Neno:
"Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua."Mathayo 10:16
Ili kuishi kondoo katikati ya mbwa-mwitu inahitajika kuwa na busara na upole ili kufikisha ujumbe ule tuliopewa kuufikishia dunia.
Inamaana kuwa kwa mkristo kupeleka kuishi hapa duniani anahitaji sana kuwa na hekima na busara kwa kuwa toka awali ulimwengu huu hupingana na injili ya YESUKRISTO.
Imeandikwa "Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia"1 Yohana 3:13
Sababu kubwa ya kuchukiwa na watu hasa wa mataifa(watu wasiomfuta MUNGU) kama mkristo ni Kwa kuwa wewe si wa dunia hii .Hauendani nao.
Kama mkristo hautakiwi kushangaa ukiona unachukiwa ,au una bezwa kwa ajili yake YESUKRISTO.Yeye YESU alitendewa hayo huku akiwa humu duniani ,ilithibitika kuwa hana kosa lakini bado aliteswa alionewa.
"Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu." Ufunuo wa Yohana 1:9
Je wewe na mimi tu na nini mpaka tusiichukiwe ?
Imeandikwa "Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu." 2 Timotheo 2:3
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!