menuz

utukufu wa MUNGU tuliopewa !!!


Somo:Sisi tuu wamoja -part 2

Walengwa:Watumishi wa MUNGU

Neno:  Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8

Theme:utukufu wa  MUNGU tuliopewa.

Tunajua kuwa ni kweli YESU ametupa ule utukufu aliopewa na BABA MUNGU kwa kusoma “Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja” Yohana 17:22,
Kuwa na Umoja kama wakristo  ni agizo kuu la kufanya ili utukufu  tuliopewa na YESU uweze kuonekana katika maisha yetu kama wakristo.
Tunatakiwa tuwe na umoja katika YESUKRISTO na sio umoja katika udini/dini yetu bali umoja katika YESUKRISTO.
Umoja katika YESUKRISTO unapingana kabisa na udini, Ingawa ndani ya udini kunaweza kuwepo umoja lakini umoja huo sii ule umoja katika YESUKRISTO.
Tusipo kuwa na umoja katika YESUKRISTO kama watumishi wa MUNGU tunafanya utukufu aliotupa MUNGU asidhihirike sana katika maisha yetu.
Kama hauna umoja katika YESUKRISTO utashindwa kumsaidia mkristo mwingine kwa kuwa hajatokea katika kanisa/huduma yako.
 Mahali popote ambapo utukufu wa MUNGU ulishuka haukuacha pakiwa vile vile bali ulileta mabadiliko ama yawe mabadiliko mazuri au mabaya kwa panapo uovu .
Utukufu wa MUNGU unaposhuka tuwapo katika kuabudu au ni sifa basi tunajikuta tunatekwa na kuhama  kuanza kunena kwa lugha na hata kufurahi sana mpaka kulia na kadhalika
Umoja unaozungumziwa hapa ni umoja katika YESUKRISTO,Umoja katika kuifanya kazi ya YESUKRISTO pasipo ubaguzi wa kanisa ,huduma ,au mtumishi gani,au eneo atokalo.
MUNGU anatambua umuhimu wa umoja katika yeye YESU ,ili utukufu aliotupa upate kuonekana.
Sisi tu wa moja.Na kama tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU.Ili utukufu wake MUNGU ung`ae maishani mwetu.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!