KIFO KILICHOVAA SURA YA UCHUMBA/NDOA.


Kuna lilo chungu kuliko mauti nalo ni hili “Kuoa au kuolewa na mtu mwenye imani tofauti nawe”-Hiki ndicho kifo kinachoumiza kuliko vyote kwa kuwa mtu atakuwa anakufa huku akishindwa jinsi ya kujisaidia kuepuka kifo hicho kwa majuto na kila aina ya uchungu ,mbali na yote ni kuacha kizazi chako chote kikiumia na migogoro mingi ulioianzisha wewe.


Imeandikwa “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.”-Mhubiri 7:26

Hapa sisemeni sana mkristo wa dhehebu fulani anaoana na wa dhehebu tofauti na yeye hapana bali nazungumzia watu wawili wa dini tofauti wanapooana huzaa mapooza na kushindwa tuu katika maisha yao.

Suleimani alikuwa mtu wa MUNGU lakini alikoseshwa na wanawake wa kigeni yaani wanawake wasiokuwa na imani moja naye ,Imeandikwa “Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.”-Nehemia 13:26

MUNGU alie hai hapendi mtu wake aoe au aolewe na mtu wa imani isiyo mwamini YEYE MUNGU wa kweli kwa kuwa watu hao hupofusha maono yao wenyewe.

Mfano wa mtu aliyeoa mtu wa imani tofauti naye ni huyu samsoni Imeandikwa “Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.”-Waamuzi 14:3

Mfano Samsoni alikuwa ni mtu wa MUNGU aliyekua amepewa nguvu kubwa ya MUNGU kwa ajili ya huduma yake lakini hata kabla ya kumaliza huduma ile alikufa baada ya kumuoa Delila ambaye alikuwa ni mwanamke wa imani ingine naye alimbembeleza ili atoe siri zote ; 

Na alipotoa ndipo alipomkabidhi kwa wafilisti wamtese na mpaka kufa kwake.
 Imeandikwa “Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.” Waamuzi 16:18

KUPENDA NI UPOFU LAKINI HAITAKIWI KUWE NI UPOFU KWA MTU ANAYEMJUA MUNGU.
Kwa wewe ambaye unamjua MUNGU hutakiwi kuwa kipofu katika kupenda mwanamke au mwanaume bali katika kila kitu tunatakiwa kuwa waangalifu kwanza.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17

Hata kabla hujamuomba MUNGU kuhusu mtu anayekupenda kama mchumba unatakiwa wewe mwenyewe upime. Je mtu huyo anaendana na viwango vya kiMUNGU au la!?,

Ndio yawezekana ana viwango vizuri vya kidunia mfano fedha,vyeo ,mzuri lakini kama hana viwango vya kiMUNGU hutakiwi kujihisha naye kwenye mahusiano yeyote.

Kitu unachotakiwa kuangalia Je imani yake ni sawa na imani yangu?,kama sivyo unabidi uachane naye hata kama unampenda kiasi gani!
Upendo wenye macho na usio na upofu ndio huu unaoangalia imani, kwa mfano wewe dada ni mkristo na anayetaka kukuchumbia ni mpagani/mbudha au muislamu hapo unabidi uachane naye kwa kuwa atakusumbua popote pale siku za mbeleni.uachane naye hata kama unampenda!.

Asilimia 99.9% ya wanandoa walioana wakiwa na imani zao tofauti mfano mwislamu ameoana na mkristo wamejikuta wakilia na kujutia maisha yao yote kutokana na migogoro isiyokwisha vizazi hata vizazi vyao vyote.

Angalizo:Watu wengi wakiona wamekataliwa kuchumbia kwa sababu ya imani zao mmoja wao hudai kubadilisha dini ili tuu apate kuolewa au kuoa ,Ukweli jambo hilo husumbua wengi kwa kuwa mtu huyo alibadilisha dini hakubadilisha akiwa anamaanisha hivyo baada ya ndoa hurudi alipotokea yaani hurudi dini yake ya awali ambayo alikuwa nayo kabla ya kuolewa /kuoa.

HASARA ZINAZOTOKEA KATIKA NDOA YA WATU WALIO NA DINI TOFAUTI
Hakuna faida kabisa ya kuoa au kuolewa na mtu wa dini yaani imani tofauti nawe hata iwe mnapendana kiasi gani kwa sababu:-

1.Mtashindwa vita zote za kiroho kwa kuwa hamna imani yenye umoja
Kutokana na dini kwa tofauti ndani ya ndoa na imani kuwa tofauti hakuna vita ya kiroho ambayo mtaishinda humo ndani ya nyumba.
Mfano: “biashara yenu imetupiwa mikosi ili isifanye vizuri,”Ninyi kama wanandoa ambao mnadini tofauti hamuwezi kutoa hiyo mikosi hata siku moja kwa kuwa mmoja ataomba kwa jina la YESU;
 mwingine ataomba kwa jina lingine ambalo si la MUNGU kiasi kwamba  hakuna kitakachojibiwa kwa kuwa MUNGU wetu hapendi kushirikiana utukufu na miungu mingine.
Kwa hiyo mtaishi katika mikosi hiyo pasipo kuweza kuitoa mikosi hiyo.

2.Kutokea kutafuta miungu mipya ya kuiabudu.
Watu wengi hujikuta wakijuta na kulia huku wakisema moyoni hawakudhani kama mpenzi wake huyo angebadilika au angekuwa hivyo;
Na hatima yao katika kutafuta suluhu ya vita ya kiroho zinazo wakabili hujikuta wakitafuta miungu mingine jambo ambalo huwaletea shida zaidi.

3.Usishangae kusalitiwa muda wowote / KUTELEKEZWA .
Ukiwa kwenye mahusiano ya mtu asiye na imani au dini moja ujue kabisa na tena ujiandae kabisa kusalitiwa muda wowote ule kwa kuwa pale ambapo wewe utaona amekusaliti labda kwenye dini yake inaruhusiwa!!!.

Utasalitiwa kwa staili za kila namna na muda mwingine utakuwa ukibembelezwa na kuhisi ni mapenzi kumbe unatafutiwa njia ya kusalitiwa Imeandikwa “Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.”- Mithali 6:24
Delila ambaye alikuwa ni mke mwenye imani tofauti na samsoni alimbembeleza sana Samsoni mumewe ili amtajie siri za nguvu zake ikiwa kama njia ya kumsaliti  pasipo samsoni kujua ,Imeandikwa “Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?” Waamuzi 14:16

Naye samsoni alisalitiwa na delila baada ya kumtajia siri ya nguvu zake.Hii ndiyo hasara kubwa ya kuoa au kuolewa na mtu asiye kuwa na imani moja pamoja nawe kwa kuwa muda wowote utajikuta ukisalitiwa.

4.KUFA KABLA YA WAKATI.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17.Hasara ingine ambayo ni kubwa kuliko kawaida kwa watu wanaoana wadini mbili tofauti ni “kufa kabla ya wakati wake” mtu anaweza akawa amekufa ila bado anaishi kama  kopo tuu,

Kwa kuwa maono yake yamefutika ,lengo la yeye kuishi duniani hawezi kulitimiza na kama ana watoto hawezi kuwasomesha tena wala kuwasaidia kwa lolote lile.
5.MIGOGORO ISIYOKWISHA KIZAZI HADI KIZAZI.
Kutokana na uhusiano wa kuwa si watu wa dini moja au imani moja ya kueleweka hivyo ndivyo itavyokuwa migogoro kila kukicha mfano watoto waabudu wapi anaposali baba? au anapo sali mama?Huo ni mgogoro ambao unajitegemea.Na migogoro mingine mingine chungu mzima!.

KITU CHA KUFANYA KAMA KWELI HUTAKI KUJUTA:
i.Kataa kuolewa na mtu asiye wa dini sawa nawe au ambaye anabadilisha dini kwa kuwa anataka akuoe au aolewe na wewe hata kama unampenda.
Kwa msimamo wako huo MUNGU atakupa mtu ambaye atakufaa kuliko huyo ambaye atakuletea maumivu maisha yako yote.
ii.Kama upo kwenye mahusiano na mtu ambaye ni dini tofauti nawe na hamjafunga ndoa pia hamna mtoto,Amua kuachana na huyo kwa kuwa kuna safari kubwa ya majuto inakuvizia kupitia huyo mtu.
Kwako wewe mapenzi hayatakiwi yawe upofu kwako ,ili usijelia vilio ambavyo wengine wanalia sasa hivi duniani kote.
 Kuwa na msimamo kwa kuwa MUNGU wako anaweza kukutafutia mtu ambaye ni mzuri zaidi ya huyo ambaye si wa dini yako ,
MUNGU anachosubiri kutoka kwako ni kuona kama una imani  na kama una imani utakuwa na msimamo wa kujenga hatima ya maisha yako kwa kuachana na mwanamke/mwanaume asiye wa dini moja nawe na kusubiria kuona MUNGU anavyokupatia wakufanana nawe!.

JE UNAONA HUNA UWEZO WA KUMUACHA HUYU ASIYE WA IMANI YAKO?,AU JE UNADHANI HUTAPATA MWINGINE UKIMKOSA HUYO ?
Omba maombi haya kwa imani na kumaanisha nawe utaona matokeo makubwa sana na ya ajabu maishani mwako:
Omba sema kimoyo moyo au kwa sauti “Baba MUNGU katika jina la YESU ninakuomba uondoe moyo wangu kwa mtu yeyote au sehemu yeyote ulipofungwa ambapo si sahihi kwa maisha yangu.Nakuomba ee MUNGU wangu ufungue moyo wangu ili uwe huru .
Nawe Baba MUNGU katika jina la Yesu nakuomba unipe mume/mke wa maisha yangu mwenye imani ya kukuamini wewe MUNGU na sio miungu mingine ,unipe huyo mume/mke ambaye atakaa nami kwa furaha na amani sikuzote.Ninakushukuru sana MUNGU kwa kuwa kwa maombi haya mtandaoni  unakwenda kunipa mtu wa kufanana nami na kuniunganisha naye kuwa mke/mme wangu milele kwa utukufu wako. Asante YESU kwa kunipa ushuhuda.”
Kupitia maombi haya moyo wako umefunguliwa nawe utakaa na kushangaa kumpata mtu sasa ambaye ni wa imani moja nawe ambaye ndiye MUNGU amependezwa wewe kuwa naye.Utashangaaa maajabu ya BWANA !!.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...