JINSI YA KUTAFSIRI NDOTO/MAONO YAKO!.



Unapo lala mwili unakuwa umekufa bali roho yako inakuwa hai sasa unachopaswa kukijua  ni kuwa aina za ndoto unazoota zinaonyesha wewe uko vipi kiroho!.

Kwa kuwa MUNGU hutumia ndoto kufikisha ujumbe wake kwetu ,Lakini pia shetani naye hutumia ndoto kufikisha maharibifu yake kwa watu wasio na YESU kupitia ndoto.


Watu wengi wameshindwa kuelewa ni nini MUNGU anasema katika maisha yao kwa kuwa tuu hawaelewi pale MUNGU anapoongea na wao kwa njia ya ndoto kwa kuwa hawawezi kutafsiri kile wanachokiota.

Ndoto ni moja wapo  ya njia ambazo MUNGU hutumia kuongea na watu wake.Muda mwingine ndoto zinakuwa hazina mafumbo ,Mfano ni huu
 Imeandikwa “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.” -Mwanzo 20:3.


Hiyo ndoto ilikuwa haihitaji tafsiri yeyote kwa kuwa  haina mafumbo yoyote na ilikuwa wazi sana kwa Abimaleki. Lakini kuna ndoto zenye mafumbo tena makubwa sana na hizo ndizo tunazo jifunza namna ya kutafsiri ndoto hizo!.


Hivyo basi yatupasa kujua namna ya kutafsiri mafumbo hayo ili tuweze kupata ujumbe ambao MUNGU ametutakia.

Kama hauoti ndoto unahitaji kuombewa maombi ya ukombozi na kama unaota ndoto na huelewi maana ya ndoto uliyoota pia unahitaji maombezi.

Ukisoma neno la MUNGU(biblia Takatifu) linaonyesha wazi kuwa hakuna aliyemjua MUNGU ambaye alishindwa kutafsiri ndoto,iwe ni ndoto yake au za wengine.
Mfano: Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.”- Mwanzo 37:9

Hiyo ni ndoto ambayo Yusufu aliiota na hiyo Ndoto ipo katika mafumbo lakini baba yake aliweza kugundua maana halisi ya ndoto ile . . . . . . . . . baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?” -Mwanzo 37:10.


Hii inamaanisha kuto-ota Ndoto ni tatizo bali si hivyo tuu bali pia na ukii ota ndoto na kuto kuelewa ni tatizo zaidi.

Vigezo pekee vitavyokuwezesha kutafsiri ndoto ya aina yeyote ile navyo ni hivi:-
1.Uwe na ROHO mtakatifu
Imeandikwa “Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie” -Mwanzo 10:8.

ROHO mtakatifu hanunuliwi bali anakuwa ndani ya mtu yeyote aliyemkubali YESUKRISTO kuwa mokozi wa maisha yake.

Unapomkiri YESU na kukubali kila alichokisema basi yeye YESU huweka msaidizi ndani yako naye atakuwa akikuongoza na kukusaidia katika mambo mengi na mengineyo ni kama haya ya kutafsiri ndoto.

Imeandikwa “kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.”- Danieli 5:12

Ndoto zote ROHO mtakatifu ndio siri pekee mwenye uwezo wa kuzitafsiri ndoto hizo tokea enzi na enzi.Hatutakiwi kutafsiri ndoto kwa kukariri bali kwa uongozi wa ROHO wa MUNGU.

2.Uwe na ushirika na MUNGU
Kigezo cha muhimu unachotakiwa uwe nacho ni kuwa mtu mwenye ushirika wa mara kwa mara na MUNGU.Kwa kuwa kwa kufanya hivyo MUNGU huongeza nguvu ya udhihirisho wa ROHO wake mtakatifu.

Angalia watu wote wenye uwezo mzuri wa katafsiri ndoto huwa wanaushirika mkubwa na MUNGU. Mfano Danieli yeye alikuwa akiomba MUNGU mara tatu(3) kwa siku,utaona ni jinsi gani alivyokuwa na ushirika mkubwa na MUNGU.

Na ndio maana alikuwa na uwezo mkubwa wa kufasiri ndoto.
“Hata Danieli, . . . . . .. . . . . . . akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.” -Danieli 6:10

Kuna hatua sita (6) zitakazo kuwezesha kutafsiri ndoto yako.
1.Changanua chanzo cha Ndoto yako
Kipengele muhimu kuliko vyote ni hiki kwa kuwa ukikijua baasi hakuna ndoto utakayoshinwa kuifasiri.
Ukitaka kutafsiri ndoto yako jaribu kuchanganua hiyo ndoto iko kwenye kundi lipi la vyanzo vyake.

Kwa kuwa kuna makundi matatu ya ndoto na vyanzo vyake ambavyo ni:-

I.Ndoto itokayo kwa MUNGU
Hizi ni ndoto rasmi ambazo huja na amani kuleta ujumbe kutoka kwa MUNGU juu yako au ya wengine kwa ajili ya kuwaombea au kuwasaidia

.
Mfano:Unaota rafiki yako anauwa sana . . . .  Kama una YESU hii ndoto inakutahadharisha kuwa umuombee huyo rafiki kwa kuwa anaweza akaumwa siku si nyingi.Na unapo muombea kweli hawezi tena kuumwa.

II.Ndoto itokanayo na MTU yaani mawazo yake.
Hizi ni ndoto zinazotokana na  mawazo ya mtu mwenyewe yaani mawazo mengi yanaomsumbua sana hukaa katika ubongo na baadae hujikuta akiyaota.

.
Mfano:Wewe umeota umepata fedha nyingi sana,Lakini kabla hujaota hiyo ndoto siku yako nzima uliitumia kuwaza ni namna gani utaweza kupata pesa nyingi.
Hivyo basi ujue tuu hiyo ndoto ni ndoto iliyotokana na WEWE mwenyewe kwa kuwa mawazo yako mengi ya kuwaza jinsi ya kupata pesa ndio yamesababishia kupata ndoto ambayo inahusu fedha.

III.Ndoto itokanayo na shetani.
Ndoto ambazo chazo chake ni shetani ,mara nyingi ndoto hizi huwatokea watu wengi ambao hawajaokoka au hawajakaa vizuri na MUNGU wa kweli..

Mfano wa ndoto hizi:kuota unakula nyama za watu, kuota unauwa, kuota unafanya mapenzi , kuota unapaa,kuota unaongea au uko karibu na watu waliokwisha kufa zamani, kuota uko uchi ,kuota umewekwa kwenye jeneza,n.k.


Ndoto za namna hiyo zinakuwa zimetoka moja kwa moja kutoka kwenye ufalme wa giza(shetani) na zinakuwa na madhara kwetu .


kwa mfano:mtu anayeota anakutana au anaongea na mtu aliyekwisha kufa siku nyingi  hizi ndoto humsababishia kifo yeye yaani roho ya mauti  inakuwa ilishamuingia ndio maana anaota watu waliokufa siku nyingi.


Zingine kama kuota unakula nyama za watu hizi humfanya mtu awe na mikosi yaani balaa ,unapokula vyakula vyao ndotoni wao hupanda bati mbaya na majanga katika maisha yako.

Kuota uko uchi ni ndoto ambazo husababisha aibu kubwa kuja kukutokea katika ulimwengu wa mwili.

Kuota unafanya mapenzi ndotoni,ndoto hizi husimamiwa na majini mahaba na unapoota mara kwa mara hizi ndoto husababisha kukosa mtoto,kutokuwa na mahusiano yeyote yaani kama upo kwenye ndoa au uchumba basi kutaanza migogoro isiyoeleweka mpaka mtaachana pia  ndoto hizi husababisha bahati mbaya mara zote katika maisha yako yaani kuna kuwa na ugumu mkubwa hata kushindwa kufanikiwa.

Kuota unapaa paa angani au hewani  hizo ni ndoto ambazo wachawi wanatumia sura yako kufanya uchawi wao kwa wengine.Kuwa makini sana na ndoto kwa kuwa muda mwingine shetani anaweza kutumia sura ya mtu mwingine unayemjua na kumuona huyo mtu kwenye ndoto akikujia na kukufanyia jambo baya ili tuu uanze ugombane naye ukidhani ni mchawi kumbe sio kwa kuwa naye anatumiwa na wachawi bila yeye mwenyewe kujijua.


Kuota mara kwa mara unaogelea kwenye ziwa au maji yeyote ujue hizo ndoto ni za kishetani zinazo sababisha kuto kuolewa,kukosa mtoto na kushindwa kuridhika na mahusiano ya kimapenzi ulio nayo .Kwa hiyo hupelekea watu kuachana,ndoa kuvunjika au kukaa pasipo amani siku zote.

Unapoota ndoto kama hizi ni bora tuu ufanye mpango wa kuombewa na watumishi sahihi ambao wana nguvu ya MUNGU  kwa kuwa ndoto hizi ni hatari sana kwa kuwa kila unapoota ndoto kama hizi shetani anakuwa amepanda mambo mabaya katika maisha yako.

Na ni YESU pekee ambaye anaweza kukuokoa na mitego hiyo ya shetani kupitia ndoto.Watu wengi hawafanikiwi si kwa sababu hawafanyi kazi kwa bidii bali kwa sababu ya ndoto hizi za shetani husababisha mikosi na bahati mbaya na hasara katika maisha yao.

2.IANDIKE NDOTO YAKO.
Ukisha ota ndoto na ukawa huielewi hapo hapo iandike na kwa kuwa utakuwa umeshaijua imetoka katika chanzo gani ?

Kama chazo cha ndoto yako ni cha WEWE mwenyewe yaani unajijua jana ulikuwa unawaza sana kuhusu jambo fulani na leo umeliota jambo hilo ujue hiyo ndoto chazo chake ni mawazo yako mwenyewe kwa hiyo iachilie mbali kwa kuwa haikusaidii.

Kama imetoka kwa shetani fanya maombi mazito ya kutoa hiyo silaha iliyopandwa katika maisha yako katika jina la YESU.Au nenda kwa watu wa MUNGU ambao wana nguvu ya MUNGU nao watakuombea na utakuwa huru na mapando ya shetani.

Kama hiyo ndoto imetoka kwa MUNGU basi iandike vizuri ukifuatisha hatua kwa hatua.
Imeandikwa “Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.”- Daniel 7:1

Watu wote wanaoweza kutafsiri ndoto zao na kupokea jumbe zao kutoka kwa MUNGU walikuwa ni watu wenye kuheshimu maono na ndoto wanazozipata na hata kuziandika.
 Imeandikwa “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.” -Ufunuo wa Yohana 2:1,

3.ICHUNGUZE NDOTO YAKO NA OMBA KWA AJILI YA NDOTO YAKO.
Hatua ya tatu(#3) ichunguze ndoto yako,kwa idadi ya watu au vitu na uombe kwa ajili ya hiyo ndoto.
Cha kujiuliza jiulize kwa nini MUNGU ameruhusu nione haya maono au hii ndoto?,

Imeandikwa “Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.” - Mithali25:2
Kumbuka baadhi ya ndoto ni kukufariji,kukutia moyo ,zingine kukuonyesha njia ya kupita lakini pia kuna ndoto ambazo ROHO mtakatifu anakuhitaji wewe usimame kwa nafasi yako kama kuhani.

Wakristo wengi wamekua wakiwaota watumishi wakubwa na mababa zao wa kiroho wakifanya mambo maovu huwa wanajiuliza inamaana gani?,


Nataka nikujuze sasa.Kwa kuwa MUNGU si mmbeya au mpenda udaku mpaka akufunulie siri za watu wengine .MUNGU hufichulia siri hizo ili uwaombee na niwewe pekee unaeweza kuwaombea watu haowakawa salama.

Kumbuka tunategemeana katika KRISTO YESU hivyo unapoonyeshwa mambo mabaya ya watu wengine unatakiwa uwaombee na sio kwa ajili ya wewe kuwasema sema vibaya.


Uwaombee tena kwa kufunga na kwa sadaka ili uwakomboe wale wanao pitia matatizo.Kwa kuwa kwa kuombea wengine kuna thawabu kubwa sana kwako unapata.

4.ITAZAMIE NDOTO YAKO & IISHI NDOTO NA UFUATISHE UJUMBE WAKO.
Angalia ndoto yako ambayo imeleta ujumbe kutoka kwa MUNGU na uanze kuifuatisha kwa kuwa nisauti ya MUNGU.



Imeandikwa  “Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.

 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.

 11 Basi tukang'oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli;

 12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.”- Matendo ya mitume 16:9-12

Hii inaonyesha kuwa ukiona ujumbe wa MUNGU unakwambia endelea mbele basi nawe pia unatakiwa uendelee mbele hata kama unadhani kukaa ni sahihi zaidi.Kwa kuwa MUNGU hujua mambo mengi tusiyoyajua.


Imeandikwa “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu”- Mathayo 1:20

Imeandikwa “Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;”- Mathayo 1:24

Hii inatuambia kuwa natupasa kutii sauti ya MUNGU kupitia ndoto.Yaani tuishi na kuenenda sawa sawa na ndoto ya MUNGU inavyotuelekeza.


Haitoshi tuu kutafsiri ndoto tuu bila kuchukulia hatua ya kuitendea kazi kwa kuwa ndoto ni ujumbe wa MUNGU.
                                                 
Kumbuka ndoto ni bayana , kwa hiyo usipuuze uyaotayo

19 comments :

  1. ahsantee sana hakika nimepata kitu

    ReplyDelete
  2. ahsantee sana hakika nimepata kitu

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Majibu yote yapo katika kuomba, Hivyo ni vyema uzidi kuomba utatambua wazi lengo na nia.💢

      Delete
  4. Mimi ni muda mrefu sasa naota napaa kila mara,.lakini kwa mazingira niyajuayo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kila ukipaa ni ishara ya shetani kukutumia .Kinachokupasa ni kuzidi kuomba zaidi ili kusudi la Mungu lijulikane.
      ✍️

      Delete
  5. Nimekua naota ndoto ya kupaa muda mrefu sana bt kwa mazingira nayoyajua. Je nifanyeje?

    ReplyDelete
  6. Nimekua naota ndoto ya kupaa muda mrefu sana bt kwa mazingira nayoyajua. Je nifanyeje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.🙏Ukiota mazuri unatakiwa uzidi kuomba ili yasipingike na yatokee kweli
      2.,🙏Kama ukiota mabaya unatakiwa uzidi kuomba ili mabaya yasitokee.
      ,💢Ukiota usilolielewa basi una wajibu wa kuomba zaidi ili upate Mwanga zaidi katika ndoto uliyoiota.
      ,,👉Maombi ni funguo🗝️ kubwa katika maisha ya mkristo

      Delete
  7. Jasiri, me Nimeokoka na nimejazwa roho mtakatifu na ninanena, nimeshtuka saa Tisa kasoro usiku nikawa nakula nikajisikia hatua kuwa kwanini naulisha mwili na roho nmeiacha na njaa, basi baadae baada ya kula nikaamua kuomba nmeomba muda kidogo nikapata wazo niombee usikuvu wa kiroho na uwezo wa kuona rohoni nijue Nini Mungu ananifundisha kupitia milango ya fahamu, baada ya dakika kama 30, nikamaliza nikalala, nmeanza kuota ndoto za mashambulizi, ila kilichonishtua Kuna ndoto nyingi zinazohusisha napaa hewani, na ilifika muda nikawa sijui jinsi ya kujikontrol, nikauliza nifanyaje nikaelekezwa jinsi ya kupaa hukohuko ndotoni, nikaenjoi sana, je ndoto hii inaweza kuhusisha uchawi kama ulivosema!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. 👉Uwe umeokoka, ubatizwa na muombaji sana unachotakiwa kujua shetani hachoki kutafuta namna mbali mbali za kutushambulia, 🔥Kitu cha muhimu kujua ni kuwa Mungu hutuonyesha katika ndoto:-
      💢1.Mipango ya shetani au yake kabla haijatokea ili tuombe kuiharibu mipango ya shetani au kuifanyia utekelezaji wa namna ya kukwepa/kujitahadharisha.

      💢2.Hali yako halisi ya kiroho ambayo uko nayo wakati uliopo.

      💢3.Hali iliyopo mahahali ulipo yaani katika hiyo s3hemu.Angalia "Mwanzo 28:16".

      Sio kila ukiota ni ishara nzuri kwa kuwa umeokoka bali yaweza kuwa ni tahadhari ya hayo yanayokuja kukumba baadae hivyo yapasa uzidi kuomba sana.

      Delete
  8. SAsante sana kwa somo zuri nimeota ninaimba baada ya kuimba nikaona nimeshirikia na watu wawili kufuga samaki bwawa tumejenga zuri sana na lina maji mazuri nikaambiwa awamu hii tukiuza samaki hawa faida tutagawana awamu nyingine bwawa hili litakua la kwako .nimeota tena Niko ktk shamba kaka Moja akanimbia yeye ni mkulima wa zabibu akanionyesha shamba akanimbia aliyekua anatunza shamba alikua anapata soda kitenge na ghahabu nami nikitunza nitapata hivyo nikakabidhiwa lisiti la shamba Mimi ninapenda kilimo na ufugaji wa samaki japo cjaanza

    ReplyDelete
  9. Ubalikiwe mtumishi wa mungu

    ReplyDelete
  10. Niliota mwaka jana nimepaa angani nikaungua nakusambaratika huko huko kushtuka usingizin n mzima ila baada ya ndoto za mwaka jana kwa mwaka huo matokeo yake si mazuri sana na mwaka huu pia nimeota tena nimeungua na moto niko jikoni jiko likalipuka nikaungua hii inamaanisha nn?? Sambamba na hilo huwa ndoto n nyingi sana.Lakni pia ni mambo mengi niliyaota ndotoni yananitokea kilekile nilichoota hicho hicho kinatokea unahisi hili tukio limejirudia kumbe ulishaliota ndotoni na mengi yako kwenye series ya target moja hapa inanifanya nishindwe kuelewa

    ReplyDelete
  11. Mi nimeota nna mwili mkubwa mpka kifua kimekua km baunsa mpka nikawa najishangaa kweny kioo

    ReplyDelete
  12. Asante kwa ufafanuzi mzuri, ubarikiwe na Mungu wa mbinguni

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...