitegua mitego yake aliyetega,mitego waliyotegeamahali popote pale ,katika jamii, iwe ni katika maji, iwe ni kwenye chakula, Naitegua mitego yote katika jina la Yesu.

Mitego ya wafu waliyoitandaza katika ulimwengu wa roho ili kwamba ninaswe nina itegua katika jina la Yesu.ninategua mitego yote iliyotegwa aridhini, iliyoko kwenye anga,iliyoko mahali popote pale ninaitegua katika jina la Yesu.

Naachilia kishindo katika ulimwengu wa roho, nina tegua mitego yako wewe shetani uliyowategea watakatifu,ili wanaswe na mitego yako,nazitegua nyavu zako,naitegua katika jina la Yesu.

Mitego uliyotega ili kunidhohofisha nina itegua katika jina la Yesu.Mitego ya mauti uliyoitega ninaitegua katika jina la Yesu, mitego ya mauti uliyoitegea kanisa ninaitegua katika jina laYesu.

Katika Zaburi 18:6 imeandikwa “Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.”

Naye daudi akasema kwa maana katika shida yangu nalimlalamikia Bwana naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Bwana isikie sauti yangu hekaluni mwako, naitegua mitego katika jina la Yesu, naitegua mitego yote katika jina laYesu.
Da
udi akasema katika shida yangu nalimuita Bwana, namii nakuita leo isikie sauti yangu hekaluni mwako, kilio changu kikaingie masikioni mwako, kilio changu kisikike kwako.
Bwana tupe akili ya kujua mitego ya adui, tufahamu jinsi gani tuikwepe mitego ya adui, Nazichana nyavu za kiroho, nazikusanya nyavu zote zilizonitanda usoni mwangu katika jina la Yesu.
 Kila tenga ninalichana katika jina la Yesu, nalichana tenga hilo katika jina Yesu, ninaliyeyusha kwa moto, Bwana tupe macho Bwana yakuona mitego yao.
Ninafanya vita juu ya wote waliosimama kinyume na maisha yangu. Wote waliosomama ili kufanya vita, ninawaponda katika jina la Yesu, kila ngome na majeshi ya giza ninawaponda katika jina la Yesu.
Kwa msaada wa Bwana ninawafuata na kuwaponda, na wote waliofanya hasira juu yangu watakuwa si kitu , nina angamiza wote, nina bomoa wote walioweka vikao ili kuniharibu, ninawaponda, ninasambaratisha wote, ninaangamiza wote katika jina la Yesu ,toweka katika jina la Yesu .

Ninabomoa kwa jina la Yesu.Ninabomoa, ninawabomoa kwa jina laYesu, ninawabomoa, kila adui alioko sehemu yoyote ili kuniangamiza ninambomoa kwa jina la Yesu.

Lazima nifike katika hatima yangu, lazima nifike katika mwisho wangu .Kila majeshi ya giza, kila nguvu za giza ninawatumia moto kwa jina la Yesu , lazima muachie katika jina  la Yesu.

 Ninawasambaratisha kwa jina laYesu kristo nawaboa wote ,nawaangamiza wote,kwa damu ya mwana kondoo.Wote mliofanya vita juu yangu mtakuwa si kitu na mtafadhaika.

Katika jina la Yesu ninaamuru mtoke, ninawaamuru mashetani wote,majini wote, mapepo yote, vibengu wote na majoka, mizimu yote, iliyoko mahali popote pale kakika maisha yangu mtoke katika jina la Yesu.

Ninawafyeka wote waliotumwa kufanya vita juu ya maisha yangu katika jina la Yesu,Wote waliotumwa maalumu kwa ajili ya kushindana na mpango wa Mungu katika maisha yangu, ninawaharibu katika jina la Yesu.

Ninawaamuru vibwengu wote na kila aina ya nguvu za giza ninawaagiza toka katika jina la Yesu kristo ,ninaamuru muachie mpango wa Mungu katika  maisha yangu.

Ninawamuru mashetani wote katika jina la Yesu, achia tumbo la uzazi wangu , nakuamuru wewe ulionishikilia tumbo langu achia katika jina la Yesu, achia moyo wangu, Achia viungo vyote vyangu katika jina la Yesu.

Kwa jina la Yesu pale waliponiweka liwe eneo langu la mauti ninakataa kukaa pale, nakataa kukaa pale, ninakataa kufia katika gereza la aibu, Nakataa katika jina la Yesu.

Nakataa katika jina la Yesu, nakataa gereza la balaa, biashara yangu itarudi tena, ninakataa kufia katika balaa.Nimetambua kuna kitu kizuri Mungu kaniandalia, kuna kitu kizuri Mungu kaniandalia katika siku zijazo.

Vita yangu ni kwa ajili ya hicho kitu, ndoa yangu inarudi tena, maisha yako yanarudi tena, watoto wangu wanarudi tena ,ajira yangu inarudi tena. mimi ni yusuph wa kizazi changu .

mimi ni Raheli wa kizazi changu shida ninayoipitia si bure bali kuna kitu ambacho si cha kawaida  ambacho MUNGU ameniwekea kinakwenda kuzaliwa miaka ijayo.naona afya yangu inarudi tena .naona mambo mazuri ya Bwana yana nifuata mimi katika jina la Yesu.
Asante Baba Mungu, ninakushukuru tena kwa jinsi ambavyo umeharibu kila hila za adui zangu, ninakushukuru kwa jinsi ulivyo mwema, kwa jinsi ulivyoifia dhambi yetu mtini.

Nakushukuru kwa jinsi ulivyomtoa mwanao awe sadaka kwa ajili ya dhambi zetu, tunakupa heshima tunakupa utukufu asante ee Baba kwa maana kwa kupitia maombi yaliopo kwenye kitabu hiki umenifungua.Amen.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!