Jinsi ya KUSIKIA SAUTI ya MUNGU

Watu wengi wanamwabudu MUNGU lakini hawawezi kumsikia MUNGU na pengine hawajui anachokisema kwao kuhusu mambo mbalimbali ya maisha yao. Sasa utajifunza au jinsi gani ya kumsikiliza MUNGU anapo nena nawe.


Watu wengi hujiuliza kwanini MUNGU asiongee nasi kwa wazi wazi  na kama sisi nasi tunavyowasiliana na wanadamu wenzetu na kuelewana ?.
Yawezekana nawe pia huwa unajiuliza swali hilo hilo ,Jibu ni hili: Imeandikwa hivi “Mungu ni Roho, ………………….” -Yohana 4:24,Jibu ni kwamba MUNGU wetu ni ROHO kama unavyojua ROHO haionekani kwa  macho ya nyama bali ni macho ya KIROHO ,na ROHO haiongei ukasikia kwa masikio haya ya mwilini bali yale masikio ya KIROHO.Hivyo ndiyo maana inakuwa si kawaida kumsikiliza MUNGU wazi wazi kama unavyo ongea na mwanadamu mwenzio.

Ukweli ni huu kuhusu kumsikiliza MUNGU kuwa kuna siri.Siri ni hii ya kuwa Kama ilivyo katika maisha ya kawaida ilivyo ngumu kuongea na mtoto mchanga naye mpaka akakuelewa nawe ukamuelewa ndivyo ilivyo katika habari ya kumsikiliza MUNGU.
Hii inamaanisha jinsi unavyokuwa kiroho zaidi ndiyo una nafasi kubwa na nzuri zaidi ya kumsikiliza MUNGU kuliko wale ambao bado ni wachanga wa kiroho.

Kumbuka tena siri kubwa ni hii kuwa “Kama wewe unavyopata shida kumsikiliza na kumuelewa mtoto mdogo au jinsi ilivyoshida kumuelezea/kumuelewesha  kitu fulani mtoto mchanga ndivyo ilivyo katika mambo ya kumskiliza na kumuelewa MUNGU”.
Hii inamaanisha katika kumsikiliza MUNGU kuna viwango tofauti tofati kulingana na jinsi ambavyo umekua KIROHO kiasi gani.

Mtu ambaye ni mchanga kiroho hivyo hivyo naye MUNGU huongea naye kichanga changa .
Kama ilivyo ki kawaida kuwa huwezi kutaka kujadiliana na mtoto mchanga ili akushauri kuhusu jambo lolote bali utacheza cheza naye tuu kwa kuwa ni mchanga na hawezi kuelewa mambo makubwa.

Kwa mtu ambaye ni mkubwa kiroho yaani amekomaa kiroho huyo MUNGU huongea naye ki-utu uzima tena hujadiliana naye kwa kuwa ana kiwango kikubwa.
Watu wengi hudhani kuokoka na kukaa muda mrefu katika wokovu ndio ukomavu au ndio kukuwa kwenyewe KIROHO,Lakini Hasha ! si hivyo hata kidogo bali ukuaji wa mtu kiroho hupimwa na MUNGU mwenyewe naye huangalia vitu vingi sana ambayo waweza kujumisha yote kwa kusema tuu kuwa hupima uaminifu wako katika mambo yake.

Hivyo basi ukitaka kusikia sauti ya MUNGU kwa undani sana na kwa uwazi sana unatakiwa ujitahidi ukuwe KIROHO naye MUNGU atasema nawe kwa uwazi zaidi.

MUNGU huongea na watu kupitia njia mbalimbali kutegemeana na kiwango cha kiroho ambacho mtu huyo amefikia.

Baadhi ya njia ambazo MUNGU hutumia kusema na watu
Kuna njia mbali mbali ambazo MUNGU hutumia kuongea na watu naye MUNGU hutumia njia hizo kwa watukutokana na viwango vyao vya KIROHO.Njia hizo baadhi zao ni :-
1.MUNGU huongea kupitia (Bibilia)NENO LA MUNGU.
Hii ni njia KUU , ya MSINGI na ya PEKEE ambayo watu wengi ambao hawajakuwa kiroho na wengine ambao wamekuwa kiroho ,MUNGU hutumia kusema nao kwa njia ya neno lake.
Imeandikwa “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.”- Yohana 1:1-2.

Unaposoma neno la MUNGU huku ukiongozwa na ROHO mtakatifu ujue kabisa hapo unamsikiliza MUNGU mwenyewe !.Tunapaswa kujua kuwa kwa njia ya ROHO mtakatifu BIBILIA ina kila sauti ya kutusaidia katika maisha yetu !.
Imeandikwa-“Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.”- Mathayo 22:29. Hii inamaanisha kwenye maandiko kuna sauti ya kila jambo yaani jambo la sasa na la yajayo ambayo itakufanya usipotee hata kidogo.


NAMNA YA KUENENDA :Soma BIBILIA yako kwa makini sana huku ukiwa umekwisha mualika ROHO mtakatifu ili akuongoze na unapoisoma tafakari ukifananisha neno la BIBILIA ulilolisoma na kitu unachotaka ndipo utapata namna ya kuenenda katika kitu ulichokuwa ukikitakia sauti kutoka kwa BWANA.
Ifuatishe sauti hiyo kwa kuwa katika hiyo kuna wokovu.


2.MUNGU huongea kupitia watu wanaokuzunguka.
Njia hii hutumiwa sana na MUNGU, yaani njia ya kuachilia sauti YAKE kwa watu wake.
Mara nyingi njia hii MUNGU huitumia kwa wale ambao wameanza kukuwa kidogo kiroho. Imeandikwa Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.”- 2 Samweli 16:23

Umesoma huo mstari kwamba mtu alipokuwa akishauriwa na Ahithofeli ilikuwa ni kama vile MUNGU mwenyewe anamshauri mtu.
Kuna watu ambao MUNGU amewajaza hekima na maneno yake kiasi kwamba kwa kila jambo ambalo unapitia katika maisha yako wao wanakuwa wana jua kabisa sauti ya MUNGU kwa ajili yako.

Wewe unapomuomba MUNGU jambo fulani mfano unamuomba MUNGU akupe kazi na baada ya kuomba MUNGU ukashangaa tuu ukakutana na mtu ambae hujawahi kumwambia kuwa unatafuta kazi na anakwambia namna ya kupata kazi, wewe hapo tambua ni MUNGU mwenyewe anamtumia huyo mtu kuongea nawe kwa habari ya kupata kazi ambako ulikuwa ukimuomba.

Unapomuomba MUNGU jambo fulani au unataka kusikia sauti ya MUNGU kwa habari ya jambo fulani na sii muda ukakutana na mtu ambaye hajui shida yako akawa anayazungumzia yale ambayo ulikuwa ukimuomba au akitaka kuyajua hapo ujue ni MUNGU mwenyewe anaongea nawe kupitia mtu huyo!.

3. MUNGU huongea kupitia matukio ya HALI mbalimbali YENYE ishara.
Hii ni ngazi kubwa zaidi ya kumsikiliza MUNGU ambayo ukitaka kusikia sauti ya MUNGU kwa viwango hivyo unabidi uwe umekua zaidi KIROHO.
Ngazi hii inayohitaji uwe na uhusiano yaani ukaribu mkubwa na MUNGU ukisaidiwa na ROHO wake mtakatifu.
MUNGU anaweza kuzungumza kwa kutumia tukio lolote au kutumia mnyama wa aina yeyote na pasipo kujali hali au mali.

ROHO mtakatifu anahisia ambazo zinaelezea hali ya mambo ya kiroho nayo huathiri mtu kama mtu huyo akiwa na uhusiano mkubwa naye huyo ROHO.
Imeandikwa “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, …………………………………..” -Luka 10:21.
Umeona kwa ROHO mtakatifu waweza kukaa na  furaha zaidi na furaha hii isiyo ya kawaida.
Imeandikwa “Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.”- Matendo ya Mitume 13:52
Inahitaji umakini kwa kuwa watu wengi huwa MUNGU huongea nao kupitia ROHO mtakatifu lakini wao huwa hawasikii neno lolote kutoka kwao,
Imeandikwa “Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,”- Waebrania 10:15

Mfano: Unaomba MUNGU labda kuhusu safari yako na unataka kujua kama kweli MUNGU amekuruhusu kwenda itakuwa salama au usubiri kidogo !.
Sasa baada ya kumuomba MUNGU ukajikuta una Amani moyoni mwako yaani AMANI ISIYO YA KAWAIDA ambayo hukuwa nayo kabla ya kuomba ,ujue MUNGU anakutaarifu kupitia ROHO wake mtakatifu kuwa hakuna shida katika safari yako.


Na pengine baada ya kuomba ukajikuta unahuzuni au hofu kubwa iliyokujia baada ya kuomba yaani hujawa nayo kabla ya kuomba lakini baada ya kuomba ndiyo huzuni hiyo ikakujia ujue MUNGU anakutaarifu jambo sio zuri katika safari yako hivyo ROHO mtakatifu hupasha hisia kwa nguvu ya MUNGU ambayo inasauti kabisa na hutoa maelekezo namna ya kufanya ,inaweza kukwambia usubiri kidogo au usiende kabisa ya tegemeana.

Angalizo kuu ni kwamba njia hii MUNGU hitumia kwa watu waliokwisha kukomaa kiroho yaani sio watu ambao ni wachanga bali ni wale ambao wanauelewa mkubwa wa mambo ya MUNGU.

Hisia zinaweza kuwa kusisimka nywele kupita kiasi ambayo mara nyingi humaanisha kuna hatari hiyo sehemu au kuna mvutano kati ya nguvu za MUNGU na za shetani,
Yaweza kuwa amani  isiyokuwa ya kawaida,furaha,huzuni isiyokuwa ya kwaida …. Na n.k
Kikubwa ni hiki njia hii MUNGU huitumia kwa wale watu waliokuwa wamekomaa kiroho ambao wana uwezo mkubwa wa kupambanua jema na baya.

4.MUNGU huongea kupitia NDOTO .
Imeandikwa “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.”- Mwanzo 20:3
MUNGU ni Yule Yule jana ,leo na hata milele hivyo kama alitumia ndoto kuzungumza na watu wa zamani hivyo hivyo hta sasa hataacha kuzungumza na watu kupitia ndoto.

Kama unataka kumsikia sana MUNGU kupitia NDOTO basi una bidi uwe  muombaji sana hasa wakati wa kwenda kulala, Mwuombe MUNGU karibia hata masaa mawili(2) kwa kuwa unapomuomba MUNGU uwepo wake huwa una shuka na katika uwepo wake huwa kuna sauti ya MUNGU ambapo kama ukiwa umelala unapata sauti ya MUNGU kwa ufasaha zaidi kwa sababu ya uwepo wake.
Mungu hatakaa aache kuongea na watu wake kupitia ndoto na katika ndoto MUNGU hutuonya,hutufundisha na kutuelekeza pia inategemeana na jinsi apendavyo
Imeandikwa “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”- Mathayo 2:12

Kwa mafundisho mengi zaidi ya jinsi ya kufsiri ndoto bonyeza hapo....  . ..http://jasirimbarikiwa.blogspot.com/2015/09/jinsi-ya-kutafsiri-ndotomaono-yako.htmll

5.MUNGU huongea kupitia MAONO / UNABII.
Imeandikwa “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”- 2 Petro 1:21.
Hii ni namna ya MUNGU ambayo huitumia kuwasiliana nasi na njia hii MUNGU huitumia kwa watu ambao wamekuwa kweli kweli kiroho yaani watu ambao ni well advanced Spiritual.

Namna pekee ya kufikia kiwango cha kumsikia MUNGU kupitia njia hii ni kupitia maombi yaani mtu anayeomba  muda mwingi na kisahihi huku akijua neno la MUNGU.

Mara nyingi imekuwa ni karama MUNGU kuongea na watu kupitia njia hii kwa kuwa kwa kipawa hicho MUNGU huweza kufungua watu kwa kuwajulisha sauti ya MUNGU kwao.

Watu waliopewa karama na vipawa hivyo ndiyo tunawaita manabii Imeandikwa “Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.”- Hesabu 12:6
Ni ahadi ya MUNGU kwamba ataongea nasi kwa njia hii kwa kuwa ataachilia ROHO yake kwetu na kwa ROHO hiyo tutapata kuona na kusikia sauti yake . Imeandikwa “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.”- Matendo ya Mitume 2:17

6.MUNGU huongea kupitia sauti KABISA masikioni mwako yaani WAZI WAZI BILA mafumbo.
Njia hii mara nyingi ni kwa neema kubwa na pia ni karama  kwa ajili ya kanisa katika kulikosoa ,kulirekebisha na kulitia moyo ili kulijenga imara.


Imeandikwa “Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”- Hesabu 12:8

Watu wote ambao MUNGU alikuwa akiongea nao waziwazi walikuwa hajafanya jambo lolote lilo wafanya wawe qualified kusikia sauti hiyo yaani watu wote waliosikia sauti ya MUNGU wazi wazi bila ya mafumbo hawajafanya jambo ambalo liliwafanya wastahili kusikia sauti hiyo bali ni neema tuu ya MUNGU.


Soma mfano wa sauli alikuwa ni mtu aliyelitesa kanisa lakini neema ya MUNGU ilimuangikia na akasikia sauti waziwazi ikimkemea kuhusu kitendo kibaya anachokifanya kuhusu kanisa  Imeandikwa “Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi” -Matendo ya Mitume 9:4

Ngazi hii haina kanuni kama sauti zingine za MUNGU kwa kuwa MUNGU kwa neema yake tuu anaweza kunena nawe kwa sauti juu ya jambo lolote lile kwa sauti yake pasipo mafumbo.
ANGALIZO KUU :Kama Ilivyo kwamba MUNGU anaweza kuzungumza na watu wake pia vivyo hivyo  shetani aweza kuongea na watu wake.
Namna pekee ya kutambua hiyo ni sauti ya MUNGU au ni ya shetani ni namna moja tuu kuwa kama sauti unayoisikia inapingana na neno la MUNGU(BIBILIA ) ujue hiyo ni sauti ya shetani na kama hiyo sauti haipingani na neno la MUNGU ujue hiyo ni ya MUNGU.

Mfano:Umekaa sehemu nawe ukasikia sauti ikikwambia “nyanyuka nenda kaibe sehemu fulani......”  na haujaona mtu yeyote akisema ,  hata kama akisema anayenena sauti hiyo ni YESU wewe ikatae na kuikemea katika jina la YESU, kwa kuwa YESU hawezi hata siku moja kujipinga  na NENO lake kwa kuwa neno lake (BIBILIA ) linakataa kuiba hivyo kataa kwa kuwa sauti hiyo ina pingana na NENO la MUNGU hivyo sii sauti ya MUNGU bali ni ya shetani.

________

24 comments :

  1. Somo zuri, kwa kuongezea kuna somo linaitwa NAMNA YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NAWE...Naamini kuna mtu ataongeza maarifa zaidi juu ya somo hili...kuwa kusoma fuata link hii >>> https://wingulamashahidi.org/2018/10/22/namna-ya-kuitambua-sauti-ya-mungu-inapozungumza-na-wewe/

    Ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  2. Unapo sema mtumishi kuwa bamna ya kutofautisha kati ya sauti ya mungu na ya shetani ni kutumia neno kama sauti ina pinga neno basi ni ya shetani wakati mwingine roho anaweza kupinga hata safari yakwenda kuhubiri na kushuhudia mfano MATENDO YA MITUME 16;6 utaona mitume wana katazwa kwenda asia kuhubiri naalie wakataza ni ROHO MTAKATIFU NA KUHUBIRI NI AGIZO LA BWANA YESU HIVO UTOFAUTI WA SAUTI SIO KWENYE NENO TU 0716806911 hii ni namba yangu ya whatsapp njoo tujadili huku mtimishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walikatazwa kwenda kuhubiri Asia lakini hawajakatazwa kuhubiri maeneo mengine. Tena walikatazwa kwa muda huo bali sio siku za maisha yao.
      Maelekezo ya namna ya kufanya kazi yake Mungu na wakati mzuri wa kutimiza sio kupinga neno.Hakuna sauti ya Mungu inayoweza kupingana na neno lake.Nilichokuwa ninakiaangazia ni msingi wa kumsikia Mungu(basic ) sasa inapotokea hayo mengine yanayopingana na msingi yanatokea kama dharura tena ni tahadhari.
      Ndio maana ni mara chache sana hivyo vitu vinavyopingana na neno kutokea.
      Mungu akitupa nafasi zaidi tutajifunza undani wa sauti ya Mungu yenye kuonekana kama inapingana na neno lakini kimsingi hakuna sauti inayotoka kwa Mungu ikapingana na neno lake.
      Namba: +255786892838

      Delete
  3. Haleluya haleluya!
    Nimejifunza sana ubarikiwe

    ReplyDelete
  4. Barikiwa nà Bwana somo limenifaa

    ReplyDelete
  5. Asante Sana mtumishi kwa somo limeeleweka Sana MUNGU akubariki Zaid na Zaid AMEEN

    ReplyDelete
  6. MUNGU wambinguni azidi kuku bariki, naomba WhatsApp number tafazali, yangu:+243826992818

    ReplyDelete
  7. Mafundisho mazuri sana.

    ReplyDelete
  8. Mungu akupe kuishi tule mezani kupitia wewe barikiwa sanaaa🙏

    ReplyDelete
  9. Barikiwa mtumishi wa Mungu

    ReplyDelete
  10. Amen, mafundisho mazuri ya kufanya ukue kiroho

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...