Mbaya zaidi mafundisho hayo hayatupeleki mbinguni bali
motoni kwa faraja isiyo na msingi.
Imeandikwa “Msifanye sanamu yo yote, wala
msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala
mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia;
kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”- Mambo ya Walawi 26:1
Kuona
watu wengi wanafanya jambo fulani haimaanishi jambo hilo ndiyo sahihi.
Imeandikwa “ Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni
mpana, na njia
ni pana iendayo
upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.”- Mathayo 7:13
Kwanza kumbuka watu wengi ndio wataoenda motoni katika siku
ya hukumu ya MUNGU na ni wachache ambao wataokolewa na YESU.Imeandikwa “Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao
ni wachache.”- Mathayo 7:14.
Hivyo basi kaa macho na ujiokoe nafsi yako kwa kuwa
wingi wa watu kuamini kitu flani haumaanishi kitu hicho ndiyo sahihi.
Mafundisho ya uongo
yalikuwepo tokea YESU alipokuwepo ,YESU aliwatahadharisha wanafunzi wake juu ya
mafundisho hayo mabaya na ya uongo. Imeandikwa “11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa
sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na
Masadukayo.
12
Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.”- Mathayo 16:11-12
Kuna makanisa mengi na
huduma nyingi ambazo zina mafundisho potovu juu ya MUNGU nayo mengineyo ni mafundisho
ya kuabudu sanamu.Ndugu MUNGU ameniruhusu leo nikwambie ibada za kuabudu sanamu
haziokoi na MUNGU hapendezwi nazo.
MAMBO AMBAYO WATU HUAMINI NI
SAHIHI NA KUMBE NI POTOFU NA NI UONGO.
Inauma sana ukija
kugundua kuwa ulitumia muda wako duniani ukiabudu katika dini yako, kutenda
matendo mazuri na kutoa kila aina ya sadaka nzuri kwa kudhani unatengeneza maisha yako baada ya
KUFA kumbe kutokana na kuabudu kwako sanamu na kushika kwako mafundisho ya
uongo, MUNGU hakusikii na wala hatakuokoa na moto wa milele !.
1.Kuomba sala kupitia mtakatifu fulani ili akuombee kwa MUNGU.
Tumepewa jina lenye nguvu kuliko majina yote nalo ni YESUKRISTO hivyo unapo omba kupitia mtakatifu fulani ni ibada
za sanamu.
i.Mtakatifu huyo alipewa utakatifu na wanadamu na sio na MUNGU kwa kuwa
wanadamu wanaweza ona mtu huyo ni mta katifu nab ado MUNGU asimuone ya kuwa ni
mtakatifu.
ii.Mtakatifu huyo ni binaadamu na
siyo MUNGU hivyo hana uwezo wala mamlaka ya kukuombea toba.
iii.MUNGU anapenda tumuombe yeye mwenyewe
kupitia jina la YESU pekee.Imeandikwa “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu
iwe timilifu. Yohana 16:24”
Hivyo kuomba sala kupitia
mtakatifu fulani si sahihi na ni matendo ya kuabudu sanamu(iwe mtakatifu huyo
amekufa au yuko hai).
2.Kuomba sala kwa bikira mariamu kama mama wa MUNGU
Mariamu alitumiwa kama
kipitisho tuu na sio mama wa YESU.Baadhi ya
makanisa humuita Mariamu mama wa MUNGU,Huo ni uongo ambao MUNGU huchukizwa nao,
Kwa kuwa YESU alikuwepo hata kabla ya kuwepo kwa dunia.
Imeandikwa
“Yesu
akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.”- Yohana 8:58
Mungu hawezi kuwa na
mama,kwa hiyo haya yote ni uongo ambao umepandwa kwenye dini na tumezaliwa na
kupokea kama ilivyo pasipo kujua mambo hayo ni machukizo sana kwa MUNGU kwa
kuwa utukufu wake unaibiwa na kupewa Mariam.
Mfano:Ni sawa na mchungaji aombee mtu mwenye
ugonjwa na ugonjwa huo ukaondoka halafu mtu huyo akasema yeye ni mponyaji,bila
kusema yeye ametumika tu lakini aliyeponya ni MUNGU.
Hivyo mariamu
alitumika tuu kumzaa YESU kwa kuwa hakumjua mwanaume yeyote kabla hajamzaa
YESU.Hivyo MUNGU atakuja kuhukumu wote ambao wanadhani mariamu ni mama wa
MUNGU.
3.Kuamini kuwa kuna dhambi ndogo ndogo na kubwa.
Kuna uongo mwingi sana kwenye
baadhi ya huduma na makanisa unao wafanya watu waamini wanaweza kufa kama wakiwa
wenye dhambi ndogo ndogo basi
watu wakimuombea anakwenda mbinguni huo ni uongo na kujidanganya tuu wenyewe.
Imeandikwa “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara
moja, na baada ya kufa hukumu;
“-Waebrania 9:27
Kwa kuwa baada ya kufa ni hukumu,
nafasi ya kutubu ni sasa unapokuwa lakini ukifa tuu basi nafasi ya kutubu huna
bali kuna hukumu tuu.
Ukweli ni huu kuwa kwa MUNGU hakuna dhambi ndogo wala kubwa
bali dhambi zote ni sawa na ukivunja amri moja ya MUNGU ni sawa na umevunja
zote.
Hivyo mafundisho yasemayo
kuna dhambi kubwa au ndogo hayo ni ya uongo na kwa hayo ni ibada za sanamu
ambazo hazimpendezi MUNGU.
4.Mahubiri yasemayo hakuna hukumu kuzimu wala moto wa milele.
Kuna mafundisho ya uongo
mwingi ambayo yanadai tuu hakuna hukumu ya moto wa milele kwa kuwa eti MUNGU ni
MUNGU wa rehema tuu.
Ndugu mafundisho hayo ni ya
uongo kwa kuwa MUNGU kweli ni wa rehema lakini pia ni MUNGU wa haki naye
hajipingi.
Imeandikwa “bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala
wao wapingao”- Waebrania
10:27
5.Mafundisho ya kumjua MUNGU pasipo kumjua YESU.
YESU ndiye mpatanishi kati
ya wanadamu na MUNGU hivyo hakuna namna ya kumjua MUNGU pasipo kumjua YESU.
Imeandikwa “Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.”- Yohana
14:6
Hivyo
hakuna jinsi ya kumfikia MUNGU pasipo YESU ambaye ni mpatanishi kati yetu na
MUNGU.
Kwa hiyo kuamini kuwa kuna
MUNGU na kutoamini habari za YESU ni matendo ya usanamu.
6.Mafundisho ya kutoku mtambua Roho mtakatifu.
Mafundisho ya uongo ambayo
hayakubaliani kuwa YESU kweli alituachia msaidizi ambaye ni Roho mtakatifu
ambaye ni Roho wa MUNGU mwenye awezaye kutusaidia.
Ni mafundisho ya uongo ya
kutoamini nguvu ya ROHO mtakatifu aliyoiacha KRISTO ndani ya kila amwaminiye
YESU.
7.Mafundisho ya mpinga KRISTO-{mohamed}
Kuna mafundisho ya uongo na
potofu ambayo yamejaza watu katika misikiti na masinagogi yanayompinga YESU.
Imeandikwa “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani,
wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.” -2 Yohana
1:7.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------Tubu
sasa kwa MUNGU na uachane na mafundisho ya uongo ambayo hayakusaidii kwa kuwa
siku ya mwisho ya hukumu hayatakuokoa.Jitenge na huduma , makanisa yenye kuhusisha
kuabudu sanamu kwa namna yeyote ile.
Kama ukifa ukiwa bado ukiishi katika mafundisho
hayo ya uongo unaenda MOJA KWA MOJA sehemu mbaya iitwayo KUZIMU, sehemu
iliyojaa mateso ya kila aina na huku ukingojea hukumu ya MUNGU.- HAPO HAPANA NAFASI YA KUTUBU TENA.
Kama kweli ndugu unataka kuishi maisha salama yaani
sasa na hata baada ya kufa kwako unabidi umfuate YESU na kuishi jinsi yeye
anavyopenda na sio dini inavyo sema bali yeye YESU.
MUNGU anakupenda na hapendi uangamizwe kwa moto wa
milele katika hukumu yake kwa kuwa moto huo ameandaliwa kwa ajili ya shetani na
wajumbe wake, lakini mpango wa kukuokoa na moto huo ni kupitia YESUKRISTO
pekee.
Naye YESU hachangamani na ibada za sanamu.Njia pekee ni
kujitenga na michanganyiko ya huduma zenye misanamu na kujiunga na huduma zenye
kuhubiri kweli ya YESU naye HATAKUACHA KAMWE ATAKUOKOA.
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!