Hatua saba(7) unazopitia pindi uombapo.
Ni vizuri kujua namna ya kusali
na kuomba MUNGU kwa kuwa sala na maombi ndio funguo kuu kwa mkristo kupokea
kutoka kwa BWANA.
Imeandikwa “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”- Wafilipi 4:6
Sio maombi ilimradi maombi ,bali
ni maombi ambayo MUNGU anajibu.
Vitu vya kuzingatia kabla
hujaanza maombi ni:-
1.Unatakiwa uwe na neno la MUNGU linalothibitisha ombi lako kwa MUNGU.
Kabla hata ya kuanza kuomba
jaribu kutafuta neno la MUNGU ambalo litathibitisha ombi unalolipeleka kwa
BWANA.
Mfano: “unataka
kumuomba MUNGU upate nyumba/ mtaji / fedha au upate utajiri” basi
muendee MUNGU ukiwa na mstari kama ilivyoandikwa
2 Wakorintho 8:9 -Maana mmejua neema ya Bwana
wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa
tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Ukamuomba
MUNGU kwa hoja kuwa “umeasema ulifanyika masikini ili sisi tuwe
matajiri ,leo naomba ule utajiri ambao kwa huo wewe ulifanyika kuwa masikini”
Au waweza kutumia huu mstari Kumbukumbu la torati 15:4 “Lakini
hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi
akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)”
Nawe
ukamuomba MUNGU kwa hoja ukimueleza kuwa “MUNGU wangu ni ahadi yako toka awali kuwa utanibarikia
mimi na hapatakuwepo masikini kati ya wale wanaokuabudu nakuomba uniondolee huu
umasikini nilionao”.
Kuna maneno
ya MUNGU mengi mengi waweza kuyatumia
tofauti na hayo ambayo unaweza kuyatumia kuthibitisha ombi lako kwa
MUNGU kwa kuwa neno la MUNGU lina pumzi hai ya MUNGU.
“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na
kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika
haki;”-2 Timotheo 3:16.
MUNGU anaangalia neno lake ili alitimize,nawe watakiwa
umkumbushe neno lake linaloshawishi kuwa
ombi lako.
Imeandikwa Maana
mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala
halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena
neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.- Ezekieli 12:25
Tena Imeandikwa “Nanyi
mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani
ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.”- Mathayo 6:7 .
2. Mahali unapotumia kuomba MUNGU
Unapotaka kuomba maombi yako
binafsi chagua mahali pazuri patulivu uweze kuomba pasipo usumbufu .
Imeandikwa “Bali
wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango
wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini
atakujazi.” -Mathayo 6:6
Kama katika sehemu unayokaa kuna kelele na vurugu ,basi
waweza kufungulia redio za injili kwa sauti kipindi wewe unasali,au simu yako au
redio ikiimba nyimbo za injili huku wewe ukisali.
Hapo utakuwa umeepuka
kelele zitazokuhamisha kwenye uwepo wa MUNGU.
3. Kumbuka kutumia jina la YESU pindi uombapo
Zingatia kuomba
kwa MUNGU kupitia jina la YESU.Imeandikwa “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo
nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.” -Yohana 14:13.
Usiombe kupitia
jina lolote bali katika jina la YESU ndilo tulilopewa lenye nguvu na mamlaka
pekee ya kufanya upokee chochote unachoomba kutoka kwa BWANA.
Kuna hatua kwa hatua unapotaka kusali au kumuomba MUNGU.
Sio kwa kukariri sala bali Ili
maombi yako yafike kwa MUNGU na kupata majibu vyema basi ni lazima uombe kwa mtiririko na kwa
mpangilio unaotakiwa.
Imeandikwa “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke,
kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno
yao kuwa mengi”-Mathayo 6:7.
Kwa hiyo kuna utaratibu wa kuomba
vyema na sio kuongea maneno tuu pasipo maana yoyote wala mpangilio.
Hatua saba(7) na mtiririko unaotakiwa kwenda nao unapotaka
kuomba nazo ni :-
1.KUMSIFU/KUMSHUKURU
Unapoanza kusali anza kwa kumsifu
MUNGU kwa kukupa uhai/uzima /afya na hata mshukuru kwa kukupa nafasi ya kusali
pia.Mtambulishe MUNGU
unayemuomba kwa kuwa kuna miungu wengi ,tena mtambulishe kwa majiina
ukimaanisha
Mfano:wewe ambaye NIKO
ambaye NIKO ,MUNGU aliye hai,MUNGU wa miungu ,MUNGU wa israel,MUNGU wa isaka
,yakobo,ibrahim.
Imeandikwa “shukuruni kwa kila jambo; maana
hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” -1 Wathesalonike 5:18
.
MUNGU anastahili kusifiwa na wenye dhambi na wasio na dhambi.MUNGU anastahili
kusifiwa hata kama uanaona hajakusaidia kitu kwa kuwa yeye MUNGU hutuchagulia
kilicho bora kuliko tufikiriavyo.
Huku ukijinyenyekeza na kuona
MUNGU ndiye yeye pekee unayemtegemea kupata msaada kutoka kwake.
2.KUTUBU DHAMBI ZAKO ZOTE.
Hatua ya pili ni kutubu dhambi zako
zote ulizowahi kuzifanya kama unazikumbuka unataja moja baada ya ingine.Omba
msamaha hata kama unajihisi au unajiona kuwa wewe ni mtakatifu,Tubu kwa ajili
ya dhambi unazozijua na zile usizojua !
Imeandikwa “Twajua ya kuwa Mungu hawasikii
wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia
huyo”-Yohana 9:31
“15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu,
nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono
yenu imejaa damu.”-Isaya 1:15
Hiyo inamaana maombi ya mwenye
dhambi ni kelele kwa MUNGU na hayasikilizwi bali mtu anapotubu kwa kumaanisha
kuacha hayo maovu basi naye MUNGU husamehe!. “9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye
ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu
wote.”-1 Yohana 1:9
Unapoomba msamaha basi kumbuka
kusamehe watu waliokukosea kwa kuwa MUNGU hata kusamehe mpaka usamehe
waliokukosea.
Imeandikwa “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na
Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” -Mathayo 6:14 .Ukiomba
msamaha utakuwa unanafasi kama mtoto wa MUNGU kusikiwa ombi lako KWAKE.
3.KUMSHUKURU/KUMSIFU MUNGU.
Hatua ya tatu ni kumshukuru na
kumsifu MUNGU kwa kukupa msamaha wa
dhambi kukupa nafasi nzuri kama mtoto wa MUNGU.
Hapa unamshukuru kwa kuwa
amekusamehe pale ulipo muomba msamehe, na una msifu kwa kuwa amekupa msamaha na
nafasi nzuri yakukusikiliza kwa lolote umuombalo.
4.KUOMBA OMBI LAKO SASA
Imeandikwa “Na huu ndio ujasiri tulio nao
kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”-1 Yohana
5:14
Hatua ya nne ni kuomba ombi lako kabisa,Hapa unaweza
ukaambatanisha maombi matatu kwa imani
huku ukiongozwa na Roho wa MUNGU.Kwa kuwa tayari unakuwa na nguvu za MUNGU.
Imeandikwa “Hata sasa hamkuomba neno kwa
jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”- Yohana 16:24.
Peleka ombi lako kwa MUNGU huku
ukiwa na mstari au neno la MUNGU linalothibitisha kupata ombi lako.
Mfano:Unataka umuombe MUNGU akuponye na
magonjwa basi waweza tumia mstari usemao
kutoka Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa
kupigwa kwake sisi tumepona.
Kwa hiyo unapomuomba MUNGU unaenda na hoja kuu ukimwambia “Eee BWANA kwa kupigwa kwako YESU
sisi tumepona nakuomba niondolee magonjwa haya!”
Katika hatua hii ya nne(4) una
mamlaka ya YESU tena waweza hata kuamuru mapepo na nguvu za giza au kufunga
kila kazi za shetani za uharibifu na ikafanikiwa.
5.KUSHUKURU NA KUMSIFU MUNGU.
Hatua ya tano(5) ya maombi yako
unatakiwa umshukuru MUNGU na kumsifu kwa kuwa MUNGU wetu hupenda kusifiwa na kushukuriwa
hivyo unapaswa kumsifu na kumshukuru MUNGU
kwa ajili ya maombi yote uliyoyapeleka kana kwamba umepata kile ulichoomba
ingawa bado katika mwili huoni kitu.
Imeandikwa “Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa
maana fadhili zake ni za milele”- Zaburi 136:26
6.KUJITABIRIA NA KUKIRI USHINDI KABLA YA KUTUKIA
Hatua ya sita (6) ya maombi
yako ni ya kujitabiria na kukiri ushindi
kabla hujauona.Kiri kwa kusema yote kwa furaha kama umeshayapata kabisa.Imeandikwa
“Kwa
kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”-
Mathayo 12:37.
Wewe mwenyewe ni nabii wa maisha
yako mwenyewe.
Imeandikwa “28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya
wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota
ndoto, na vijana wenu wataona maono; ”-Yoeli 2:28
Mfano:Ulikuwa unamuomba
MUNGU upate mpenyo wa kibiashara au akutoe kwenye umasikini basi
anza kukiri na kujitabiria kwa kusema asante MUNGU kwa kuwa utanifanya niwe tajiri wa aina yake
,najiona nikisaidia watu wasiojiweza, leo BWANA amenikubalia ombi langu nitakuwa
na fedha nyingi zisizo za kawaida.
Jitabiri makubwa kadiri uwezavyo
huku ukiamini kila unachojitabiria na kukikiri .Usiogope kujitabiria mambo makubwa kwa kuwa si wewe ambaye
unaenda kuyafanya bali ni MUNGU mwenyewe.
7.KUSHUKURU NA
KUMSIFU MUNGU
Mshukuru MUNGU kwa sadaka ya
fedha ya kuifanya kazi ya BWANA.
Hatua ya saba(7) ni kumshukuru na kumsifu MUNGU
kwa kukuwezesha kufanya maombi vyema teka mwanzo mpaka mwisho.Mshukuru MUNGU
kwa ROHO wake mtakatifu aliyekusaidia kusali ipasavyo!.
Kama yalikuwa ni maombi ya
mfululizo yaani maombi ya kitu fulani labda ulikuwa kwa muda mrefu unaombea
nchi,labda familia,labda ndoa yako au chochote kilichokuwa kina kusumbua kwa
muda mrefu ,ikiwezekana nenda kanisani au katika watu wenye matatizo na kutolea
sadaka ya kumshukuru.
Imeandikwa “Mtolee Mungu dhabihu za
kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako”- Zaburi 50:14
Kwa kutoa sadaka ya shukurani kwa ajili ya
lile jambo ulilomuomba MUNGU kwa imani.
Itakuwa vyema zaidi kwa kuwa kwa sadaka
hiyo utakuwa umeweka kumbukumbu kwa MUNGU na hatasahau kulijibu ombi lako kamwe.
Asante sana kwa mawaida
ReplyDeletemazuri
asante sana kwa ufuatiliaji na MUNGU akubariki !.
DeleteMUNGU hakubariki sana mtumishi Wa mungu
ReplyDeleteamina, Utukufu kwa MUNGU.
DeleteAmen 🙏🏼
ReplyDeleteUbarikiwe na MUNGU, nakuomba uzidi kufuatilia mafundisho mengineyo.
DeleteAmen mafundisho mazuri yamenibariki sana na kukupa njia na muongozo jinsi ya kuomba kwa Mungu wangu. Barikiwa sana.
ReplyDeleteasante sana kwa ufuatiliaji na MUNGU akubariki !
DeleteMungu akubariki sana, pia nina swali Je, ni siku hipi inayo faa sana mtu kuwa kwenye mfungo
ReplyDeleteAmina.Siku inayofaa sana kufunga ni siku yoyote ile,ila itafaa zaidi siku yenyewe uwe na na muda wa kuomba, kusoma neno la Mungu na kulitafakari kwa utulivu.Kitu kikubwa cha kuzingatia ni kuongozwa na Roho mtakatifu katika kila kitu unachokifanya.
DeleteUbarikiwe Sana mtumishi wa Mungu
ReplyDeleteamina, Utukufu kwa MUNGU.
DeleteAsante Mtumishi wa Mungu, nilikuwa sijui kuomba kwa Mpangilio lkn kwa ninamshukuru Mungu nimejua. Ubarikiwe sana mtumishi
ReplyDeleteamina, Utukufu kwa MUNGU.Nakuomba uzidi kufuatilia masomo mengine mbali mbali ili uzidi kukuwa kiroho.
DeleteHalleluyah
ReplyDeleteAmina,asante sana kwa ufuatiliaji na MUNGU akubariki
DeleteAmen 🙏
ReplyDelete🙏
DeleteMungu akubariki mno maana nimepata Jambo... Mtumishi nisaidie kwa ufupi tofauti ya kuomba na kusali 🙏
ReplyDeleteNi vitu vinavyo endana sana lakini kuna tufauti ndogo tuu.Kuomba lazima uwe unahitaji au shida binafsi ukimpelekea MUNGU, Lakini Kusali ni kumwendea MUNGU ukiwa huna hitaji bali kama desturi njema ya kumfuata MUNGU iinaandamana na kuabudu .
DeleteAmeen barikiwaa
ReplyDeleteLeo nimejifunza kitu kipya, kwanza nikuomba kwa mpangilio alf kuacha kulalamika wakati wakuomba asante sana na ubarikiwe
ReplyDeleteNimejifunza Namna ya kuomba ubarikiwe mtumishi
ReplyDeleteUbarikiwe SANA
DeleteUbalikiwe sana
ReplyDeleteAsante Kwa somo zuri. Ubarikiwe sana
ReplyDeleteAhsante mtumishi wa mungu hakika somo lako n kama dhabihu moyon mwangu
ReplyDeleteAMEN, mafundisho mazuri sana
ReplyDeleteAsante mtumishi
ReplyDelete