menuz

MAONO ALIYO ONYESHA NA YESU MWENYEWE

Ni maelezo mafupi ya ushuhuda wa dada mmoja aitwaye BERNARDA alipata nafasi ya kuonana na  YESU uso kwa uso naye  YESU alimuonyesha vitu vingi ikiwepo na jinsi dunia itavyoisasha.

WAWEZA KUUSOMA USHUHUDA WOTE HAPO http://www.freecdtracts.com/testimony/bernarda_fernandez.htmlKWA LUGHA YA KIINGEREZA..

Ndipo nikaona malaika saba(7) wakiwa wamebeba  bakuli za dhahabu kila mmoja,Pia nikaona malaika wengine saba(7) wakiwa na tarumbeta kila mmoja.Nikamuuliza YESU hawa ni malaika wa nini?,
BWANA akanijibu ”hawa malaika saba(7) ambao kila mmoja ana bakuli,Hizo bakuli zimejazwa hasira ya MUNGU,si muda mrefu watamwaga duniani tarumbeta itapolia.

YESU akaniambia wale ambao ni watu wangu(kanisa) yaani wale wanaoishi kwa kutii amri zake MUNGU watakuwa wamekwisha kunyakuliwa.Hawatakuwepo duniani katika kipindi cha dhiki kuu(great tribulation).

Kabla ya (mtu wa uovu)mpinga kristo mwenyewe kudhihirisha wazi wazi duniani kanisa langu litakuwa limeshatwaliwa kwa kuwa wale ambao wanaishi kweli kwa kutii amri zangu watakuwa wamesikia tarumbeta na watapata nguvu ya kunyakuliwa na kujikuta wamekutana name angani kuelekea Makazi mapya.
1thessalonians 4:16

"Nilikuwa na BWANA YESU akanionyesha jinsi unyakuo wa watu wake utavyokuwa nikaona maono”maelf kwa maelfu ya watu kutoka pembe nne za dunia wakinyakuliwa kwa muda mdogo sana,Nikaona magazeti na tv na redio zikitoa habari ya dharura yaani breaking news kuwa kuna maelfu ya watu sehemu mbali mbali wamepotea .YESU akaniambia kuwa hili jambo litatokea mapema tuu .

Ndipo ghafla nikaona mtu wa uovu ambaye ndio mpinga KRISTO akajitokeza na kuimbiadunia kuwa anailetea “amani na usalama”.Hapo nikaona dunia yote ikawa imesahau lile tukio la kupotelewa na watu wengi na kuanza kumsikiliza huyu MPINGA KRISTO

 Nikawaona wale malaika saba(7) wenye bakuli zilizo na hasira ya MUNGU yakimwagwa katika dunia watu wakawa wanalia na kukimbia kimbia.BWANA YESU akaniambia angalia hawa watu baadhi yao ni wakristo tena wengine ni wachungaji kabisa.

Nikamuuliza YESU sasa kwa nini watu wako umewa acha na wengine ni wachungaji kabisa waliokuwa wakifundisha neno lako.YESU akanijibu akisema Ndio wachungaji hawa walikuwa wanahubiri neno langu lakini walikuwa hawaishi kama neno langu linavyosema."

Ndugu sasa anza kuishi kama MUNGU anavyotaka tuko katika siku za mwisho sana.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!