menuz

UNYAKUO-UJIO WAKE YESUKRISTO

Watu wengi wanajua ishara ambazo YESU alizitabiri zitazo onyesha ukaribu wa kuja kwake lakini hawajui ni kwa namna gani atakuja duniani jambo lilopelekea MUNGU kuniruhusu kuandika na kufundisha ni kwa namna gani YESU atakuja kuchukua watu wanaotenda mapenzi yake !.


ANGALIZO:
 YESU haji kuchukua kila mtu aliopo kanisani bali atakuja kumchukua kila mtu anayetenda mapenzi yake.

YESU anaheshimu na kuja kumchukua mtu anayeTENDEA kazi neno lake.

Wanaolisikia neno la MUNGU ni wengi,wanaolijua neno la MUNGU ni wengi lakini WANAOLITENDA neno la MUNGU ni wachache.

Saa na muda wakuokoka ni sasa na sio hapo atakapokuja YESU au utapokufa,Muda wenye neema ya wewe kuweza kuokolewa ni sasa ,anza kumkiri YESU kuwa BWANA na mokozi wako kwa sala hii fupi naye atakuokoa saa hii .
MPOKEE YESU LEO  naye ataokoa maisha yako kwa kuomba sala hii fupi ya toba sasa !.
   Omba kwa imani sema  “BABA MUNGU wewe uliyeniumba mimi na vyote vya ulimwengu huu, ninakushukuru kwa neema yako ya kunikomboa siku hii ya leo kupitia mtandao huu. Ninakuomba katika jina la YESU unirehemu na unitakase dhambi zangu zote nilizo zifanya kwakujua ama kutojua iwe ni kwa kuwaza, kunena au kutenda .
Leo ninaamua kukufuata wewe YESU KRISTO,leo nimeamua kujikabidhi kwako ili niishi kwa kadirii ya maagizo yako na sio kwa maagizo yangu,niishi kwa kadri Wewe upendezwavyo na sio kwa jinsi nitakavyo mimi.Unisaidie nienende katika mwenendo ukupendezao wewe BWANA MUNGU na unijalie neema ya kuutunza wokovu huu ulionipa mpaka mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Asante YESU kwa kunipa zaidi ya niliyoyaomba.”.
Sasa umeokolewa KAMA UMESALI SALA HIYO ,unachotakiwa kufanya ni kuishi sawa sawa na YESU anavyopenda na kwa kujua mengi basi ungana na kanisa lililo hai nawe utakulia huko na kujifunza mambo makubwa zaidi jinsi ya kuwa mwaminifu hata kufa nawe ili upokee taji ya uzima wa milele.
Hapo uliposali sala hiyo hapo juu umeokolewa na moto wa milele na pia umeokolewa na kuonewa na shetani kwa kuwa msaada wa MUNGU uu karibu sana nawe kuliko mwanzo.

“ENDTIME”-TUPO KATIKA SIKU ZA MWISHO; KARIBU SANA YESU  ANAKUJA.
Ni kweli hizi ni siku za mwisho sana kwa kuwa mapema na hivi punde tuu YESU atanakuja kulichukua kanisa lake yaani watu wanaotenda mapenzi yake.

Imeandikwa “.. ………..; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”- Mathayo 24:42.
Ni kweli hakuna ajuaye siku wala saa ya kuja kwake lakini YESU alitoa ishara zake tutakazo ziona kama maandalizi ya kuja kwake YESU duniani.Tunasema yesu yu karibu kwa kuwa kila ishara aliyoisema kutokea kipindi  cha kuja kwake zi mesha tokea.

1.TAIFA MOJA KUPIGANA NA TAIFA /UFALME KUPIGANA NA UFALME.
Kweli kumeshakuwa na vita mbali mbali kwa taifa moja kwenda kupigana na taifa jingine hii ni ishara ambayo BWANA YESU ametupa ili tukiiona imetokea hiyo tujue kwamba ndiyo anakuja kwa kuwa katika wakati ni kama uchungu wa mwanamke anapotaka kujifungua.
 Imeandikwa“Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; . . . . . . . . . . Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8
Kweli nchi nyingi zimekuwa katika vita na wewe kama mkristo ulisha jihoji na kuona unabidi uwe macho kiasi gani kwa kuwa YESU yu karibu kuja?.

2.KUTAKUWA NA NJAA.

YESU alisema dalili ya yeye yu karibu kuja kulichukua kanisa nayo ni kuwa na njaa kali.
 Hii ni ishara ambayo inaonekana mahali mbali mbali ,nchi nyingi zimekuwa na njaa kali kitu ambacho si kawaida. Imeandikwa “. . . . . . . . . .  . . . kutakuwa na njaa,…………Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8


3.KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI MAHALI MBALI MBALI.
Imeandikwa “………………..na matetemeko ya nchi mahali mahali.Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8.
Matetemeko ambayo si ya kawaida kama vile tsunami na mengineyo yanaashiria YESU yu karibu kurudi kuja kuchukua watu wanaotenda mapenzi yake.

4.MANABII WENGI WA UONGO WATATOKEA.
Kumekuwako na manabii wengi wa uongo duniani ambao wamekuwa wakimpinga YESU na wengine wakijiita wao ni YEHOVA,YESU wote manabii hao wa uongo wamekuwa wakidanganya wengi lakini haya yote ni udhihirisho kuwa YESU anakuja mapema sana.
Imeandikwa “Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.”- Mathayo 24:11

5.UPENDO WA WENGI KUPOA NA MAASI KUONGEZEKA.
Kwa kipindi hiki imekuwa kawaida kusikia vikundi mbali mbali vya kigaidi tena vikijisifu kwa kuua,kulawiti,kubaka kufanya kila aina ya ubaya na uharibifu.
Hata baada ya kufanya mabaya hayo yote badala ya kujutia wao hujisifia na kujinadi kuwa wametenda hayo.

Imeandikwa “Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.”- Mathayo 24:12
Mambo hayo yanadhihirisha ujio wake YESU upo karibu sana kwa kuwa alishasema kuwa upendo wa wengi utapoa na maasi yataongezeka hii ndio ishara ya ujio wake.

Kama kweli hauhitaji hukumu ya moto wa milele ndugu ni bora ung`ang`ane na YESU kwa kuwa si muda mrefu YESU anakuja kuhukumu na ndio huo utakapo onekana mwisho wa dunia hii.

Je siku hizo watu duniani watakuaje !?
Waweza kujiuliza siku hizo ambazo YSU anakuja watu duniani watakuwa wanafanya nini,au watashindwa kufnya kazi zao au ?,kutakuwa na nini? .Lakini  Watu duniani watakuwa kama vile:-

1.Kama ilivyokuwa siku za nuhu ndivyo itavyokuwa siku hizo za kuja kwake YESUKRISTO.
YESU atakapokuwa anakuja watu watakuwa wakila ,wakinywa ,wa kuoa  watakuwa wakioa,wa kuolewa watakuwa wakiolewa kama kawaida,

Imeandikwa “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.
 27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.”- Luka 17:26-27

2.Kama ilivyokuwa siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa siku atakayokuja YESUKRISTO.
Siku ya kuja kwake YESU itakuwa kama siku za Nuhu yaani watu wakila,wakinywa.
Imeandikwa “28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
 29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
 30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.”- Luka 17:28-30

Kwa maana ingine ni kwamba siku ambayo YESU “Mwana wa Adamu” atakapo kuja itakuwa siku kama zingine hakutakuwa kuna chochote cha kushtua sana zaidi kwa wanadamu kiasi cha kufanya kuigundua siku hiyo kwa namna yeyote ile KABLA YA UNYAKUO.

Je YESU atakuja duniani tena kwa namna gani ?- “UNYAKUO”
Je unadhani YESUKRISTO atakuja je duniani ?,Je unadhani dunia hii itakwisha vipi?.Ni kweli hakuna ajuaye saa wala muda wa kuja kwake YESU lakini Je unadhani atakuja vipi kuwachukua watu wanaotenda mapenzi yake ?.

YESU atakuja kwa namna ya unyakuo,yaani kunyakua watu waliompendeza siku zote na kuishi katika kutenda mapenzi yake.
Imeandikwa16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.”- 1 Wathesalonike 4:16

Waliokufa katika wokovu wa YESUKRISTO watafufuliwa kwanza na kupewa nguvu mpya kumlaki YESU mawinguni kwa muda wa haraka sana.

 “17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”-1 Wathesalonike 4:16-17
Ndipo YESU atanyakuwa wale ambao walio hai na waliodumu katika kutenda matendo yanayompendeza yeye YESU.

Imeandikwa“Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,”- 1 Wakorintho 15:51.YESU atawabadilisha na kuwapa watu wake nguvu ndani yao watu wale ambao wanatenda mapenzi yake siku hiyo ya mwisho nao watanyakuliwa na hilo tendo linaitwa unyakuo.

Watakatifu walioko duniani watanyakuliwa na BWANA YESU na kukutana naye mawinguni katika muda wa kufumba na kufumbua.

Imeandikwa 19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
 20 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.”- Isaya 26:19-20

Hakuna atayeweza kushuhudia tukio hilo la unyakuo kwa kuwa litachukua muda mdogo sana yaani kufumbua na kufumba macho.

Imeandikwa“kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”- 1 Wakorintho 15:52

Hakuna mtu atayeweza kuona hali jinsi tukio hilo litavyotokea kwa kuwa litatokea kwa ghafla sana na kwa haraka.
Imeandikwa “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”-Mathayo 24:27


ISHARA AMBAYO WATU WOTE WALIO BAKIA  DUNIANI  WATAIONA IKITOKEA
Hakuna mtu ataweza kushuhudia unyakuo huo kwa makini kwa kuwa utafanyika kwa haraka sana lakini kuna ishara ambayo watu waliobakia katika hii dunia wataiona nayo kwa baadhi yao itawafanya wajue kuwa YESU ameshakwisha jitwalia watu wake.Nazo ni:-
1.Watu wengi watakuwa hawapo duniani
Duniani kote kutatangazwa kuwa na upotevu wa watu kwa kuwa watu wengi watakuwa wamenyakuliwa hivyo dunia nzima itakuwa imeshindwa kuelewa ni nini kimetokea mpaka watu mbali mbali hawapo.
Imeandikwa“ Luka 17:34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
 35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
 36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.” -Luka 17:34-36

Ndugu ukiona au ukisikia idadi kubwa ya watu wamepotea potea ndani ya siku moja dunia nzima wewe ujue YESU ameshachukua watu wake na wewe umebaki……. …..cha kufanya utatakiwa usome makala inayoitwa BAADA YA UNYAKUO…………nawe utajua cha kufanya..c

Idadi kubwa ya watu watapatwa na mshtuko kutokana na kutokuwaona ndugu au jamaa zao wakaribu kwa ghafla.
Imeandikwa “40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
 41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. ”- Mathayo 24:40-41

Wanawake wanyonyeshao na wajawazito wote watajikuta hawana watoto wao kwa kuwa YESU atakuwa amesha wanyakua.
Hapo ndipo kutapo kuwa na kuchanga nyikiwa kwa wanawake wengi ambao ni wenye ujauzito au watoto wadogo kwa kuwa wengi wao hawatajua ni nani aliyewaiba au ni kitu gani kimetokea.!


DUNIA ITAKUWA KATIKA MISUKOSUKO MI KUBWA KWA MUDA KIDOGO KUTOKANA NA WATU KUONA UPOTEVU MKUBWA WA WATU!.
-----------------------------------------------------je nini baada ya kunyakuliwa kwa wateule wa MUNGU kitatokea ………..fuatilia blog hii kwa makala ingine.--------------------------------------------------------------

Lakini katika kipindi ambacho YESU hajaja bado yeye anatuonya tena sana kuwa tuwe macho yaani tusikate tama kutenda yale mema na kudumu katika utakatifu aliotuagiza kwa  kuwa kwa utakatifu huo tutafanikiwa kwenda mbinguni.
Imeandikwa “Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”- Mathayo 24:42.

Usimuache YESU wala usikate tama kwa kuwa yu karibu sana kujia watu wake. Imeandikwa “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”- Luka 21:36
Soma post inayoelezea BAADA YA UNYAKUO ujue mambo yatakayotokea baada ya unyakuo.

2 comments:

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!