SIRI ZA MBINGUNI NA KUZIMU SEHEMU YA TATU(3)

Mwisho wa dunia hii uwadia hivi karibuni.Hivyo uwe mtu wa kukesha a kuomba(1 Petro 5:7).Namshukuru MUNGU kwa ajili ya hii neema juu ya maisha yangu. “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.” ( Zaburi 28:7 ).Bwana aliniahidi kunitembelea tarehe 9 februari ,2013 na akafanya.Yeye ni MUNGU mwaminifu sana.( Zaburi 33:11).

Siku ya tarehe 9 ya mwezi wa February 2013, mishale ya saa Saba(7) mchana, Nilikuwa nimejilaza kitandani na nikasikia sauti ikisema, “Huu ndio muda mwanangu, Jiandae mwenyewe sasa hivi !” Ndipo nikaanza kuomba damu ya YESU inisafishe na kunitakasa na kunifanya niwe safi.Ghafla usingizi mzito ukanijia.Nilipofumbua macho , nikajikuta kwenye chumba ambacho nilikutana na YESU mara ya kwanza.Nikamuona YESUKRISTO anaingia.Akasema, “Mwanangu, nataka nikuonyeshe mambo mengi leo , kwa ajili ya siku za mwisho, Kwa kuwa hii ni mara yam wish kukutembelea wewe.Unatakiwa uwaambie kile ulichokiona kwa sababu haukuwa unawaambia watu wengi kuhusu yale niliyokuwa nakuonyesha wewe kipindi cha nyuma”.Bwana akaanza kulia kwa sababu ya haya.Nilikuwa na huzuni alipokuwa akilia kwa ajili ya uzembe wangu.Tulipotoka katika kile chumba , Bwana akaniambia mimi, “Mwanangu, njoo. Ngoja nikuonyeshe Hukumu Kuu.”Ndipo tukafika mbele ya enzi kubwa.

WAUAJI
Tulipofika mbele ya enzi kubwa nikamuona mwanamke pale akisema, “Nisamehe sana.” Bwana akaniambia mimi, “Muangalie yule mwanamke anaeye lia.Anajua hawezi kuingia mbinguni na ndio maana analia.”Nikamuuliza Bwana niambie mimi sababu ,kwa nini anahayo mawazo.Bwana akanijibu, “Mwanangu, muangalie.”Tazama nikaona historia ya maisha yake.Alikuwa mKristo alipokuwa duniani.Alikuwa akitafuta mtu wa kumuoa na Bwana akamwambia kuwa mvumilivu, lakini tamaa yake ya kuolewa ilikuwa kubwa mno.Haku subiri muda wa Bwana.Badala yake akamuua rafiki yake kwa sumu, rafiki yake akafariki(Mathayo 5:21).Ndipo akafanya mpango akaolewa na huyo mume wa rafiki yake.Baadae mume wake akagundua kuwa ndiye aliye husika kumuua mke wakeyaani mke wake wa kwanza.Mwanaume huyo naye akamuua yule mwanamke pia kwa sumu na ndiyo maana mwanamke yule alikuwa akilia sana mbele ya enzi ya hukumu( Luka 11:47).
Bwana akasema, “Nalimuonya asifanye hayo lakini hakunisikiliza mimi na sasa yuko analilia kusaidiwa na ili apate nafasi ya pili.Hio haiwezekani, ufalme wangu ni sehemu takatifu.Sio sehemu ya wauaji.Nilikuonya utubu lakini hukunisikiliza mimi.Umechelewa kwa wewe!”(Isaya 59:1-3).Bwana akamwambia, “Ondoka kwangu !” na nikaona kimbunga kikubwa kikambeba mpaka kuzimu !.(Mathayo 25:41,46).Usiue au usinyonge kwa sababu afanyaye hayo ni hatari kwa hukumu.Tubu sasa na uokolewe.Tukaondoka hiyo sehemu.
Tafadhali elewa hii:KRISTO anakuja tuu kwa ambao ni WAAMINIFU,WAKESHAO,WAANGALIFU.Sio tuu yatosha kuwa unasifa za kuingia mbinguni bali unatakiwa uendelee kila muda kuwa safi , tayari kwa ujio wake.Fanya maisha yako yaone kila siku tazamia maisha yako ya milele.Haitoshi kuonya na kuwaangalia wengine.
Unatakiwa pia ujiangalie na wewe mwenyewe na kuendelea mbele na wokovu wako kwa ajili ya roho yako.Popote unapofikiri ujio wake KRISTO na ukajawa na hofu au mashaka, hiyo inaonyesha kuna kitu hakiko sawa katika maisha yako na unatakiwa kumruhusu Roho mtakatifu kufanya kazi yake ndani yako.(Wafilipi 2:12-13).
Ni bora uende nae kwenye unyakuo kuliko kuachwa.Kama ukiachwa, mpinga KRISTO atakukejeli na kudharau Imani yako, utakuwa kwenye adhabu kubwa kwa ajili uliijua kweli na ukaiacha.Vipi kama ukifa kabla ya unyakuo? Unatakiwa uwe tayari kwa kurudi kwa Bwana.Kama ukifa na ukawa hata unadoa moja kwenye vazi lako utatupwa.[Note:Hii sentensi itasababisha kutoeleweka sana kwenye kanisa, 1 Yohana 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.]. Kama unaendelea kumtenda dhambi MUNGU na wafikiri bado una muda wakutubu unajidanganya mwenyewe.Ni bora utubu dhambi zako SASA kwa sababu kesho inaweza ikawa umechelewa kwa wewe. “USIUE ! ”
Bwana akanichukua mimi mpaka Kuzimu.Tukapita kwenye handaki lile lile ambalo tulipita mara ya kwanza na tukafika kuzimu.Kuzimu imejiongeza yenyewe kwa sababu shetani anafanya kazi kwa bidii. (Isaya 5:14)
MIAKA 250 AKIWA KUZIMU.
Nalimuona mtu akilia na kupiga kelele ndani ya Kuzimu ya moto akisema,”Uko hapa kuniokoa mimi?,Nipo hapakwa miaka 250.Nimekusubiri kuona kama nitampata mokozi, lakini nilishakata tamaa.Lakini sasa nimekuona wewe, nina mashaka kama uko hapa kuniokoa mimi.” Bwana akamwambia, “Nilituma watumishi wangu wengi kwako kukwambia utubu lakini hukunisikiliza mimi.Walikueleza ukweli kuhusu kuzimu ya moto lakini uliwaambia sio kweli; ni utani na ukadhani maisha yako ni mazuri tuu.Ulitumia muda wako tuu kwenye kunywa pombe, kwenda hoteli moja baada ya ingine, kufanya uzinzi (1 Wakorintho 6:9-11, Yakobo 4:4).Ulikuwa ukiumwa sana kiasi kutaka kufa , lakini sikuruhusu ufe ili uweze kutubu na kuokolewa lakini haukutaka kusikia jina langu likitajwa.Sasa ndio unakumbuka kumtafuta mokozi.Siwezi kukuokoa tena.Umechelewa” (Mithali 1:24-33)
Bwana YESU alikuwa akilia alipokuwa akiongea na huyo mtu kwa sababu hafurahii kifo cha mwenye dhambi.(Ezekieli 18:30-32).Hapa ulipo duniani unayo nafasi ya kutubu, lakini baada ya kufa, hakuna tena nafasi ya kutubu.YESUKRISTO ndiye pekee mwokozi wa wote wanao ishi lakini sio waliokufa.
Pumzi yako ni nafasi yako.(Muhubiri 12:1-8) tukatoka hiyo sehemu.
BINTI YA MTOTO WA MIAKA 15
Bwana akanichukua mpaka sehemu ingine ya kuzimu.Nikamuona mtoto akilia sana.Kulikuwa na funza na wadudu wengine wengi sana mwilini mwake.Anapomtoa mmoja ,funza wengine wengi wanakuja katika sehemu hiyo aliyomtoa.Alipotuona ,alikuwa akilia ili kupata msaada.Nikamuuliza sababu ya yeye kuwepo hapo.Akaniambia historia ya maisha yake,akasema “Nilipokuwa duniani, nilipenda kwenda kumbi za starehe kucheza(clubs to dance), [1 Timotheo 5:6].Wazazi wangu hawajawahi kunionya kwa sababu nilikuwa ndiye mtoto pekee walionizaa.Nilipenda kutembea na wavulana kufanya ngono nao.( 1 Wathesalonike 4:3-8)(Waefeso 5:3-6), nilisikia kuhusu kuzimu lakini sikutaka kuwasikiliza.Marafiki zangu wengi waliniambia nitubu nami nikawa nawachukia.Nilikuja kupata ujauzito na mama yangu akanikumbusha juu ya ndoto zangu za kuja kuwa mwanasheria.Kwa sababu ya hiyo niliamua kutoa ujauzito na kwenye hali ya kutoa nikafariki nami.Ndipo nimeishia hapa kuzimu na nipo hapa kwa miaka kumi sasanikiteswa na kuungua moto.Nikiondoa funza mmoja basi wengi zaidi huja.Tafadhali nisaidie.Sasa nipo tayari kutubu.” Nilipatwa na huzuni kubwa sana kusikia hayo.Bwana akamwambia , “Huwezi kutubu tena.Umechelewa.” Bwana alikuwa akilia kwa uchungu sana kwa ajili ya huyo mtoto lakini hakuweza kumuokoa.Yule mtoto alilia kwa kupiga makelele sana akisema, “Hapana ! hapana ! hapana! Hapana ! Nimoto sana nataka nife !”Lakini hakuweza kupata kufa.(Ufunuo 9:6) Nikamuomba Bwana anitoe huko kwa sababu sikuweza kuvumilia kuangalia mateso wanayopata.
Wazazi nisikilizeni,Mfundishe mtoto wako katika njia ya Bwana.Wafundishe Neno la MUNGU.Wasahihishe pale walipofanya makosa tofauti na maagizo ya Bwana.(Waefeso 6:1-4) (1 Yohana 2:1-6). Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).Tukatoka hiyo sehemu na kwenda sehemu ingine.
MTOTO WA KIKE WA MIAKA 14
Tunatakiwa tuwe makini na kujiondoa wenyewe kutoka kwenye dunia ya dhambi kwa sababu uvumbuzi mwingi unatuharibu sisi mbele za Bwana(Mhubiri 7:29).Bwana akanionyesha msichana akiwa Kuzimu, Mateso aliyokuwa akiyapata yalikuwa mazito na ya kutisha na likuwa akipiga makelele, “Inatosha ! inatosha! Inatosha ! Tafadhali nitoe !” Alikuwa akitumia mkono wake wa kushoto kuziba sikio lake kipindi akijichua(masturbating) na kitu cha moto sana kwa mkono wake wa kuume.{alikuwa akilazimishwa na mapepo kujiingiza hicho chuma cha moto ukeni na kukitoa mara zote }.Alikuwa akilia kwa uchungu lakini hakuacha kufanya vitendo hivyo.
Nikamuuliza yeye kwanini anafanya hivyo huko motoni nilipata historia ya maisha yake, “Nilikuwa na miaka 14 nilipofariki.Nilipokuwa duniani, nilipenda kusikiliza miziki ya kidunia.Na muda wowote nilipozisikia nilikuwa napatwa hisia za mapenzi ambazo zilinipelekea kujichua(masturbate).Niliwahi sikia kuhusu sehemu hii ya mateso, lakini siku amini kama iko kweli.Watumishi wengi wa MUNGU walinionya kuhusu miziki ya kidunia lakini niliwaita wapumbavu.Walinionya kwenye mahubiri yao kuwa kujichua/punyeto (masturbation) ni dhambi , lakini niliwaambia MUNGU ni mwenye rehema.Sasa nimeamini sio wajinga.Sababu ya kujishika sikio ni kwa sababu bado nazisikia nyimbo za kidunia na zinaniumiza sana.Nilikuwa najichua kutumia kitu nilipokuwa duniani ndiyo sababu ya kunitesa mimi motoni kwa jinsi hii.Tafadhali nisaidie mimi, siwezi kuacha na inaniumiza sana !”
Bwana akamwambia , “Siwezi kukusaidia wewe tena.Umefanya neema yangu kuwa si kitu ulipokuwa duniani, lakini mahali hapa,hakuna tena neema zaidi.Umechelewa kwa wewe kutubu !” Alikuwa akipiga kelele na kulia lakini Bwana alimwambia, “Siwezi kubadili maneno yangu.Yameandikwa tayari.Neno langu litasimama milele(Mathayo 24:35)(Mathayo 13:31) Wazazi,tafadhali mjali na uwatunze watoto wako(2 Wakorintho 12:14)(Waefeso 6:1).Kumbuka hasira ya MUNGU inakuja kwa watoto wasio watii.(Wakolosai 3:6)Tukatoka hapo na kwenda sehemu ingine.
MTU WA MIAKA 25
Bwana akanichukua mpaka sehemu ingine kuzimu ambapo niliona mtu akilia kwa sauti, “Nitasikia !, nitasikia ! tafadhali niko tayari kusikia !”Nikamuuliza kwa nini ndipo akasema, “Nilipokuwa duniani, nilipenda kufanya mapenzi na wasichana hasa wanaojiuza/makahaba.Rafiki yangu aliniambia nitubu na niokolewe lakini nikamjibu sitaki kusikia ujinga huo wa mahubiri-Niko tayari kwenda motoni,we niache kivyangu.Lakini sasa nipo tayari kusikia na kutubu.Tafadhali ! tafadhali nisaidie mimi ! ”
Bwana akamwambia, “Nilikupa neema ya kutosha mpaka ulipokufa umri wa miaka 25, lakini hukusikiliza maonyo yangu.Sasa unaomba kusikia.Umechelewa !,Hakuna mtu awezaye kukwambia kuhusu MIMI hapa kwa sababu kila mtu aliyepo hapa anatafuta njia ya kutoka humu.Kila roho ifikayo hapa haiwezi tena kutoka.Umechelewa(1 Wathesalonike 4:3).Mwili wako sio kwa ajili ya uasherati(1 Wakorintho 6:13).”
Mtu huyo akalia.Akimuomba Bwana amtoe hiyo sehemu ,sikuwa na muangalia tena na tukatoka hiyo sehemu ya kuzimu.
UFALME WA MUNGU
Bwana akanichukua na kunipeleka Mbinguni.Bwana YESUKRISTO asifiwe ! Baraka kwa Bwana Mungu wa Israel kutoka milele na milele ! Ameni na Ameni(Zaburi 41:13).Mbinguni ni pazuri sana.Ardhi yake ni kama kioo.Nilikuwa nafuraha na nilidhani kuwa nitabaki hapo na kuishi milele.Nikasikia sauti nzuri za malaika zikimsifu MUNGU(Zaburi 103:1-3).Bwana akasema, “Waambie watu wangu kuwa ufalme wangu upo kweli.Wamebarikiwa watakao urithi.”Kulikuwa na maua mengi mazuri(Zaburi 119:129-135).

MTI WA UZIMA
Bwana akanichukua mimi mpaka sehemu ambayo niliona Mti wa Uzima kwa mbali.Ulikuwa mzuri,unang`aa kama dhahabu(Ufunuo 22:2).Bwana akasema, “Nimeulinda Mti wa Uzima kwa ajili ya watu wangu.Waambie wamebarikiwa wale wazifanyazo na kutii amri zangu, hao ndio wenye haki kwenye Mti wa Uzima.”(Ufunuo 22:14) tukaendelea mbele.
WATOTO WALIOTOLEWA MIMBA DUNIANI
Bwana akanipeleka sehemu ingine mbinguni kulikuwa na ukumbi mkubwa na nikawaona watoto wengi wadogo waliojawa na utukufu wa MUNGU.Walikuwa wakimsifu MUNGU(Zaburi 86:11-13).Bwana akasema, “Hawa ni watoto ambao wanawake wanawatoa uja uzito wao(arboted) duniani.Wanamilikiwa nami na watakuwa katika ufalme wangu tukufu.”(Zaburi 89:1-2) Ndipo tukatoka hiyo sehemu.
MALAIKA GABRIEL AKATUTEMBELEA
Kipindi Bwana anaongea nami, tazama nikamuona malaika.Alikuwa mrefu na mzuri, amevaa taji katika kichwani.Bwana akaniambia, “Ni malaika Gabrieli.”Nilikuwa na furaha kukutana nae na Bwana akaniongoza kunichukua mimi kwenda sehemu mbali mbali Mbinguni ili niwezekuwaambia wengine nilichokiona.
MFALME DAUDI
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka kwenye jumba kubwa sana.Akasema, “Ni nyumba ya mfalme Daudi”Nikasema nataka kumuona mfalme Daudi uso kwa uso.Tukaenda ndani ya chumba chake na nikamuona mfalme Daudi akimsifu MUNGU kwa zaburri na kucheza(Zaburi 34:1-6).Nikamsalimu na akaniita jina langu, “Senayon, Karibu”.Nilishangazwa kwa kuwa alikuwa analijua jina langu.Akasema, “Senayon, haumsifu MUNGU.Hutaki kucheza kwa MUNGU.Unapomsifu MUNGU nakucheza kwa Ajili yake, neema Yake inakuwa karibu na wewe.”Nikamuuliza . “Umejuaje hayo?, je uliniona nilipokuwa duniani? Au unayajua tuu maisha yangu ya duniani ?”
Akawa anacheka na akasema, “Sijisemei kwa uwezo wangu”..Baadae nikagundua ni MUNGU anaongea na mimi kupitia yeye.Akanipa mimi kitabu kidogo akaniambia, “Kula !Kula hicho !.”Nilipokila hicho kitabu nikawa na kiu sana.Nikamwambia , “Nina kiu.Nina kiu.”Wakanipa mimi damu ya YESUKRISTO kuinywa.Nilipokunywa nilikuwa natetema kama vile nimepatwa na baridi kali kwa muda wa zaidi ya dakika tano.
Nilipokuwa natetema;Malaika Gabrieli na Mfalme Daudi walikuwa wamepiga magoti wakisema, “UTUKUFU KWA MUNGU!”(Zaburi 29:1-11).Nilipoacha kutetema baada ya muda ndipo mfalme Daudi akaniambia, “Sasa utamsifu MUNGU na kucheza kwake.Waambie watu wamsifu MUNGU na neema Yake itakuwa karibu nao.”
Malaika Gabrieli akasema, “Senayon,unavitu vingi vya kuona, Tuondoke.”Nikamwambia, “Hapana,sitaki kuondoka kumuacha Mfalme Daudi, tafadhali .”
Bali hakunisikia na tukaondoka pale kwa mfalme Daudi.
NYUMBA YA NABII ELIYA
Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye nyumba ingine kubwa na nzuri sana.Aliniambia ni ya nabii Eliya.Nilikuwa nafuraha iliyopitiliza.Nikamwambia, “Nataka nimuone!”Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwenye nyumba ambapo alitoka mvulana kijana mzuri sana na kuniambia “Senayon karibu !” Nilikuwa nafuraha sana kumuona yeye.Nikamwambia, “Ulikuwa shujaa sana duniani.Nimesoma kuhusu wewe kwenye Bibilia.”Naye akanijibu, “Kuna moto unawaka ndani ya moyo wako.Utakuwa shujaa kuliko mimi.”(2 Wakorintho10:4-5).Aliniambia mengi kuhusu mimi.Malaika Gabrieli akaniambia, “Senayon, tunatakiwa tutoke sasa hapa kwa sababu unavitu vingi vya kuona.”Tukatoka na kwenda kwenye nyumba ingine.
NYUMBA YA MTUME PAULO
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka sehemu ingine ambako kulikuwa na nyumba kubwa sana ,Nayo imetengenezwa kwa dhahabu, na imepambwa na mawe mazuri sana.Akaniambia, “Hii ni nyumba ya mtume Paulo.”Nikasema nataka nimwone yeye.Yeye amekuwa mfano wa kuigwa wakristo wengi.Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye hiyo nyumba, tazama nikamuona kijana mdogo amepumzika kwenye chumba kizuri. Senayon,” akesema , “Karibu sana.Ninayo furaha kukuona wewe.”Nilishangaa kuona anajua jina langu.Wanajua yote kwa sababu ya utukufu wa MUNGU uko pamoja nao.Na haikuwa muhimu mimi kuwa ambia jina langu kwa sababu wao walini jua jina langu kwa nguvu ya MUNGU.
Akaanza kuniambia historia yake kwenye kitabu cha Matendo(Matendo 8:1-4)(Matendo 9:1-31).Alipomaliza, aliniambia, “Nimtumia neema ambayo YESU amenipa mimi na sikuifanyia mchezo.”Akanipa kitabu kidogo na kuniambia, “Kula !, Kula hicho !.”Nilipokula sikuwa na kiu na kiukweli kilikuwa kitamu.Mtume Paulo akaniambia, “Sasa utahubiri injili na kufundisha shuhuda za YESUKRISTO.Utafundisha baadhi ya nyaraka(epistles) zangu ambazo bado sikuziandika.”(Warumi 8:35-39)Wote kwa pamoja Malaika Gabrieli na Mtume Paulo tulikuwa tukimsifu MUNGU.(Warumi 4:20-25)(2 Wakorintho 5:13-18).Ndipo tukamuacha .Nilikuwa na furaha.Mbingu imejawa na uzuri na utukufu wa MUNGU.(Ufunuo 21:18).
NYUMBA YA BABA ABRAHAMU
Ndipo Malaika Gabrieli akanichukua kwenda sehemu ingine Mbinguni ambako kulikuwa kuna nyumba nzuri iliyopambwa kwa maua na mawe mazuri.Akasema ni nyumba ya baba Abrahamu.Nikamuomba anipeleke nimuone baba Abrahamu.Nikafika pale na kumuona Baba Abrahamu, nikamwambia, “Baba wa imani, Baba wa imani.”Akaanza kunipa mimi ushauri kuhusu vitu vingi katika maisha yangu.Aliniambia, “Unatakiwa uwe na imani katika lolote unalomuomba BABA na kuwa mvumilivu katika hali yeyote ile”(Yeremia 33:3) (Mathayo 17:20) Imani ni hakika.(Mathayo 21:21-22)(Waebrania 11:1).Tukatoka hapo.
MALAIKA SABA(7) WAKIWA NA TARUMBETA NA WATANO(5) WAKICHEZA.
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka sehemu ingine ambako niliwaona malaika watano(5) wakicheza kwa furaha.Pia nikaona malaika saba(7) wakiwa na matarumbeta.Nikamuuliza Malaika Gabrieli aniambie kuhusu kazi ya hao malaika.Akaniambia kama mtu akimpa maisha yake YESUKRISTO duniani , ndipo wao hao malaika saba(7) hupuliza tarumbeta kama ishara kwa roho moja inapotubu.Malaika watano(5) wanakuwa wakicheza na mbingu nzima hushangilia.Pia kama roho ikiingia mbinguni wao pia husherehekea kwa hiyo roho.(Luka 15:7).Kuna furaha kubwa mbinguni juu ya mtu mmoja mwenye dhambi akitubu.(Luka 15:10).
WASHINDI
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye kumbi kubwa.Akanipa mimi upanga ili niunyanyue juu.Nilipounyanyua nikajikuta mwenyewe kwenye uwanja wa vita.Nikaona watu wasio hesabika wamefungwa chini.Kulikuwa na mapepo wengi waliowafunga hao watu.Baadhi yao bado wana silaha za vita.Zimeandikwa migongoni mwao , “WASHINDI”.Walikuwa wakiwapiga mapepo ili kuwaweka huru wale waliofungwa.Ambao wamewekwa huru huyo mtu hukimbia mpaka kwenye chumba kiitwacho “SEHEMU YA SIRI YA MUNGU ALIYE JUU” Nikamuuliza Malaika Gabrieli kunitafsiria akasema, “Washindi ni wakristo hai wa kweli(1 Yohana 5:4-5) nawale waliofungwa chini ni wadhambi.Wale mapepo wanawasimamia ili waendelee kukaa kifongoni ili waende kuzimu ya moto.(1 Petro 5:8-9)Kupambana na mapepo wale waliowafunga inamaana ‘kuhubiri kwa wadhambi na kuwaombea’.Chumba wanachokimbilia ni salama ambacho ni YESUKRISTO.(Mathayo 11:28-30) na hiyo ndiyo sababu kinaitwa ‘SEHEMU YA SIRI YA MUNGU ALIYE JUU’(Zaburi 91:1)”.Unatakiwa uombe sana ili MUNGU akufungue wewe kutoka kwenye pepo ambaye yupo kwenye hiyo kazi ya kupeleka watu kuzimu ya moto.
UTAKASO
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka sehemu nzuri sana mbinguni, iliyopambwa kwa dhahabu safi.Nayo ardhi ilikuwa nyeupe na safi kama glasi.Kulikuwa na maua mengi mazuri na mawe mazuri mengi.Niliona dhahabu zilizo pachikwa.Nikamwambia Malaika Gabrieli kwamba ntaka niguse dhahabu zilizopachikwa juu.Akanibeba juu kwenye mabega yake ili niweze kugusa.Nikamwambia malaika Gabrieli sitaki kuondoka hiyo.Nilikuwa nikilia kwafuraha kwasababu sehemu ile ilikuwa nzuri sana.(Ufunuo 21:18-19).
Malaika Gabrieli alisema, “Hapana.Unavitu vingi vya kuona hapa na ni muhimu sana uvione”.Nilizidi kumwomba nikimwambia,”tafadhali sitaki kuishi maisha yale ya dunia.tafadhali fanya jambo kuhuso hicho.”Malaika Gabrieli alisema, “Senayoni njoo twende zetu”.Tukatoka tukaenda kwenye bwawa la damu ya YESUKRISTO.Malaika Gabrieli akaniuliza, “Sanayon, unakumbuka hii sehemu ?”Nikamjibu, “Ndio.Niliona hili bwawa la damu kipindi cha kwanza na YESUKRISTO.”Malaika Gabrieli akasema, “Sawa uko sahihi.”Tulikuwa tukisimama pale kwa zaidi ya dakika tano lakini hakutoa neno hata moja kwangu.Mara, Nikaona mwanga wa Blue mzuri.Huo mwanga ukanichukua mpaka kwenye hilo bwawa la damu ambapo kulikuwa na mkono usio onekana ukaanza kuniosha ndani ya ziwa la damu.Iliniumiza mimi na nilikuwa nikilia.Nikamuomba Malaika Gabrieli kunitoa lakini alikuwa amepiga magoti akisema, “UTUKUFU UWE KWA MUNGU KUTOKA MILELE HADI MILELE, MFALME WA WAFALME NA UZURI WAKE MUNGU !”(Zaburi 95:1-6).

Tazama ! Nikaona mwili wangu duniani uko kitandani.Kitu fulani cheusi kilikuwa kikitoka nje ya mwili wangu.Nilishangaa kuona hicho kitu kuwa kilikuwa ndani yangu mimi(Zaburi 51:12-15).Kipindi ambapomkono usioonekana ulipomaliza kuniosha mimi, mwanga halisi ukanitoa nje ya bwawa la damu(Zaburi 51:8-11).Tazama 1nikasikia sauti kubwa ikisema, “Sasa utakumbuka kile ulichokiona na utaishi vile nitakavyo, wewe sio tena mtu wa kawaida kwa sababu nimekutakasa wewe.”Hiyo sauti ikaanza kuongea kuhusu kaka ambaye alinifundisha mimi kwenye njia za Bwana, Jina lake ni IJAWJAW EAMON MARK.Bwana akaniambia mengi kuhusu yeye kwamba atalitimiza agano lake naye na amempa vazi la ukamilifu.Sauti ikaniambia kuhusu watu wengi.Nikamuuliza Malaika Gabrieli, “Tafadhali, Nataka nione nani ninayemsikia sauti yake.”Malaika Gabrieli akajibu, “Sina nguvu ya kukupeleka pale , lakini nifuate mimi.”Tukatoka hiyo sehemu.
ENZI YA BABA MUNGU
Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwa YESUKRISTO.Akamuelezea YESUKRISTO kuwa nataka kumuona BABA na mwisho nikagundua kuwa ni BABA aliyekuwa aliyenichukua mimi kwenye bwawa la damu.YESU akatabasamu na kunishika mikono yangu akisema, “Wataka kumuona BABA ?”.Nikamjibu, “Ndio.”
Katika kwenda kumuona BABA ,tulipita katika ukumbi ambapo kulikuwa na malaika wengi.Mara wakapiga magoti na kusema, “UTUKUFU UWE KWA MUNGU !”(Zaburi 84:11).
Tulipotoka kwenye huo ukumbi ,na tazama nikaona mwanga mkali kwenye enzi.Ulikuwa mwanga kama moto unaowaka.Ingawa tulikuwa mbali sana kiasi cha maili nyingi lakini nilihisi nataka kuanguka.Sikuwa na nguvu ya kutembea kuelekea kwene enzi tena.Nikamuomba Bwana nikisema, “Tafadhali nirudishe.” Bwana YESUKRISTO akaniambia, “Huyo ni BABA,Hutaki kumuona TENA?”Nikamwambia , “Ndio,tafadhali, tafadhali, Nataka kufa.Siwezi kupumua zaidi.”YESU akatabasamu na kunirudisha kwa malaika Gabrieli.
VITABU MBELE YA MALAIKA.
Malaika Gabrieli akanichukua mimi mpaka kwenye chumba kibwaa ambako kuna makundi ya malaika.baadhi walikuwa wakiandika majina na wengine wakifuta majina kutoka kwenye vitabu.Nilipewa nafasi ya kutembelea malaika wa nne(4) kati ya wengi.Nikamuliza malaika Gabrielii anielezee kila kitu akatabasamu.Malaika wa kwanza ni malaika anayehusika na kitabu cha uzima.Malaika Gabrieli alisema, “Hiki kitabuni kitabu ambacho kina majina ya wale walio okoka wapya na wale wakristo wakweli na walio okolewa.”(Ufunuo 3:5).
Nikauliza sababu ya malaikaa kufuta baadhi ya majina na kuandika majina mengine.Naye akanijibu, “Wale walioacha wokovu waliorudi nyuma.”(Ufunuo 2:4-5).Nikamuuliza tena, “Unamaanisha majina yao yanfutwa milele kutoka kwenye Kitabu cha Uzima ?.”Akatabasamu na kusema, “HAPANA.Hiki ni kitabu kitakatifu na hakiwezi kuwa na majina ya wenye dhambi.”Nikamwambia, “Niambie hayo majina yanayofutwa yanawekwa wapi ?”.Akanichukua mpaka kwa malaika mwingine ambaye naye alikuwa akiandika na kufuta baadhi ya majina.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ndio kitabu cha waliorudi nyuma katika wokovu na kina majina ya wote walio iacha njia ya Bwana.Sababu ya malaika kufuta baadhi ya majina ni kwa sababu ya wale waliokuwa wamerudi nyuma na kuiacha njia ya Bwana wamemrudia MUNGU,Majina yao huandikwa tena katika kitabu cha Uzima.(Ufunuo 20:15)”Majina aliyokuwa akiyafuta ni majina ya waliorudi nyuma katika wokovu (Yeremia 3:22).Akanichukua na kunipeleka kwa malaika mwingine aliye kuwa akifanya kazi kwa bidii sana.Hata hivyo alikuwa akiandika tuu majina, nasio kuyafuta.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ni kitabu chenye majina ya wote ambao huishia Kuzimu ya moto kila siku.Kitaitwa kitabu cha hukumu(The condemnation Book).’”Malaika Gabrieli aliniambia, “Majina yanaandikwa ni yale ya ambao walikufa bila kuwa na YESUKRISTO maishani mwao.”(Ufunuo 20:12).Tukatoka hapo na kwenda sehemu ingine.
Malaika Gabrieli akanichukua mpaka kwa malaika mwingine ambaye alikuwa anaandika tuu majina bali hayafuti.Malaika Gabrieli akasema, “Hiki ni kitabu chenye majina ya wale wanaotoa zaka zao.”(Malaki 3:8-12).Malaika alikuwa akiandika majina na kupiga kelele akisema, “Amelipa ! amelipa !” Na mara nikamuona malaika akaja pale.Akafungua chumba kizuri na katika kile chumba kulikuwa kuna vitu vingi vizuri vya dhahabu kwenye maboksi.Malaika akaingia katika hicho chumba na kuchukua moja ya vitu vya vyahabu nzuri kuenda zake.Nikamuuliza Malaika Gabrieli aniambie nini kilichokuwa ndani ya boksi ambacho malaika amekichukua na kuenda nacho.Malaika Gabrieli akanijibu, “Ndio.Ni baraka kubwa kutoka kwa Bwana kwa yule aliyetoa fungu la kumi(zaka) kwa uaminifu.”(Obadia 1:15).Tukatoka hiyo ssehemu.
DAKIKA TANO (5) ZAIDI.
Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye ukumbi ambao kulikuwa na malaika wengi wakisema, “Bwana ni muda.Acha watu wetu waje.”Nikamuona Bwana YESUKRISTO akilia kama mtoto akisema, “Acha tuwape DAKIKA TANO ZAIDI !” Baada ya hapo Malaika Gabrieli alinionyesha mimi maandalizi yote kwa ajili ya unyakuo yako tayari.Kila kitu kii tayari Mbinguni na YESUKRISTO anasubiri kuambiwa NENDA kutoka kwa BABA MUNGU(2 Wathesalonike 5:2-6).Tena Malaika Gabrieli alinipeleka kwenye ukumbi mwingine ambako kulikuwa na mavazi mazuri mengi sana.Yalikuwa yamepambwa na uzuri,kushangaza na utukufu kwa dhahabu safi.Nilimuuliza malaika Gabrieli, “Ni watu gani wataomiliki hayo mavazi mazuri !?” Naye akanijibu, “Haya ni mavazi ya Wakristo watayavaa kwa ajili ya ndoa ya mwanakondoo.”(Ufunuo 19:7-9)
Nilimuuliza Malaika Gabrieli anionyeshe mimi vazi langu.Naye alilionyesha moja ya vazi na kusema , “Hili vazi ni lako.” Nilikuwa na furaha ya ajabu na ndani yangu nikijisemea, “Sitaenda kuzimu ya moto.” na tazama nikasikia sauti kubwa ikisema, “TAZAMA NAKUJA HARAKA; SHIKA SANA ULICHO NACHO USITAKE MTU YEYOTE AKUNYANG’ANYE TAJI YAKO !”(Ufunuo 3:11).Niliogopa sana niliposikia hiyo sauti kwa sababu inamaanisha “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.”(1 Wakorintho 10:12) (1 Wakorintho 9:24-27).Tukatoka sehemu hiyo na kwenda sehemu ingine.

UTEMBELEO WA MALAIKA URIELI
Malaika Gabrieli alinichukua mpaka kwenye nyumba nzuri sana .Tulipofika pale tuka kaa kwenye kiti.Mara ghafla nikasikia kiashiria kikubwa Mbinguni na malaika akapiga magoti na kuanza kusema, “Utukufu uwe kwa MUNGU,Yeye anastahili kupokea utukufu wote.AMENI !” Malaika Gabrieli akaniambia mimi niangalie.Tazama !nkaona malaika akikimbia na kupiga kelele akisema, “Ushindi ! Ushindi ! Ushindi !” Malaika akakimbia kwa YESU nakusema, “AMEINGIA ! AMEINGIA ! ”Nikamuona mtu akija kwenye Ufalme wa Mungu.Malaika akamkimbilia kumchukua kumuingiza ndani kwa sababu alikuwa tayari amechoka.Afadhali ameweza kuingia mbinguni ! Malaika Gabrieli akasema, “Malaika anayepiga kelele ‘USHINDI ! USHINDI !’ alikuwa ni malaika mlinzi wa yule mtu aliyeingia Mbinguni.”Mbingu yote ilijawa na furaha kwa sababu ya mtu aliyefanikiwa kuingia.Malaika Gabrieli akatoka nje ya chumba na kuniambia, “Senayon, unakaribishwa !”na alinikabidhi kwa Malaika Urieli ili kunionyesha baadhi ya vitu Mbinguni.
Malaika Urieli akanichukua mpaka sehemu ingine na kuniambia, “ANGALIA! .ANGALIA !.”Nikaona Ufalme wa Shetani.Shetani alikuwa akiwapa mapepo amri ili kuvamia Wakristo kwa sababu ya yule mtu aliyefanikiwa kuingia mbinguni.Shetani alisema, “Msiruhusu yeyote yule kukwepa mitego yetu na uvumbuzi wetu.Lazima tuzipate roho zao !.”Nikaona mapepo , yakikimbia na kasi kubwa kwa sababu roho moja imefanikiwa kuingia mbinguni.
Malaika Urieli alinichukua mimi kwenda sehemu na kusema, “Angalia duniani.”NIkaona dunia imeonekana ndogo sana na chafu sana kama sehemu ya kuweka uchafu.Mara ghafla ! nikaona mishale mingi ikaanza kuanguka duniani.Nikamuona Mtu Mzee aliyepokea mishale michache.Baadhi ya mishale hiyo iliangukia watu wengine waliopo duniani.Nikaona moto ukija duniani lakini yule Mtu Mzee akausimamisha ule moto na kuurudisha ulipotoka.Nikamuuliza Malaika Urieli, “Tafadhali nitafsirie hiki kwa sababu ni maajabu sana kwangu.”Malaika Urieli akasema, “Mtu Mzee uliyemuona ni YESUKRISTO, na mishale michache iliyompata katika mwili wake ilikuwa ni mishale ambayo shetani anatuma kinyume na watoto wa MUNGU.(Zaburi 91:1-7).Mishale mingine iliyo anguka kwenye dunia ilikuwa ni mishale kutoka kwa shetani kwa watenda dhambi.(Zaburi 92:7) Moto uliouona ni mipango ya shetani ya kuharibu dunia lakini Kristo hakuruhusu hicho kitokee.”(Isaya 60:1-2)

MALAIKA AKIWA NA TAARIFA MBAYA ZA MTU
Malaika Urieli akanichukua mpaka sehemu ambayo niliona malaika wengi wakitoa taarifa mbaya kwa Bwana.Malaika wa kwanza alikuja na kumwambia Bwana, “Mwishowe , Amepoteza roho yake.Nilimuonya lakini hakunisikiliza mimi.”(Marko 8:36).
Malaika wa pili akamwambia Bwana, “Bwana, yule mtu amefanya uzinzi.Nilimuonya asifanye lakini akamruhusu shetani kuutumikisha moyo wake.”Bwana akamuuliza malaika, “Ulimwambia akiri kosa lake ?”Malaika akajibu , “Ndio, lakini kila akitaka kukiri yule mwanamke aliyefanya naye uzinzi anajitokeza na huyu hushindwa kukiri tena anapomuona yule mwanamke aliyefanya naye uzinzi.”Bwana anamwambia, “Endelea kumwambia akiri na kuacha (dhambi zake )naye ataokolewa.”(Mithali 28:13)
Malaika akajibu, “Sawa BWANA.” Na akaondoka zake. 
Malaika wa tatu akaja naye alikuwa malaika mlinzi wa mchungaji W.F Kumuyi.Malaika akamwambia Bwana, “Bwana, shetani ametuma baadhi ya watu waovu kwenye huduma ya DEEPER CHRISTIAN LIFE (Kanisa la Mchungaji W.F Kumuyi), kifanyike nini ?” Bwana akamjibu, “Mwambie Kumuyi, mtumishi wangu awe muombaji na nitampa USHINDI.”Malaika asema, “Haya BWANA.”Akaenda zake(1 wathesalonike 5:17).Malaika wengi walikuwa wakija pale.Kitu kilichokuwa nikikisikia sana ni, “Mwishowe, amepoteza roho yake.”
                                                        NYUMBA YA MCHUNGAJI E.A ADEBOYEKipindi malaika aliyekuwa akitoa taarifa kuhusu mchungaji W.F.Kumuyi alipo ondoka, Nilimuuliza Bwana kama mchungaji E.A.Adeboye ni mtumishi wake au sio.Bwana akasema, “Ndio mchungaji Adeboye ni mtumishi wangu na mimi ndiye mwanzilishi wa REDEEMED CHRISTIAN CHURCH.Angalia ile nyumba.” Nikaangalia na kuona nyumba kubwa mbinguni.Bwana akasema, “Hio ndiyo nyumba ya mchungaji Adeboye , mtumishi wangu.”
Nilipiga kelele, “Hii nyumba kubwa ! unahakika atakuja kuingia ?” Bwana akasema, “Ndio kama akiendelea kufanya mapenzi Yangu na kuzidi kuvuna watu kwa Ufalme Wangu.”(Mathayo 28: 19-20).
Nikamuuliza Bwana anionyeshe nyumba yangu.Bwana akatabasamu na kusema, “Iangalie mwanangu.” Nikaona nyumba ndogo nzuri.Bwana akaniambia ni yangu.Nikacheka na kusema, “Lakini sijawahi lipa fungu la kumi.” Bwana akatabasamu na akasema, “Sio zaka pekee zinazo jenga nyumba hapa, lakini, pia unapowahubiria na kuwa ambia watu kuhusu Mimi na wokovu, hiyo ndiyo thawabu inayojenga nyumba huku mbinguni; unaponiletea watu hiyo nayo ni thawabu kubwa ya kujenga nyumba yako mbinguni.pia unapo waombea watu hiyo ni thawabu ingine kubwa inayopelekea kujenga nyumba.Unapotenda vyema kwa wengine nayo ni thawabu kubwa kwa wewe kujenga nyumba mbinguni.Kama watu wanataka kujenga nyumba hapa wanatakiwa watii kile nilichokueleza wewe.Hivyo, unayo hii nyumba kwa sababu umekuwa ukichukua muda mwingi kuomba kwa ajili ya wenginehaswa katika kundi Nililolianzisha:THE OVERCOMERS GROUP, na pia kwa sababu unawaambia watu kuhusu Mimi na kuleta watu Kwangu.”(Marko 1:15)
Malaika Urieli akanichukua mpaka kwa malaika Gabrieli ambaye alinionyesha mimi jinsi hizi shuhuda zitavyokuwa kubwa duniani.Aliniambia mambo mengi ya siri kuhusu mimi.Malaika Gabrieli alinichukua mimi mpaka kwenye kumbi kubwa na tazama , Nikaona malaika wengi wakiimba sifa kwa Bwana.Walicheza vyombo vingi kulitukuza jina la MUNGU aliye JUU.Nikajiunga nao nikimsifu Bwana.Nyimbo zilikuwa zakuvutia.Sauti za malaika zilikuwa nzuri sana.Kulikuwa hakuna aibu mbinguni.Malaika walikuwa wakicheza.Wengine walikuwa wakiruka mara ghafla wakapiga magoti na kuanza kusema, “Utukufu uwe kwa MUNGU !”(Ufunuo 5:9-14) Nilikuwa na furaha kuwa kati yao nilipenda niwe pale milele, kumsifu MUNGU wa Utukufu(Ufunuo 4:11).Tukatoka.
Malaika Gabrieli akanichukua kunirudisha mpaka kwa Bwana Yesukristo.Bwana Yesukristo akaniambia, “Mwanangu, niambie mimi, nini unachotaka kuona hapa au kipi unachotaka mimi nikuonyeshe ?” Nikajibu, “YESUKRISTO , mapenzi yako yatimizwe kwa sababu unajua vyote ninavyotaka kuviona hapa.”
Akanichukua mimi na huku akitabasamu akisema, “Mwanangu,Njoo.
MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU
Bwana akanichukua mpaka sehemu moja mbinguni kuna kioo kikubwa sana.Kwenye kioo hiko kimeandikwa matunda tisa(9) ya Roho mtakatifu.Bwana akaniambia, “Matunda yako tisa(9) ya Roho mtakatifu yanatakiwa yawe yamekamilika.Kama tuu moja limekosekana, huyo mtu hawezi kuja kwenye ufalme wa MUNGU kwa sababu viwango vyangu vya mbinguni vinasimama milele.”(Wagalatia 5:22-23)
UNYAKUO
Ujio wake Bwana YESUKRISTO,kutokea kwa YESUKRISTO katika anga kupokea Utukufu wake kwa tumaini kuu la wote wamwaminio.Ni mara na yeyote asiyenyakuliwa na KRISTO ataporudi ata “aachwa”(Mathayo 24:42-44).
Bwana akasema, “Mwanangu,njoo nikuonyeshe jinsi unyakuo utavyokua.Angalia kwa umakini sana.” Tazama ! nikaona kanisa kubwa duniani.Lina zaidi ya watu milioni tatu (3) wakiwa wapo kanisani, kulikuwa na kitu kama kongamano.Kufumba na kufumbua unyakuo ukatokea na tuu wanafunzi watatu (3) kati ya milioni tatu (3) wakaondoka na Bwana YESUKRISTO.Wengine wote wakaachwa ! (Marko 13:30-37).
Nikamuona muanzilishi wa hilo kanisa naye alikuwa ameahwa na alipiga magoti pale pale na kusema, “Oh Bwana, nina makanisa 200 na sikuwahi hubiri kweli, lakini sasa nimeachwa ,tafadhali nisamehe mimi.” Bwana akasema, “Umechelewa(unaweza ukatengeneza) tuu kama utavumilia na kukataa kupokea alama ya mnyama.”(Ufunuo 13:16-18) (Ufunuo 19:20).
Kama wewe ni mchungaji au muhudumu ambaye huihubiri kweli, kumbuka huwezi jitetea mwenyewe mbele ya MUNGU(1 Petro 5:2-4).
Nikaona shule ambapo mkuu wa shule alikuwa akihutubia wanafunzi.Mara ghafla ,mkuu wa hiyo shule akanyakuliwa na wanafunzi wakabaki (1 Petro 4:7).Nikaona mwalimu alikuwa akifundisha wanafunzi, mara nikaona wanafunzi watatu(3) na mwalimu wamenyakuliwa, wanafunzi wengine wote wamebaki.(2 Petro 3:9-14).
Nilimuona mama mjamzito alikuwa akienda zake nyumbani .Ujauzito wake ukapotea kwa sababu mtoto alinyakuliwa lakini mwanamke aliachwa(Mathayo 24:40-51). Kulikuwa na huzuni kubwa dunia nzima (Mathayo 25:31-46).Wakristo wengi walikuwa wameachwa kwa sababu ya dhana zao juu ya dhambi aliozigundua mwanadamu(Zaburi 106:39-40).
Bwana akasema, “Hivyo ndivyo unyakuo utakavyotokea.Ni muda wa kwenda duniani .YEYE ALIYE NA SIKIO NA ASIKIE ROHO WA BWANA AAMBIACHO KANISA.KESHENI NA KUOMBA ! ” Ndipo Bwana akanirudisha duniani.
OMBI LA MSAMAHA
Kama uko tayari kumpa maisha yako YESUKRISTO omba sala ifuatayo:
Unirehemu mimi, MUNGU kutokana na uzuri wa upendo wako; kutokana na neema zako ondoa maanguko yangu.Nioshe kutoka kwenye maovu yangu na unisafi dhambi zangu.Ninatambua makosa yangu na dhambi zangu,tazama nilizaliwa katika uovu na mama yangu alichukua ujauzito wangu dhambini.Tazama natamani kweli ndani yangu na maficho yangu yajue hekima yako.
Nifanye nisikie furaha na amani yako ;Mifupa iliyovunjika iingiwe furaha yako na urejesho wako.Ficha uso wangu kutoka kwenye dhambi, ondoa kila ovu langu na uniumbie moyo safi,Oh Bwana ; na uweke tena sawa roho yangu.
Usiniondoe kutoka kwenye uwepo wako na usimchukue Roho wako mtakatifu kutoka kwangu.Nirejeshe furaha ya wokovu na kuniinua nikiwa na uhuru wako rohoni mwangu.(Zaburi 51).Andika majina yangu kwenye kitabu cha Uzima.Na iwe furaha kuu Mbinguni juu ya wokovu wa roho yangu katika Jina la YESUKRISTO,Nimeomba.Amen !.
Tafadhali nakuomba SHARE kwa mwenzio; na kwa shuhuda nyingi zaidi tembelea; www.jasirimbarikiwa.blogspot.com .SHARE kwa wengine nao.

5 comments :

  1. Nimeipenda SAA MUNGU AKUBARIKI KWA JINA LA YESU KRISTO

    ReplyDelete
  2. MUNGU akubaliki mtumishi akupe afya njema ili kupitia wewe nasisi tubalikiwe

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...