Watumishi




watumishi
Somo:Sisi tuu wamoja  kama BABA yetu aliye mbinguni-part 1


Neno:  Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 1 Yohana 5:8

Theme:umoja ni asili ya MUNGU

Kama watumishi wa BWANA sisi tunatakiwa kumuiga MUNGU katika utendaji wa kazi yake kwa kuwa wamoja kuineza kweli yake YESUKRISTO.
MUNGU ametuumba kwa mfano wake hata katika utendaji wetu kwa kuwa YEYE ni mwenye umoja , 
“Mimi na Baba tu umoja.” Yohana 10:30. 
basi nasi pia tumeumbwa tutende kazi katika umoja huo huo siku zetu zote.
 Kama watumishi wa MUNGU hatuna umoja tutakosa ujasiri wa kufaidi karama mbalimbali ambazo MUNGU ametujalia,

Kwa kuwa MUNGU ametoa karama mbalimbali,kama ilivyo andikwa Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; “Warumi 12:6.

Kuna mtu mwingine ana karama ya unabii, mwingine kufundisha na kadhalika .
Lakini kama watumishi wa BWANA hatuna umoja  yule mtumishi ambaye hana karama ya unabii na anahitaji unabii atakosa ujasiri wa kuhitaji huduma ya huyu mtumishi ambaye amepewa na MUNGU karama ya unabii,

Vivyo hivyo huyu mtumishi mwenye karama ya unabii akihitaji mafundisho atashindwa kupata kwa kuwa hana umoja katika YESUKRISTO.

Sisi tu wa moja.Na kama tu wa moja basi tuwe na umoja kama BABA yetu aliye mbinguni alivyo na umoja yaani MUNGU baba,MWANA na ROHO MTAKATIFU

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...