Jina
langu ninaitwa Emmanueli Senayon;Nina umri wa miaka 18, kutokea nchini
Naijeria.
NIMEKUTANA NA YESUKRISTO.
Mwaka
2012 mwezi Novemba, Nilikuwa mgonjwa sana na wazazi wangu wakanichukua na
kunipeleka hospitalini.Daktari akasema damu yangu i chini sana na nilikuwa na
kifua kikuu{TB}(tuberculosis).
Ilikuwa taarifa mbaya sana hasa kwa wazazi
wangu kwa kuwa hawakuweza kumudu gharama
za kunihudumia pale hospitalini, hivyo wakanichukua na kunirudisha nyumbani
bila matumaini yeyote.
Nilipokuwa
kwenye kitanda nikipumzika, Nikaanza kuhisi kitu cha ajabu na mwili wangu wote
ukazidi kuwa dhaifu isiyokuwa kawaida.Nikajikuta mwenyewe niko nje ya mwili
katika chumba cheupe haswaa.YESUKRISTO akanitokea, Sura yake ilikuwa inang`aa
na alikuwa mzuri sana lakini nikagundua hakuwa na furaha.Akanishika mkono wangu
na kunichukua mimi hadi nje ya chumba hicho na nikajikuta nimesimama mbele ya enzi
kubwa.
Nikamwona
Baba MUNGU katika enzi yake.Sikuweza kuona sura yake ,mwili wake ulikuwa kama
moto uwakao, amejaa nguvu na utukufu.Nikaona makundi ya malaika wakiwa na
mavazi meupe mbele ya enzi, na walijaa utukufu.Wale malaika wamebeba vitabu
kwenye mikono yao.Nikaona watu wasiohesabika mbele ya enzi[UFUNUO 20:11] nao walikuwa
wakienda mmoja baada ya mwingine kupokea hukumu yao na kila mtu alipofika mbele
ya enzi, malaika walifungua vitabu mikononi mwao na MUNGU ndiye anayehukumu
huyo mtu.
Watu
wengi waliosimama wakisikia MUNGU akiwaambia “ONDOKA KWANGU”.
MUNGU
aliwahukumu na hasira kali na sauti yake ikasikika kwa mlio mkuu [EZEKIELI
43:8].Pale MUNGU anaposema “ONDOKA
KWANGU”,Kulikuwa na kimbunga kikubwa kinachomzoa mtu huyo na kumtoa
hapo.[MATHAYO 25:41].Watu wote waliokuwa mbele ya enzi walikuwa wakiogopa sana
kusimama mbele za MUNGU.Wao malaika hawaiti jina la mtu yeyote lakini kila mtu
anajua inapofikia zamu yake ya kupokea hukumu[2 wakorintho 5:10].Yeyote
aliyefanya uovu alitwaliwa na kimbunga kwenda kwenye adhabu isiyo isha[Mathayo
25:46].
Kwa
kuwa uko hai ,Bado una neema ya dhahabu kutubu kutoka kwenye dhambi zake na
kuaha uovu wako.Hasira ya MUNGU ni kama moto uwakao[SEFANIA 2:1-3] na dunia ni
bonde la kufanya maamuzi[YOELI
3:14].Uamuzi wako uache uwe KRISTO;kabidhi maisha yako kwa YESUKRISTO na
kuipuka hasira ya MUNGU.Haijalishi dhambi gani ulioifanya, YESU atakusamehe
yote yote[HOSEA 14:4], [HABAKKUKI 2:13].
YESUKRISTO
AKANIPELEKA KUZIMU YA MOTO
Ndipo
YESUKRISTO akanitoa hapo na kunipeleka kuzimu iwakayo moto.Kuelekea kuzimu
tulipitia handaki ambapo tulipotoka tuu kwenye hilo handaki tukawa tumefika
sehemu ambayo ina giza kweli kweli.Ilikuwa ni sehemu yenye giza kubwa na sauti
za kutisha za vilio na kutisha.
Nikauliza,
‘Bwana tuko wapi ?’ naye akasema, “huu
ni ufalme wa shetani, kuzimu ya moto”.Kuzimu inatisha sana kuna giza
zito.Niliona mapepo wengi ;walikuwa wakubwa na wabaya sana.Mapepo hayo yalikuwa
yanafanya kazi kwa kasi sana bila ya kuchoka.[1 PETRO 5:8].Bwana akaniambia
mimi , “wanapanga jinsi ya kuleta watu sehemu hii”.
Kuzimu
ya moto iko kama ziwa, na kila mmoja ana sehemu yake katika kitengo tofauti
tofauti.Kuna watu wengi kuzimu wako kwenye moto wanaomba nafasi ya sekunde,
lakini hakuna kibali na haiwezekani.[MIKA 3:4].
Kitengo
cha kwanza Bwana alichonionyesha nisehemu ambayo ni ya wachungaji walioikosa
mbingu.Niliona wachungaji wengi wako kuzimu katika mashimo yao kuna kitu
kamaubao watangazo ambako umeandikwa jina la huyo mchungaji,jina la hilo kanisa
alilokuwa akilichunga jumuisha na sababu iliyopeleka kuzimu.Kila mchungaji
alikuwa ana mapepo yaliyokuwa yanamtesa.Walikuwa wakilia na kuomba rehema kwa
YESU, lakini YESU alilia na kuwaambia “nilipokuwa nikiwaonya ninyi hamkunisikiliza
na sasa mpo katika sehemu hii.siwajui ninyi !”.[Mithali 1:24-31].
Ndipo
Bwana akaniambia, “kuzimu imejiongeza na hakuna ajaye huku atayeweza kurudi tena”.[Mithali
2:19],[ Isaya 4:14].
Niliona kitu
kikubwa na cha kushangaza sana ! “Watu wangu,tutawezaje kuikwepa kuzimu kama
tukidharau wokovu mkuu?” [Waebrania 2:3].
MCHUNGAJI OSHOFFA
Nilimuona
mtu akiwaka moto kuzimu, mapepo walikuwa wakimtesa kwa silaha zao na vifaa
vyao.Mtu huyo alikuwa akiomba rehema na alilia kwa uchungu sana.
Nikamuuliza
Bwana, “Huyu ni nani?”.Bwana akaniambia, “ni mchungaji oshoffa, muanzilishi wa
makanisa ya ‘CELESTIA KANISA LA KRISTO’,KANISA LA VAZI JEUPE”.Bwana
akaniambia siri ya mtu huyu; “alijiwekea agano na shetani kuwavuta watu
kwa mafundisho ya giza, uponyaji kutumia mishushumaa, marashi na sabuni.Huwaambia
watu watumie hivyo vitu na waende kuoga kwenye mito, na kuwadanganya kwa nguvu
ya shetani”.
Bwana
aliongeza “yeye alifundisha mafundisho ya uongo ili tuu ajulikane kama mtu mkubwa
wa Mungu”.[Efeso 4:14] Bwana alisema, “NILIMUONYA YEYE LAKINI
ALIKATAA”.
Bwana
YESU alimwambia mtu huyu “SIKUJUI WEWE”,YESU alilia kama mtoto; huyu mtu alikataa
msalaba wa KRISTO tuu kwa sababu ya umaarufu.Sasa yupo kuzimu akiomba rehema
kwa Bwana kutokana na uovu aliokuwa nao.[ 2 Timotheo 2:12,19].
Nataka
nikueleweshe kuwa haijalishi hali yeyote usiamini au mafundisho tofauti na kwa
hayo “Hutaweza kujitetea mbele za Bwana”.[Tito 1:16],[Yeremia 23:24].Watu wengi
wapo kuzimu kutokana na mafundisho yao.[Wafilipi 2:5].
YUDA ISKARIOTE.
Nikamuona
mtu mwingine akiwa kuzimu;,mapepo yamemfanya alale juu ya kitu kama chuma
ambayo ni mfano wa meza,Walikuwa wakimuumiza na aina za vifaa mbali
mbali.Nikaona chuma kikubwa ambacho pepo anakitumia kumtesea na kukitumbukiza
kupitia kwenye tumbo la huyo mtu.Kilikuwa kinapita kwenye tumbo na huyo mtu
alikuwa akilia kwa uchungu sana.
Mara akatokea pepo ambaye alikuwa ana kisu
kikubwa cha chuma mkononi mwake, akakata katikati ya kichwa cha mtu huyo,
mapepo kumi walikusanyika ,kulikuwa na funza wengi na n`nge.Walikuwa
wakiingilia kichwa cha mtu huyu na baadae kurejea tena.Mtu huyo alikuwa akilia
zaidi kama upepo wa ziwa.Iliniuma mimi sana kuona hayo.Bwana akaniambia, “HUYO
NI MMOJA WA WANAFUNZI WANGU, YUDA ISKARIOTE”.
Nikauliza
mapepo sababu ya kumtesa yeye kiasi
hicho,na pepo akaniambia “Kama asinge
mfichua mtu huyu wa Nuru(YESUKRISTO) kwa watu ili wamuue , basi kazi ya wokovu
isingedhihirika”.Mapepo yalikuwa yakipiga kelele yakimwambia, “Kwa nini umemsaliti?”,aliendelea
kumtesa.[Mathayo 10:4],[Mathayo 20:18].
Unatakiwa
uwe makini kwa kile unachokifanya usimsaliti YESUKRISTO ! “Ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa
Adamu !”.[Mathayo
26:24].Wale ambao wamejifunza kutoka kwa Bwana na kuelewa Neno la MUNGU
wanatakiwa waruhusu “neno la KRISTO kukaa ndani yao”.[Wakolosai 3:16-17].Kwa
yule ambaye anarudi nyuma,Bwana anasema “ROHO YANGU HAINA
FURAHA NAYE.”.[Waebrania 10:38].Kama wewe ni mtumishi wa MUNGU jichunguze
mwenyewe na utoe kikwazo katika maisha yako.---MOTO WA KUZIMU UNATISHA KWELI.
MFALME
AHABU NA YEZEBELI.
Bwana
alinionyesha mtu aliyekuwa amekaa amefungwa kwenye kiti cha chuma.Hicho kiti
kilikuwa cha moto sana na chekundu kama kaa.Ingawa alikuwa akipiga yowe kwa
uchungu sana badomapepo yaliendelea kumtesa na mikuki wakiwa na hasira kali.Mtu
huyo akaanza kumuomba YESU nafasi yakutoka kwenye moto.Nikajiuliza huyu anaweza
kuwa nani, Bwana alijua mawazo yangu na kuniambia mimi “NI MFALME AHABU”.
Ghafla
nikamuona mwanamke ambae mapepo yalikuwa yakimtesa sana.Walikuwa wakimpiga na
kwa mikuki alipokuwa akilia na kupiga
kelele.Bwana akaniambia, “HUYO NI YEZEBELI,NABII WA UONGO AMBAO ALIKUWA
AKIWASHAWISHI WATU KUMTENDA DHAMBI MUNGU”.[Ufunuo 2:20].
Unabidi
uwe makini kwa sababu kuna manabii wengi wa uongo, wanaofundisha mafundisho potofu ambao kwa hayo
mafundisho wajiwekea utajiri wao wenyewe.Waanajiita wenyewe waokozi na
kudanganya watu kwa uongo wa shetani.KAMA WAKIKATAA KUTUBU,WATAKUWA NA NAFASI
YAO KUZIMU YA MOTO.[ 2Wathesalonike 1:8]
MTOTO
WA MIAKA SITA(6).
Nilimuona
mtoto mdogo akiwa kuzimu,mapepo yalikuwa yakimtesa huyo mtoto kwa mikuki,Huyo
mtoto alipotuona sisi alilia na kuomba msaada ili atolewe motoni, lakini Bwana
akasema “MIMI SIO MUNGU WA WASIOTII”.Huyo mtoto alikuwa jeuri sana alipokuwa
duniani, alikuwa akisumbua wazazi wake kipindi mchungaji anapotoa Neno.Wazazi
wake walipomsahihisha aliwafokea.Aliumwana na alipokufa ,sasa yupo kuzimu
milele.Bwana akasema,”HAMNA MTOTO ASIYETII ATAKAYERITHI UFALME WA MUNGU”.[Waefeso
6:1-2].
REVEREND PATRICK R. COONEY
Bwana
alinionyesha mimi mtu mmoja aliyekuwa kuzimu,alikuwa akifahamika kama PATRICK
COONEY alipokuwa hapa duniani.Mapepo yalikuwa yanakata kata mwili wake kwa
misumeno, mateso yalikuwa makali sana.Walikuwa wakimkejeli na kumcheka na kusa
pekee alilokuwa nalo ni kutokana na mafundisho yake.Alipelekwa kuzimu kwa
sababu ya kuinamia mara kwa mara [inayosemekana]
SURA YA MTAKATIFU MARIA.[Kutoka 20:3-4].
Ni
huzuni sana watu wengi wanaishia milele kuzimu kutokana na mambo kama
haya.Nilikuwa na huzuni kubwa na Bwana akaniambia “KAMA KWELI UNAHUZUNI, UTAWAAMBIA
ULICHOKIONA”.
Unatakiwa
ufungue moyo wako na kusema “hapana” juu ya uongo wa shetani.Tunatakiwa tutoke
kwenye mafundisho yenye kumfanya KRISTO atukatae sisi.[2 Wakorintho 6:14-18],
USIINAMIE KUABUDU MTAKATIFU MARIA TENA.
KITENGO CHA WENYE KUJIWEKA KIKAHABA.
Niliwaona
watu wengi katika hiki kitengo,Bwana akanionyesha picha zo walivyokuwa duniani
nao kwa sura walikuwa wazuri lakini sasa wapo kuzimu ni wabaya sana.Mapepo
yalikuwa yakiwatesa kwa kutumia mikuki kuwapiga na kuwabana sehemu zao za siri,
walikuwa wakilia na kutafuta wafe lakini ilishindikana.[Ufunuo 9:6]
YESU
alilia, nao watu walikuwa wanamuomba BWANA awatoe, nao walikuwa wakiapa katika
maisha yao watafanya mapenzi YAKE kama wakitolewa kwenye moto, Lakini Bwana
hachezi au kutania na NENO lililotoka kwenye kinywa chake[Wakolosai 3:5-6].Imeshaandikwa
kwenye NENO kuwa yeyote anayetenda uovu hata urithi ufalme wa MUNGU[1Wakorintho
6:9-10].
KITENGO CHA WALIOSIKIA KUHUSU KRISTO NA WAKAKATAA
KUTUBU.
Kuna watu wengi kuzimu ambao walisikia habari za wokovu,lakini
walikataa kutubu dhambi zao.Nao walidhani watakuja mbinguni kwa kazi za mili na
damu yao, Tofauti na hayo sasa wameishia kuzimu inayowaka milele[ 1Wakorintho
15:50].
Walikuwa wakilia, lakini Bwana alisema “walipewa neema kubwa ya kutubu
dhambi zao pindi walipokuwa duniani lakini walisema ‘kesho’ na kuzidi kesema
kesho!,kesho!.b aadhi walisema ‘hakuna moto wa kuzimu’.baadhi yao waliwapiga
watumishi wangu niliowatuma kwao, na sasa wapo kuzimu wakiomba nafasi ya
pili.....siwajui ninyi”.[Mithali 1:24-28].
Bwana YESU akaniambia, “niliwaonyesha njia ya kuepuka moto wa
kuzimu lakini walinichukia mimi na njia yangu na kuchagua maisha ya kufurahia
dunia.hata niliwapa ofa ya neema
walipokuwa wakitaka kufa lakini lakini waliiharibu”.
Bwana akasema tena, “walinichukia mimi na kupenda kifo
.........sio kifo tuu cha duniani bali pia adhabu ya milele ndani ya kuzimu”.[Mithali
8:35-36]
Tubu kutoka kwenye dhambi yako kwa kuwa kuzimu hakuna kutubu.Wale
wote wanaokataa kutubu wanatupwa kwenye adhabu ya milele.[Ufunuo 21:8].
KITENGO CHA WAKRISTO
WALIORUDI NYUMA.
Kulikuwa kuna mateso makali sana kwa wale waliorudi nyuma na kumwacha
YESU, Mapepo yalikuwa yakikata ndimi zao, wakikata miili yao na kuwapiga kwa
silaha zenye ncha kali.Walilia kwa uchungu sana, walikuwa wakijilaumu wao
wenyewe wakisema “oh,kwa nini niligeuka nyuma?,Alinionya lakini sikusikia !”.Mapepo
huwaambia “kaeni kimya!,Aliwapa ninyi neema lakini mkaichezea.Hutaweza kutoka
huku,tutawatesa mpaka hukumu itapowekwa!” .......na wakaendelea
kuwatesa[Ezekieli 18:24].Mapepo yalikuwa yakiwaambia “u wangu milele”.
Tafadhali sana kama umeokoka usijerudi ulimwengu, wote ambao ni
waKristo kuna hatari kubwa ya kurudi nyuma na kumuacha Bwana.[2 Petro 2:20-22].
SHIMO
LANGU MWENYEWE
Bwana alinionyesha shimo langu kuzimu.Nilipatwa na huzuni , lakin
Bwana akaniambia, “KILA MTU DUNIANI ANA SHIMO LAKE HUKU MOTONI(kuzimu), NA KAZI
YA MAPEPO NI KUHAKIKISHA ANAKULETA HUKU KUZIMU”.Unatakiwa uwe na uhakika kuwa
hutaenda kwenye shimo hilo kwa sababu ni la moto sana, moto wake ni kama asidi.
ENZI
YA SHETANI
Tukatoka hapo na Bwana akanichukua mpaka kwenye enzi ya
shetani.Nikaona mapepo katika enzi hiyo wakubwa,warefu,wanene na wapana.shetani
alikuwa amejificha na ghafla akaniangalia mimi.Akaniita jina langu ,“’Senayon, umekuja hapa kuona siri
zetu.Sitakuruhusu umshirikishe yeyote siri zetu! ,Nita kuuwa wewe, naapa”.Na
Bwana YESU akaniambia, “USIOGOPE, MIMI NI MAISHA YAKO”.[Isaya 41:10-11].
Ndipo mda mwingine tukawa hatuonekani kwa shetani, na Bwana
akaniambia mimi “VITU VYOTE HAVIONEKANI KWA SHETANI,SHETANI HAJUI VITU VYOTE
LAKINI VITU VYOTE VIKOWAZI KWA MUNGU”.
Kwa mara ya kwanza siku amini hiki kwa
sababu duniani wote tulikuaga tunajua shetani ni mwenye nguvu sana.Bwana naye
akajua mawazo yangu na akanichukua nyuma kwenye enzi ya shetani.Nikagundua
shetani hakujua kuwa tuko pale nyuma.Bwana akaniambia “ITA JINA LANGU” na
nikaita kimya kimya “YESU!” na nguvu isiyokuwa ya kawaida ikatikisa kuzimu na
shetani akaanguka chini kutoka kwenye enzi yake.Ndipo shetani alipogeuka nyuma
na tukawa tumeonekana, shetani aliita jina langu kwa sauti “SENAYON” na Bwana
akaniambia, “IJARIBU NGUVU ILIYO KATIKA JINA LANGU”.na nikaamuru shetani kufa
kwa dakika tatu(3) kwa jina la YESU,Nguvu iliyotoka katika jina la YESU
ikatoboa roho kama kitu kama ukuta na mwili wake wote aliouficha ukaanguka
chini.[Wafilipi 2:9-11].Na mara baada ya dakika tatu(3),Bwana akaiachia roho
yake naye shetani akarudi tena na ule mwili wake uliojificha.Alipoinuka tuu
alitoa sauti akiwa na hasira kubwa sana na gadhabu.Nikaona mapepo mengi
yakimkimbilia na kukusanyika wakiwa na mishale mikononi mwao.Na wote wakaja
kinyume chetu, ndipo nikaona mbingu imefunguka na nikaona mshale haswaa,kiasi
kwamba kwa mshale mmoja unaweza kuja kuharibu mishale yote ya shetani.
Nataka niwaambie kuna nguvu katika jina la YESU kwa jina lake
kila goti litapigwa.[Wafilipi 2:9-11],[Marko 16:17-19], [Yohana 14:14], [Yohana
16:23].Kuna nguvu katika jina la YESU,liite kwa imani na mapepo watakimbia
kutoka kwako; lakini utapoita jina la YESU bila kutubu utakuwa kwenye hatari.
MALAIKA WALIO ANGUKA
Bwana alinichukua mpaka kwenye ukumbi mkubwa kuzimu,
niliona mapepo waliofungwa chini kwenye siti.Bwana akaniambia hao ni malaika
walioanguka,nika muuliza sababu kwa nini wamefungwa.Bwana akaniambia,
“WANANGUVU SANA NA KAMA WAKIACHILIWA, WATALETA ROHO NYINGI KUZIMU, WANANGUVU
SANA”. Bwana akaniambia “WATA ACHILIWA BAADA YA UNYAKUO KUSUMBUA DUNIA NA
KUTESA WATU KWA AJILI YA ALAMA YA MNYAMA”.[ 2Petro 2:4].
Mmoja wa mapepo hayo
akaniambia “Senayon, Bwana amekuonyesha ushuhuda mzuri lakini kama nikikukuta
wewe duniani, nitakuuwa”.
Tulipotoka mahali pale nikagundua kunakitu kimeshika
nguo yangu.Nilipotazama nyuma, nikaona pepo ndiyo aliye nishika nguo yangu na
alitokea chini.Kwa sababu ya Nuru ya Kristo hakuweza kuja karibu yangu
zaidi.
Bwana akaniambia “NI KUHANI MKUU WA SHETANI[Beelzebuli][Mathayo 12:24].Pepo
aliniambia “hatuta kuruhusu kushuhudia na kushirikisha wengine na hutafichua
siri zetu, tutaku ua”.
Bwana akaniambia “MWAMURU !”.Kwa hiyo nikamuamuru kwa
jina la YESU kuanguka ndipo upepo mkali ukaja ukampiga mpaka chini na akarudi
sehemu yake.Bwana pia akanionyesha roho za usumbufu, na jinsi wanavyonitumia
silaha zao ovu za kishetani, lakini Bwana akarudisha zaidi kwao, na
wakakimbia.[Zaburi 91:1].Kwa kadiri ya muda Bwana alivyokuwa akinishika mkono
wangu, Uwepo wake ulifukuza hofu yangu, na sikuwa na huzuni kuhusu nikionacho.
SHANGAZI YANGU
Nikaona mwanamke kwa mbali akiwa motoni , mapepo yalikuwa
yakimtesa sana [Nahumu 2:10].Alikuwa akilia
kwa kadiri alivyoniangalia mimi na nikamuuliza Bwana, “Huyu ni
nani?”.Bwana akaniambia, “NI RUTI, SHANGAZI YAKO”[mzaliwa wetu wa kwanza].Alikufa
miaka mingi iliyopita ,huzuni kubwa kiasi gani;alikuwa pale kwa sababu hakumjua
Bwana.Sikuwa na furaha na nilikuwa nafikiri nami pia naweza nisiingie
mbinguni.Bwana alijua mawazo yangu yote na kuniambia , “MIMI NI MAISHA YAKO”.Nilitaka
aniahidi kwamba sitaishia kuzimu naye YESU akasema “....KAMA UNALIJUA JINA
LANGU !”.Mara zote ameniambia “USIOGOPE,MIMI NI MAISHA YAKO !”.
KANISA
Kanisa linatakiwa liamke na livae silaha zote za
MUNGU.Niliona kundi la mapepo, wamekusanyika na nikaona kitabu kikubwa mbele
yao.Wakaanza kufungua na mara wakafungua kurasa na wakasema “Ndio,tunakwenda
kupambana na kanisa”,wakafunga kitabu.Ghafla ,mapepo yasiyoweza kuhesabika
wakatokea wakiwa na mishale mikononi mwao kuirushia kanisa.Nilishangaa , ndipo
Bwana akaniambia, “HIYO NI MISHALE YA USINGIZI NA UDHAIFU, WANAITUMIA HIYO ILI
WATU WANGU WASIOMBE, WASIFUNGE NA KUZAA KWENYE UFALME WANGU”.Mapepo yote yana
lengo moja na lengo lao ni kupeleka watu kuzimu.Kanisa linatakiwa liamke,
tunatakiwa tuombe kinyume na nguvu zisizo onekana zilizo panga kinyume na
kanisa[Efeso 5:14].
Niliona pepo lenye nguvu sana,nalo lilijigeuza na
kuonekena kama mwanamke mzuri ambaye alionekana mtaratibu na kama mkristo
mzuri.Aliingia kanisa moja kumvamia kaka ambaye si muda amempokea
YESUKRISTO.Alikuja tuu ili amtongoze huyo kaka ili apoteze wokovu wake.[Yoeli
1:14] “ Tuitishe kutano kwa kudhamiria kabisa na kulia kwa Bwana ili aamshe
kanisa, kwa sababu wale walio lala wanapotea”[1 Wakorintho 15:18].
Kanisa linahitaji uamsho wa kiMUNGU, tujijengee maisha
ya maombi na kuharibu kila mbegu ambayo Bwana hakuipanda katika kanisa.[
2Wakorintho 10:4-5].Kuna mapepo wengi sana siku hizi wanaotenda kama
watu.Wanataka kutongoza kanisa[2 wakorintho 10:13-15].Ili sisi tuweze
kuwashinda ni lazima tuvae silaha zote za MUNGU[Efeso 6:10-18].Kumbuka hizi ni
nyakati za hatari[2 Timotheo 3:1-7].
WAKRISTO WANAOMLINDA SHETANI.
Bwana alinifundisha somo na kuniambia,
“WAKRISTO WENGI NI WALINZI WA SHETANI”.Nikajiwazia mwenyewe, “Inawezekana vipi
kwa mKristo anayeomba kinyume na shetani amlinde shetani?”.
Bwana akaniambia “kuna
vitu kwenye maandiko ambavyo nimeviwekea hatia.shetani anajua kila kitu
nilichokiwekea hatia na anatendea kazi hivyo.Baadhi ya waKristo huwaambia
wenzao ‘si dhambi’ huku ni dhambi.shetani anatafuta njia kuhakikisha kufanya
dhambi kama sio dhambi”.Kwa
Mkristo pia anayesema “si dhambi” na huku ni dhambi, huyo hujiweka mwenyewe
kuwa mlinzi wa shetani[1 Petro 3:3].
YESU akasema “nimeonya kuhusu mavazi ya kidunia, lakini
baadhi husema ‘sio mungu alichomaanisha, ni imani yetu’.....baadhi husema kuvaa
hereni sio dhambi,mwanangu sijasema tuu hereni lakini hata kuvaa dhahabu au
siliva.wanaovaa ili kuupendeza kumwili”.[yakobo 5:3]. “Usihusike na
muonekano wa nje unaotegemea vito(jewelry), au uzuri wa nguo, au mpangilio wa
nywele”.Tuna uzuri wa aina mbili ,uzuri wetu wa nje na uzuri wa ndani.
Na usiwe muonekano wa kupaka rangi nywele, kuvaa
dhahabu au kuvaa nguo ya mapambo[1 Petro 3:3].Bwana alisema “kama
mKristo yeyote akisema ‘si dhambi’ wao ni walinzi wa shetani” na anayekuwa
mlinzi wa shetani hawezi kuingia katika ufalme wangu”.
Bwana akasema “mwanangu, soma nilichokisema katika kitabu [Kumbukumbu
la torati 22:5],nawaonya watu wanitii mimi, kwasababu mwanamke anapovaa mavazi
ya mwanaume au mwanaume anapovaa mavazi ya mwanamke ,wanamlaani mungu wa
mbinguni na dunia, akisema hayuko sahihi katika kazi yake”.
Bwana alilia na kusema “mwanangu,mtu anamlaani muumba
wake, na bado nawapa neema ya kutubu.lakini kama mtumishi wangu yeyote akikataa
kutubu, na kuendelea kumlinda shetani ,nitawatapika nje ya mdomo wangu” [Ufunuo
3:15-16].
SHABAHA YA SHETANI
Bwana aliniambia shabaha ya shetani
maisha ya maombi ya mtu,Mara maisha ya maombi yakifungwa basi uamuzi wako kwa MUNGU nao umefungwa.Mtu naye
anaanguka na kuwa majeruhi pindi maisha ya kufunga na kuomba yamefungwa.
Unatakiwa udhibiti sana na
kujiongoza katika maisha ya kuomba.Pindi maombi ya mtu yanapo athiri ufalme wa
giza ,shetani hujaribu kutafuta njia za kuzima nguvu ili moto uwe mdogo na
ufe.[ 1 Petro 5:8].
Bwana aliniambia, “Angalia
mtu yule ambaye mapepo yanamtesa kwa hasira”.Bwana akaniambia, “Alipokuwa
duniani kulikuwa sikuzote kuna mvurugano na maharibifu makuu kwenye ufalme wa
giza pindi aombapo.Na Nilikuwa napenda hicho......maombi yake yalikuwa
yanamzuia shetani na kuharibu mipango yake yote.”
Shetani na wajumbe wake wakaanza
kutafuta shabaha ya kuondoa maisha ya maombi ya yule mtu. Na wakamshikilia
kupitia kinyongo, chuki na uchungu katika moyo wake juu ya ndugu mwingine
kanisani.Bwana akasema, “Nilimuonya, lakini alikataa kunisikiliza
mimi”.Mtu huyo alipatwa na ajali na kufa,[Mathayo 5:44] na sasa yupo
kuzimu ya moto.Kuna wanakwaya wengi wenye chuki ndani ya mioyo yao juu ya
wenzao katika Kristo.Hii ni mara mmoja anapoonekana kuwa anakipawa kikubwa
kuliko mwingine.Ndipo watu wanaendeleza wivu na majivuno kwa sababu ya hayo,
wafanyayo hayo wako katika hatari ya kuzimu.[Mathayo 18:4].
MPANGO WA MUNGU.
Bwana aliniambia, “Mpango
wa MUNGU ni mkubwa kwa mwanadamu.Na pale popote MUNGU anapokuwa na mpango na
maisha ya mtu, mipango ya shetanini kuharibu ahadi na mpango wa MUNGU”.Nikamuuliza
YESUKRISTO “Shetani anaweza kuharibu ahadi na mpango wa MUNGU kwa mtu ?”.
Bwana
akasema, “NDIO”,na Bwana anielezea, “Kwenye
kila mpango na ahadi ya MUNGU kwa mtu, mara zote kuna vigezo, na katika hivyo
vigezo, kuna neema na rehema....Neema ni nafasi ya kufanya marekebisho kama mtu
akivunja kigezo chochote.Rehema ni kwa ajili ya mtu kusamehewa na MUNGU.Shetani
atahakikisha unavunja vigezo.Kipindi MUNGU ameweka ahadi na Abraham, Vigezo MUNGU
alivyompa ni kutembea naye kwa uaminifu”.
[Mwanzo 17:1-7].Mungu
anampango kwa ajili ya maisha yako na vigezo vimeandikwa kwenye
maandiko[Wagalitia 5:19-21].Sio hayo tuu MUNGU mwenyewe atakwambia mengi
zaidi.Usipoteze neema katika vigezo vya MUNGU na rehema itakunyanyua
juu.[Zaburi 91:11-12].
MKE WA MCHUNGAJI W.F KUMUYI AKIWA KWENYE UFALME WA
MUNGU.
Tukatoka kuzimu ya moto na Bwana
akanichukua mpaka mbinguni.Nilimuona mwanamke mbinguni, alikuwa mzuri sana,
alitoka nje kwenye nyumba kubwa sana nzuri naye ndiye aliyekuwa mmiliki wa
nyumba hiyo !.
Alikuja kwangu na sura ya kutabasamu, mawazo yake yalikuwa nami
nimefika mbinguni kama mkazi.Nilishangaa nikijiuliza anaweza kuwa nani kwa kuwa
utukufu wa MUNGU ulikuwa umembadili uzuri wa dunia.Bwana akaniambia, “Ni
mke wa mchungaji W.F KUMUYI, Mtumishi wangu”.Nilikuwa na furaha kwa
kuwa alikuwa amejaa utukufu wa MUNGU.Mbingu ni nzuri sana sehemu yote ilikuwa
imejaa utukufu wa MUNGU.
Bwana akanionyesha mimi mto wa
damu, nao ulikuwa baridi na umetulia na ilikuwa kama bwawa la kuogelea, Popote
tunapomtenda dhambi MUNGU na tukaomba msamaha na kutuosha naye hutuosha kwenye
mtu huo wa damu.
Bwana
akanionyesha tarumbeta zitakazotumika kwa unyakuo.Akaniambia ,
“UJIO WANGU UKO KARIBU SANA”.Tarumbeta zilikuwa zinang`aa na
zimetengenezwa na dhahabu safi.Bwana alinionyesha maandalizi ya Unyakuo.
Bwana
akanichukua mimi kwenda kwenye ukumbi mkubwa na nikaona watakatifu wengi akiwa
wamevaa mavazi meupe kabisa, wakiwa wanaimba,wakimsifu MUNGU, wakipaza sauti
kwa Bwana-Utukufu wa MUNGU ulikuwa kati yao.Mbinguni ni kuzuri, kulikuwa
kunanga`aa kila sehemu kwa sababu mwanga wote pale ulikuwa utukufu wa MUNGU.
NYUMBA
KUBWA SANA YA MWANAMKE, MBINGUNI.
Bwana
akanionyesha nyumba nzuri na kubwa sana mbinguni, Nikashangazwa ni nani anaweza
kuwa mmiliki wa nyumba hii.Bwana akaniambia “Ni ya mwanamke na jina lake ni
Margret.Amevuna roho nyingi sana kwenye ufalme wangu !.Roho alizovuna haziwezi
hesabiwa na mtu, Ni tuu MUNGU mwenyewe .Kazi yake imejenga hii nyumba”.
[Mathayo
10:7] Alisalimisha maisha yake Kwangu, na vitu vya duniani vilikuwa si kitu
kwake, Sasa ameishia katika utukufu wa ufalme wangu.Mkristo yeyote anayekataa
kuvuna roho(watu) kuja kwenye ufalme wangu hawezi kuingia katika utukufu
wangu”.[Mathayo 28:19-20],[Mathayo 10:32].
NJIA
YA KUZIMU YA MOTO.
Bwana
alinionyesha mimi njia ya kwenda kuzimu, ilikuwa ina watu wengi katika ile
njia.Baadhi wanaonekana kama wakristo lakini walikuwa wakiendea katika njia ya
kuzimu.Baadhi wameshikana mikono, mume amemshika mkono mkewe huku wakielekea
kuzimu, mke akimshika mkono mume,Wazazi wameshika watoto wao mikono na baadhi
wakienda wo wenyewe.Na kulikuwa kuna mzigo mikubwa mgongoni mwa kila mmoja
wao.Kwa kadiri YESU alivyo kuwa akiwatazama ndivyo alivyozidi kulia kama mtoto.
Niliona
kitu kilichonishangaza sana mimi; Niliona kundi la watu nao walikuwa wanawake
na walikuwa wakijaribu kwa jitihada zote kupita kuingia njia ya mbinguni,
lakini nguvu ilikuwa ikiwarudisha nyuma kuwatoa.Ndipo Bwana akaniambia ,
“Kisicho kisafi hakiwezi kupita kwenye njia Yangu”.[Isaya
35:8-9].Nikamuuliza, “Kitu gani kisicho
kisafi kwao ?” .Bwana akaniambia, “Ni mavazi yao, wanavaa hereni, weavon, mapambo
kichwani mwao(attachments), mikufu, vito.Wanavaa nguo za kiume, wanajaribu hata
kujiremba wao wenyewe---Wanataka kupita kwenye njia yangu.Hiyo HAIWEZEKANI !
utii ni bora kuliko dhabihu !”.....Akaendelea kulia.
[Isaya
3:16-24],[1 Petro 3:3],[Kumbukumbu la torati 22:5].Bwana akalia kwa uchungu na
akalia kwa sauti kama mwanamke wodini.Ninyi mnaodhani unaweza kufanya vyovyote
unavyodhani baada ya kumpa maisha yako KRISTO, Unajidanganya mwenyewe
!.Usisikilize uongo wa shetani, unapozaliwa upya ,ya zamani yamepita [2
wakorintho 5:17].
NJIA
YA MBINGUNI
Bwana
alinionyesha mimi njia ya kuelekea mbinguni.Niliona watu lakini sio wengi kama
kwenye njia ya kwenda kuzimu.Kwenye hiyo njia niliona baadhi wakiendelea mbele,
baadhi wanasonga kwa furaha, na wengine wakicheza kumsifu MUNGU.[2 Wakorintho
13:9], [2 Wakorintho 12:9].
Muda
kidogo nikagundua wako wachache zaidi na hakuna milima mirefu katika njia ile ,
ambayo mtu akifika hapo anatakiwa apande ndipo ashuke kuendelea na safari.Nikagundua
kuna baadhi ya watu walisha vuka vile vilima lakini wanaanza kurudi nyuma,
walikuwa wamechoka kuendelea mbele.
Kama
wewe ni mKristo wa aina hiyo, umechoshwa na majaribu, shida,umasikini na vitu
vingine vingi.Na unadhani uamuzi mzuri ni kuacha wokovu, hivyo acha na umrudie
YESUKRISTO kwa kuwa u kama mtu aliyemkimbia jambo lenye kutisha tuu/hofu na
kuangukia kwenye shimo la simba.Bwana bado anakuhitaji wewe,lakini unatakiwa
uvumilie. “Tunatembea kupitia mateso mengi ili kuingia kwenye ufalme wa
MUNGU”[Matendo 14:22].Rudi kwa YESUKRISTO naye atakuokoa !,Kumbuka mateso ya
wale waliorudi nyuma kuacha kumfuata YESUKRISTO yalivyo kule kuzimu ya moto
[Yeremia 3:21-22].
Niliona
baadhi wamesimama wakiwa hawaendi,wapo tu wamesimama hapo hapo.Kama wewe
umKristo wa aina hiyo unafikiri niendelee kumtumikia MUNGU au niache, Unabidi
uache mawazo maovuna usonge mbele.Chaguo zuri ni kusonga mbele hivyo omba upata
nguvu ya kuendelea mbele[Waefeso 6:18].
Nikaona
wengine wakitambaa, walikuwa wakipenda kuendelea katika njia hiyo, lakini
walikuwa wamechoka.Kama wewe umKristo wa aina hiyo unaogopa wazazi wako zaidi
kuliko unavyoogopa vitu vya KRISTO, unatakiwa uache.Hii ni hatari sana na
baadhi yenu wazazi wenu wanawatesa ninyi, wanawafanya ili mmtende MUNGU
dhambi.Unatakiwa uombe na kusema “hapana” kwa maamuzi ambayo ni tofauti na
mpango wa MUNGU, Bwana anasema, “USIOGOPE”[Mathayo 10:28].
Omba
upate nguvu ya kusimama na kuanza kusonga mbele kwa sababu MUNGU wetu ni mwenye
nguvu.Lia Kwake, naye Atakusikia maombi yako[Efeso 6:14-18],[Yeremia 33:3].YESU
alilia kwa uchungu na ilikuwa huzuni--- Bwana akaniambia mimi “Kimetokea
nini mpaka umekuwa na huzuni ?,Kama kweli una huzuni, ndipo utawaambia watu
kile ulichokiona”.
TUBU SASA
Ni
muda wa kutubu kutoka kwenye dhambi yeyote.Haijalishi ni dhambi ya aina gani
ambayo umeitenda,MUNGU ni mwaminifu kukusamehe wewe dhambi zako zote[Warumi
10:9-10].YESUKRISTO anapenda roho yakona hataki roho yako iende kuzimuya
moto[Habakuki 2:13].MUNGU alimtuma mwanawe wa pekee,YESUKRISTO kufa kwa ajili
ya dhambi zako na zangu !,Yeyote amwaminiye Yeye hata angamia lakini atakuwa na
uzima wa milele[Yohana 3:16].YESUKRISTO ni njia pekee ,ya Kweli, na uzima na hakuna atayeweza kuja
kwa Baba pasipo kwa njia ya YESUKRISTO [Yohana 14:6].
Tubu
sasa na uokolewe[Matendo 17:30-31].Kama ukotayari kumpa maisha yako KRISTO basi
omba sala hii:-
Bwana YESU, Najijua mwenyewe
kama mwenye dhambi , Najijua niko gizani, lakini sasa niko tayari kufanya kile
onachotaka mimi nikifanye.Tafadhali nisamehe dhambi zangu zote,nioshe mimi
katika mto wa damu yako, niponye,nitie nguvu,nipe uweza, na nguvu zaidi dhidi
ya mwili na achilia ufalme wako uje ndani ya moyo wangu.Andika jina langu
katika kitabu cha uzima na iwe furaha kubwa mbinguni juu ya wokovu wa roho
yangu.Katika jina la YESUKRISTO nimeomba .Ameni.
Tafadhali
nakuomba u SHARE kwa wengine nao wapate habari hizi za wokovu lakini ,Kwa
shuhuda nyingi zaidi angalia kwenye www.jasirimbarikiwa.blogspot.com. Ubarikiwe !.
Sifa kwa Mungu
ReplyDeleteAmina
DeleteAmen
ReplyDeleteHaleluya
DeleteAsanti kwa mungu kutujaria kujua hakika Kuna binguni , na jehanamu . WA pendwa tujitahidi kufanya mapezi ya mungu na tutafika binguni. Ephssian 6:10
ReplyDeleteHio maoni yako imekua małefu saidi tena umequiti mandalo mengi sana. Hio ukweli umechanganyikana na Uongo. Na Unasema ułomułka. Mungu?!!ni kweli
ReplyDelete