Kuna taswira tatu(3) zinazoweza kuathiri mwenendo wa mtu
yeyote.
Yote katika taswira zote lakini MUNGU ana sema je ! kuhusu
wewe ndiyo twasira halisi na sio vinginevyo
Aina ya taswira nazo ni:-
1.Taswira
ya wewe mwenyewe unajionaje!.
2.Taswira
ya watu wanakuona je!.
3.Taswira
ya MUNGU anakuona je!.
Imeandikwa “…………. . . .Je! Makutano hao wanasema ya
kuwa mimi ni nani?
19 Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine,
Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
20 Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani?
Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu.
21 Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu
neno hilo;” LUKA 9:18-21
Hii inatuonyesha kuna mitazamo au taswira ambazo watu
husema kwetu lakini zingine si sahihi kwa kuwa YESU hakuwa Eliya wala Yohana mbatizaji.Kwa
hiyo taswira ambayo ni ya kweli na ni ya kipekee kwetu ambayo kwa hiyo tunaweza
kuitegemea ni moja tuu nayo ni MUNGU anasema je juu yetu nasio watu au wewe
mwenyewe unajiona je!,
1.Taswira ya wewe mwenyewe unajionaje
!.
Taswira inayotokana jinsi wewe mwenyewe
unavyojiona unajiona je?,Je wajiona ni
mvivu au mchapa kazi !.Hata kwa sura tuu waweza kuta mtu ni mzuri wa sura
lakini yeye mwenyewe hajioni kuwa ni mzuri bali anajiona ni mbaya.
Hii yote haisaidii bali utafute MUNGU
anakuona je !?,hiyo ndiyo taswira sahihi kwa kuwa kama MUNGU anmekuumba kwa
mfano wake hauta kaa hata siku moja
kujiona wewe u mbaya kisura au mtazamo ,hivyo kila kitu katika maisha
yako jitegemeze kwenye taswira ya MUNGU kwa kuwa kwa hiyo haina hata chembe ya
uongo.
2.Taswira ya watu wanakuona je
Imeandikwa “…………. . . .Je! Makutano hao wanasema ya
kuwa mimi ni nani?
19 Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine,
Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.”-Luka 9:19
Ni taswira inayotokana na watu wanaokutazama
au wanaokujua wanasema je kuhusu wewe au wanakusifu vipi!.Nayo kwa twasira hii
hatutakiwi kuitegemea bali kutegemea taswira ya MUNGU anatuona je.
3.Taswira ya MUNGU anakuona je!.
Watu wanaweza kusema wewe ni mbaya sana au ni mshamba
labda kwa kuwa umeokoka lakini MUNGU anakuona wewe ni mzuri sana na tena mjanja
sana kuliko wote.
Kuna watu wengi wanapenda kuonekana wema machoni pa watu
lakini MUNGU hawahesabii watu hao wema wowote juu yao.
Kunawatu wanaojiita na kujiona wao ni masikini lakini
MUNGU hawaoni kuwa masikini bali huwahesabu kuwa matajiri. Imeandikwa-“Naijua dhiki yako na umaskini wako,
(lakini u tajiri) . . . . . . . . . . . . . . . . . . .”- Ufunuo wa yohana 2:9.Hata tuwe tunajiona
vipi lakini hali ambayo MUNGU anatuona ndiyo sahihi kwetu
Kuna
wengine ambao hujiona kuwa kanisa lao ni jema sana lakini MUNGU huwa anawaona
ni kanisa la shetani
Imeandikwa-“…………..
hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.”-Ufunuo wa yohana 2:9. Hivyo maisha yetu yanatakiwa
kuitegema taswira ya MUNGU juu yetu kwa kuwa hiyo ndiyo pekee amabayo ni ya
ukweli,
Hivyo kama MUNGU
anatuona vibaya tunatakiwa tubadilike hata kama watu au wewe wajiona uu
mtakatifu kwa kuwa viwango vya utakatifu vya MUNGU ni tofauti na viwango vya
wanadamu.
Mfano wakati sara mke wa ibrahimu anapojiona anajiona yuu
tasa lakini MUNGU alimuon akuwa ni mama wa mataifa mengi,Wakati Ayubu anapo ona
ameachwa na MUNGU lakiniMUNGU anamuona ndiye rafiki wa kujivunia na mcha MUNGU kweli kweli.Hivyo basi mtazamo
yote hiyo hatupaswi kuifuata isipokuwa ule mtazamo wa MUNGU .Haijalishi wewe
unajiona je au watu wanakuona je wewe tegemea MUNGU anakuona JE!
Tunatakiwa
tubadilike na kutojali watu wanatuona je au sisi tunajionaje bali tujali MUNGU
anatuonaje !.hiyo ndiyo pekee tunayotakiwa kuijali katika maisha yetu.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!