menuz

Taswira tatu(3) zinazo athiri mwenendo wako !.

Kuna taswira tatu(3) zinazoweza kuathiri mwenendo wa mtu yeyote.
Yote katika taswira zote lakini MUNGU ana sema je ! kuhusu wewe ndiyo twasira halisi na sio vinginevyo
Aina ya taswira nazo ni:-
1.Taswira ya wewe mwenyewe unajionaje!.
2.Taswira ya watu wanakuona je!.
3.Taswira ya MUNGU anakuona je!.

Imeandikwa “…………. . . .Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?
 19 Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.

 20 Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu.
 21 Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo;” LUKA 9:18-21

Hii inatuonyesha kuna mitazamo au taswira ambazo watu husema kwetu lakini zingine si sahihi kwa kuwa YESU hakuwa Eliya wala Yohana mbatizaji.Kwa hiyo taswira ambayo ni ya kweli na ni ya kipekee kwetu ambayo kwa hiyo tunaweza kuitegemea ni moja tuu nayo ni MUNGU anasema je juu yetu nasio watu au wewe mwenyewe unajiona je!,

1.Taswira ya wewe mwenyewe unajionaje !.
Taswira inayotokana jinsi wewe mwenyewe unavyojiona  unajiona je?,Je wajiona ni mvivu au mchapa kazi !.Hata kwa sura tuu waweza kuta mtu ni mzuri wa sura lakini yeye mwenyewe hajioni kuwa ni mzuri bali anajiona ni mbaya.

Hii yote haisaidii bali utafute MUNGU anakuona je !?,hiyo ndiyo taswira sahihi kwa kuwa kama MUNGU anmekuumba kwa mfano wake hauta kaa hata siku moja  kujiona wewe u mbaya kisura au mtazamo ,hivyo kila kitu katika maisha yako jitegemeze kwenye taswira ya MUNGU kwa kuwa kwa hiyo haina hata chembe ya uongo.


2.Taswira ya watu wanakuona je
Imeandikwa “…………. . . .Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?
 19 Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.”-Luka 9:19
Ni taswira inayotokana na watu wanaokutazama au wanaokujua wanasema je kuhusu wewe au wanakusifu vipi!.Nayo kwa twasira hii hatutakiwi kuitegemea bali kutegemea taswira ya MUNGU anatuona je.

3.Taswira ya MUNGU anakuona je!.
Watu wanaweza kusema wewe ni mbaya sana au ni mshamba labda kwa kuwa umeokoka lakini MUNGU anakuona wewe ni mzuri sana na tena mjanja sana kuliko wote.
Kuna watu wengi wanapenda kuonekana wema machoni pa watu lakini MUNGU hawahesabii watu hao wema wowote juu yao.

Kunawatu wanaojiita na kujiona wao ni masikini lakini MUNGU hawaoni kuwa masikini bali huwahesabu kuwa matajiri. Imeandikwa-“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) . . . . . . . . . . . . . . . . . . .”- Ufunuo wa yohana 2:9.Hata tuwe tunajiona vipi lakini hali ambayo MUNGU anatuona ndiyo sahihi kwetu

Kuna wengine ambao hujiona kuwa kanisa lao ni jema sana lakini MUNGU huwa anawaona ni kanisa la shetani
Imeandikwa-“………….. hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.”-Ufunuo wa yohana 2:9. Hivyo maisha yetu yanatakiwa kuitegema taswira ya MUNGU juu yetu kwa kuwa hiyo ndiyo pekee amabayo ni ya ukweli,
Hivyo kama MUNGU anatuona vibaya tunatakiwa tubadilike hata kama watu au wewe wajiona uu mtakatifu kwa kuwa viwango vya utakatifu vya MUNGU ni tofauti na viwango vya wanadamu.

Mfano wakati sara mke wa ibrahimu anapojiona anajiona yuu tasa lakini MUNGU alimuon akuwa ni mama wa mataifa mengi,Wakati Ayubu anapo ona ameachwa na MUNGU lakiniMUNGU anamuona ndiye rafiki wa kujivunia  na mcha MUNGU kweli kweli.Hivyo basi mtazamo yote hiyo hatupaswi kuifuata isipokuwa ule mtazamo wa MUNGU .Haijalishi wewe unajiona je au watu wanakuona je wewe tegemea MUNGU anakuona JE!


Tunatakiwa tubadilike na kutojali watu wanatuona je au sisi tunajionaje bali tujali MUNGU anatuonaje !.hiyo ndiyo pekee tunayotakiwa kuijali katika maisha yetu.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!