menuz

KWA WANADAMU NI SIRI LAKINI SI KWA MUNGU"KUPIGA PUNYETO"


KWA WANADAMU NI SIRI LAKINI SI KWA MUNGU
“KUPIGA PUNYETO / PUCHU / PULI / KUJICHUA“masturbation”.
Kweli yaweza kuwa ni siri kwa wanadamu lakini haiwezi kuwa siri kwa MUNGU kwa kuwa MUNGU anajua mambo yote hata yale yaliyositirika na kufichika.

Kitendo cha kujichua yaani masturbation kina starehe ndogo na kuwa na madhara mengi kuliko kawaida, kujichua kuna madhara ya kimwili na kiroho pia.

Tatizo la kujichua si kwa wanaume tuu bali ni hata kwa wanawake ,na sii kwa wasiooa na kuolewa bali hata kwa walio olewa na walio oa baadhi yao hujikuta wakipendela kujichua pasipo kujua kuwa kuna roho za giza ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuwasababisha waendelee kujichua tuu.

Kuna wakristo wanawake zao lakini bado wanaona bora kujichua kuliko kulala na wake zao,Kuna wanawake ambao wana waume zao kabisa lakini hawaoni raha ya kufanya tendo la ndoa na waume zao kama vile wakijichua wao binafsi.
Wewe haujajiumba bali umeumba na MUNGU kwa ajili ya kumtukuza yeye MUNGU pekee kwa kuwa mwili wako ni hekalu la ROHO mtakatifu “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”- 1 Wakorintho 6:19

Mbaya zaidi ni kwamba shetani anazidi kuboresha utendaji wa dhambi kwa kuwa tengenezea watu mashine za kujichua kwa kuwa anajua kwajinsi wanadamu wanavyozidi kutenda dhambi na ndivyo yeye anaweza kutenda kazi ndani yao.

Kujichua au kupiga puchu kumekuwa kwa staili mbali mbali  mpaka zingine zimekuwa ni za kitaalamu sana zilizoendelezwa  na shetani ili watu wajichue kupitia mashine,midoli yaani setoyz maalumu kwa ajili ya kujichua .Kujichua husababisha matatizo ya kisaikolojia na kuathiri mfumo wa mwili na roho pia!.

Ukweli ni kuwa kujichua ni chukizo mbele za MUNGU. Imeandikwa “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”- Warumi 1 :26-27

Hawezi kufanya punyeto/kujichua/masturbation pasipo kuwa na hisia za kutamani kufanya tendo la ndoa na kwa kuwa na mawazo tuu ya kutamani kufanya ngono ni dhambi mbele za MUNGU kwa kuwa imeandikwa“lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”- Mathayo 5:28

Hivyo si mpango wa MUNGU watu wakae katika maisha ya kujichua ,kupiga puli, kurusha ndege na kuwaka tamaa.

Ni afadhali tena ni heri mtu aoe au aolewe kuliko kuendelea kujichua “Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”- 1 Wakorintho 7:9

Vitu vinavyosababisha kujichua.....
Tamaa ya kufanya,uzinzi, uasherati na tamaa kubwa ya kufanya mapenzi huchangia kujikuta unajaribiwa kufanya masturbation yaani punyeto.Kuna vitu vinachochea kujichua vitu hivyo ni pamoja na:-

i.Kuangalia picha za kawaida zenye hisia kali au hata picha za ngono yaani (PORNOGRAPHY).
Picha zenye unusu uchi za kwenye mitandao au tamthilia zenye kuonyesha matamanio matamanio hupelekea mtu kuwaza kuanza kujichua

ii.Kushawishika kumakinika na mavazi ya uchi na yenye hisia kali kuyatazama.
Mavazi ya ajabu ajabu yenye kuwekaushawishi kutokana na kukaa wazi kwa mwili.

iii.Mapepo na majini
Kuwa makini kwa kuwa kujichua ni moja ya kazi ambazo shetani anapata nafasi kujiingiza katika maisha ya watu kwa kuwa kuna mapepo na majini kwa ajili ya kuwafanya watu wasipende kuolewa wala wasioe ila wapende kujichua tuu.

Watu wengi wana mapepo na majini yanayosimamia kabisa kuwahamasisha kujichua mara kwa mara na hata kuwafanya wasiwe na hamu na wake zao wala wasiwe na hamu na waume zao bali wawe na hamu kubwa tuu ya kujichua.

iv.Upweke ulio na uvivu mkubwa.
Uvivu ni hali mbaya sana kwa kuwa mara nyingi mtu anaokuwa mvivu naye shetani humtafutia kazi au jambo la kipuuzi ili ulijaribu na hapo unapojaribu siku moja nivyo inavyo endelea siku zote kukuathiri katika maisha yako.

Kwanini unatakiwa uache kujichua?/Hasara za kujichua !
Kujichua kunaleta madhara kimwili na kiroho pia yaani kujichua kwa mtu wa jinsia ya aina yeyote ile huleta madhara kattika mwili wake pia na roho yake.

Madhara ya kimwili yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:- 
1.Kusahau sahau kusikokuwa kwa kawaida
Kujichua kukute kule kuna sababisha madhara makubwa kisaikolojia ambayo hupelekea kushindwa kukumbuka vizuri.Sio kana kwamba ni kusahau kwa kawaida bali ni kule kusahau kusikokuwa kwa kawaida.

2.Kunyonyoka au kuishiwa na nywele.
Kufanya sana kujichua kulikokithiri husababisha kutokuuota kwa nywele kichwani na kwapani hasa kwa wadada.

3.Kichwa kuuma na kutapika mara  kwa mara
Mtiririko wa damu huathirika sana pindi mtu anapojichua kwa kuwa mwili wa mtu huyo utahitaji ajifikirishe kama yupo na mwanamke kumbe hana mwanamke.Au yupo na mwanaume kumbe hana mwanaume.

Mwishowe mfumo wa damu huleta kutokusawazika na kuchangia maumivu makali ya kichwa(chronic head-ache)

4.Kuishiwa nguvu za mwili sana
Mtu anayejichua huishiwa na nguvu isivyo kawaida kwa kuwa kabla anakuwa anauwezo mkubwa wa kujichua mara nyingi sana akijisikia raha pasipo kujali nguvu zinazopotea. 

5.Kutokupenda kuwa na ushirika na wengine
Mtu anayejichua huwa mara nyingi hapendi sana kushirikiana na wengine kwa kuwa tendo hilo la kujichua hufanyika sirini pasipo mtu yeyote.

6.Huchangia matatizo ya nguvu za kike na kiume.
Watu wengi hawajui kuwa matatizo mengi ya nguvu za kike/kiume hutokana na kujichua.

Madhara ya kiroho yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:- 
Moja ya tatizo kubwa la kiroho litokanalo na kujichua au kupiga punyeto ni kukosa ukaribu na MUNGU wako unakosa ushirika na MUNGU wako.Ni mbaya kuwa kijana mzuri lakini uzuri wako hauonekani mbele ya MUNGU kwa sababu ya kujichua.

i.Unakuwa najisi.
Imeandikwa “Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni.”- Mambo ya Walawi 15:17.Unapojichua unafanya MUNGU akuone wewe u najisi utaona ni hasara kubwa kiasi gani kwa aliye kuumba akuone kuwa u najisi.

ii.Unashindwa kudumu kutokana na kukosa neema ya MUNGU…
Imeandikwa “Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”- 1 Yohana 2:17.Duniani si makazi yetu bali tu wapitaji kwa kuwaktu akifa atahukumiwa kwa yale aliyoyatenda kipindi alipo kuwa hai duniani.

Kwa hiyo kwa sababu ya dhambi ya kuwaka tamaa ya ngono inayopelekea hadi kufanya punyeto inaweza sababisha wewe kuto enda katika makazi ya mbinguni na kukufanya uende makazi ya motoni milele.
iii.Kujichua ni kunaabudu sanamu pasipo kujijua…
Unapojichua unakua unaabudu sanamu pasipo kujijua,huwezi amini bali neno la MUNGU ndivyo linavyotueleza kuwa kila afanyaye tamaa mbaya ni sawa na anaye abudu sanamu.

Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”- Wakolosai 3:5

Ikwepe hatari hii ya kujiona kana kwamba unamwabudu MUNGU wa kweli na kumbe MUNGU haoni kama unamwabudu yeye bali sanamu, kwa sababu ya kujichua ambako ni sawa na kuabudu sanamu.

JINSI YA KUACHA KUJICHUA NA KUDHIBITI MADHARA YAKE KUACHANA NA VISABABISHI NA KUUTUMIA MUDA NA WENGINE KWA UZURI
Ukiweza kuzuia tamaa ya mwili ujue umeweza kuzuia kufanya kujichua Imeandikwa “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?”- Yakobo 4:1.

BADILI MWENENDO WAKO KWA KUKATAA KUWA HUNA LA KUFANYA.
Amua leo kuacha kabisa kujichua /kupiga punyeto/kupiga puchu/kurusha ndege/ kwa kuwa MUNGU ana mipango mizuri na mikubwa nawe ila kinacho kuchelewesha ni huku kujichua.

Kuna vijana wengi tena ambao hawajaoa au kuolewa na bado wajitahidi na kuweza kuacha kabisa kujichua na wanafurahia uhusiano wao na MUNGU.Nawe unaweza amua leo,amua sasa!

Baadhi ya hatua za kuacha kujichua ni hizi:-
1.Muda uliokuwa ukiutumia kuangalia porno tumia muda huo huo kusikiliza na kuangalia mafundisho ya neno la MUNGU kutoka kwa watumishi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

2.Badala ya kuangalia video za ngono sasa angalia video za mahubiri ya injili

3.Badala ya kusoma magazeti yenye picha za uchi yaani zenye kuleta msisimko sasa anza kusoma BIBILIA kusoma magazeti yenye neno la MUNGU.

4.Acha kufuatilia mitandao ya ngono sasa anza kufuatilia mitandao ya watumishi wa MUNGU soma mafundisho yao na udownload video zao zisikilize.

5.Tumia muda wako ule ule uliokuwa unajichua /kupiga punyeto kuanza kuomba MUNGU.Kama ulikuwa unajichua mara 5 kwa siku ndivyo hivyo hivyo unabidi ubadilike na uanze kuomba MUNGU mara 5 kwa siku.

6.Ulikuwa ujifunza staili mbali mbali za kujichua sasa ziache zote na uanze kujifunza njia mbali mbali za kumjua MUNGU,jifunze namna ya kusoma neno la MUNGU, jifunze namna ya kuomba na kufunga kisahihi, jifunze namna ya kuombea wengine kisahihi.

7.Pendelea kufanya mazoezi ya mwili kama vile kukimbia kila jioni na asubuhi kwa ajili ya kupunguza taratibu madhara yaliyopata mwili kutokana na kujichua/kupiga punyeto.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------     “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”- Wagalatia 5:13
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuacha KUJICHUA/KUPIGA PUNYETO inawekana kabisa badilika sasa utakuwa kijana ,mwanamke/mwanaume bora mwenye kupendeza zaidi  katika afya yako,roho yako hata kwa MUNGU wako.

Usiishi kama wengine wanavyoishi bali ishi kwa kuwa wewe ni wa MUNGU basi unabidi umfuate MUNGU kweli kweli  kwa kuzikimbia tamaa zote za ujanani.

 Imeandikwa “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”- 2 Timotheo 2:22



IELEWE OFISI YA KINABII


#####  IELEWE OFISI YA KINABII                            #####

Huduma ya kinabii ni moja kati ya huduma tano(5) ambazo MUNGU ameziweka katika kanisa lake.Imeandikwa “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, 
wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.”-1 Wakorintho 12:28.


Kuna manabii wengi sana mpaka sasa na huduma zao zimeenea sana duniani kwa mafanikio makubwa sana!.Lakini bado watu wengi hawazielewi huduma hizo, kwa namna moja au nyingine.

Watu wengi hawaelewi manabii gani ni wauongo na manabii wa aina gani ni manabii wa ukweli ?,Watu wengi hawana ufahamu kuhusu huduma za kinabii ?

Hawa ndio manabii wa uongo!.
Neno la MUNGU linaeleza wazi kabisa kuwa kutatokea manabii wa uongo na akafahamisha ni namna gani unaweza kuwatambua!.Imeandikwa “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.”-Mathayo 7:15

Namna ya kuwatambua manabii wa uongo
Imeandikwa “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”-1 Yohana 4:1.


MUNGU anatuambia tusiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwa kuwa kuna weza kuwa na manabii waongo humo humo. Mtu anaweza kupima na kujaribu roho kuwa ni nabii wa ukweli au wa uongo kwa kutumia neno la MUNGU na kwa maombi.


Imeandikwa Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?  Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.”-Mathayo 7:16-18

Wewe ukiona mtu wanamuita watu ni nabii na unataka kumtambua kuwa kama ni nabii wa kweli au wa uongo, wewe angalia matunda yake yaani tabia zake na matokeo ya tabia zake.

Matunda ni tabia, Wote tunajua mtu hawezi kuwa ni Nabii au mtumishi wa MUNGU huku akiwa amejaa tabia mbaya kama vile uongo,uzinzi,rushwa,chuki,kupenda fedha,uuaji,hasira,chuki,majivuno na kadhalika.

Tabia au matunda yanayoendana na Nabii wa kweli ni upendo,furaha,uvumilivu,utuwema,amani na watu wote !.

...............Nabii wa uongo        VS       Nabii wa kweli...................
1.Nabii wa uongo huongozwa na roho wa giza katika kutenda kazi  hivyo manabii hao hawawezi kuona shida kutenda uovu wa aina yeyote kwa kuwa roho za giza ndio furaha yao.      
                                                 Wakati
Nabii wa kweli huongozwa na ROHO wa MUNGU katika kutenda kazi hivyo manabii hao mar azote hujihadhari na kutenda uovu kwa kuwa ROHO wa MUNGU hapendi na hawezi kuendana na uovu.

Imeandikwa Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”- Yohana 10:10
2.Nabii wa uongo anatabiri vyovyote na inaweza itokee au isitokee !.
                                                    Wakati
Kila anachotabiri Nabii wa kweli ni lazima kitokee kwa kuwa huonyeshwa na MUNGU mwenyewe na MUNGU hawezi kukosea kwa kuwa anajua mwisho kabla ya mwanzo.

Imeandikwa “Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope”-Kumbukumbu la Torati 18:22

3.Furaha kubwa ya Nabii wa uongo ni kupata watu wengi ili apate umaarufu na fedha nyingi zaidi kwa njia ya sadaka bila kujali watu hao wanampendeza MUNGU au la!.

                                                                          Wakati
Furaha kubwa ya Nabii wa ukweli ni kupata watu wengi ambao atawafundisha kuzishika amri za YESU na kuona wanaishi katika mapenzi ya MUNGU maisha yao yote hata kama hapati kiasi chochote cha fedha.

4. Nabii wa uongo hujali sana wale wenye fedha na mali ,pia kutojali sana watu wasio na fedha wenye shida yaani wajane,yatima nk
                                                                         Wakati
Nabii wa ukweli hujali wote na hutumia nguvu zake,fedha zake kwa hali yeyote kuwasaidia wenye shida ,wajane,yatima na wanyonge.

5.Nabii wa uongo hutumia ishara,miujiza na maajabu ya uongo kuwavuta watu wengi kwake na sio kwa YESU.
                                                                          Wakati
Nabii wa kweli hutumia ishara,miujiza ya kweli kuwavuta watu wengi kwa YESU.

            Ofisi ya kinabii na silaha zake !.......

Silaha kubwa katika ofisi ya kinabii ni MANENO.Kuna neno la kinabii kupitia mafunuo na Neno la MUNGU kupitia bibilia.Watu wengi hawaifahamu utendaji wa kinabii na huduma hiyo kiujumla hasa kutokana na uendeshwaji wake hutegemea mafunuo kutoka kwa MUNGU sio wanadamu!.

Nabii ni mtu ambaye anakuwa na karama ya unabii yaani utabiri.Imeandikwa Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.”- 1 Wakorintho 12:4

Nabii anakuwa na ROHO yule yule mtakatifu lakini  ROHO huyo huachilia karama ya unabii na utabiri ndani yake.Watu wengi ambao leo tunawaita manabii hawakujijua kipindi wanakuwa kama 
wao watakuwa manabii.

Watu hao huanza kuota ndoto zenye kutokea ,kuona maono wazi wazi mchana kabisa na kwa kuonyeshwa huko husema  kile wanachokiona na kubadilisha maisha ya watu kwa kuwageuza ili wamfuate YESU.

Kazi ya kinabii muda mwingine inakuwa ni kazi yenye mzigo mzito kwa upande mwingine kwa kuwa inahitaji nabii awe muombaji sana kwa kuwa ROHO mtakatifu hujifunua kwa mafunuo na maono kwa nabii baada ya kuomba sana.

Hivyo nabii wa kweli na mwenye kuipenda kazi hiyo anatakiwa awe ni mtu wa maombi sana kwa kuwa atavyoomba sana ndivyo MUNGU humuonyesha mambo mengi sana kwa ajili ya watu wake!.

Nyanja tatu(3) ambazo nabii anaweza kuzigusa pindi atumiwapo na MUNGU.


i.Unabii wa undani (Insight prophecy)
Mungu anaweza kumtumia nabii na kumuonyesha chanzo cha shida yako na Nabii  akakwambia hata kama hakuwa anaishi siku hizo ulizopata hayo matatizo.

Mfano katika biblia MUSA alikuwa nabii wa BWANA na ndiye aliyeandika kitabu cha mwanzo ambacho ni unabii  wa undani kwani aliandika habari za mwazo kuwa MUNGU aliziumba mbingu huku kiukweli yeye hakuwepo kipindi hicho.

Lakini MUNGU alimjulisha nabii MUSA kuhusu mwanzo utadhani naye alikuwepo siku hizo na hivyo ndivyo MUNGU huwatumia mnabii katika unabii wa undani.

ii.Unabii wa mbele(Foresight prophecy)
Unabii unaoongelea mambo ya mbele yaani utabiri wa siku zijazo kuhusiana na chochote.Mfano katika bibilia ni kwamba MUNGU ameshamuonyesha Manabii DANIEL,ISAYA,EZEKIEL kuhusu siku za mwisho wa dunia utakuwaje
”-
Hivyo ndivyo MUNGU anavyoweza kumtumia Nabii kwa 

kumuonyesha vitu vitakavyotokea siku za mbele yetu!.

iii.Unabii wa kuzidi siri(Oversight prophecy)
Imeandikwa “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake”-. Amosi 3:7

MUNGU anaweza kumtumia nabii kwa kumuonesha siri zake juu ya yajayo au hata juu ya mambo ya waumini wake !.

Makosa makuu manne(4) yanayofanyika katika huduma nyingi za kinabii  .
Kweli kuna manabii wa ukweli wengi sana lakini mara nyingi kumekuwa na mapungufu makubwa katika huduma hizo na yanakomaa sana ingawa makosa hayo yalianza kidogo kidogo.

Baadhi ya makosa hayo katika huduma hizo za kinabii ni yafuatayo:-

1.Kuwa na mafundisho haba ya NENO la MUNGU hasa kwa wale walio wachanga kiroho.
Imeandikwa“…… naye Neno alikuwa Mungu”-Yohana 1:1.Neno la MUNGU ni MUNGU mwenyewe pia ni sauti ya MUNGU kwa watoto wake.

Huduma nyingi zinazo anza za kinabii zimekuwa na mafundisho haba ya NENO la MUNGU kwa sababu ya unabii, ishara na miujiza hivyo kufanya watu wengi ambao ni wachanga kiroho kudumaa na kubaki kumtegemea nabii kwa kila jambo hata kwa yale ambayo wao wenyewe wangeweza kuyafanya.

Neno ndiye MUNGU mwenyewe kwa hiyo kama halisisitizwi kukaa ndani ya watu.Hao watu watakuwa watu wakupenda miujiza na ishara na unabii lakini hawamjui MUNGU na ndiyo maana baadhi yao wakipatwa na jaribu kidogo tuu huanguka kabisa.

Utawala wa kanisa ukiwa mzuri utaunda mashemasi ,wachungaji wasaidizi na wengineo kwa ajili ya kufundisha hawa watu ambao ni wapya katika wokovu.

Mfano unakuta mtu alikuwa muislam na baada ya kutabiriwa na nabii na kufunguliwa kutoka kwenye matatizo yanayomkabili basi naye akaamua aokoke lakini baada ya kuokoka anatakiwa apatiwe mtu ambaye atamfundisha masomo ya awali ili azidi kukulia wokovu, kitu ambacho hakitendeki katika huduma nyingi za kinabii zinazo anza.
Imeandikwa “Nikwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”- Waefeso 4:12

Mungu aliweka huduma hizi kwa ajili ya kujenga watoto wake hata wao pia waweze kujitegemea na kukua kiroho huku wakimjua MUNGU lakini watamjua vipi kama hawasisitiziwi kulishika neno la MUNGU.
2.Kutegemeza waumini kwa Nabii badala ya YESUKRISTO.
Kosa  kubwa ambalo huduma nyingi zinazo anza za kinabii hutendeka ni hili la kuwategemeza waumini kwa Nabii kana kwamba yeye ndiye anayetenda badala ya YESUKRISTO.

Badala ya kutumia miujiza kama chambo cha kuvuta watu ili kuwafundisha kweli ya YESU.Kumekuwa na makosa kuwa huduma nyingi za kinabii kuwa sehemu ya kushangaa miujiza sana badala ya kumjua YESU kiasi kwamba kama miujiza haipo basi watu nao hawakai tena kanisani.

3.Kutojali kujengea waumini misingi mizuri ya kukua kiroho kwa kuijua kweli.
Waumini wamefundishwa kama jambo baya likiwapata basi moja kwa moja wampigie simu Nabii nasio Waombe kwa YESU msaada.

Waumini wameshawekewa msingi kuwa majibu yao yote yamatatizo yao watayapata kutoka kwa Nabii na sio kwa YESU kupitia nabii.

Kosa ambalo hufanya waumini kuwa wategemezi na kudumaa katika uchanga wa kiroho maisha yao yote.Kwa kuwa hawajawahi jengewa misingi imara ya kiroho misingi ya kufunga ,kuomba na kusoma neno la MUNGU.

4.Kuiba utukufu wa MUNGU na kujivuna kwa sababu ya upako.
Kutokana na miujiza na ishara zinazo onekana na kutendwa na nguvu ya YESU kupitia manabii zake basi baadhi ya hao manabii hujikuta wakijaribiwa kujivuna na kuiba utukufu wa MUNGU.

Imekuwa kama kawaida kwa kosa hili kwa baadhi ya manabii ambao huiba utukufu wa MUNGU kwa kujitukuza .Manabii hutumiwa na MUNGU kufanya ishara hizo nao hujaribiwa kujiweka katika nafasi ya kuutengeneza miujiza hio.

Mfano:Mtu alikuwa anaumwa na haoni na MUNGU anamtumia nabii wake kumponya huyo mtu Basi Nabii hujikuta akisema “alikuja akiwa anaumwa macho nami nimemponya” kitu ambacho ni kosa kubwa kuwa alitakiwa kusema “MUNGU amenitumia kumponya mtu huyu”.

Umuhimu wa nabii katika maisha yako.
Kuna baadhi ya watu hawajui umuhimu wa manabii lakini kiukweli nabii ni mtu muhimu sana kwa kuwa ndiye sauti ya MUNGU kwa watu wake.
Baadhi ya vitu vitavyokuonyesha umuhimu wa manabii navyo ni  baadhi yake ni:-

ü  MUNGU hujenga na kuunganisha familia zilizo tengana kwa kumtumia NABII

ü  MUNGU huwatumia manabii kuwatia moyo mitume katika kujenga kanisa Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli.”- Ezra 5:1


ü  MUNGU hutumia manabii kuwaweka madarakani watawala ambao MUNGU amewapenda waongoze. Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana.”- 1 Samweli 15:1

ü  MUNGU hutumia manabii zake kuonya watu na matukio yajayo.27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. 28


   Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.”-Matendo ya Mitume 11:27-28