Somo:Hatujijui
kama yeye MUNGU anavyotujua!-part 1
Walengwa:
couple/single
Neno: “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, . . . . .” Mwanzo 1:26
Theme:Sababu kuu ya
kuoa au kuolewa
“Ndoa na iheshimiwe na
watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU
atawahukumia adhabu” Waebrania 13:4
MUNGU ndiye aliyetuumba
sisi sote,yaani watu wote wale wanao mjua MUNGU na wasio mjua.Imeandikwa “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na
wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mwanzo
1:26
Hivyo hatujijui kama
yeye MUNGU aliotutengeneza, aliyetuumba anavyotujua!.Hatujui hata siku za
maisha yetu kwa nguvu zetu bali ni kwa unabii utokao kwake MUNGU tena kwa
mapenzi yake.
Imeandikwa “(Kwani
sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli
tu;)” Ayubu 8:9.
Yeye MUNGU anajua kila
kitu juu yetu, anajua uwezo tulionao,anajua tuishi namna gani ndio itakuwa
vyema zaidi,anajua kitu gani tusifanye kisije kikaharibu uumbaji wake juu yetu
kwa namna yoyote ile.
MUNGU aliyetuumba
anasema sii vyema mtu aishi pekee yake na akamfanyia msaidizi.
Imeandikwa“BWANA MUNGU akasema, Si vema huyo
mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Mwanzo 2:18
Ni nani wakumpinga MUNGU yeye aliyetuumba kwa kuwa yeye amesema sii vyema mtu kuishi
pekee yake.
Hakuna mtu aliyejiumba
,hakuna hata mtu mmoja aliye jitengeneza.Na yule aliyetuumba anajua ni jinsi
gani tunatakiwa tuwe mke na mume.
Katika maisha ya
kawaida tuu,Mtu anayefinyanga (mfinyanzi) akitengeneza chungu cha udongo ,hata
kile chungu kiende wapi yeye mfinyanzi akikiona tuu anakijua, tena kwa undani
sana.
Atakijua na kukumbuka
alitumia udongo gani ?,anajua uwezo wa
chungu hicho,kinaweza kufa ukikigonga na kitu kigumu,anajua aliweka mapambo
gani ? na vyote katika chungu hicho yeye mfinyanzi anajua kwa sababu yeye ndiye
aliyekifinyanga.
Je ? kama sisi wanadamu
tunajua mambo yote hayo juu ya kile kitu tunacho kitengeneza,Si zaidi ajuavyo
MUNGU juu yetu kwa kuwa YEYE ndio aliyotuumba.
Yeye anayetujua zaidi
anatuambia si vyema mtu aishi pekee yake.Kwa hiyo kuna haja ya mtu kooa au
kuolewa kwa kuwa yeye MUNGU anayetujua zaidi anatuambia kuwa sii vyema mtu
kuishi pekee yake.
Hivyo BWANA asema
mwanamke kuishi pasipo kuolewa sii vyema na mwanaume aishiye bila kuoa sii
vyema.
Sababu ya mtu kuoa au
kuolewa ni moja tuu kuwa yeye hajajiumba na aliyemuumba ambaye ni MUNGU anasema
sii vyema mtu kuishi pekee yake.
“Kwa sababu hiyo ........................................................”
Waefeso 5:31.
Andiko limeanza kwa
kusema kwa sababu hiyo,sababu yenyewe ni “Kwasababu
hatujijui sana na kiundani kama MUNGU aliyetuumba anavyotujua,na kwa agizo lake
si vyema mtu aishi pekee yake..”
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!