Showing posts with label MBINGU NA KUZIMU. Show all posts
Showing posts with label MBINGU NA KUZIMU. Show all posts

Mtu mmoja(1) akiingia mbinguni, watu elfu moja(1000) wanaingia kuzimu-.Ushuhuda na Mchungaji Park Yong Gyu.


Ushuhuda wa Mbingu na Kuzimu, 1-1000, na Mchungaji Park Yong GyuMchungaji Park alikuwa amefariki kutokana na shinikizo la damu. Lakini kwa neema ya Mungu, maisha yake yaliongezwa kwa miaka 20 nyingine.
Hata hivyo, kwa miaka minne ya kwanza, hakuweza kuzungumza kutokana na hali yake. Alikuwa na umri wa miaka 50 hivi alipofufuliwa. Wakati wa kifo chake, Bwana alimpeleka mbinguni na kuzimu.Nataka ujue ukiwa na kiburi na majivuno utajiletea laana.
Nilikuwa na kanisa kubwa la washiriki 5000 lakini nilipigwa na Mungu kutokana na kiburi changu. Sasa namcha Mungu. Nilikuwa nikimiliki mali nyingi sana zenye kufikia thamani ya dola za kimarekani milioni 150, ambazo ni sawa na bilioni 349.86 za kitanzania.
Nilikuwa na magari matano(5) ya kifahari, Lakini baada ya haya niliyoyaona kwa neema ya MUNGU, niliyatoa yote na kuyagawa. Wokovu hauwezi kupatikana kwa mali zako bali kwa imani. Tafadhali, ninawasihi mashemasi, wazee, na viongozi wengine katika makanisa yao kumtumikia MUNGU chini ya wachungaji wenu kwa mioyo yenu yote.

Mnamo Desemba 19, baada ya kumaliza chakula changu cha mchana na nilipokuwa nikipumzika, nilianza kuhisi maumivu makali. Nilihisi kana kwamba nitakufa. Maumivu hayakuvumilika. Kisha nikapoteza fahamu. Nilipozinduka, watu waliokuwa karibu nami walisema miezi minne imepita.
Nilikuwa katika hali tete na nikiwa katika hali hiyo, daktari alikuwa amesema kwamba ningekufa.Kweli mara tu baada ya kufa, mara nikaona watu wawili wakiingia chumbani kwangu.
Lakini watu hawa walikuwa wameingia kwenye chumba changu kupitia ukuta. Nilipiga kelele, “Nani, wewe ni nani!! Nyumba yangu itabomoka ukifanya hivyo!!” Kisha malaika wakasema, “Sisi ni malaika tulioshuka kutoka mbinguni. Sisi tunatoka katika ufalme wa Mungu.” Nuru angavu ilimulika kutoka kwa malaika. Malaika waliniweka kati yao.
Nikauliza, “Mlikujaje ?”Walinijibu “Umekufa, familia yako inalia kwa huzuni nyingi huko,Baba MUNGU amependezwa kukupa muda zaidi wa kuishi. Ila kwa sasa, anataka kukuonyesha mbingu na kuzimu.
Atakuonyesha nawe utakwenda shuhudia kwa watu wa duniani. Kupitia ushuhuda wako idadi ya watu wanaoishia kuzimu ipunguzwe na idadi ya wanaokwenda mbinguni iongezeke. Hii itakuwa shabaha yako. Mungu alituagiza tukuambie usichelewe. Ukichelewa, hutaweza kuzuru mbinguni na kuzimu.” Malaika wa kulia kwangu alijitambulisha. “Ninafanya kazi kwa ajili ya Yesu katika ufalme wake. Yesu aliniita na kuniamuru nishuke duniani, akaniamuru nikupeleke mbinguni.
Kisha malaika aliyesimama upande wangu wa kushoto akajitambulisha. Alisema, "Wakati ulipozaliwa na hadi ulipokufa, nilikuwa pamoja nawe." Wakati huo, sikuelewa malaika alikuwa anamaanisha nini. Sasa najua. Yeye ni malaika wangu mlezi. Mimi nikasema, “Siwezi kwenda! Sitakwenda! Mimi ni mchungaji! Siwezi kukutana na Bwana katika hali hii ya kimwili. 
 
Ninataka kumwona nikiwa mtu mwenye afya njema. Pengine naenda kupokea karipio zaidi kuliko pongezi kutoka kwa Bwana. Nina kiburi mimi na majivuno, sasa nimelaaniwa na ni mgonjwa. Je, ninawezaje kuingia mbinguni? Ninaogopa sana. Tafadhali rudi mbinguni na umwombe Bwana aniponye. Kisha urudi na kunipeleka mbinguni kupitia ndoto yangu.
Tafadhali malaika omba rehema kwa niaba yangu.” Lakini malaika hawakusikiliza hoja yangu. Walinivua nguo zangu na kusema kwamba zilikuwa chafu sana kuvaliwa mbinguni. Kisha wakanivalisha gauni jeupe. Walishika mikono yangu na tukaruka moja kwa moja hadi mbinguni. Tuliruka kupitia mawingu na nilipotazama chini, niliona dunia ikizidi kuwa ndogo. Waliponiruhusu niende, ndani ya futi 3 kutoka kwangu, niliona Barabara ya Dhahabu isiyo na mwisho.
Tulikuwa bado tunaruka na kwa kasi kubwa. Kuangalia mbele, niliona mwanga mkali unaowaka. Sikuweza kutazama moja kwa moja kwenye mwanga.
 
 Nikawauliza wale malaika, Nuru inatoka wapi? Malaika akajibu, "Inatoka mbinguni." Nilipotazama mbele, nilijiwazia, “Lo! Ni kubwa!” Mbele yangu niliona makundi ya watu waliovalia mavazi meupe wakiruka mbele.
Niliwauliza wale malaika, “Ni nani hao?” Malaika akajibu, “Hao ndio waliokuwa wamemtumikia Mungu kwa uaminifu na kumtumaini Yesu kwa kutii na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu kwa moyo wao wote. Miili yao imekufa duniani. Sasa ni nafsi zinazoelekea mbinguni.”Malaika mwingine akaendelea, “Kuna milango kumi na miwili(12) mbinguni. Wakati nafsi iliyookolewa inapokuja mbinguni, lazima iingie kupitia mojawapo ya milango hiyo.” Tulikuwa tumesimama kwenye lango la kusini lakini lilikuwa limefungwa.
Tulipokuwa tukingoja, nilimuuliza malaika, “Malaika, kwa nini lango hili halifunguki?” Malaika akajibu, "Ni kwa sababu huimbi wimbo wa kuabudu wa mbinguni." Niliuliza, “Malaika, mimi nilikuwa na kiburi na majivuno sana na matokeo yake nimelaaniwa na ugonjwa. Siko vizuri kuimba nyimbo za kuabudu za duniani. Je, ninawezaje kuimba nyimbo za kuabudu za mbinguni wakati sijawahi kuzisikia kabla?” Malaika akajibu, “Umesema kweli. Lakini bado unapaswa kujitayarisha kuabudu.
Wewe ni mtu wa kujivunia lakini jiandae kuimba.” Malaika walianza kuimba. Walipokuwa wakiimba, nilianza kuimba pamoja nao. Ikawa asili kwangu! Lakini basi, waliacha kuimba baada ya muda mfupi. Niliuliza, “Kwa nini umeacha kuimba? Nilikuwa nikifurahia.” Kisha nikagundua tayari tumeingia kwenye geti.
 
 Kwa jinsi mbingu ilivyo nzuri ,sitaweza kamwe kuelezea matukio ya mbinguni kwa maneno yangu ya kidunia. Nikasema, “Bwana! Asante sana! Ingawa, nilikuwa na kiburi na majivuno sana na kulaaniwa kwa ugonjwa, bado umenileta mbinguni ili kunionyesha pande zote. Tukio la mbinguni lililojitokeza mbele ya macho yangu lilikuwa lisiloelezeka. Kisha nikasikia sauti ya Mungu, “Mchungaji wangu mpendwa Park, Yong Gyu, ninakukaribisha.
Umefunga safari ndefu hapa.” Sauti ya Bwana ilijaa upendo na huruma. Nilijibu huku nikilia kwa machozi, “Bwana,….” Malaika walinisimamisha kulia mara moja, huku akisema “Umekuwa mchungaji kwa miaka 20. Je, hujui maandiko ya MUNGU?,kuwa mbinguni hakuna machozi. 
 
Tafadhali acha!” Sikuweza hata kulia.
Kisha Bwana akaniuliza maswali matano(5).
1. “Ulitumia muda gani kusoma Neno (biblia)? 2. Ulitoa kiasi gani cha sadaka?
3. Je, umehubiria watu mara ngapi?
4. Je, ulitoa zaka ipasavyo?
5. Ulitumia muda gani katika maombi?” Sikuweza kujibu swali la tano.
Bwana alinikemea kwa swali la tano. BWANA akaniambia “Baada ya kuwa mchungaji mkuu wa kanisa, umekuwa mvivu sana katika maombi. Na umekuwa na shughuli nyingi sana yakupasa ujue kuwa si kisingizio Kwangu!” Ilinibidi nitubu baadaye. Bwana aliendelea na kuniambia, “Malaika watakuonyesha sehemu nyingi mbinguni na kuzimu. Angalia kote kama unavyotaka. 
 
Utaondoka baada ya kushuhudia sehemu nyingi tofauti mbinguni na kuzimu.” Lakini Bwana hakuni ruhusu nione sura yake.Malaika walinipeleka kwanza sehemu tatu tofauti mbinguni. Sehemu ya kwanza, niliona watoto wadogo wakiishi pamoja. Sehemu ya pili ilikuwa mahali ambapo watu wazima waliishi. Sehemu ya tatu ilikuwa ni ya wale waliofika mbinguni kana kwamba kwa bahati bahati. Ingawa walifika mbinguni, walikuwa wameifika kwa aibu.
 
Watu wengi sana walikuwa wameniuliza watoto wadogo walikuwa na umri gani. Nadhani wanaonekana kufikia umri wa kusoma chekechea. Sikuweza tambua kuhusu jinsia ila kila mtoto alikuwa na malaika wake mtoto wa kuongozana nao. Mbinguni, roho nyingi zitakuwa na makao yao binafsi (Yohana 14:22). Hata hivyo, kulikuwa na wengine ambao hawakuwa na nyumba.
Nitalieleza hili baadaye. Isitoshe, watoto hawakuwa na nyumba zao binafsi pia. Niliuliza, “Watoto pia ni nafsi, kwa nini hawana nyumba zao wenyewe?”Malaika akajibu, “Kama vile watu duniani wanahitaji vifaa vya kujenga nyumba zao, sisi mbinguni pia tunahitaji vifaa vya kujenga hapa. Wakati mtu anatumikia kanisa na wengine kwa uaminifu kwa Bwana, matendo hayo yatakuwa nyenzo kwa ajili ya nyumba ya mtu mbinguni. 
 
Vifaa vinapotolewa, malaika waliopewa kazi ya kujenga nyumba ya mtakatifu wataenda kufanya kazi ya kuijenga. Watoto walio chini ya umri wa uwajibikaji hawajajenga nyenzo zozote za kujenga nyumba. Kwa maneno mengine, hawakuwa na wakati au nafasi ya kupata tuzo/nyenzo zao. Ndiyo maana hawana nyumba.”Niliendelea na maswali yangu, Na kuuliza “Nitafanya nini duniani ili kutoa nyenzo(materials) zaidi kwa ajili ya kujengea nyumba yangu?”
 
Malaika wakajibu, “Kuna mambo saba(7) ambayo mtu lazima afanye yatayosababisha mbinguni kupata vifaa/nyezo(materials) vitakavyo wezesha kujenga nyumba yake mbinguni.
1. La kwanza ni mkusanyiko wako wa ibada na sifa kwa Mungu.
2. Pili ni muda wako binafsi wa kusoma biblia.
3. Tatu, muda wako binafsi wa kusali.
4. Nne, muda wako ulioutumia kuhubiri injili kwa watu.
5. Tano, sadaka ya uaminifu ya mtu kwa Bwana.
6. Sita, zaka zao za utii kwa Mungu.
7. Mwisho, muda wao walioutumia kutumikia kanisa kwa njia yoyote ile.
 
Haya ni matendo au kazi za utii ambazo ndani yake mtu hukusanya nyenzo/vifaa kwa ajili ya kujengewa makao yao ya mbinguni. Ikiwa moja itakosekana katika maeneo haya, hawatakuwa na vifaa vya kujenga nyumba yao.Kulikuwa na watu wengi mbinguni na wasio na nyumba.
Wengi ambao hawakuwa na nyumba walikuwa wachungaji, mashemasi, wazee, n.k. Niliuliza kwa udadisi, “Watoto wanaishi wapi wakati huo?” Malaika wakajibu, "Wanaishi hapa." Nilipotazama pande zote, walikuwa wamekusanyika katika bustani yote ya maua. Bustani ya maua ilikuwa nzuri sana na harufu nzuri. Tukio hilo lilikuwa zaidi ya vile ningeweza kuelezea kwa maneno yangu. Sehemu ya pili ilikuwa kwa watu wazima waaminifu.
 
Kuna tofauti kati ya wokovu na thawabu. Mahali hapa palikuwa na nyumba nyingi sana. Nyumba zilijengwa kwa vito vya kupendeza na mawe adimu. Baadhi ya nyumba zilikuwa juu kama maghorofa ya juu zaidi duniani. Watu hao ambao walikuwa wamemtumikia Bwana kwa uaminifu walipokuwa wakiishi duniani walijenga nyumba zao kwa vito vya kupendeza na mawe adimu. Katika mahali hapa, watu wote walionekana wana wastani wa umri wa miaka 20 hadi 30.
 
  Hakuna wagonjwa, wazee, au vilema.Nilimuulizia mzee niliyemjua akiwa duniani, mzee anayeitwa, Oh, Im Myung. Alikufa akiwa na umri wa miaka 65. Alikuwa mtu mfupi sana, yaani mrefu kama mtoto wa darasa la 2 katika shule ya msingi. Alikuwa ameugua ugonjwa adimu unaoitwa rickets. Hata hivyo kwenye biblia, alikuwa amesoma hadi uzamivi(PHD). Alikuwa ameandika maoni mengi. Nilikutana naye Mbinguni, na hapo alikuwa mrefu na mzuri. Hakuwa mgonjwa tena bali mzima wa afya.
 
 Mbinguni ni mahali pazuri sana!! Mimi nimejawa na shauku kamili ya matarajio ya mbingu! Tafadhali amini ninachosema wapendwa!Sehemu ya tatu ni mahali ambapo waliookolewa kwa aibu wamekusanyika. Kijiji hiki ni kikubwa sana kwa ukubwa. Mahali hapa ni kubwa mara kadhaa kuliko mahali ambapo roho zilikaa mahali pa pili ambapo nyumba zimetengenezwa kwa vito na mawe adimu. Nilifika mahali hapa nikiendesha gari la dhahabu. Nilikuwa nimefika kwa kasi kubwa. Mahali hapa palikuwa mbali sana na sehemu nzuri za mbinguni. Niliwauliza malaika, “Naona nyika kubwa na mashamba. Kwa nini sioni nyumba?"Malaika akajibu, "Unachoona ni nyumba."
 
 Niliona nyumba kubwa pana za gorofa. Umbo la nyumba hizo lilinikumbusha banda kubwa la kuku au aina fulani ya ghala. Nyumba hizi zilikuwa chakavu sana. Kijiji hiki na nyumba zilikuwa kwa ajili ya roho zilizookolewa kwa aibu. Kulikuwa na nyumba nyingi kubwa zenye sura mbovu. Kijiji hiki ni kikubwa mara kadhaa kuliko mahali ambapo roho zilizotuzwa hukaa. Malaika akasema, “Je, unaziona nyumba mbili kubwa, moja kulia kwako na nyingine kushoto kwako?Nikajibu, “Ndiyo, ninaona.”Malaika alisema kwamba alitaka kunionyesha nyumba hizo mbili haswa. Alisema, “Nyumba za upande wa kulia ni kwa wale waliokuwa wachungaji duniani. Makao ya kushoto ni ya wale waliokuwa wazee wa kanisa duniani.”
 
 Tulipofika mbele ya nyumba hizo mbili, nikawaona wakiwa wacheshi.. Tulipofungua mlango na kuingia, Taya langu lilishuka mawazo yangu ya kwanza yalikuwa, ‘banda la kuku.’ Badala ya maelfu ya kuku wanaoishi kwenye banda lao, niliona nafsi. Malaika walinishauri niangalie kwa makini sana kwa sababu ningewatambua baadhi ya wachungaji waliokuwa maarufu huku duniani. Kweli nilitambua wachungaji wengi kutoka kwa historia.
 
 Nilimchagua mchungaji mmoja na kumuuliza malaika, “Ninamfahamu yule kasisi wa Korea! Ninajua jinsi alivyokuwa maarufu na kazi aliyokuwa amemfanyia Bwana. Kwa nini yuko hapa? Sielewi." Malaika wakajibu, “Hakuwahi kutoa vifaa vyovyote vya ujenzi kwa ajili ya nyumba yake.” Hii ndiyo sababu anaishi katika nyumba ya jamii.” Niliuliza kwa udadisi, “Hii ilifanyikaje? Kwa nini hakuwa na nyenzo yoyote? Malaika akajibu, “Alipokuwa mchungaji akitekeleza majukumu yake kama mchungaji, alipenda kusifiwa na watu. Alipenda kuheshimiwa. Alipenda kuhudumiwa. 
 

Hakukuwa na dhabihu na utumwa kwa upande wake.” Mchungaji huyu aliheshimiwa sana huko Korea na ni nguli(icon) kwenye historia ya Kikristo ya Kikorea. Lakini hakuwa na thawabu kubwa mbinguni !!. Mchungaji, tafadhali sikiliza! Inabidi uwaongoze watu kwa zaidi ya ibada za jumapili asubuhi. Lazima uwatembelee majumbani mwao. Lazima uwatunze maskini, viwete na wazee. Wachungaji ambao wametumikia bila kutoa maisha yao na kupenda kuheshimiwa hawana thawabu mbinguni. Baada ya kushuhudia tukio hili mbinguni na baada ya kurudi duniani, mara moja nilitoa mali yangu yote ikiwa ni pamoja na magari yangu matano ya kifahari. Maisha yetu ni ya kitambo tu. Katika Biblia, maisha ya wastani ni takriban miaka 70 hadi 80.Mungu pekee ndiye anayejua ni lini mtu atakufa. Mtu yeyote anaweza kufa kabla ya umri wa miaka 70 au 80. Nilikuwa nimeamua kutoa kila kitu hata nguo zangu.
 
 Watu niliowaona wamepokea wokovu kwa aibu walikuwa wachungaji, wazee, mashemasi, na waamini walei. Kulikuwa na umati wa wazee na mashemasi katika nyumba ile tambarare iliyochakaa. Lakini bila shaka, bado ni bora kuliko kuzimu. Hata hivyo, kwa nini mtu yeyote bado angependa kuingia mbinguni kwa njia hiyo? Sitaishia mahali pa aibu. Hata nguo zao zilikuwa chakavu. Ikiwa mtu anasema hawezi kufika kanisani kwa sababu hawana nguo nzuri, basi lazima umpatie baadhi. Ikiwa mtu huyo anasema hana Biblia, lazima umtolee.
 
 Ikiwa mtu anasema hana miwani ya kusoma, lazima umpatie. Ni lazima utoe chochote unachoweza pia ili mtu huyu aweze kuongozwa kwa Bwana. Wale wanaoishi katika nyumba bora zaidi ni wale ambao walikuwa wamehubiri mara nyingi.” Ni matakwa gani ili Wakristo wapokee makao hayo mazuri mbinguni? Hebu tuijadili. Kwanza, tunapaswa kuinjilisha kwa watu wengi zaidi kadri iwezekanavyo.Niliuliza swali muhimu. Je, tunapaswa kueneza injili jinsi gani? Malaika akajibu na kusema, “Fikiria kwamba kuna mtu asiyeamini ambaye hamjui Bwana. Mara tu unapoamua kuinjilisha mtu huyo, vifaa vya ujenzi vya nyumba zako vitatolewa. 
 
Unapowaombea wokovu bila kukoma, vifaa vingi vya ujenzi vinatolewa. Lazima uendelee kuwachunguza, kuwatembelea na kuendelea na uinjilisti wako. Kisha malaika akanisindikiza hadi mahali ambapo watakatifu waliishi katika nyumba nzuri. Hapa ndipo walipoishi watakatifu waliohubiri sana. Mahali nilipochukuliwa nilihisi kama mbinguni katikati mwa jiji. Katika historia ya Kikristo, kuna watu wanne ambao wana nyumba kubwa na nzuri zaidi.
 
 Malaika alinionyesha nyumba ya mwinjilisti wa Marekani D.L. Moody. Nyumba ya pili niliyoiona ilikuwa nyumba ya Mchungaji wa Uingereza John Wesley na ya tatu ilikuwa mwinjilisti wa Kiitaliano. Nyumba ya nne ilikuwa nyumbani kwa Mwinjilisti wa Kikorea Mchungaji Choi, Gun Nung. Watu hawa wanne wana nyumba kubwa zaidi mbinguni. Malaika waliniambia kwamba hawa wanne walikuwa wametumia maisha yao yote kuhubiri injili kwa watu hata hadi wakati wa kufa kwao. Ndani ya waumini wa Korea, kulikuwa na mwamini mlei ambaye alikuwa na nyumba kubwa. Muumini huyu mlei alikuwa amejenga majengo mengi ya kanisa pamoja na mali zake zote alikuwa amewapa maskini magunia elfu tatu ya mchele. 
 
Alisaidia kwa siri maelfu ya wachungaji na viongozi kwa kutumia fedha zake. Alisaidia wanafunzi wanaosoma theolojia au shule ya biblia na masomo yao. Pia alikuwa amemchukua mchungaji (umri wa miaka 65) nyumbani kwake na kumtunza vizuri. Kanisa lake mwenyewe lilikuwa limemfukuza. Kisha ghafla, nikasikia malaika akipaza sauti, “Nyenzo/vifaa vinakuja!” Nilimuuliza malaika aliye kulia kwangu kuhusu nyenzo hizo. Alijibu, “Vifaa hivi ni vya shemasi kutoka kanisa dogo ambaye anatoka nchini. Kwa kweli, yeye hupokea vifaa kila siku. Ingawa yeye ni maskini, yeye huja kwenye ibada ya asubuhi kila siku, anawaombea washiriki 87 wa kanisa kila siku.
 
 Anapomaliza kusali, anasafisha kanisa.” Nilimsikia malaika mwingine akipiga kelele, “Utoaji maalum! Binti wa shemasi amempa mama yake pesa kidogo aliyokuwa nayo. Hata hivyo, shemasi hakuitumia yeye mwenyewe. Alinunua mayai matano na jozi mbili za soksi kwa mchungaji wa kanisa. Ingawa inaweza kuonekana kuwa sadaka ndogo, alikuwa ametoa vyote alivyokuwa navyo kwa siku hiyo. Hiki kilikuwa nyenzo maalum kwa ajili ya nyumba yake mbinguni.” Pili, wale ambao pia wana nyumba kubwa ni wale ambao wamejenga majengo ya kanisa au majengo mengine kwa ajili ya Ufalme wa MUNGU kwa mali zao.
 
 Mbinguni nilikutana pia na mzee anayeitwa Choi. Miongoni mwa wazee wote wa Korea na mashemasi walio mbinguni, alikuwa na nyumba nzuri zaidi. Nyumba yake ilikuwa juu sana kuliko jengo refu zaidi nchini Korea. Choi alikuwa amejenga makanisa mengi nchini Korea kwa utajiri wake. Nilimuuliza malaika, “Vipi kuhusu nyumba yangu? Je, iko katika mchakato wa kujengwa? Malaika akasema, Ndiyo.
Niliomba kuona nyumba yangu, Lakini waliniambia hairuhusiwi. Niliendelea kuomba. Baada ya kuomba kwa bidii, malaika walisema kwamba sasa Bwana ameruhusu. Tuliingia kwenye gari na kusafiri mbali sana hadi sehemu nyingine. Tulipokuwa tukiondoka, nilimuuliza malaika, “Hii itatuchukua muda gani?” Wakawawanasema kwamba ninazungumza sana. Hatimaye, baada ya muda fulani, malaika walinijulisha kwamba tumefika. Nilijawa na shauku kubwa. 
 
Nikauliza, “Nyumba yangu iko wapi?” Malaika akajibu, “Iko pale!” Lakini ilionekana kana kwamba mahali hapo palikuwa pazuri kwa bado haijakamilika kujengwa. Nililia, Nikieleza“Mngewezaje kunifanyia hivi? Hii inawezaje kutokea? Nyumba yangu inawezaje kuwa katika kutokamilika ?. Niliuza nyumba yangu pekee ili kujenga kanisa. Kanisa hili hatimaye lilikua na washiriki elfu tano. Niliandika vitabu vingi vilivyoongozwa na Roho Mtakatifu.
 
Kitabu kimoja kikawa kinauzwa zaidi. Kwa mapato ya vitabu, nilijenga shule za Kikristo. Shule hiyo ilizaa wachungaji 240. Wakati wa utumishi kama mkuu, nilikuwa nimetoa zaidi ya ufadhili wa masomo 400 kwa zaidi ya watoto 400 maskini. Nimewajengea wajane nyumba za kuishi. Hii yote iligharimu kiasi kikubwa cha pesa. Kwa hivyo hii inawezaje kuwa? Kwa nini nyumba yangu iko katika hali ya kuendelezwa ? Nimekasirika sana!” Malaika akajibu kwa ukali, “Hustahili kuishi katika makao mazuri kama haya mbinguni kwa sababu umeheshimiwa na watu mara nyingi. Kila wakati ulikuwa umejenga au umefanya kitu kizuri, ulisifiwa na watu. 
 
Uliheshimiwa hata na habari za kilimwengu. Kwa hiyo, kazi zenu zote ni bure.” Nilimuuliza malaika, “Kwa nini nina vyumba vidogo hivyo?” Hata hivyo, kwa kuwa tayari nilikuwa hapa, niliamua kuangalia nyumba yangu katika eneo la maendelezo. Nyumba yangu ilikuwa katikati ya nyumba zingine tatu. Nyumba yangu ilikuwa na safu tatu(3).
Nyumba hiyo ilikuwa na vyumba vingi vidogo kwenye orofa mbili za kwanza. Malaika akajibu, "Vyumba hivi ni vya wana wako na binti zako." "Nina watoto wanne tu" Hapana, si kwa ajili ya watoto wako wa udongo(yaani wa uzazi) bali ni kwa ajili ya wale uliowahubiria na kuokolewa.” Malaika alisema kwamba ilikuwa juu ya paa. 
 
Sikuipenda. Chumba changu hata hakijaisha. Kwa sauti ya hasira nilisema, “Ni ndogo sana! Kwa nini ni vigumu kumaliza?” Niliipenda! Nikauliza, “Chumba changu kikuu kiko wapi?” Malaika akajibu, “Hata wewe hujafa. Hatuwezi kumaliza nyumba au chumba chako kwa sababu hatujui ikiwa nyenzo zaidi zitatolewa. Unaelewa?" Tuliingia chumbani kwangu.
 
Niliona vyeti viwili vikining'inia ukutani. Nilikwenda kusoma kile kilichosema. Cheti cha kwanza kilichoelezwa nilipokuwa na umri wa miaka 18 nikiishi katika kituo cha watoto yatima. Siku ya Krismasi, nilikuwa nikirudi kwenye ibada ya asubuhi ya asubuhi. Nilikuwa nimemwona mzee mmoja akitetemeka barabarani. Nikavua koti langu na kumpa. Tendo hilo lilikuwa limenipa thawabu mbinguni. Cheti cha pili kilieleza tukio lilelile lakini kilikuwa cha kununua mkate kwa pesa kidogo niliyokuwa nayo kwa yule mzee. Kiasi sio suala. Tendo lazima liambatane na imani ya kweli.
 
** *NILITEMBELEA KUZIMU***
Malaika wawili(2) walinisindikiza hadi kuzimu. Wakasema, "Sasa utatembelea kuzimu." Hujui ukubwa wa kuzimu. Nilivyoiona nilipiga kelele, “Ni kubwa sana! Ni kubwa sana!” Hapa ndipo mahali ambapo roho zilizolaaniwa na kupokea laana ya milele zinawekwa.
Nilihisi kana kwamba mahali hapa palikuwa pakubwa mara elfu moja kuliko dunia. Nusu ya kuzimu ilikuwa na rangi nyekundu na nusu nyingine ilikuwa nyeusi sana. Niliwauliza malaika, “Kwa nini sehemu hii ni nyekundu?” Malaika wakajibu, “Je, hujui? Inawaka kiberiti.
 
 Nusu nyingine ni giza. Watu wakitenda dhambi na kuishia hapa, watateswa kutoka pande zote mbili.” “Mahali hapa ni pakubwa sana! Ni roho ngapi zilizo humu ndani?" Malaika akajibu, "Je, unaamini kuna mbingu na kuzimu?" “Ndiyo, ninaamini!” “Kuna wingi wa makanisa duniani na makanisa mengi yamejaa watu wengi.
Hata hivyo, wengi wao si wakristo wa kweli. Ni wahudumu wa kanisa tu. Makanisa ya kweli yataamini kabisa mbinguni na kuzimu. Maisha ya wakristo wengi yako katika machafuko kwa sababu hawaamini kabisa mbinguni na kuzimu. Nafsi moja(1) inapoingia mbinguni, roho elfu moja(1000) zilizolaaniwa huingia kuzimu. Kiwango cha uwiano wa mbinguni na kuzimu ni 1 kwa 1000." 
 
Chuo cha theolojia nilichokuwa nimesoma ni mojawapo ya shule kubwa zaidi za theolojia za kihafidhina nchini. Sikuamini katika mbingu na hadithi za kuzimu. Lakini sasa, mimi ndiye ninayeandika matukio kama haya ili kuwashuhudia wengine. Ingawa unaweza kuamini na kuwa Mkristo, ukiishi maisha yako kulingana na mapenzi ya mapepo, utaishia kuzimu.Mimi ni mchungaji wa Presbyterian. Mimi ni mzungumzaji maarufu.
 
Nimehitimu kutoka shule moja kubwa zaidi ya theolojia nchini Korea. Mahali pa kwanza waliponipeleka ni mahali pa salfa. Je, unaweza hata kufikiria jinsi moto wa kuzimu unavyoweza kuwa mkali? Hakuna mtu atakayeweza kuhimili joto kali. Kuzimu utasikia kauli tatu tu. Kwanza, ni joto sana na wanahisi kama kufa. Pili, wana kiu sana na wanahisi kufa. Tatu, utasikia wengi wakiomba maji. Ni ya milele! Watu wengi husema tuko huru katika Kristo na wanaishi maisha yao jinsi wanavyotamani.
Nikamwuliza yule malaika, “Wale waliomo humu ndani, wamefanya nini?” Malaika akajibu, "Kundi la kwanza ni la wasioamini." Wale ambao hawakuwa wamehubiria familia zao wenyewe lazima watubu! Malaika akaendelea, “Kundi la pili ni wale waliomwamini Yesu lakini hawakutubu dhambi zao.” Tunapaswa kutubu dhambi zetu na kukiri kwa Bwana.
 
Hatupaswi kutenda dhambi. Kuomba msamaha kwa midomo tu sio kutubu. Kwa moyo wa toba na wa dhati, lazima tutubu! Kisha niliwaona wachungaji, wazee, na mashemasi wengi kuzimu. Nilimuuliza malaika, “Ninawajua. Walikuwa wamemtumikia Mungu kwa uaminifu walipokuwa duniani. Walikuwa wamekufa wakati fulani uliopita. Sote tulifikiri walikuwa mbinguni pamoja na Mungu. Lakini sasa, ninawaona wote kuzimu na wanalia kwamba kuna joto sana! Sababu yao ni nini humu ndani?” Kulikuwa na idadi kubwa ya wachungaji, wazee, mashemasi na waamini walei wote. 
 
Wakiwa kwenye vitanda vyao vya kifo, walifikiri wamefanya kazi nzuri kwa hiyo hawakutubu mambo hayo. Hii ndiyo sababu walitupwa katika moto wa kuzimu.” Malaika akajibu, “Mchungaji Park Yong Gyu, mtu anaweza kuonekana kuwa mfuasi wa kweli wa Kristo kwa nje lakini Mungu anaujua moyo. Hawakuweka Jumapili Takatifu. Kwa kweli walipenda kupata pesa siku za Jumapili. Mashemasi na wazee wengi walikuwa wamekosoa mahubiri ya wachungaji wao. Hawakutoa zaka ipasavyo. Hawakuomba. 
 
Hawakuwa wamehubiri injili kwa watu hata kidogo. Wengi wa wazee hawa na mashemasi walikuwa wamewasumbua wachungaji wao na wangekuja kinyume na mamlaka yao. Walikuwa wameingilia kazi na shughuli za wachungaji wao. Kisha nikaona mfalme na mwana mfalme ambao walikuwa wamewatesa wakristo huko Korea kwanza. Mfalme na mkuu huyu aliwakata vichwa waumini wengi wa kwanza huko Korea. 
 
Waliwekwa katikati ambayo ilikuwa mahali pa moto zaidi kuliko zote. Pia nilimwona Hitler, Stalin, Mao Zedong, na mchungaji maarufu kutoka Korea kaskazini aitwaye Mchungaji Kang, na shujaa maarufu wa Kijapani, na mengi zaidi. Kisha tukafika mahali pa giza sana. Sikuweza kuona mahali ningekanyaga. Nilipaza sauti, “Malaika! Malaika! Ni giza sana! Ninawezaje kuona chochote?" Malaika walinipigapiga bega na kusema, “Subiri kidogo tu.” Ndani ya dakika chache, niliweza kuona. Niliona idadi isiyohesabika ya watu uchi.
 
 Wote walikuwa na wadudu wanaotambaa kwenye miili yao.
Hakuna hata inchi moja iliyosalia kwani miili yao yote ilikuwa imefunikwa kabisa na wadudu. Watu waliokuwa uchi walijaribu kuwafukuza wadudu hao huku wakisaga meno yao. Niliuliza, “Watu hawa walifanya nini walipokuwa wakiishi duniani?” “Ni wale ambao wamekosoa na kupinga mambo ya MUNGU. Hawakuwa waangalifu kwa yale waliyoambiana.”
Niliona mapepo yakitoboa na kuchoma matumbo ya watu kwa mundu. Vilio vyao vilikuwa havivumiliki kwangu.
 
 Nilimuuliza msindikizaji wangu, “Malaika, watu hawa walifanya nini walipokuwa wakiishi duniani? “Watu hawa walikuwa na kazi, nyumba, na familia lakini hawakuwa na cha kumtolea Mungu.
Hawakuwasaidia maskini, makanisa yao, au makusudi mengine ya kimungu. Walikuwa wabahili sana na wachoyo. Hata walipokutana na maskini, waliwapuuza na hawakujali. Walijijali wenyewe na familia zao tu. Walivaa vizuri, walilishwa, na walikuwa na maisha ya starehe.
 
Ndio maana matumbo yao yamechomwa kwa sababu matumbo yao yalijaa uchoyo. Lilikuwa ni tukio la kuogofya sana. Baada ya kushuhudia tukio kama hilo, niliporudi duniani, nilitoa pesa na mali zangu zote kwa wengine. Wokovu hauwezi kupatikana kwa pesa au mali. Ni kwa imani. Kuzimu ni mahali pabaya na pabaya. Ni mateso ya milele! Kisha nikaona vichwa vyao vimekatwa na msumeno mkali sana.
Nilimuuliza malaika kwa mara nyingine tena, “Watu hawa walifanya nini ili kustahili mateso ya kutisha namna hii?” Malaika akajibu, “Akili zao zilitolewa na Mungu kufikiria mema na yenye manufaa. Lakini watu hawa walikuwa wamefikiria mambo machafu. Walifikiria mambo ya ashiki(tamaa za ngono).”
 
Kilichofuata nikaona watu wakichomwa visu na kukatwa vipande vipande. Mtazamo huo ulikuwa wa kutisha. Nikauliza, “Vipi kuhusu watu hawa?” Walifanya nini hata kuteswa namna hiyo?” “Hawa walikuwa wazee na mashemasi ambao hawakutumikia makanisa yao. Kwa kweli, hawakutaka hata kufanya kazi au kutumikia! Mambo pekee ambayo walikuwa wamependa yalikuwa kupokea na kupokea kutoka kwa kundi.” 
 
Niliwaona wazee, mashemasi, na waamini walei wengine wakiteswa na mapepo. Mashetani walitoboa tundu kwenye ndimi zao na kuweka waya kupitia ndimi za wao kwa wao. Kisha mapepo yakawakokota watu kwa sime. Nikauliza tena, “Walifanya nini duniani?” Malaika akajibu, “Walikuwa wametenda aina nne tofauti za dhambi.
Kwanza, walikuwa wamewakosoa wachungaji wao. Wangezungumza mambo mabaya kuhusu wachungaji wao. Walikuwa nyuma wakiuma na kuwadhihaki wachungaji wao. " Nawasihi waliofanya vitendo hivyo WATUBU, WATUBU!! Malaika aliendelea, “Pili, walitukana kanisa kwa maneno yao. Walikuwa wamewasumbua Wakristo wengine hadi kufikia hatua ambayo hata waamini waliathiriwa na wakaacha kwenda kanisani na hata kuwafanya wengine waache kuamini. 
 
Walifanya yote waliyoweza ili kuwazuia Wakristo waaminifu wasifanye kazi ya Mungu. Waovu hao waliwafanya wengi waaminifu wajikwae. Mwisho, kuna wanandoa ambao walikunywa pombe na kuwatusi watu wa familia zao. Niliona mapepo yakiwatoboa wanaume na wanawake kwenye matumbo yao kwa msumari mkubwa sana wenye ncha kali. Nikauliza, “Walifanya nini?” Hawakuwa wametubu kamwe. “Hawa ni wanaume na wanawake ambao walikuwa wameishi pamoja lakini hawakuwa wameoana. 
 
Hawa wana hatia ya kutoa mimba kwani pia walipata ujauzito. Niliona kundi lingine la watu. Mashetani hao walikuwa wakipasua midomo yao kana kwamba mtu anapasua nyama au mboga. Niliuliza, “Kwa nini watu hawa wanateswa namna hiyo?” Malaika akasema, “Hawa ni wana, mabinti, wakwe zao na wakwe zao ambao walikuwa wamewajibu vibaya wazazi wao.
 
Walichopaswa kufanya ni kusema, ‘samahani’ badala ya kufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Wengi wao walikuwa wametumia lugha ya matusi. Walikuwa wamewashambulia wazazi wao kwa lugha kali. Walikuwa waasi. Ndiyo maana midomo yao inakatwakatwa.”Ndugu, sisi sote tutakufa siku moja. Hatujui siku tutakufa.
Tafadhali jitayarishe. Kuwa tayari kwenda mbinguni. Tafadhali sameheaneni mara kwa mara kadri inavyohitajika.Tubu kwa toba ya kweli na ufanye hivyo siku zote.Ndugu zangu wapendwa, nilikuwa napuuza shuhuda hizo. Nilikuwa mchungaji wa Kipresbiteri ambaye alipuuza mambo kama hayo. Lakini sasa, lazima nishuhudie na nishuhudie kwako kile nilichoona.Tafadhali usisite kuishi maisha matakatifu. 
 
Tafadhali epuka adhabu na hukumu mbaya. Okoka! Msiishi kwa ajili ya miili yenu bali mtiini Ufalme wa Mungu. Tafadhali ombea wale wasiomjua Yesu. Kuinjilisha na kuzaa matunda. Tafadhali omba mapema asubuhi na uitakase Jumapili kuwa Takatifu. Tafadhali toa zaka kwa Bwana ipasavyo. Jikusanyieni thawabu zenu mbinguni na sio duniani. Nakuombea na kukubariki katika Jina la YESU!Kumbuka KUSHIRIKISHA wengine ujumbe huu : ubarikiwe!.

SIRI ZA MBINGUNI NA KUZIMU SEHEMU YA TATU(3)

Mwisho wa dunia hii uwadia hivi karibuni.Hivyo uwe mtu wa kukesha a kuomba(1 Petro 5:7).Namshukuru MUNGU kwa ajili ya hii neema juu ya maisha yangu. “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.” ( Zaburi 28:7 ).Bwana aliniahidi kunitembelea tarehe 9 februari ,2013 na akafanya.Yeye ni MUNGU mwaminifu sana.( Zaburi 33:11).

Siku ya tarehe 9 ya mwezi wa February 2013, mishale ya saa Saba(7) mchana, Nilikuwa nimejilaza kitandani na nikasikia sauti ikisema, “Huu ndio muda mwanangu, Jiandae mwenyewe sasa hivi !” Ndipo nikaanza kuomba damu ya YESU inisafishe na kunitakasa na kunifanya niwe safi.Ghafla usingizi mzito ukanijia.Nilipofumbua macho , nikajikuta kwenye chumba ambacho nilikutana na YESU mara ya kwanza.Nikamuona YESUKRISTO anaingia.Akasema, “Mwanangu, nataka nikuonyeshe mambo mengi leo , kwa ajili ya siku za mwisho, Kwa kuwa hii ni mara yam wish kukutembelea wewe.Unatakiwa uwaambie kile ulichokiona kwa sababu haukuwa unawaambia watu wengi kuhusu yale niliyokuwa nakuonyesha wewe kipindi cha nyuma”.Bwana akaanza kulia kwa sababu ya haya.Nilikuwa na huzuni alipokuwa akilia kwa ajili ya uzembe wangu.Tulipotoka katika kile chumba , Bwana akaniambia mimi, “Mwanangu, njoo. Ngoja nikuonyeshe Hukumu Kuu.”Ndipo tukafika mbele ya enzi kubwa.

WAUAJI
Tulipofika mbele ya enzi kubwa nikamuona mwanamke pale akisema, “Nisamehe sana.” Bwana akaniambia mimi, “Muangalie yule mwanamke anaeye lia.Anajua hawezi kuingia mbinguni na ndio maana analia.”Nikamuuliza Bwana niambie mimi sababu ,kwa nini anahayo mawazo.Bwana akanijibu, “Mwanangu, muangalie.”Tazama nikaona historia ya maisha yake.Alikuwa mKristo alipokuwa duniani.Alikuwa akitafuta mtu wa kumuoa na Bwana akamwambia kuwa mvumilivu, lakini tamaa yake ya kuolewa ilikuwa kubwa mno.Haku subiri muda wa Bwana.Badala yake akamuua rafiki yake kwa sumu, rafiki yake akafariki(Mathayo 5:21).Ndipo akafanya mpango akaolewa na huyo mume wa rafiki yake.Baadae mume wake akagundua kuwa ndiye aliye husika kumuua mke wakeyaani mke wake wa kwanza.Mwanaume huyo naye akamuua yule mwanamke pia kwa sumu na ndiyo maana mwanamke yule alikuwa akilia sana mbele ya enzi ya hukumu( Luka 11:47).
Bwana akasema, “Nalimuonya asifanye hayo lakini hakunisikiliza mimi na sasa yuko analilia kusaidiwa na ili apate nafasi ya pili.Hio haiwezekani, ufalme wangu ni sehemu takatifu.Sio sehemu ya wauaji.Nilikuonya utubu lakini hukunisikiliza mimi.Umechelewa kwa wewe!”(Isaya 59:1-3).Bwana akamwambia, “Ondoka kwangu !” na nikaona kimbunga kikubwa kikambeba mpaka kuzimu !.(Mathayo 25:41,46).Usiue au usinyonge kwa sababu afanyaye hayo ni hatari kwa hukumu.Tubu sasa na uokolewe.Tukaondoka hiyo sehemu.
Tafadhali elewa hii:KRISTO anakuja tuu kwa ambao ni WAAMINIFU,WAKESHAO,WAANGALIFU.Sio tuu yatosha kuwa unasifa za kuingia mbinguni bali unatakiwa uendelee kila muda kuwa safi , tayari kwa ujio wake.Fanya maisha yako yaone kila siku tazamia maisha yako ya milele.Haitoshi kuonya na kuwaangalia wengine.
Unatakiwa pia ujiangalie na wewe mwenyewe na kuendelea mbele na wokovu wako kwa ajili ya roho yako.Popote unapofikiri ujio wake KRISTO na ukajawa na hofu au mashaka, hiyo inaonyesha kuna kitu hakiko sawa katika maisha yako na unatakiwa kumruhusu Roho mtakatifu kufanya kazi yake ndani yako.(Wafilipi 2:12-13).
Ni bora uende nae kwenye unyakuo kuliko kuachwa.Kama ukiachwa, mpinga KRISTO atakukejeli na kudharau Imani yako, utakuwa kwenye adhabu kubwa kwa ajili uliijua kweli na ukaiacha.Vipi kama ukifa kabla ya unyakuo? Unatakiwa uwe tayari kwa kurudi kwa Bwana.Kama ukifa na ukawa hata unadoa moja kwenye vazi lako utatupwa.[Note:Hii sentensi itasababisha kutoeleweka sana kwenye kanisa, 1 Yohana 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.]. Kama unaendelea kumtenda dhambi MUNGU na wafikiri bado una muda wakutubu unajidanganya mwenyewe.Ni bora utubu dhambi zako SASA kwa sababu kesho inaweza ikawa umechelewa kwa wewe. “USIUE ! ”
Bwana akanichukua mimi mpaka Kuzimu.Tukapita kwenye handaki lile lile ambalo tulipita mara ya kwanza na tukafika kuzimu.Kuzimu imejiongeza yenyewe kwa sababu shetani anafanya kazi kwa bidii. (Isaya 5:14)
MIAKA 250 AKIWA KUZIMU.
Nalimuona mtu akilia na kupiga kelele ndani ya Kuzimu ya moto akisema,”Uko hapa kuniokoa mimi?,Nipo hapakwa miaka 250.Nimekusubiri kuona kama nitampata mokozi, lakini nilishakata tamaa.Lakini sasa nimekuona wewe, nina mashaka kama uko hapa kuniokoa mimi.” Bwana akamwambia, “Nilituma watumishi wangu wengi kwako kukwambia utubu lakini hukunisikiliza mimi.Walikueleza ukweli kuhusu kuzimu ya moto lakini uliwaambia sio kweli; ni utani na ukadhani maisha yako ni mazuri tuu.Ulitumia muda wako tuu kwenye kunywa pombe, kwenda hoteli moja baada ya ingine, kufanya uzinzi (1 Wakorintho 6:9-11, Yakobo 4:4).Ulikuwa ukiumwa sana kiasi kutaka kufa , lakini sikuruhusu ufe ili uweze kutubu na kuokolewa lakini haukutaka kusikia jina langu likitajwa.Sasa ndio unakumbuka kumtafuta mokozi.Siwezi kukuokoa tena.Umechelewa” (Mithali 1:24-33)
Bwana YESU alikuwa akilia alipokuwa akiongea na huyo mtu kwa sababu hafurahii kifo cha mwenye dhambi.(Ezekieli 18:30-32).Hapa ulipo duniani unayo nafasi ya kutubu, lakini baada ya kufa, hakuna tena nafasi ya kutubu.YESUKRISTO ndiye pekee mwokozi wa wote wanao ishi lakini sio waliokufa.
Pumzi yako ni nafasi yako.(Muhubiri 12:1-8) tukatoka hiyo sehemu.
BINTI YA MTOTO WA MIAKA 15
Bwana akanichukua mpaka sehemu ingine ya kuzimu.Nikamuona mtoto akilia sana.Kulikuwa na funza na wadudu wengine wengi sana mwilini mwake.Anapomtoa mmoja ,funza wengine wengi wanakuja katika sehemu hiyo aliyomtoa.Alipotuona ,alikuwa akilia ili kupata msaada.Nikamuuliza sababu ya yeye kuwepo hapo.Akaniambia historia ya maisha yake,akasema “Nilipokuwa duniani, nilipenda kwenda kumbi za starehe kucheza(clubs to dance), [1 Timotheo 5:6].Wazazi wangu hawajawahi kunionya kwa sababu nilikuwa ndiye mtoto pekee walionizaa.Nilipenda kutembea na wavulana kufanya ngono nao.( 1 Wathesalonike 4:3-8)(Waefeso 5:3-6), nilisikia kuhusu kuzimu lakini sikutaka kuwasikiliza.Marafiki zangu wengi waliniambia nitubu nami nikawa nawachukia.Nilikuja kupata ujauzito na mama yangu akanikumbusha juu ya ndoto zangu za kuja kuwa mwanasheria.Kwa sababu ya hiyo niliamua kutoa ujauzito na kwenye hali ya kutoa nikafariki nami.Ndipo nimeishia hapa kuzimu na nipo hapa kwa miaka kumi sasanikiteswa na kuungua moto.Nikiondoa funza mmoja basi wengi zaidi huja.Tafadhali nisaidie.Sasa nipo tayari kutubu.” Nilipatwa na huzuni kubwa sana kusikia hayo.Bwana akamwambia , “Huwezi kutubu tena.Umechelewa.” Bwana alikuwa akilia kwa uchungu sana kwa ajili ya huyo mtoto lakini hakuweza kumuokoa.Yule mtoto alilia kwa kupiga makelele sana akisema, “Hapana ! hapana ! hapana! Hapana ! Nimoto sana nataka nife !”Lakini hakuweza kupata kufa.(Ufunuo 9:6) Nikamuomba Bwana anitoe huko kwa sababu sikuweza kuvumilia kuangalia mateso wanayopata.
Wazazi nisikilizeni,Mfundishe mtoto wako katika njia ya Bwana.Wafundishe Neno la MUNGU.Wasahihishe pale walipofanya makosa tofauti na maagizo ya Bwana.(Waefeso 6:1-4) (1 Yohana 2:1-6). Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).Tukatoka hiyo sehemu na kwenda sehemu ingine.
MTOTO WA KIKE WA MIAKA 14
Tunatakiwa tuwe makini na kujiondoa wenyewe kutoka kwenye dunia ya dhambi kwa sababu uvumbuzi mwingi unatuharibu sisi mbele za Bwana(Mhubiri 7:29).Bwana akanionyesha msichana akiwa Kuzimu, Mateso aliyokuwa akiyapata yalikuwa mazito na ya kutisha na likuwa akipiga makelele, “Inatosha ! inatosha! Inatosha ! Tafadhali nitoe !” Alikuwa akitumia mkono wake wa kushoto kuziba sikio lake kipindi akijichua(masturbating) na kitu cha moto sana kwa mkono wake wa kuume.{alikuwa akilazimishwa na mapepo kujiingiza hicho chuma cha moto ukeni na kukitoa mara zote }.Alikuwa akilia kwa uchungu lakini hakuacha kufanya vitendo hivyo.
Nikamuuliza yeye kwanini anafanya hivyo huko motoni nilipata historia ya maisha yake, “Nilikuwa na miaka 14 nilipofariki.Nilipokuwa duniani, nilipenda kusikiliza miziki ya kidunia.Na muda wowote nilipozisikia nilikuwa napatwa hisia za mapenzi ambazo zilinipelekea kujichua(masturbate).Niliwahi sikia kuhusu sehemu hii ya mateso, lakini siku amini kama iko kweli.Watumishi wengi wa MUNGU walinionya kuhusu miziki ya kidunia lakini niliwaita wapumbavu.Walinionya kwenye mahubiri yao kuwa kujichua/punyeto (masturbation) ni dhambi , lakini niliwaambia MUNGU ni mwenye rehema.Sasa nimeamini sio wajinga.Sababu ya kujishika sikio ni kwa sababu bado nazisikia nyimbo za kidunia na zinaniumiza sana.Nilikuwa najichua kutumia kitu nilipokuwa duniani ndiyo sababu ya kunitesa mimi motoni kwa jinsi hii.Tafadhali nisaidie mimi, siwezi kuacha na inaniumiza sana !”
Bwana akamwambia , “Siwezi kukusaidia wewe tena.Umefanya neema yangu kuwa si kitu ulipokuwa duniani, lakini mahali hapa,hakuna tena neema zaidi.Umechelewa kwa wewe kutubu !” Alikuwa akipiga kelele na kulia lakini Bwana alimwambia, “Siwezi kubadili maneno yangu.Yameandikwa tayari.Neno langu litasimama milele(Mathayo 24:35)(Mathayo 13:31) Wazazi,tafadhali mjali na uwatunze watoto wako(2 Wakorintho 12:14)(Waefeso 6:1).Kumbuka hasira ya MUNGU inakuja kwa watoto wasio watii.(Wakolosai 3:6)Tukatoka hapo na kwenda sehemu ingine.
MTU WA MIAKA 25
Bwana akanichukua mpaka sehemu ingine kuzimu ambapo niliona mtu akilia kwa sauti, “Nitasikia !, nitasikia ! tafadhali niko tayari kusikia !”Nikamuuliza kwa nini ndipo akasema, “Nilipokuwa duniani, nilipenda kufanya mapenzi na wasichana hasa wanaojiuza/makahaba.Rafiki yangu aliniambia nitubu na niokolewe lakini nikamjibu sitaki kusikia ujinga huo wa mahubiri-Niko tayari kwenda motoni,we niache kivyangu.Lakini sasa nipo tayari kusikia na kutubu.Tafadhali ! tafadhali nisaidie mimi ! ”
Bwana akamwambia, “Nilikupa neema ya kutosha mpaka ulipokufa umri wa miaka 25, lakini hukusikiliza maonyo yangu.Sasa unaomba kusikia.Umechelewa !,Hakuna mtu awezaye kukwambia kuhusu MIMI hapa kwa sababu kila mtu aliyepo hapa anatafuta njia ya kutoka humu.Kila roho ifikayo hapa haiwezi tena kutoka.Umechelewa(1 Wathesalonike 4:3).Mwili wako sio kwa ajili ya uasherati(1 Wakorintho 6:13).”
Mtu huyo akalia.Akimuomba Bwana amtoe hiyo sehemu ,sikuwa na muangalia tena na tukatoka hiyo sehemu ya kuzimu.
UFALME WA MUNGU
Bwana akanichukua na kunipeleka Mbinguni.Bwana YESUKRISTO asifiwe ! Baraka kwa Bwana Mungu wa Israel kutoka milele na milele ! Ameni na Ameni(Zaburi 41:13).Mbinguni ni pazuri sana.Ardhi yake ni kama kioo.Nilikuwa nafuraha na nilidhani kuwa nitabaki hapo na kuishi milele.Nikasikia sauti nzuri za malaika zikimsifu MUNGU(Zaburi 103:1-3).Bwana akasema, “Waambie watu wangu kuwa ufalme wangu upo kweli.Wamebarikiwa watakao urithi.”Kulikuwa na maua mengi mazuri(Zaburi 119:129-135).

MTI WA UZIMA
Bwana akanichukua mimi mpaka sehemu ambayo niliona Mti wa Uzima kwa mbali.Ulikuwa mzuri,unang`aa kama dhahabu(Ufunuo 22:2).Bwana akasema, “Nimeulinda Mti wa Uzima kwa ajili ya watu wangu.Waambie wamebarikiwa wale wazifanyazo na kutii amri zangu, hao ndio wenye haki kwenye Mti wa Uzima.”(Ufunuo 22:14) tukaendelea mbele.
WATOTO WALIOTOLEWA MIMBA DUNIANI
Bwana akanipeleka sehemu ingine mbinguni kulikuwa na ukumbi mkubwa na nikawaona watoto wengi wadogo waliojawa na utukufu wa MUNGU.Walikuwa wakimsifu MUNGU(Zaburi 86:11-13).Bwana akasema, “Hawa ni watoto ambao wanawake wanawatoa uja uzito wao(arboted) duniani.Wanamilikiwa nami na watakuwa katika ufalme wangu tukufu.”(Zaburi 89:1-2) Ndipo tukatoka hiyo sehemu.
MALAIKA GABRIEL AKATUTEMBELEA
Kipindi Bwana anaongea nami, tazama nikamuona malaika.Alikuwa mrefu na mzuri, amevaa taji katika kichwani.Bwana akaniambia, “Ni malaika Gabrieli.”Nilikuwa na furaha kukutana nae na Bwana akaniongoza kunichukua mimi kwenda sehemu mbali mbali Mbinguni ili niwezekuwaambia wengine nilichokiona.
MFALME DAUDI
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka kwenye jumba kubwa sana.Akasema, “Ni nyumba ya mfalme Daudi”Nikasema nataka kumuona mfalme Daudi uso kwa uso.Tukaenda ndani ya chumba chake na nikamuona mfalme Daudi akimsifu MUNGU kwa zaburri na kucheza(Zaburi 34:1-6).Nikamsalimu na akaniita jina langu, “Senayon, Karibu”.Nilishangazwa kwa kuwa alikuwa analijua jina langu.Akasema, “Senayon, haumsifu MUNGU.Hutaki kucheza kwa MUNGU.Unapomsifu MUNGU nakucheza kwa Ajili yake, neema Yake inakuwa karibu na wewe.”Nikamuuliza . “Umejuaje hayo?, je uliniona nilipokuwa duniani? Au unayajua tuu maisha yangu ya duniani ?”
Akawa anacheka na akasema, “Sijisemei kwa uwezo wangu”..Baadae nikagundua ni MUNGU anaongea na mimi kupitia yeye.Akanipa mimi kitabu kidogo akaniambia, “Kula !Kula hicho !.”Nilipokila hicho kitabu nikawa na kiu sana.Nikamwambia , “Nina kiu.Nina kiu.”Wakanipa mimi damu ya YESUKRISTO kuinywa.Nilipokunywa nilikuwa natetema kama vile nimepatwa na baridi kali kwa muda wa zaidi ya dakika tano.
Nilipokuwa natetema;Malaika Gabrieli na Mfalme Daudi walikuwa wamepiga magoti wakisema, “UTUKUFU KWA MUNGU!”(Zaburi 29:1-11).Nilipoacha kutetema baada ya muda ndipo mfalme Daudi akaniambia, “Sasa utamsifu MUNGU na kucheza kwake.Waambie watu wamsifu MUNGU na neema Yake itakuwa karibu nao.”
Malaika Gabrieli akasema, “Senayon,unavitu vingi vya kuona, Tuondoke.”Nikamwambia, “Hapana,sitaki kuondoka kumuacha Mfalme Daudi, tafadhali .”
Bali hakunisikia na tukaondoka pale kwa mfalme Daudi.
NYUMBA YA NABII ELIYA
Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye nyumba ingine kubwa na nzuri sana.Aliniambia ni ya nabii Eliya.Nilikuwa nafuraha iliyopitiliza.Nikamwambia, “Nataka nimuone!”Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwenye nyumba ambapo alitoka mvulana kijana mzuri sana na kuniambia “Senayon karibu !” Nilikuwa nafuraha sana kumuona yeye.Nikamwambia, “Ulikuwa shujaa sana duniani.Nimesoma kuhusu wewe kwenye Bibilia.”Naye akanijibu, “Kuna moto unawaka ndani ya moyo wako.Utakuwa shujaa kuliko mimi.”(2 Wakorintho10:4-5).Aliniambia mengi kuhusu mimi.Malaika Gabrieli akaniambia, “Senayon, tunatakiwa tutoke sasa hapa kwa sababu unavitu vingi vya kuona.”Tukatoka na kwenda kwenye nyumba ingine.
NYUMBA YA MTUME PAULO
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka sehemu ingine ambako kulikuwa na nyumba kubwa sana ,Nayo imetengenezwa kwa dhahabu, na imepambwa na mawe mazuri sana.Akaniambia, “Hii ni nyumba ya mtume Paulo.”Nikasema nataka nimwone yeye.Yeye amekuwa mfano wa kuigwa wakristo wengi.Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye hiyo nyumba, tazama nikamuona kijana mdogo amepumzika kwenye chumba kizuri. Senayon,” akesema , “Karibu sana.Ninayo furaha kukuona wewe.”Nilishangaa kuona anajua jina langu.Wanajua yote kwa sababu ya utukufu wa MUNGU uko pamoja nao.Na haikuwa muhimu mimi kuwa ambia jina langu kwa sababu wao walini jua jina langu kwa nguvu ya MUNGU.
Akaanza kuniambia historia yake kwenye kitabu cha Matendo(Matendo 8:1-4)(Matendo 9:1-31).Alipomaliza, aliniambia, “Nimtumia neema ambayo YESU amenipa mimi na sikuifanyia mchezo.”Akanipa kitabu kidogo na kuniambia, “Kula !, Kula hicho !.”Nilipokula sikuwa na kiu na kiukweli kilikuwa kitamu.Mtume Paulo akaniambia, “Sasa utahubiri injili na kufundisha shuhuda za YESUKRISTO.Utafundisha baadhi ya nyaraka(epistles) zangu ambazo bado sikuziandika.”(Warumi 8:35-39)Wote kwa pamoja Malaika Gabrieli na Mtume Paulo tulikuwa tukimsifu MUNGU.(Warumi 4:20-25)(2 Wakorintho 5:13-18).Ndipo tukamuacha .Nilikuwa na furaha.Mbingu imejawa na uzuri na utukufu wa MUNGU.(Ufunuo 21:18).
NYUMBA YA BABA ABRAHAMU
Ndipo Malaika Gabrieli akanichukua kwenda sehemu ingine Mbinguni ambako kulikuwa kuna nyumba nzuri iliyopambwa kwa maua na mawe mazuri.Akasema ni nyumba ya baba Abrahamu.Nikamuomba anipeleke nimuone baba Abrahamu.Nikafika pale na kumuona Baba Abrahamu, nikamwambia, “Baba wa imani, Baba wa imani.”Akaanza kunipa mimi ushauri kuhusu vitu vingi katika maisha yangu.Aliniambia, “Unatakiwa uwe na imani katika lolote unalomuomba BABA na kuwa mvumilivu katika hali yeyote ile”(Yeremia 33:3) (Mathayo 17:20) Imani ni hakika.(Mathayo 21:21-22)(Waebrania 11:1).Tukatoka hapo.
MALAIKA SABA(7) WAKIWA NA TARUMBETA NA WATANO(5) WAKICHEZA.
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka sehemu ingine ambako niliwaona malaika watano(5) wakicheza kwa furaha.Pia nikaona malaika saba(7) wakiwa na matarumbeta.Nikamuuliza Malaika Gabrieli aniambie kuhusu kazi ya hao malaika.Akaniambia kama mtu akimpa maisha yake YESUKRISTO duniani , ndipo wao hao malaika saba(7) hupuliza tarumbeta kama ishara kwa roho moja inapotubu.Malaika watano(5) wanakuwa wakicheza na mbingu nzima hushangilia.Pia kama roho ikiingia mbinguni wao pia husherehekea kwa hiyo roho.(Luka 15:7).Kuna furaha kubwa mbinguni juu ya mtu mmoja mwenye dhambi akitubu.(Luka 15:10).
WASHINDI
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye kumbi kubwa.Akanipa mimi upanga ili niunyanyue juu.Nilipounyanyua nikajikuta mwenyewe kwenye uwanja wa vita.Nikaona watu wasio hesabika wamefungwa chini.Kulikuwa na mapepo wengi waliowafunga hao watu.Baadhi yao bado wana silaha za vita.Zimeandikwa migongoni mwao , “WASHINDI”.Walikuwa wakiwapiga mapepo ili kuwaweka huru wale waliofungwa.Ambao wamewekwa huru huyo mtu hukimbia mpaka kwenye chumba kiitwacho “SEHEMU YA SIRI YA MUNGU ALIYE JUU” Nikamuuliza Malaika Gabrieli kunitafsiria akasema, “Washindi ni wakristo hai wa kweli(1 Yohana 5:4-5) nawale waliofungwa chini ni wadhambi.Wale mapepo wanawasimamia ili waendelee kukaa kifongoni ili waende kuzimu ya moto.(1 Petro 5:8-9)Kupambana na mapepo wale waliowafunga inamaana ‘kuhubiri kwa wadhambi na kuwaombea’.Chumba wanachokimbilia ni salama ambacho ni YESUKRISTO.(Mathayo 11:28-30) na hiyo ndiyo sababu kinaitwa ‘SEHEMU YA SIRI YA MUNGU ALIYE JUU’(Zaburi 91:1)”.Unatakiwa uombe sana ili MUNGU akufungue wewe kutoka kwenye pepo ambaye yupo kwenye hiyo kazi ya kupeleka watu kuzimu ya moto.
UTAKASO
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka sehemu nzuri sana mbinguni, iliyopambwa kwa dhahabu safi.Nayo ardhi ilikuwa nyeupe na safi kama glasi.Kulikuwa na maua mengi mazuri na mawe mazuri mengi.Niliona dhahabu zilizo pachikwa.Nikamwambia Malaika Gabrieli kwamba ntaka niguse dhahabu zilizopachikwa juu.Akanibeba juu kwenye mabega yake ili niweze kugusa.Nikamwambia malaika Gabrieli sitaki kuondoka hiyo.Nilikuwa nikilia kwafuraha kwasababu sehemu ile ilikuwa nzuri sana.(Ufunuo 21:18-19).
Malaika Gabrieli alisema, “Hapana.Unavitu vingi vya kuona hapa na ni muhimu sana uvione”.Nilizidi kumwomba nikimwambia,”tafadhali sitaki kuishi maisha yale ya dunia.tafadhali fanya jambo kuhuso hicho.”Malaika Gabrieli alisema, “Senayoni njoo twende zetu”.Tukatoka tukaenda kwenye bwawa la damu ya YESUKRISTO.Malaika Gabrieli akaniuliza, “Sanayon, unakumbuka hii sehemu ?”Nikamjibu, “Ndio.Niliona hili bwawa la damu kipindi cha kwanza na YESUKRISTO.”Malaika Gabrieli akasema, “Sawa uko sahihi.”Tulikuwa tukisimama pale kwa zaidi ya dakika tano lakini hakutoa neno hata moja kwangu.Mara, Nikaona mwanga wa Blue mzuri.Huo mwanga ukanichukua mpaka kwenye hilo bwawa la damu ambapo kulikuwa na mkono usio onekana ukaanza kuniosha ndani ya ziwa la damu.Iliniumiza mimi na nilikuwa nikilia.Nikamuomba Malaika Gabrieli kunitoa lakini alikuwa amepiga magoti akisema, “UTUKUFU UWE KWA MUNGU KUTOKA MILELE HADI MILELE, MFALME WA WAFALME NA UZURI WAKE MUNGU !”(Zaburi 95:1-6).

Tazama ! Nikaona mwili wangu duniani uko kitandani.Kitu fulani cheusi kilikuwa kikitoka nje ya mwili wangu.Nilishangaa kuona hicho kitu kuwa kilikuwa ndani yangu mimi(Zaburi 51:12-15).Kipindi ambapomkono usioonekana ulipomaliza kuniosha mimi, mwanga halisi ukanitoa nje ya bwawa la damu(Zaburi 51:8-11).Tazama 1nikasikia sauti kubwa ikisema, “Sasa utakumbuka kile ulichokiona na utaishi vile nitakavyo, wewe sio tena mtu wa kawaida kwa sababu nimekutakasa wewe.”Hiyo sauti ikaanza kuongea kuhusu kaka ambaye alinifundisha mimi kwenye njia za Bwana, Jina lake ni IJAWJAW EAMON MARK.Bwana akaniambia mengi kuhusu yeye kwamba atalitimiza agano lake naye na amempa vazi la ukamilifu.Sauti ikaniambia kuhusu watu wengi.Nikamuuliza Malaika Gabrieli, “Tafadhali, Nataka nione nani ninayemsikia sauti yake.”Malaika Gabrieli akajibu, “Sina nguvu ya kukupeleka pale , lakini nifuate mimi.”Tukatoka hiyo sehemu.
ENZI YA BABA MUNGU
Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwa YESUKRISTO.Akamuelezea YESUKRISTO kuwa nataka kumuona BABA na mwisho nikagundua kuwa ni BABA aliyekuwa aliyenichukua mimi kwenye bwawa la damu.YESU akatabasamu na kunishika mikono yangu akisema, “Wataka kumuona BABA ?”.Nikamjibu, “Ndio.”
Katika kwenda kumuona BABA ,tulipita katika ukumbi ambapo kulikuwa na malaika wengi.Mara wakapiga magoti na kusema, “UTUKUFU UWE KWA MUNGU !”(Zaburi 84:11).
Tulipotoka kwenye huo ukumbi ,na tazama nikaona mwanga mkali kwenye enzi.Ulikuwa mwanga kama moto unaowaka.Ingawa tulikuwa mbali sana kiasi cha maili nyingi lakini nilihisi nataka kuanguka.Sikuwa na nguvu ya kutembea kuelekea kwene enzi tena.Nikamuomba Bwana nikisema, “Tafadhali nirudishe.” Bwana YESUKRISTO akaniambia, “Huyo ni BABA,Hutaki kumuona TENA?”Nikamwambia , “Ndio,tafadhali, tafadhali, Nataka kufa.Siwezi kupumua zaidi.”YESU akatabasamu na kunirudisha kwa malaika Gabrieli.
VITABU MBELE YA MALAIKA.
Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwenye chumba kibwaa ambako kuna makundi ya malaika.baadhi walikuwa wakiandika majina na wengine wakifuta majina kutoka kwenye vitabu.Nilipewa nafasi ya kutembelea malaika wa nne(4) kati ya wengi.Nikamuliza malaika Gabrielii anielezee kila kitu akatabasamu.Malaika wa kwanza ni malaika anayehusika na kitabu cha uzima.Malaika Gabrieli alisema, “Hiki kitabuni kitabu ambacho kina majina ya wale walio okoka wapya na wale wakristo wakweli na walio okolewa.”(Ufunuo 3:5).
Nikauliza sababu ya malaikaa kufuta baadhi ya majina na kuandika majina mengine.Naye akanijibu, “Wale walioacha wokovu waliorudi nyuma.”(Ufunuo 2:4-5).Nikamuuliza tena, “Unamaanisha majina yao yanfutwa milele kutoka kwenye Kitabu cha Uzima ?.”Akatabasamu na kusema, “HAPANA.Hiki ni kitabu kitakatifu na hakiwezi kuwa na majina ya wenye dhambi.”Nikamwambia, “Niambie hayo majina yanayofutwa yanawekwa wapi ?”.Akanichukua mpaka kwa malaika mwingine ambaye naye alikuwa akiandika na kufuta baadhi ya majina.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ndio kitabu cha waliorudi nyuma katika wokovu na kina majina ya wote walio iacha njia ya Bwana.Sababu ya malaika kufuta baadhi ya majina ni kwa sababu ya wale waliokuwa wamerudi nyuma na kuiacha njia ya Bwana wamemrudia MUNGU,Majina yao huandikwa tena katika kitabu cha Uzima.(Ufunuo 20:15)”Majina aliyokuwa akiyafuta ni majina ya waliorudi nyuma katika wokovu (Yeremia 3:22).Akanichukua na kunipeleka kwa malaika mwingine aliye kuwa akifanya kazi kwa bidii sana.Hata hivyo alikuwa akiandika tuu majina, nasio kuyafuta.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ni kitabu chenye majina ya wote ambao huishia Kuzimu ya moto kila siku.Kitaitwa kitabu cha hukumu(The condemnation Book).’”Malaika Gabrieli aliniambia, “Majina yanaandikwa ni yale ya ambao walikufa bila kuwa na YESUKRISTO maishani mwao.”(Ufunuo 20:12).Tukatoka hapo na kwenda sehemu ingine.
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka kwa malaika mwingine ambaye alikuwa anaandika tuu majina bali hayafuti.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ni kitabu chenye majina ya wale wanaotoa zaka zao.”(Malaki 3:8-12).Malaika alikuwa akiandika majina na kupiga kelele akisema, “Amelipa ! amelipa !” Na mara nikamuona malaika akaja pale.Akafungua chumba kizuri na katika kile chumba kulikuwa kuna vitu vingi vizuri vya dhahabu kwenye maboksi.Malaika akaingia katika hicho chumba na kuchukua moja ya vitu vya vyahabu nzuri kuenda zake.Nikamuuliza Malaika Gabrieli aniambie nini kilichokuwa ndani ya boksi ambacho malaika amekichukua na kuenda nacho.Malaika Gabrieli akanijibu, “Ndio.Ni baraka kubwa kutoka kwa Bwana kwa yule aliyetoa fungu la kumi(zaka) kwa uaminifu.”(Obadia 1:15).Tukatoka hiyo ssehemu.
DAKIKA TANO (5) ZAIDI.
Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye ukumbi ambao kulikuwa na malaika wengi wakisema, “Bwana ni muda.Acha watu wetu waje.”Nikamuona Bwana YESUKRISTO akilia kama mtoto akisema, “Acha tuwape DAKIKA TANO ZAIDI !” Baada ya hapo Malaika Gabrieli alinionyesha mimi maandalizi yote kwa ajili ya unyakuo yako tayari.Kila kitu kii tayari Mbinguni na YESUKRISTO anasubiri kuambiwa NENDA kutoka kwa BABA MUNGU(2 Wathesalonike 5:2-6).Tena Malaika Gabrieli alinipeleka kwenye ukumbi mwingine ambako kulikuwa na mavazi mazuri mengi sana.Yalikuwa yamepambwa na uzuri,kushangaza na utukufu kwa dhahabu safi.Nilimuuliza malaika Gabrieli, “Ni watu gani wataomiliki hayo mavazi mazuri !?” Naye akanijibu, “Haya ni mavazi ya Wakristo watayavaa kwa ajili ya ndoa ya mwanakondoo.”(Ufunuo 19:7-9)
Nilimuuliza Malaika Gabrieli anionyeshe mimi vazi langu.Naye alilionyesha moja ya vazi na kusema , “Hili vazi ni lako.” Nilikuwa na furaha ya ajabu na ndani yangu nikijisemea, “Sitaenda kuzimu ya moto.” na tazama nikasikia sauti kubwa ikisema, “TAZAMA NAKUJA HARAKA; SHIKA SANA ULICHO NACHO USITAKE MTU YEYOTE AKUNYANG’ANYE TAJI YAKO !”(Ufunuo 3:11).Niliogopa sana niliposikia hiyo sauti kwa sababu inamaanisha “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.”(1 Wakorintho 10:12) (1 Wakorintho 9:24-27).Tukatoka sehemu hiyo na kwenda sehemu ingine.

UTEMBELEO WA MALAIKA URIELI
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye nyumba nzuri sana .Tulipofika pale tuka kaa kwenye kiti.Mara ghafla nikasikia kiashiria kikubwa Mbinguni na malaika akapiga magoti na kuanza kusema, “Utukufu uwe kwa MUNGU,Yeye anastahili kupokea utukufu wote.AMENI !” Malaika Gabrieli akaniambia mimi niangalie.Tazama !nkaona malaika akikimbia na kupiga kelele akisema, “Ushindi ! Ushindi ! Ushindi !” Malaika akakimbia kwa YESU nakusema, “AMEINGIA ! AMEINGIA ! ”Nikamuona mtu akija kwenye Ufalme wa Mungu.Malaika akamkimbilia kumchukua kumuingiza ndani kwa sababu alikuwa tayari amechoka.Afadhali ameweza kuingia mbinguni ! Malaika Gabrieli akasema, “Malaika anayepiga kelele ‘USHINDI ! USHINDI !’ alikuwa ni malaika mlinzi wa yule mtu aliyeingia Mbinguni.”Mbingu yote ilijawa na furaha kwa sababu ya mtu aliyefanikiwa kuingia.Malaika Gabrieli akatoka nje ya chumba na kuniambia, “Senayon, unakaribishwa !”na alinikabidhi kwa Malaika Urieli ili kunionyesha baadhi ya vitu Mbinguni.
Malaika Urieli akanichukua mpaka sehemu ingine na kuniambia, “ANGALIA! .ANGALIA !.”Nikaona Ufalme wa Shetani.Shetani alikuwa akiwapa mapepo amri ili kuvamia Wakristo kwa sababu ya yule mtu aliyefanikiwa kuingia mbinguni.Shetani alisema, “Msiruhusu yeyote yule kukwepa mitego yetu na uvumbuzi wetu.Lazima tuzipate roho zao !.”Nikaona mapepo , yakikimbia na kasi kubwa kwa sababu roho moja imefanikiwa kuingia mbinguni.
Malaika Urieli alinichukua mimi kwenda sehemu na kusema, “Angalia duniani.”NIkaona dunia imeonekana ndogo sana na chafu sana kama sehemu ya kuweka uchafu.Mara ghafla ! nikaona mishale mingi ikaanza kuanguka duniani.Nikamuona Mtu Mzee aliyepokea mishale michache.Baadhi ya mishale hiyo iliangukia watu wengine waliopo duniani.Nikaona moto ukija duniani lakini yule Mtu Mzee akausimamisha ule moto na kuurudisha ulipotoka.Nikamuuliza Malaika Urieli, “Tafadhali nitafsirie hiki kwa sababu ni maajabu sana kwangu.”Malaika Urieli akasema, “Mtu Mzee uliyemuona ni YESUKRISTO, na mishale michache iliyompata katika mwili wake ilikuwa ni mishale ambayo shetani anatuma kinyume na watoto wa MUNGU.(Zaburi 91:1-7).Mishale mingine iliyo anguka kwenye dunia ilikuwa ni mishale kutoka kwa shetani kwa watenda dhambi.(Zaburi 92:7) Moto uliouona ni mipango ya shetani ya kuharibu dunia lakini Kristo hakuruhusu hicho kitokee.”(Isaya 60:1-2)

MALAIKA AKIWA NA TAARIFA MBAYA ZA MTU
Malaika Urieli akanichukua mpaka sehemu ambayo niliona malaika wengi wakitoa taarifa mbaya kwa Bwana.Malaika wa kwanza alikuja na kumwambia Bwana, “Mwishowe , Amepoteza roho yake.Nilimuonya lakini hakunisikiliza mimi.”(Marko 8:36).
Malaika wa pili akamwambia Bwana, “Bwana, yule mtu amefanya uzinzi.Nilimuonya asifanye lakini akamruhusu shetani kuutumikisha moyo wake.”Bwana akamuuliza malaika, “Ulimwambia akiri kosa lake ?”Malaika akajibu , “Ndio, lakini kila akitaka kukiri yule mwanamke aliyefanya naye uzinzi anajitokeza na huyu hushindwa kukiri tena anapomuona yule mwanamke aliyefanya naye uzinzi.”Bwana anamwambia, “Endelea kumwambia akiri na kuacha (dhambi zake )naye ataokolewa.”(Mithali 28:13)
Malaika akajibu, “Sawa BWANA.” Na akaondoka zake. 
Malaika wa tatu akaja naye alikuwa malaika mlinzi wa mchungaji W.F Kumuyi.Malaika akamwambia Bwana, “Bwana, shetani ametuma baadhi ya watu waovu kwenye huduma ya DEEPER CHRISTIAN LIFE (Kanisa la Mchungaji W.F Kumuyi), kifanyike nini ?” Bwana akamjibu, “Mwambie Kumuyi, mtumishi wangu awe muombaji na nitampa USHINDI.”Malaika asema, “Haya BWANA.”Akaenda zake(1 wathesalonike 5:17).Malaika wengi walikuwa wakija pale.Kitu kilichokuwa nikikisikia sana ni, “Mwishowe, amepoteza roho yake.”
                                                        NYUMBA YA MCHUNGAJI E.A ADEBOYEKipindi malaika aliyekuwa akitoa taarifa kuhusu mchungaji W.F.Kumuyi alipo ondoka, Nilimuuliza Bwana kama mchungaji E.A.Adeboye ni mtumishi wake au sio.Bwana akasema, “Ndio mchungaji Adeboye ni mtumishi wangu na mimi ndiye mwanzilishi wa REDEEMED CHRISTIAN CHURCH.Angalia ile nyumba.” Nikaangalia na kuona nyumba kubwa mbinguni.Bwana akasema, “Hio ndiyo nyumba ya mchungaji Adeboye , mtumishi wangu.”
Nilipiga kelele, “Hii nyumba kubwa ! unahakika atakuja kuingia ?” Bwana akasema, “Ndio kama akiendelea kufanya mapenzi Yangu na kuzidi kuvuna watu kwa Ufalme Wangu.”(Mathayo 28: 19-20).
Nikamuuliza Bwana anionyeshe nyumba yangu.Bwana akatabasamu na kusema, “Iangalie mwanangu.” Nikaona nyumba ndogo nzuri.Bwana akaniambia ni yangu.Nikacheka na kusema, “Lakini sijawahi lipa fungu la kumi.” Bwana akatabasamu na akasema, “Sio zaka pekee zinazo jenga nyumba hapa, lakini, pia unapowahubiria na kuwa ambia watu kuhusu Mimi na wokovu, hiyo ndiyo thawabu inayojenga nyumba huku mbinguni; unaponiletea watu hiyo nayo ni thawabu kubwa ya kujenga nyumba yako mbinguni.pia unapo waombea watu hiyo ni thawabu ingine kubwa inayopelekea kujenga nyumba.Unapotenda vyema kwa wengine nayo ni thawabu kubwa kwa wewe kujenga nyumba mbinguni.Kama watu wanataka kujenga nyumba hapa wanatakiwa watii kile nilichokueleza wewe.Hivyo, unayo hii nyumba kwa sababu umekuwa ukichukua muda mwingi kuomba kwa ajili ya wenginehaswa katika kundi Nililolianzisha:THE OVERCOMERS GROUP, na pia kwa sababu unawaambia watu kuhusu Mimi na kuleta watu Kwangu.”(Marko 1:15)
Malaika Urieli akanichukua mpaka kwa malaika Gabrieli ambaye alinionyesha mimi jinsi hizi shuhuda zitavyokuwa kubwa duniani.Aliniambia mambo mengi ya siri kuhusu mimi.Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye kumbi kubwa na tazama , Nikaona malaika wengi wakiimba sifa kwa Bwana.Walicheza vyombo vingi kulitukuza jina la MUNGU aliye JUU.Nikajiunga nao nikimsifu Bwana.Nyimbo zilikuwa zakuvutia.Sauti za malaika zilikuwa nzuri sana.Kulikuwa hakuna aibu mbinguni.Malaika walikuwa wakicheza.Wengine walikuwa wakiruka mara ghafla wakapiga magoti na kuanza kusema, “Utukufu uwe kwa MUNGU !”(Ufunuo 5:9-14) Nilikuwa na furaha kuwa kati yao nilipenda niwe pale milele, kumsifu MUNGU wa Utukufu(Ufunuo 4:11).Tukatoka.
Malaika Gabrieli akanichukua kunirudisha mpaka kwa Bwana Yesukristo.Bwana Yesukristo akaniambia, “Mwanangu, niambie mimi, nini unachotaka kuona hapa au kipi unachotaka mimi nikuonyeshe ?” Nikajibu, “YESUKRISTO , mapenzi yako yatimizwe kwa sababu unajua vyote ninavyotaka kuviona hapa.”
Akanichukua mimi na huku akitabasamu akisema, “Mwanangu,Njoo.
MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU
Bwana akanichukua mpaka sehemu moja mbinguni kuna kioo kikubwa sana.Kwenye kioo hiko kimeandikwa matunda tisa(9) ya Roho mtakatifu.Bwana akaniambia, “Matunda yako tisa(9) ya Roho mtakatifu yanatakiwa yawe yamekamilika.Kama tuu moja limekosekana, huyo mtu hawezi kuja kwenye ufalme wa MUNGU kwa sababu viwango vyangu vya mbinguni vinasimama milele.”(Wagalatia 5:22-23)
UNYAKUO
Ujio wake Bwana YESUKRISTO,kutokea kwa YESUKRISTO katika anga kupokea Utukufu wake kwa tumaini kuu la wote wamwaminio.Ni mara na yeyote asiyenyakuliwa na KRISTO ataporudi ata “aachwa”(Mathayo 24:42-44).
Bwana akasema, “Mwanangu,njoo nikuonyeshe jinsi unyakuo utavyokua.Angalia kwa umakini sana.” Tazama ! nikaona kanisa kubwa duniani.Lina zaidi ya watu milioni tatu (3) wakiwa wapo kanisani, kulikuwa na kitu kama kongamano.Kufumba na kufumbua unyakuo ukatokea na tuu wanafunzi watatu (3) kati ya milioni tatu (3) wakaondoka na Bwana YESUKRISTO.Wengine wote wakaachwa ! (Marko 13:30-37).
Nikamuona muanzilishi wa hilo kanisa naye alikuwa ameahwa na alipiga magoti pale pale na kusema, “Oh Bwana, nina makanisa 200 na sikuwahi hubiri kweli, lakini sasa nimeachwa ,tafadhali nisamehe mimi.” Bwana akasema, “Umechelewa(unaweza ukatengeneza) tuu kama utavumilia na kukataa kupokea alama ya mnyama.”(Ufunuo 13:16-18) (Ufunuo 19:20).
Kama wewe ni mchungaji au muhudumu ambaye huihubiri kweli, kumbuka huwezi jitetea mwenyewe mbele ya MUNGU(1 Petro 5:2-4).
Nikaona shule ambapo mkuu wa shule alikuwa akihutubia wanafunzi.Mara ghafla ,mkuu wa hiyo shule akanyakuliwa na wanafunzi wakabaki (1 Petro 4:7).Nikaona mwalimu alikuwa akifundisha wanafunzi, mara nikaona wanafunzi watatu(3) na mwalimu wamenyakuliwa, wanafunzi wengine wote wamebaki.(2 Petro 3:9-14).
Nilimuona mama mjamzito alikuwa akienda zake nyumbani .Ujauzito wake ukapotea kwa sababu mtoto alinyakuliwa lakini mwanamke aliachwa(Mathayo 24:40-51). Kulikuwa na huzuni kubwa dunia nzima (Mathayo 25:31-46).Wakristo wengi walikuwa wameachwa kwa sababu ya dhana zao juu ya dhambi aliozigundua mwanadamu(Zaburi 106:39-40).
Bwana akasema, “Hivyo ndivyo unyakuo utakavyotokea.Ni muda wa kwenda duniani .YEYE ALIYE NA SIKIO NA ASIKIE ROHO WA BWANA AAMBIACHO KANISA.KESHENI NA KUOMBA ! ” Ndipo Bwana akanirudisha duniani.
OMBI LA MSAMAHA
Kama uko tayari kumpa maisha yako YESUKRISTO omba sala ifuatayo:
Unirehemu mimi, MUNGU kutokana na uzuri wa upendo wako; kutokana na neema zako ondoa maanguko yangu.Nioshe kutoka kwenye maovu yangu na unisafi dhambi zangu.Ninatambua makosa yangu na dhambi zangu,tazama nilizaliwa katika uovu na mama yangu alichukua ujauzito wangu dhambini.Tazama natamani kweli ndani yangu na maficho yangu yajue hekima yako.
Nifanye nisikie furaha na amani yako ;Mifupa iliyovunjika iingiwe furaha yako na urejesho wako.Ficha uso wangu kutoka kwenye dhambi, ondoa kila ovu langu na uniumbie moyo safi,Oh Bwana ; na uweke tena sawa roho yangu.
Usiniondoe kutoka kwenye uwepo wako na usimchukue Roho wako mtakatifu kutoka kwangu.Nirejeshe furaha ya wokovu na kuniinua nikiwa na uhuru wako rohoni mwangu.(Zaburi 51).Andika majina yangu kwenye kitabu cha Uzima.Na iwe furaha kuu Mbinguni juu ya wokovu wa roho yangu katika Jina la YESUKRISTO,Nimeomba.Amen !.
Tafadhali nakuomba SHARE kwa mwenzio; na kwa shuhuda nyingi zaidi tembelea; www.jasirimbarikiwa.blogspot.com .SHARE kwa wengine nao.

SIRI ZA MBINGUNI NA KUZIMU-sehemu ya kwanza na Emmanueli Senayon

Jina langu ninaitwa Emmanueli Senayon;Nina umri wa miaka 18, kutokea nchini Naijeria.

NIMEKUTANA NA YESUKRISTO.
Mwaka 2012 mwezi Novemba, Nilikuwa mgonjwa sana na wazazi wangu wakanichukua na kunipeleka hospitalini.Daktari akasema damu yangu i chini sana na nilikuwa na kifua kikuu{TB}(tuberculosis).
Ilikuwa taarifa mbaya sana hasa kwa wazazi wangu  kwa kuwa hawakuweza kumudu gharama za kunihudumia pale hospitalini, hivyo wakanichukua na kunirudisha nyumbani bila matumaini yeyote.
Nilipokuwa kwenye kitanda nikipumzika, Nikaanza kuhisi kitu cha ajabu na mwili wangu wote ukazidi kuwa dhaifu isiyokuwa kawaida.Nikajikuta mwenyewe niko nje ya mwili katika chumba cheupe haswaa.YESUKRISTO akanitokea, Sura yake ilikuwa inang`aa na alikuwa mzuri sana lakini nikagundua hakuwa na furaha.Akanishika mkono wangu na kunichukua mimi hadi nje ya chumba hicho na nikajikuta nimesimama mbele ya enzi kubwa.

Nikamwona Baba MUNGU katika enzi yake.Sikuweza kuona sura yake ,mwili wake ulikuwa kama moto uwakao, amejaa nguvu na utukufu.Nikaona makundi ya malaika wakiwa na mavazi meupe mbele ya enzi, na walijaa utukufu.Wale malaika wamebeba vitabu kwenye mikono yao.Nikaona watu wasiohesabika mbele ya enzi[UFUNUO 20:11] nao walikuwa wakienda mmoja baada ya mwingine kupokea hukumu yao na kila mtu alipofika mbele ya enzi, malaika walifungua vitabu mikononi mwao na MUNGU ndiye anayehukumu huyo mtu.

Watu wengi waliosimama wakisikia MUNGU akiwaambia “ONDOKA KWANGU”.
MUNGU aliwahukumu na hasira kali na sauti yake ikasikika kwa mlio mkuu [EZEKIELI 43:8].Pale MUNGU anaposema “ONDOKA KWANGU”,Kulikuwa na kimbunga kikubwa kinachomzoa mtu huyo na kumtoa hapo.[MATHAYO 25:41].Watu wote waliokuwa mbele ya enzi walikuwa wakiogopa sana kusimama mbele za MUNGU.Wao malaika hawaiti jina la mtu yeyote lakini kila mtu anajua inapofikia zamu yake ya kupokea hukumu[2 wakorintho 5:10].Yeyote aliyefanya uovu alitwaliwa na kimbunga kwenda kwenye adhabu isiyo isha[Mathayo 25:46].

Kwa kuwa uko hai ,Bado una neema ya dhahabu kutubu kutoka kwenye dhambi zake na kuaha uovu wako.Hasira ya MUNGU ni kama moto uwakao[SEFANIA 2:1-3] na dunia ni bonde  la kufanya maamuzi[YOELI 3:14].Uamuzi wako uache uwe KRISTO;kabidhi maisha yako kwa YESUKRISTO na kuipuka hasira ya MUNGU.Haijalishi dhambi gani ulioifanya, YESU atakusamehe yote yote[HOSEA 14:4], [HABAKKUKI 2:13].

YESUKRISTO AKANIPELEKA KUZIMU YA MOTO
Ndipo YESUKRISTO akanitoa hapo na kunipeleka kuzimu iwakayo moto.Kuelekea kuzimu tulipitia handaki ambapo tulipotoka tuu kwenye hilo handaki tukawa tumefika sehemu ambayo ina giza kweli kweli.Ilikuwa ni sehemu yenye giza kubwa na sauti za kutisha za vilio na kutisha.

Nikauliza, ‘Bwana tuko wapi ?’ naye akasema, “huu ni ufalme wa shetani, kuzimu ya moto”.Kuzimu inatisha sana kuna giza zito.Niliona mapepo wengi ;walikuwa wakubwa na wabaya sana.Mapepo hayo yalikuwa yanafanya kazi kwa kasi sana bila ya kuchoka.[1 PETRO 5:8].Bwana akaniambia mimi , “wanapanga jinsi ya kuleta watu sehemu hii”.

Kuzimu ya moto iko kama ziwa, na kila mmoja ana sehemu yake katika kitengo tofauti tofauti.Kuna watu wengi kuzimu wako kwenye moto wanaomba nafasi ya sekunde, lakini hakuna kibali na haiwezekani.[MIKA 3:4].

Kitengo cha kwanza Bwana alichonionyesha nisehemu ambayo ni ya wachungaji walioikosa mbingu.Niliona wachungaji wengi wako kuzimu katika mashimo yao kuna kitu kamaubao watangazo ambako umeandikwa jina la huyo mchungaji,jina la hilo kanisa alilokuwa akilichunga jumuisha na sababu iliyopeleka kuzimu.Kila mchungaji alikuwa ana mapepo yaliyokuwa yanamtesa.Walikuwa wakilia na kuomba rehema kwa YESU, lakini YESU alilia na kuwaambia “nilipokuwa nikiwaonya ninyi hamkunisikiliza na sasa mpo katika sehemu hii.siwajui ninyi !”.[Mithali 1:24-31].
Ndipo Bwana akaniambia, “kuzimu imejiongeza na hakuna ajaye huku atayeweza kurudi tena”.[Mithali 2:19],[ Isaya 4:14].
Niliona kitu kikubwa na cha kushangaza sana ! “Watu wangu,tutawezaje kuikwepa kuzimu kama tukidharau wokovu mkuu?” [Waebrania 2:3].

MCHUNGAJI OSHOFFA
Nilimuona mtu akiwaka moto kuzimu, mapepo walikuwa wakimtesa kwa silaha zao na vifaa vyao.Mtu huyo alikuwa akiomba rehema na alilia kwa uchungu sana.

Nikamuuliza Bwana, “Huyu ni nani?”.Bwana akaniambia, “ni mchungaji oshoffa, muanzilishi wa makanisa ya ‘CELESTIA KANISA LA KRISTO’,KANISA LA VAZI JEUPE”.Bwana akaniambia siri ya mtu huyu; “alijiwekea agano na shetani kuwavuta watu kwa mafundisho ya giza, uponyaji kutumia mishushumaa, marashi na sabuni.Huwaambia watu watumie hivyo vitu na waende kuoga kwenye mito, na kuwadanganya kwa nguvu ya shetani”.

Bwana aliongeza “yeye alifundisha mafundisho ya uongo ili tuu ajulikane kama mtu mkubwa wa Mungu”.[Efeso 4:14] Bwana alisema, “NILIMUONYA YEYE LAKINI ALIKATAA”.
Bwana YESU alimwambia mtu huyu “SIKUJUI WEWE”,YESU alilia kama mtoto; huyu mtu alikataa msalaba wa KRISTO tuu kwa sababu ya umaarufu.Sasa yupo kuzimu akiomba rehema kwa Bwana kutokana na uovu aliokuwa nao.[ 2 Timotheo 2:12,19].
Nataka nikueleweshe kuwa haijalishi hali yeyote usiamini au mafundisho tofauti na kwa hayo “Hutaweza kujitetea mbele za Bwana”.[Tito 1:16],[Yeremia 23:24].Watu wengi wapo kuzimu kutokana na mafundisho yao.[Wafilipi 2:5].

YUDA ISKARIOTE.
Nikamuona mtu mwingine akiwa kuzimu;,mapepo yamemfanya alale juu ya kitu kama chuma ambayo ni mfano wa meza,Walikuwa wakimuumiza na aina za vifaa mbali mbali.Nikaona chuma kikubwa ambacho pepo anakitumia kumtesea na kukitumbukiza kupitia kwenye tumbo la huyo mtu.Kilikuwa kinapita kwenye tumbo na huyo mtu alikuwa akilia kwa uchungu sana.

Mara akatokea pepo ambaye alikuwa ana kisu kikubwa cha chuma mkononi mwake, akakata katikati ya kichwa cha mtu huyo, mapepo kumi walikusanyika ,kulikuwa na funza wengi na n`nge.Walikuwa wakiingilia kichwa cha mtu huyu na baadae kurejea tena.Mtu huyo alikuwa akilia zaidi kama upepo wa ziwa.Iliniuma mimi sana kuona hayo.Bwana akaniambia, “HUYO NI MMOJA WA WANAFUNZI WANGU, YUDA ISKARIOTE”.

Nikauliza mapepo sababu ya kumtesa  yeye kiasi hicho,na pepo akaniambia “Kama asinge mfichua mtu huyu wa Nuru(YESUKRISTO) kwa watu ili wamuue , basi kazi ya wokovu isingedhihirika”.Mapepo yalikuwa yakipiga kelele yakimwambia, “Kwa nini umemsaliti?”,aliendelea kumtesa.[Mathayo 10:4],[Mathayo 20:18].

Unatakiwa uwe makini kwa kile unachokifanya usimsaliti YESUKRISTO ! “Ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu !”.[Mathayo 26:24].Wale ambao wamejifunza kutoka kwa Bwana na kuelewa Neno la MUNGU wanatakiwa waruhusu “neno la KRISTO kukaa ndani yao”.[Wakolosai 3:16-17].Kwa yule ambaye anarudi nyuma,Bwana anasema “ROHO YANGU HAINA FURAHA NAYE.”.[Waebrania 10:38].Kama wewe ni mtumishi wa MUNGU jichunguze mwenyewe na utoe kikwazo katika maisha yako.---MOTO WA KUZIMU UNATISHA KWELI.

MFALME AHABU NA YEZEBELI.
Bwana alinionyesha mtu aliyekuwa amekaa amefungwa kwenye kiti cha chuma.Hicho kiti kilikuwa cha moto sana na chekundu kama kaa.Ingawa alikuwa akipiga yowe kwa uchungu sana badomapepo yaliendelea kumtesa na mikuki wakiwa na hasira kali.Mtu huyo akaanza kumuomba YESU nafasi yakutoka kwenye moto.Nikajiuliza huyu anaweza kuwa nani, Bwana alijua mawazo yangu na kuniambia mimi “NI MFALME AHABU”.
Ghafla nikamuona mwanamke ambae mapepo yalikuwa yakimtesa sana.Walikuwa wakimpiga na kwa mikuki alipokuwa akilia na kupiga  kelele.Bwana akaniambia, “HUYO NI YEZEBELI,NABII WA UONGO AMBAO ALIKUWA AKIWASHAWISHI WATU KUMTENDA DHAMBI MUNGU”.[Ufunuo 2:20].
Unabidi uwe makini kwa sababu kuna manabii wengi wa uongo,  wanaofundisha mafundisho potofu ambao kwa hayo mafundisho wajiwekea utajiri wao wenyewe.Waanajiita wenyewe waokozi na kudanganya watu kwa uongo wa shetani.KAMA WAKIKATAA KUTUBU,WATAKUWA NA NAFASI YAO KUZIMU YA MOTO.[ 2Wathesalonike 1:8]

MTOTO WA MIAKA SITA(6).
Nilimuona mtoto mdogo akiwa kuzimu,mapepo yalikuwa yakimtesa huyo mtoto kwa mikuki,Huyo mtoto alipotuona sisi alilia na kuomba msaada ili atolewe motoni, lakini Bwana akasema “MIMI SIO MUNGU WA WASIOTII”.Huyo mtoto alikuwa jeuri sana alipokuwa duniani, alikuwa akisumbua wazazi wake kipindi mchungaji anapotoa Neno.Wazazi wake walipomsahihisha aliwafokea.Aliumwana na alipokufa ,sasa yupo kuzimu milele.Bwana akasema,”HAMNA MTOTO ASIYETII ATAKAYERITHI UFALME WA MUNGU”.[Waefeso 6:1-2].

REVEREND PATRICK R. COONEY
Bwana alinionyesha mimi mtu mmoja aliyekuwa kuzimu,alikuwa akifahamika kama PATRICK COONEY alipokuwa hapa duniani.Mapepo yalikuwa yanakata kata mwili wake kwa misumeno, mateso yalikuwa makali sana.Walikuwa wakimkejeli na kumcheka na kusa pekee alilokuwa nalo ni kutokana na mafundisho yake.Alipelekwa kuzimu kwa sababu ya kuinamia mara kwa mara [inayosemekana] SURA YA MTAKATIFU MARIA.[Kutoka 20:3-4].

Ni huzuni sana watu wengi wanaishia milele kuzimu kutokana na mambo kama haya.Nilikuwa na huzuni kubwa na Bwana akaniambia “KAMA KWELI UNAHUZUNI, UTAWAAMBIA ULICHOKIONA”.
Unatakiwa ufungue moyo wako na kusema “hapana” juu ya uongo wa shetani.Tunatakiwa tutoke kwenye mafundisho yenye kumfanya KRISTO atukatae sisi.[2 Wakorintho 6:14-18], USIINAMIE KUABUDU  MTAKATIFU MARIA TENA.

KITENGO CHA WENYE KUJIWEKA KIKAHABA.
Niliwaona watu wengi katika hiki kitengo,Bwana akanionyesha picha zo walivyokuwa duniani nao kwa sura walikuwa wazuri lakini sasa wapo kuzimu ni wabaya sana.Mapepo yalikuwa yakiwatesa kwa kutumia mikuki kuwapiga na kuwabana sehemu zao za siri, walikuwa wakilia na kutafuta wafe lakini ilishindikana.[Ufunuo 9:6]
YESU alilia, nao watu walikuwa wanamuomba BWANA awatoe, nao walikuwa wakiapa katika maisha yao watafanya mapenzi YAKE kama wakitolewa kwenye moto, Lakini Bwana hachezi au kutania na NENO lililotoka kwenye kinywa chake[Wakolosai 3:5-6].Imeshaandikwa kwenye NENO kuwa yeyote anayetenda uovu hata urithi ufalme wa MUNGU[1Wakorintho 6:9-10].

KITENGO CHA WALIOSIKIA KUHUSU KRISTO NA WAKAKATAA KUTUBU.
Kuna watu wengi kuzimu ambao walisikia habari za wokovu,lakini walikataa kutubu dhambi zao.Nao walidhani watakuja mbinguni kwa kazi za mili na damu yao, Tofauti na hayo sasa wameishia kuzimu inayowaka milele[ 1Wakorintho 15:50].

Walikuwa wakilia, lakini Bwana alisema “walipewa neema kubwa ya kutubu dhambi zao pindi walipokuwa duniani lakini walisema ‘kesho’ na kuzidi kesema kesho!,kesho!.b aadhi walisema ‘hakuna moto wa kuzimu’.baadhi yao waliwapiga watumishi wangu niliowatuma kwao, na sasa wapo kuzimu wakiomba nafasi ya pili.....siwajui ninyi”.[Mithali 1:24-28].
Bwana YESU akaniambia, “niliwaonyesha njia ya kuepuka moto wa kuzimu lakini walinichukia mimi na njia yangu na kuchagua maisha ya kufurahia dunia.hata niliwapa ofa  ya neema walipokuwa wakitaka kufa lakini lakini waliiharibu”.
Bwana akasema tena, “walinichukia mimi na kupenda kifo .........sio kifo tuu cha duniani bali pia adhabu ya milele ndani ya kuzimu”.[Mithali 8:35-36]
Tubu kutoka kwenye dhambi yako kwa kuwa kuzimu hakuna kutubu.Wale wote wanaokataa kutubu wanatupwa kwenye adhabu ya milele.[Ufunuo 21:8].
KITENGO CHA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA.
Kulikuwa kuna mateso makali sana kwa wale waliorudi nyuma na kumwacha YESU, Mapepo yalikuwa yakikata ndimi zao, wakikata miili yao na kuwapiga kwa silaha zenye ncha kali.Walilia kwa uchungu sana, walikuwa wakijilaumu wao wenyewe wakisema “oh,kwa nini niligeuka nyuma?,Alinionya lakini sikusikia !”.Mapepo huwaambia “kaeni kimya!,Aliwapa ninyi neema lakini mkaichezea.Hutaweza kutoka huku,tutawatesa mpaka hukumu itapowekwa!” .......na wakaendelea kuwatesa[Ezekieli 18:24].Mapepo yalikuwa yakiwaambia “u wangu milele”.

Tafadhali sana kama umeokoka usijerudi ulimwengu, wote ambao ni waKristo kuna hatari kubwa ya kurudi nyuma na kumuacha Bwana.[2 Petro 2:20-22].

SHIMO LANGU MWENYEWE
Bwana alinionyesha shimo langu kuzimu.Nilipatwa na huzuni , lakin Bwana akaniambia, “KILA MTU DUNIANI ANA SHIMO LAKE HUKU MOTONI(kuzimu), NA KAZI YA MAPEPO NI KUHAKIKISHA ANAKULETA HUKU KUZIMU”.Unatakiwa uwe na uhakika kuwa hutaenda kwenye shimo hilo kwa sababu ni la moto sana, moto wake ni kama asidi.
ENZI YA SHETANI
Tukatoka hapo na Bwana akanichukua mpaka kwenye enzi ya shetani.Nikaona mapepo katika enzi hiyo wakubwa,warefu,wanene na wapana.shetani alikuwa amejificha na ghafla akaniangalia mimi.Akaniita jina langu ,“’Senayon, umekuja hapa kuona siri zetu.Sitakuruhusu umshirikishe yeyote siri zetu! ,Nita kuuwa wewe, naapa”.Na Bwana YESU akaniambia, “USIOGOPE,  MIMI NI MAISHA YAKO”.[Isaya 41:10-11].
Ndipo mda mwingine tukawa hatuonekani kwa shetani, na Bwana akaniambia mimi “VITU VYOTE HAVIONEKANI KWA SHETANI,SHETANI HAJUI VITU VYOTE LAKINI VITU VYOTE VIKOWAZI KWA MUNGU”.

Kwa mara ya kwanza siku amini hiki kwa sababu duniani wote tulikuaga tunajua shetani ni mwenye nguvu sana.Bwana naye akajua mawazo yangu na akanichukua nyuma kwenye enzi ya shetani.Nikagundua shetani hakujua kuwa tuko pale nyuma.Bwana akaniambia “ITA JINA LANGU” na nikaita kimya kimya “YESU!” na nguvu isiyokuwa ya kawaida ikatikisa kuzimu na shetani akaanguka chini kutoka kwenye enzi yake.Ndipo shetani alipogeuka nyuma na tukawa tumeonekana, shetani aliita jina langu kwa sauti “SENAYON” na Bwana akaniambia, “IJARIBU NGUVU ILIYO KATIKA JINA LANGU”.na nikaamuru shetani kufa kwa dakika tatu(3) kwa jina la YESU,Nguvu iliyotoka katika jina la YESU ikatoboa roho kama kitu kama ukuta na mwili wake wote aliouficha ukaanguka chini.[Wafilipi 2:9-11].Na mara baada ya dakika tatu(3),Bwana akaiachia roho yake naye shetani akarudi tena na ule mwili wake uliojificha.Alipoinuka tuu alitoa sauti akiwa na hasira kubwa sana na gadhabu.Nikaona mapepo mengi yakimkimbilia na kukusanyika wakiwa na mishale mikononi mwao.Na wote wakaja kinyume chetu, ndipo nikaona mbingu imefunguka na nikaona mshale haswaa,kiasi kwamba kwa mshale mmoja unaweza kuja kuharibu mishale yote ya shetani.
Nataka niwaambie kuna nguvu katika jina la YESU kwa jina lake kila goti litapigwa.[Wafilipi 2:9-11],[Marko 16:17-19], [Yohana 14:14], [Yohana 16:23].Kuna nguvu katika jina la YESU,liite kwa imani na mapepo watakimbia kutoka kwako; lakini utapoita jina la YESU bila kutubu utakuwa kwenye hatari.

MALAIKA WALIO ANGUKA
Bwana alinichukua mpaka kwenye ukumbi mkubwa kuzimu, niliona mapepo waliofungwa chini kwenye siti.Bwana akaniambia hao ni malaika walioanguka,nika muuliza sababu kwa nini wamefungwa.Bwana akaniambia, “WANANGUVU SANA NA KAMA WAKIACHILIWA, WATALETA ROHO NYINGI KUZIMU, WANANGUVU SANA”. Bwana akaniambia “WATA ACHILIWA BAADA YA UNYAKUO KUSUMBUA DUNIA NA KUTESA WATU KWA AJILI YA ALAMA YA MNYAMA”.[ 2Petro 2:4].
Mmoja wa mapepo hayo akaniambia “Senayon, Bwana amekuonyesha ushuhuda mzuri lakini kama nikikukuta wewe duniani, nitakuuwa”.
Tulipotoka mahali pale nikagundua kunakitu kimeshika nguo yangu.Nilipotazama nyuma, nikaona pepo ndiyo aliye nishika nguo yangu na alitokea chini.Kwa sababu ya Nuru ya Kristo hakuweza kuja karibu yangu zaidi.

Bwana akaniambia “NI KUHANI MKUU WA SHETANI[Beelzebuli][Mathayo 12:24].Pepo aliniambia “hatuta kuruhusu kushuhudia na kushirikisha wengine na hutafichua siri zetu, tutaku ua”.
Bwana akaniambia “MWAMURU !”.Kwa hiyo nikamuamuru kwa jina la YESU kuanguka ndipo upepo mkali ukaja ukampiga mpaka chini na akarudi sehemu yake.Bwana pia akanionyesha roho za usumbufu, na jinsi wanavyonitumia silaha zao ovu za kishetani, lakini Bwana akarudisha zaidi kwao, na wakakimbia.[Zaburi 91:1].Kwa kadiri ya muda Bwana alivyokuwa akinishika mkono wangu, Uwepo wake ulifukuza hofu yangu, na sikuwa na huzuni kuhusu nikionacho.

SHANGAZI YANGU
Nikaona mwanamke kwa mbali akiwa motoni , mapepo yalikuwa yakimtesa sana [Nahumu 2:10].Alikuwa akilia  kwa kadiri alivyoniangalia mimi na nikamuuliza Bwana, “Huyu ni nani?”.Bwana akaniambia, “NI RUTI, SHANGAZI YAKO”[mzaliwa wetu wa kwanza].Alikufa miaka mingi iliyopita ,huzuni kubwa kiasi gani;alikuwa pale kwa sababu hakumjua Bwana.Sikuwa na furaha na nilikuwa nafikiri nami pia naweza nisiingie mbinguni.Bwana alijua mawazo yangu yote na kuniambia , “MIMI NI MAISHA YAKO”.Nilitaka aniahidi kwamba sitaishia kuzimu naye YESU akasema “....KAMA UNALIJUA JINA LANGU !”.Mara zote ameniambia “USIOGOPE,MIMI NI MAISHA YAKO !”.

KANISA
Kanisa linatakiwa liamke na livae silaha zote za MUNGU.Niliona kundi la mapepo, wamekusanyika na nikaona kitabu kikubwa mbele yao.Wakaanza kufungua na mara wakafungua kurasa na wakasema “Ndio,tunakwenda kupambana na kanisa”,wakafunga kitabu.Ghafla ,mapepo yasiyoweza kuhesabika wakatokea wakiwa na mishale mikononi mwao kuirushia kanisa.Nilishangaa , ndipo Bwana akaniambia, “HIYO NI MISHALE YA USINGIZI NA UDHAIFU, WANAITUMIA HIYO ILI WATU WANGU WASIOMBE, WASIFUNGE NA KUZAA KWENYE UFALME WANGU”.Mapepo yote yana lengo moja na lengo lao ni kupeleka watu kuzimu.Kanisa linatakiwa liamke, tunatakiwa tuombe kinyume na nguvu zisizo onekana zilizo panga kinyume na kanisa[Efeso 5:14].

Niliona pepo lenye nguvu sana,nalo lilijigeuza na kuonekena kama mwanamke mzuri ambaye alionekana mtaratibu na kama mkristo mzuri.Aliingia kanisa moja kumvamia kaka ambaye si muda amempokea YESUKRISTO.Alikuja tuu ili amtongoze huyo kaka ili apoteze wokovu wake.[Yoeli 1:14] “ Tuitishe kutano kwa kudhamiria kabisa na kulia kwa Bwana ili aamshe kanisa, kwa sababu wale walio lala wanapotea”[1 Wakorintho 15:18].
Kanisa linahitaji uamsho wa kiMUNGU, tujijengee maisha ya maombi na kuharibu kila mbegu ambayo Bwana hakuipanda katika kanisa.[ 2Wakorintho 10:4-5].Kuna mapepo wengi sana siku hizi wanaotenda kama watu.Wanataka kutongoza kanisa[2 wakorintho 10:13-15].Ili sisi tuweze kuwashinda ni lazima tuvae silaha zote za MUNGU[Efeso 6:10-18].Kumbuka hizi ni nyakati za hatari[2 Timotheo 3:1-7].

WAKRISTO WANAOMLINDA SHETANI.
Bwana alinifundisha somo na kuniambia, “WAKRISTO WENGI NI WALINZI WA SHETANI”.Nikajiwazia mwenyewe, “Inawezekana vipi kwa mKristo anayeomba kinyume na shetani amlinde shetani?”.

Bwana akaniambia “kuna vitu kwenye maandiko ambavyo nimeviwekea hatia.shetani anajua kila kitu nilichokiwekea hatia na anatendea kazi hivyo.Baadhi ya waKristo huwaambia wenzao ‘si dhambi’ huku ni dhambi.shetani anatafuta njia kuhakikisha kufanya dhambi  kama sio dhambi”.Kwa Mkristo pia anayesema “si dhambi” na huku ni dhambi, huyo hujiweka mwenyewe kuwa mlinzi wa shetani[1 Petro 3:3].

YESU akasema “nimeonya kuhusu mavazi ya kidunia, lakini baadhi husema ‘sio mungu alichomaanisha, ni imani yetu’.....baadhi husema kuvaa hereni sio dhambi,mwanangu sijasema tuu hereni lakini hata kuvaa dhahabu au siliva.wanaovaa ili kuupendeza kumwili”.[yakobo 5:3]. “Usihusike na muonekano wa nje unaotegemea vito(jewelry), au uzuri wa nguo, au mpangilio wa nywele”.Tuna uzuri wa aina mbili ,uzuri wetu wa nje na uzuri wa ndani.

Na usiwe muonekano wa kupaka rangi nywele, kuvaa dhahabu au kuvaa nguo ya mapambo[1 Petro 3:3].Bwana alisema “kama mKristo yeyote akisema ‘si dhambi’ wao ni walinzi wa shetani” na anayekuwa mlinzi wa shetani hawezi kuingia katika ufalme wangu”.
Bwana akasema “mwanangu, soma nilichokisema katika kitabu [Kumbukumbu la torati 22:5],nawaonya watu wanitii mimi, kwasababu mwanamke anapovaa mavazi ya mwanaume au mwanaume anapovaa mavazi ya mwanamke ,wanamlaani mungu wa mbinguni na dunia, akisema hayuko sahihi katika kazi yake”.
Bwana alilia na kusema “mwanangu,mtu anamlaani muumba wake, na bado nawapa neema ya kutubu.lakini kama mtumishi wangu yeyote akikataa kutubu, na kuendelea kumlinda shetani ,nitawatapika nje ya mdomo wangu” [Ufunuo 3:15-16].

SHABAHA YA SHETANI
Bwana aliniambia shabaha ya shetani maisha ya maombi ya mtu,Mara maisha ya maombi yakifungwa basi uamuzi  wako kwa MUNGU nao umefungwa.Mtu naye anaanguka na kuwa majeruhi pindi maisha ya kufunga na kuomba yamefungwa.
Unatakiwa udhibiti sana na kujiongoza katika maisha ya kuomba.Pindi maombi ya mtu yanapo athiri ufalme wa giza ,shetani hujaribu kutafuta njia za kuzima nguvu ili moto uwe mdogo na ufe.[ 1 Petro 5:8].

Bwana aliniambia, “Angalia mtu yule ambaye mapepo yanamtesa kwa hasira”.Bwana akaniambia, “Alipokuwa duniani kulikuwa sikuzote kuna mvurugano na maharibifu makuu kwenye ufalme wa giza pindi aombapo.Na Nilikuwa napenda hicho......maombi yake yalikuwa yanamzuia shetani na kuharibu mipango yake yote.”

Shetani na wajumbe wake wakaanza kutafuta shabaha ya kuondoa maisha ya maombi ya yule mtu. Na wakamshikilia kupitia kinyongo, chuki na uchungu katika moyo wake juu ya ndugu mwingine kanisani.Bwana akasema, “Nilimuonya, lakini alikataa kunisikiliza mimi”.Mtu huyo alipatwa na ajali na kufa,[Mathayo 5:44] na sasa yupo kuzimu ya moto.Kuna wanakwaya wengi wenye chuki ndani ya mioyo yao juu ya wenzao katika Kristo.Hii ni mara mmoja anapoonekana kuwa anakipawa kikubwa kuliko mwingine.Ndipo watu wanaendeleza wivu na majivuno kwa sababu ya hayo, wafanyayo hayo wako katika hatari ya kuzimu.[Mathayo 18:4].
MPANGO WA MUNGU.
Bwana aliniambia, “Mpango wa MUNGU ni mkubwa kwa mwanadamu.Na pale popote MUNGU anapokuwa na mpango na maisha ya mtu, mipango ya shetanini kuharibu ahadi na mpango wa MUNGU”.Nikamuuliza YESUKRISTO “Shetani anaweza kuharibu ahadi na mpango wa MUNGU kwa mtu ?”.

Bwana akasema, “NDIO”,na Bwana anielezea, “Kwenye kila mpango na ahadi ya MUNGU kwa mtu, mara zote kuna vigezo, na katika hivyo vigezo, kuna neema na rehema....Neema ni nafasi ya kufanya marekebisho kama mtu akivunja kigezo chochote.Rehema ni kwa ajili ya mtu kusamehewa na MUNGU.Shetani atahakikisha unavunja vigezo.Kipindi MUNGU ameweka ahadi na Abraham, Vigezo MUNGU alivyompa ni kutembea naye kwa uaminifu”.

[Mwanzo 17:1-7].Mungu anampango kwa ajili ya maisha yako na vigezo vimeandikwa kwenye maandiko[Wagalitia 5:19-21].Sio hayo tuu MUNGU mwenyewe atakwambia mengi zaidi.Usipoteze neema katika vigezo vya MUNGU na rehema itakunyanyua juu.[Zaburi 91:11-12].

MKE WA MCHUNGAJI W.F KUMUYI AKIWA KWENYE UFALME WA MUNGU.
Tukatoka kuzimu ya moto na Bwana akanichukua mpaka mbinguni.Nilimuona mwanamke mbinguni, alikuwa mzuri sana, alitoka nje kwenye nyumba kubwa sana nzuri naye ndiye aliyekuwa mmiliki wa nyumba hiyo !.

Alikuja kwangu na sura ya kutabasamu, mawazo yake yalikuwa nami nimefika mbinguni kama mkazi.Nilishangaa nikijiuliza anaweza kuwa nani kwa kuwa utukufu wa MUNGU ulikuwa umembadili uzuri wa dunia.Bwana akaniambia, “Ni mke wa mchungaji W.F KUMUYI, Mtumishi wangu”.Nilikuwa na furaha kwa kuwa alikuwa amejaa utukufu wa MUNGU.Mbingu ni nzuri sana sehemu yote ilikuwa imejaa utukufu wa MUNGU.
Bwana akanionyesha mimi mto wa damu, nao ulikuwa baridi na umetulia na ilikuwa kama bwawa la kuogelea, Popote tunapomtenda dhambi MUNGU na tukaomba msamaha na kutuosha naye hutuosha kwenye mtu huo wa damu.
Bwana akanionyesha tarumbeta zitakazotumika kwa unyakuo.Akaniambia , “UJIO WANGU UKO KARIBU SANA”.Tarumbeta zilikuwa zinang`aa na zimetengenezwa na dhahabu safi.Bwana alinionyesha maandalizi ya Unyakuo.
Bwana akanichukua mimi kwenda kwenye ukumbi mkubwa na nikaona watakatifu wengi akiwa wamevaa mavazi meupe kabisa, wakiwa wanaimba,wakimsifu MUNGU, wakipaza sauti kwa Bwana-Utukufu wa MUNGU ulikuwa kati yao.Mbinguni ni kuzuri, kulikuwa kunanga`aa kila sehemu kwa sababu mwanga wote pale ulikuwa utukufu wa MUNGU.
NYUMBA KUBWA SANA YA MWANAMKE, MBINGUNI.
Bwana akanionyesha nyumba nzuri na kubwa sana mbinguni, Nikashangazwa ni nani anaweza kuwa mmiliki wa nyumba hii.Bwana akaniambia “Ni ya mwanamke na jina lake ni Margret.Amevuna roho nyingi sana kwenye ufalme wangu !.Roho alizovuna haziwezi hesabiwa na mtu, Ni tuu MUNGU mwenyewe .Kazi yake imejenga hii nyumba”.
[Mathayo 10:7] Alisalimisha maisha yake Kwangu, na vitu vya duniani vilikuwa si kitu kwake, Sasa ameishia katika utukufu wa ufalme wangu.Mkristo yeyote anayekataa kuvuna roho(watu) kuja kwenye ufalme wangu hawezi kuingia katika utukufu wangu”.[Mathayo 28:19-20],[Mathayo 10:32].

NJIA YA KUZIMU YA MOTO.
Bwana alinionyesha mimi njia ya kwenda kuzimu, ilikuwa ina watu wengi katika ile njia.Baadhi wanaonekana kama wakristo lakini walikuwa wakiendea katika njia ya kuzimu.Baadhi wameshikana mikono, mume amemshika mkono mkewe huku wakielekea kuzimu, mke akimshika mkono mume,Wazazi wameshika watoto wao mikono na baadhi wakienda wo wenyewe.Na kulikuwa kuna mzigo mikubwa mgongoni mwa kila mmoja wao.Kwa kadiri YESU alivyo kuwa akiwatazama ndivyo alivyozidi kulia kama mtoto.

Niliona kitu kilichonishangaza sana mimi; Niliona kundi la watu nao walikuwa wanawake na walikuwa wakijaribu kwa jitihada zote kupita kuingia njia ya mbinguni, lakini nguvu ilikuwa ikiwarudisha nyuma kuwatoa.Ndipo Bwana akaniambia , “Kisicho kisafi hakiwezi kupita kwenye njia Yangu”.[Isaya 35:8-9].Nikamuuliza, “Kitu gani kisicho kisafi kwao ?” .Bwana akaniambia, “Ni mavazi yao, wanavaa hereni, weavon, mapambo kichwani mwao(attachments), mikufu, vito.Wanavaa nguo za kiume, wanajaribu hata kujiremba wao wenyewe---Wanataka kupita kwenye njia yangu.Hiyo HAIWEZEKANI ! utii ni bora kuliko dhabihu !”.....Akaendelea kulia.
[Isaya 3:16-24],[1 Petro 3:3],[Kumbukumbu la torati 22:5].Bwana akalia kwa uchungu na akalia kwa sauti kama mwanamke wodini.Ninyi mnaodhani unaweza kufanya vyovyote unavyodhani baada ya kumpa maisha yako KRISTO, Unajidanganya mwenyewe !.Usisikilize uongo wa shetani, unapozaliwa upya ,ya zamani yamepita [2 wakorintho 5:17].
NJIA YA MBINGUNI
Bwana alinionyesha mimi njia ya kuelekea mbinguni.Niliona watu lakini sio wengi kama kwenye njia ya kwenda kuzimu.Kwenye hiyo njia niliona baadhi wakiendelea mbele, baadhi wanasonga kwa furaha, na wengine wakicheza kumsifu MUNGU.[2 Wakorintho 13:9], [2 Wakorintho 12:9].

Muda kidogo nikagundua wako wachache zaidi na hakuna milima mirefu katika njia ile , ambayo mtu akifika hapo anatakiwa apande ndipo ashuke kuendelea na safari.Nikagundua kuna baadhi ya watu walisha vuka vile vilima lakini wanaanza kurudi nyuma, walikuwa wamechoka kuendelea mbele.

Kama wewe ni mKristo wa aina hiyo, umechoshwa na majaribu, shida,umasikini na vitu vingine vingi.Na unadhani uamuzi mzuri ni kuacha wokovu, hivyo acha na umrudie YESUKRISTO kwa kuwa u kama mtu aliyemkimbia jambo lenye kutisha tuu/hofu na kuangukia kwenye shimo la simba.Bwana bado anakuhitaji wewe,lakini unatakiwa uvumilie. “Tunatembea kupitia mateso mengi ili kuingia kwenye ufalme wa MUNGU”[Matendo 14:22].Rudi kwa YESUKRISTO naye atakuokoa !,Kumbuka mateso ya wale waliorudi nyuma kuacha kumfuata YESUKRISTO yalivyo kule kuzimu ya moto [Yeremia 3:21-22].

Niliona baadhi wamesimama wakiwa hawaendi,wapo tu wamesimama hapo hapo.Kama wewe umKristo wa aina hiyo unafikiri niendelee kumtumikia MUNGU au niache, Unabidi uache mawazo maovuna usonge mbele.Chaguo zuri ni kusonga mbele hivyo omba upata nguvu ya kuendelea mbele[Waefeso 6:18].

Nikaona wengine wakitambaa, walikuwa wakipenda kuendelea katika njia hiyo, lakini walikuwa wamechoka.Kama wewe umKristo wa aina hiyo unaogopa wazazi wako zaidi kuliko unavyoogopa vitu vya KRISTO, unatakiwa uache.Hii ni hatari sana na baadhi yenu wazazi wenu wanawatesa ninyi, wanawafanya ili mmtende MUNGU dhambi.Unatakiwa uombe na kusema “hapana” kwa maamuzi ambayo ni tofauti na mpango wa MUNGU, Bwana anasema, “USIOGOPE”[Mathayo 10:28].

Omba upate nguvu ya kusimama na kuanza kusonga mbele kwa sababu MUNGU wetu ni mwenye nguvu.Lia Kwake, naye Atakusikia maombi yako[Efeso 6:14-18],[Yeremia 33:3].YESU alilia kwa uchungu na ilikuwa huzuni--- Bwana akaniambia mimi “Kimetokea nini mpaka umekuwa na huzuni ?,Kama kweli una huzuni, ndipo utawaambia watu kile ulichokiona”.

TUBU SASA
Ni muda wa kutubu kutoka kwenye dhambi yeyote.Haijalishi ni dhambi ya aina gani ambayo umeitenda,MUNGU ni mwaminifu kukusamehe wewe dhambi zako zote[Warumi 10:9-10].YESUKRISTO anapenda roho yakona hataki roho yako iende kuzimuya moto[Habakuki 2:13].MUNGU alimtuma mwanawe wa pekee,YESUKRISTO kufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu !,Yeyote amwaminiye Yeye hata angamia lakini atakuwa na uzima wa milele[Yohana 3:16].YESUKRISTO ni njia pekee  ,ya Kweli, na uzima na hakuna atayeweza kuja kwa Baba pasipo kwa njia ya YESUKRISTO [Yohana 14:6].

Tubu sasa na uokolewe[Matendo 17:30-31].Kama ukotayari kumpa maisha yako KRISTO basi omba sala hii:-
     Bwana YESU, Najijua mwenyewe kama mwenye dhambi , Najijua niko gizani, lakini sasa niko tayari kufanya kile onachotaka mimi nikifanye.Tafadhali nisamehe dhambi zangu zote,nioshe mimi katika mto wa damu yako, niponye,nitie nguvu,nipe uweza, na nguvu zaidi dhidi ya mwili na achilia ufalme wako uje ndani ya moyo wangu.Andika jina langu katika kitabu cha uzima na iwe furaha kubwa mbinguni juu ya wokovu wa roho yangu.Katika jina la YESUKRISTO nimeomba .Ameni.

Tafadhali nakuomba u SHARE kwa wengine nao wapate habari hizi za wokovu lakini ,Kwa shuhuda nyingi zaidi angalia kwenye www.jasirimbarikiwa.blogspot.com. Ubarikiwe !.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...