menuz

Tunategemeana ili utukufu wake MUNGU uonekane maishani mwetu.


Somo:Huduma iliyo katika umoja katika KRISTO YESU -part 4
Walengwa:Watumishi/Rafiki za MUNGU

Neno:  Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8
Theme:Tunategemeana ili  utukufu wake MUNGU uonekane maishani mwetu.

Katika kuitenda kazi ya BWANA tunategemeana kama watumishi, na kila mtumishi wa BWANA amepewa kazi yake na BWANA na atapoimaliza atalipwa kwa hiyo.
Hivyo hakuna  haja ya kuwa na udini badala ya UKRISTO kwa kuwa yeye MUNGU huwa katika umoja katika kuzitenda kazi zake.

Imeandikwa“Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?” 1 Wakorintho 3:4
Utaona hapo Apolo na Paulo hawa wote ni watumishi waliotumiwa  na BWANA lakini tatizo ni kwamba wakristo wanaoongozwa  wameshaweka umoja katika kuutetea udini(u-Apolo na uPaulo)  badala kuutetea u-YESUKRISTO.

“Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama BWANA alivyompa.” 1 Wakorintho 3:5

Kutokuwa na umoja na ushirikiano na huduma zingine  ni kubaya sana na kuna maanisha kwamba unaweza wewe pekee/ninyi pekee yenu bila msaada wa mtu yeyote kutoka kanisa lingine au huduma ingine.

Kitu ambacho sii kweli kabisa ,kwa kuwa ni kweli kabisa tunamtegemea MUNGU kutusaidia yeye pekee lakini mara nyingine hutusaidia  watumishi wake kupitia watumishi wengine.

Unapopata msaada wa kuhudumiwa kama mtumishi wa MUNGU kutoka kwenye kanisa lingine au huduma ingine haimaanishi wao ni wazuri sana kuliko wewe.
Kumbuka YESU alibatizwa na Yohana kutoka hapo kila mtu akaendelea na huduma yake.Yohana alikuwa huduma yake na YESU alikuwa na huduma yake lakini ili mbidi Yohana kumbatiza YESU.

 je ?kama hatutokuwa na shirikiano na umoja tutawezaje kufanikiwa vyema katika kuhudumu vyema.
Imeandikwa“Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni MUNGU.” 1 Wakorintho 3:6
Sisi tuu wamoja.Na kama tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!