menuz

Kwa nini ushindwe vita yako kiroho !!


Mambo yanayofanya kushindwa vita yako

Kuna mambo ambayo yanaweza kuwa chanzo cha kushindwa katika vita unayopitia.Mtu anapo acha kutenda sawa sawa na matakwa ya Mungu, mtu huyo anakuwa anajiendea katika njia ya kushindwa.

i.Kushindwa kungoja kutoka kwa Bwana.

Wokovu wetu katika vita yoyote tuipitiayo inategemea msaada kutoka kwa Bwana. Imeandikwa “Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.” Zaburi 25:3.
Tunaposhindwa kungoja mpaka kukata tamaa hata tusimuulizie tena Mungu kwa habari ya vita yetu, tunapoteza muujiza wetu.
Imeandikwa “Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.”  Marko 12:36

Ni ahadi ya Mungu kusaidia pale tunapopitia vita ,misuko suko au mambo magumu kimaisha.Lakini pia inabidi kuwa na sabira ili kupokea msaada mkuu kutoka kwa Bwana maana hacheleweshi wala hawaishi.

Bwana huonyesha njia sahii ya kuendea njia ya kushinda kipindi mtu anapopitia vita katika maisha yake, kipindi anapopitia matatizo makubwa lakini yaitaji kutokata tamaa kumngoja Bwana kwa maombi bila kuchoka.“Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.” Mithali 8:34

ii.Maungamanisho na ushirika mbovu

Kama mtu anauhusiano mkubwa na watu waovu au makundi mabaya yasio mtii Mungu, Basi mtu huyo anajiwekea nafasi kubwa ya kushindwa. kwa kuwa watu hao wanauwezo mkubwa wa ushawishi katika kutenda uovu kitu ambacho ni kinyume na sheria ya Bwana.

Imeandikwa “Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego” mithali 22: 24-25
Jaribu kujenga urafiki na watu ambao wana hekima ya Mungu, jaribu kuwa karibu kujiunga na kikundi cha kujifunza neno la Mungu kanisani badala ya kuwa na makundi mengi ya watu ambao hawamuamini Mungu kwa kuwa siku ya taabu yako hawata weza kukusaidia chochote.

Mtu anapokuwa akishirikiana na makundi yasiyo muamini Mungu kwa ukaribu sana, mtu hyo anaweza kushawishiwa kuiacha njia ya Bwana na hao watu kiraisi sana.

Imeandikwa “Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; . . . . . . . . . . .kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao” 1 Samweli 15:24.
Sauli alitii sauti ya watu na sio sauti ya Mungu kwa kuwa watu  wengi alio ambatana naye walikuwa hawamtii Mungu hata wakaweza kumshawishi kumuasi Bwana.

Imeandikwa Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”  mithali13:20 .Tunapokuwa na ushirika na wenye hekima nasi tunakuwa na hekima, Bali tunapojiungamanisha na watu wasio mtii Mungu tunajiwekea kushindwa.

iii.Kusahau matendo makuu ya Bwana aliyowahi kukutendea

Kusahau matendo makuu ya Bwana aliyokwisha kutkutendea kunafanya ushindwe katika vita upitiayo.Mtu anapopitia hali ngumu ya shida halafu akasahau mambo ambayo Mungu aliwahi kumtendea zamani ,basi mtu huyo hukusa imani na Mungu na kushindwa.

Wana wa israeli walikuwa wakisahau  matendo makuu ya Mungu katika safari yao kwamba ndiye Mungu  Yeye aliye wawezesha kuvuka bahari ya shamu na akawauwa adui zao.

Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.

 Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufaa” kutoka 14:28-30

 Imeandikwa wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.” Kutoka 16:3

Wana wa israeli walitendewa mambo makuu sana na Mungu katika kutolewa nchi ya utumwa misri, lakini pamoja na ishara zote ambazo Mungu alizokuwa akiwatendea,

wao walisahau makuu yote ambayo Mungu aliwatendea, kipindi tuu wakutanapo na vita na kuanza kumnungunikia musa kwamba ni bora angewaacha misri waendelee kuwa watumwa kuliko kupambana na vita .

Mungu hapendi tusahau jambo lolote alilotutendea maishani mwetu, kwa kuwa tunaposahau inapelekea kutoamini uweza wake Mungu.

Mungu alichukizwa na tabia za wana wa israeli za kusahau matendo aliyowatendea “Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.

Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.” Hesabu 14:11-12 .

Unaweza kujiuliza ni mambo gani mimi Mungu aliyonitendea makuu?, ukaona kama hakuna !!.

Ila ukweli ni mambo mengi makuu sana aliyokutendea Bwana.Kama ukidhani hakuna, kumbuka hata wewe kuwa hai ni jambo kubwa ambalo Mungu amekutendea kwa kuwa wapo ambao hawajaweza kufikia umri wako wakiwa hai, 

Kwa hiyo katika shida yako mkumbuke Mungu kwa hilo na uweke imani kuu kwa kukushindia vita yako ulio nayo sasa.
Kama vita yako ni kupata ada ya wanao, basi kumbuka kuna watu wasio na watoto lakini Mungu amekuwezesha wewe kuwapata hilo ni jambo kuu .Kwa hiyo katika shida yako mkumbuke Mungu kwa hilo na uweke imani kuu kwa kukushindia vita yako uliyo nayo sasa.

Unapopatwa na vita yeyote ,magumu yoyote yale usisahau hata jambo moja ambalo Bwana aliwahi kukutendea kwa kuwa kupitia hilo jambo ndilo itakuwa shuhuda yako ya kukupa nguvu kuona hata vita ambayo unaipitia sasa yeye Mungu anaweza kukuokoa.

upendo wa awali wa Yesu kushindwa kukumbuka Yesu ndiye aliyekushindia mambo ya nyuma na kusahau ijinsi alivyokupigania.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!