Kwanini inanibidi nichukue gharama zote kuacha
kuangalia picha za ngono(porno) ? .
Kazi ya shetani ni kuhamasisha watu kutenda dhambi
sana kwa kuwa mwisho wa dhambi ni mauti na kazi ya MUNGU ni kuhamasisha watu
kutenda mema zaidi kwa kuwa mwisho wa mema ni uzima wa milele.
Kuna vitu vya thamani na vikubwa sana unavipoteza
pindi tuu unapoangalia picha za ngono/porno. Mikanda hiyo ya ngono imekuwa na
majina tofauti tofauti kama vile pilau,picha za bluu,mijengo na mengineyo.
Nini kinatokea pale tunapoangalia picha za
uchi/ngono?,Jibu ni tunaamsha tamaa za mwili na tunakwenda kinyume na MUNGU kwa
kutokukubali kuongozwa na ROHO wa MUNGU bali tunakuwa tumekubali kuutii miili
yetu.
Imeandikwa “lakini
mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini
naye moyoni mwake.” -Mathayo 5:28
Kwa hiyo mtu yeyote anapoangalia picha za ngono/uchi
anakuwa amezini moja kwa moja bila kujijua.Kwa hiyo vitu anavyovikosa baada ya
kuangalia picha za ngono/porno ni:-
1.Unakosa
ROHO mtakatifu
Mtu
anapoangalia mikanda ya ngono(kutenda dhambi) basi ROHO mtakatifu wa MUNGU
anaondoka katikati yake.
ROHO
mtakatifu kazi yake ni kumpa ulinzi ,kumuongoza na kumfunulia mambo ya sirini ya
siku zijazo.
2.Unakosa uwepo wa MUNGU
Unapoangalia
mikanda ya ngono unakosa nguvu ya MUNGU inayoweza kukuletea msaada katika
maisha ya kawaida pasipo wewe kujua.
Mfano
:malaika wa MUNGU wanaokulinda kila mara wanaacha kukulinda pale mtu
anapoangalia mikanda ya ngono(atendapo dhambi).
3.Unakosa uhusiano na MUNGU
Unapoangalia
picha za ngono uhusiano unapovunjika na MUNGU maana yake jina lako linakuwa
halipo katika kitabu cha uzima wa milele kwa hiyo unakuwa haupo katika majina
ya wataokwenda mbinguni.
HAKUNA FAIDA YA KUANGALIA
PICHA ZA NGONO(PORN).
Wimbi la picha za uchi na mikanda ya ngono/porno
katika mitandao ni wimbi la kazi za shetani kwa kuwa yeye hupenda watu wafanye
dhambi zaidi ili kwa kuwa mwisho wa dhambi ni mauti.
Watu wengi wamekuwa wakiangalia picha za ngono/porno
kupitia mitandao mbalimbali na blog bila kujua hasara za kuangalia picha hizo
katika maisha yao ya kiroho na kimwili pia.
Imeandikwa “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala
uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu”-Waefeso 5:3
1.Kuangalia mikanda ya ngono/porno kuna leta laana.
Imeandikwa “wenye macho yajaayo uzinzi, . . . . . . . .
. . . . . mioyo iliyozoezwa kutamani,
wana wa laana;” -2 Petro 2:14
Kuna laana inajitengeneza pale mtu anapojizoesha
kuangalia picha za ngono.
Imeandikwa “Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu
wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na
wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu
ya damu ya watoto wako, uliyowapa;” -Ezekieli 16:36
Imeandikwa “basi,
tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao
wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu
yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote.”- Ezekieli
16:37
Kwa hiyo sii vyema kuziangalia picha hizo za ngono
zinazochochea kutokea laana ambazo zitaziba kuonekana kwa baraka katika maisha
yetu.
2.Picha za
ngono(porno) zina athiri mtazamo hasa katika kufikiri yaani mawazo
Mawazo mabaya huwa yanamtawala mara zote mtu
aangaliae picha za ngono Imeandikwa “Kwa maana moyoni
hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na
matukano;”-Mathayo 15:19
Mtu ambaye amezoea kuangalia picha za ngono(porn)
kila anapoona watu wengine mitaani yeye anawaona au anaweza anza
wawazia/imagine wakiwa uchi na kuwaona wakiwa uchi hata kama amevaa nguo yeye
atawafikiria/imagine wanavyokuaga uchi huwa wanakuaje.
Mtazamo utabadilika kwa kuona ni vyema kuangalia picha
za ngono kuliko kuwa na mwenzi wako.
Inafanya watu wengi wanaoangalia picha za
ngono(porn) kutoridhika pale wanapofanya mapenzi na wake au waume zao kwa kuwa
walitazamia kupata kulingania na kile walichokuwa wakikiona katika mikanda ya
ngono.
Mfano :Mikanda ya ngono inapoonyesha mwanaume mmoja anawaingilia kingono wanawake wanne(4). Basiii hiyo hali inaathiri huyo anaye tazama kwa kuwa naye atatamani apate wanawake wengi kiasi hicho ili kufaidi kama alivyoona katika mikanda hiyo.
3.Kuangalia picha
za ngono(porno) kuna gharimu muda na hata kukupotezea muelekeo.
Imeandikwa “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje,
mkiukomboa wakati.Tuukomboe wakati”- Wakolosai 4:5
Duniani tupo kwa muda kidogo tuu na kila mtu amepewa
lengo na kusudi la kuwepo hapa duniani.
Pia ametupa muda wa kutimiza hayo
makusudi sasa unapokuta mtu anaopenda sana kuangalia picha hizi za ngono anaweza
jikuta muda wake mwingi ukitumika kuangalia picha za ngono/porno katika blog na
website badala ya kulenga kile ambacho ni lengo lake kuwepo duniani kwalo.
Imeandikwa “mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni
za uovu.”- Waefeso 5:16
4.Unakuwa mtumwa
wa kuangalia picha za ngono(pornography/porn).
Ukweli
usiopingika ni huu kuwa kwa kadri unavyozidi kuangalia picha za ngono(porn)
ndivyo hivyo unapakuwa na kiu kubwa ya kuangalia picha za ngono(porn)
tena na tena.
Hatutakiwi tuwe watumwa wa kuangalia picha za uchi
bali tuwe vijana wenye msimamo katika kutimiza kazi au kusudi la MUNGU alilotuwekea hapa duniani huku
tukiukomboa wakati.
5.Kuangalia
picha za ngono(porn) kunaalika roho chafu.
Mtu anapoangalia picha za uchi anajikuta taratibu
anavutwa kufanya vitu vingine kama vile labda awali alikuwa hana tabia za
uzinzi basi baada ya kuwa anaangalia hizi picha za uchi basi anaanza uzinzi,au
umalaya .
Kuangalia picha za ngono(porn) kunaalika roho ya uzinzi,umalaya,ushoga,roho
ya kupiga punyeto hata uvivu.
Njia za kuacha kuangalia picha au mikanda
ya ngono/porno
Imeandikwa “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa
Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”- Warumi 8:14
Kama watoto wa MUNGU hatutakiwi kuongozwa na mwili
bali na ROHO wa MUNGU na ROHO wa MUNGU hupingana na matendo ya mwili.
Imeandikwa “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo
haya, uasherati, uchafu, ufisadi,”-Wagalatia 5:19
Hatutakiwi kujiendekeza kufanya matendo ya mwili kwa
kuwa matendo ya mwili hatutaweza kuyatimiza kamwe na mwisho wa matendo ya mwili
ni kifo/mauti.
Pima
mwenyewe Baada ya kuangalia hizo picha za ngono umepata nini?, na umekosa nini
?,
Ukisha tathimini ndipo uchukue gharama kubwa ya kuamua kuacha kuangalia picha
hizo za ngono kwa maombi na kwa neno la MUNGU.
Usijiulize kwa
nini unapenda kuangalia picha za ngono(porno) bali penda kujua nini
kinachokufanya uangalie picha hizo.
Mipaka yetu kama watoto wa MUNGU kwa
kuwa tuu hekalu la ROHO mtakatifu.
1.Hatuufuati
mwili bali tunafuata ROHO wa MUNGU aliye ndani yetu.
“Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;” -1 Wakorintho 6:19
Ili tuwe watu wakubwa wa kiroho hatutakiwi kuufuata
mwili kwa kuwa sisi sii mali yetu wenyewe bali ya MUNGU.Hivyo basi inatubidi
tuishi kama yeye MUNGU aliyetuumba anavyopenda sisi kuishi.
Imeandikwa “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru;
lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”
-Wagalatia 5:13
2.Kuwaza
kwetu na kuwe na mipaka katika ROHO mtakatifu.
Ili tuache kuangalia
picha za ngono inabidi tujifunze kuwa za sawa sawa na ROHO wa MUNGU apendavyo
na sio kuwaza mambo ambayo ROHO wa MUNGU hatayapenda .
Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika
nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada
ya sanamu;”- Wakolosai 3:5
3.Ujana
wako usiwe kigezo cha kukufanya uende
kinyume na taratibu za MUNGU
MUNGU anatuonya kama wanawe kuwa ujana wetu isiwe ni
kisingizio au kigezo chochote chakutufanya kuwaka tamaa aua kuishi maisha ya
kutenda dhambi bali tuwe mfano na kielelezo na wenye msimamo katika kuacha
kuangalia picha za ngono.
“Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate
haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo
safi.”- 2 Timotheo 2:22
4.Vita
vikubwa vimo ndani yetu na sio nje ya mwili
Imeandikwa “Vita
vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa
zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?” -Yakobo 4:1
Vita vipo vikubwa hasa pale unapotaka kuacha
kuangalia picha za ngono sasa hapo unatakiwa ujiwekee msimamo katika kutenda
mazuri ya kila namna ili kukuwezesha kuacha kuangalia picha za ngono.
Dunia inapita na pia kuna taji kubwa la kukabidhiwa
kama mtoto wa MUNGU baada ya kuishi duniani.
“Na
dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu
hata milele.” -1 Yohana 2:17
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!