Ubatizo ni nini ?.
Ubatizo ni tendo la
imani la kuunganishwa na YESUKRISTO katika kifo chake kwa ishara ya
kutumbukizwa kwenye maji na kuibuka.
Unapobatizwa jua kuwa utu wa mwanzo/wa dhambi(wa kale) unazikwa
pale unapozama kwenye maji na unapotoka kwenye maji unakuwa unafufuka na utu
mpya(utu wa YESUKRISTO).
Utu wa kale-
ni misingi ya mababu ya kuabudu mizimu,majinamizi,mizuka
na miungu ya ajabu ajabu n.k.
Utu mpya-
ni misingi mizuri ya
kumpenda YESU na kuwa na agano sahihi naye YESUKRISTO.
TUNAPOENDA KUBATIZWA TUNATAKIWA TUENENDE KWA IMANI MIOYONI MWETU.
Ubatizo ni tendo na
hatuokolewi kwa matendo bali kwa imani. Imeandikwa “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.”- Yakobo 2:17.
Tunapoendea kubatizwa tunatakiwa tufanye je kisahihi ?,Tunatakiwa tuende tukiamini mioyoni mwetu kuwa
tunapobatizwa tunakuwa tunamkiri YESU hadharani kuwa tumeamua kuungana naye milele.
Pia tunapobatizwa
tunatakiwa tuenende huku tukiamini
kuwa kwa kubatizwa tunakuwa tumeshiriki naye kwa kufa naye YESU na tunapotoka
ndani ya maji tunafufuka naye kutoka katika wafu kwa ushindi wa msaada wa ROHO
wake mtakatifu.
Imeandikwa
“Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na
katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua
katika wafu.”-Wakolosai 2:12
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!