menuz

Ulinzi wa jina la YESU juu ya utendaji wa utukufu wake !!



Somo:tuu wamoja katika YESU KRISTO -part 3

Walengwa:Watumishi/Rafiki za MUNGU

Neno:  Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8

Theme:Ulinzi wa jina la YESU juu yautendaji wa utukufu WAKE.

Jina la YESU linatulinda sisi kama wakristo ili tuu tuwe na umoja katika yeye YESU.Imeandikwa“. . . . . . . . . . . . . . . . . Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” Yohana 17:11
Utukufu huo wa MUNGU ambao ametupa sisi kama wanawe hauwezi kuonekana katika maisha yako kama hatuko ndani yake MUNGU.
Kuishi ndani ya MUNGU ni kuishi kama MUNGU atakavyo,anasema utii amri zake zote “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA,
 aliwaamuru, kumpenda BWANA, MUNGU wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.” Yoshua 22:5

Mkristo aliye na umoja hudadisi kwa kujiuliza , “je huyu mtu anamjua YESU ?,ametoka katika kanisa linalo mjua YESU.
Kama ni kauli za mkristo aliye na umoja husema ,Sisi kama watu ambao tuna YESU huwa hatufanyi hivyo!.”
Lakini yule Mkristo asiyekuwa na umoja hudadisi kwa kuuliza , “Je mtu huyu ana mjua mchungaji wetu ?,ametokea kanisa gani ?,
ametokea huduma gani ?. Kama ni kauli za mkristo asiye na umoja husema “Sisi kwenye kanisa letu huwa hatufanyi hivyo.”

Kama tukiwa wamoja kama watumishi wa MUNGU hatutabaguana kwa kusema labda hutachangia hudumaa hii ,nakusema mimi ntakuwa nachangia huduma hii ingine pekee yake.
Tukiwa na umoja hutaweza kusikia mtumishi mmoja anamsema mtumishi mwenzake kwa lolote lile,Kwa kuwa akianguka mtumishi mmoja ni sawa na tumeanguka wote kwa kuwa tu wamoja,hivyo tutakuwa katika hali ya kumsaidia na sii kumsema vibaya au kumuacha apotee na kuzidi kuaibika.
Tunaposhindwa kuwa na umoja kama watumishi wa BWANA tunakosa kuiga ule ukamilifu wa MUNGU.
Sisi tu wa moja.Na kama tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU. Nao ulinzi wa jina la YESU juu ya utendaji wa utukufu wake MUNGU utadhihirika zaidi katika maisha yetu.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!