Kuna lilo
chungu kuliko mauti nalo ni hili “Kuoa
au kuolewa na mtu mwenye imani tofauti nawe”-Hiki ndicho kifo kinachoumiza
kuliko vyote kwa kuwa mtu atakuwa anakufa huku akishindwa jinsi ya kujisaidia
kuepuka kifo hicho kwa majuto na kila aina ya uchungu ,mbali na yote ni kuacha
kizazi chako chote kikiumia na migogoro mingi ulioianzisha wewe.
Imeandikwa “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani,
mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo;
yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na
yeye.”-Mhubiri 7:26
Hapa sisemeni sana mkristo wa dhehebu fulani anaoana na wa
dhehebu tofauti na yeye hapana
bali nazungumzia watu wawili wa dini tofauti wanapooana huzaa mapooza na
kushindwa tuu katika maisha yao.
Suleimani alikuwa mtu wa MUNGU lakini alikoseshwa na
wanawake wa kigeni yaani wanawake wasiokuwa na imani moja naye ,Imeandikwa “Je!
Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa
mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake,
naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.”-Nehemia
13:26
MUNGU alie hai hapendi mtu wake aoe au aolewe na mtu wa
imani isiyo mwamini YEYE MUNGU wa kweli kwa kuwa watu hao hupofusha maono yao
wenyewe.
Mfano wa mtu aliyeoa mtu wa imani tofauti
naye ni huyu samsoni Imeandikwa “Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia,
Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote,
hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.”-Waamuzi
14:3
Mfano Samsoni alikuwa ni mtu wa MUNGU aliyekua amepewa nguvu
kubwa ya MUNGU kwa ajili ya huduma yake lakini hata kabla ya kumaliza huduma
ile alikufa baada ya kumuoa Delila ambaye alikuwa ni mwanamke wa imani ingine
naye alimbembeleza ili atoe siri zote ;
Na alipotoa ndipo alipomkabidhi kwa
wafilisti wamtese na mpaka kufa kwake.
Imeandikwa “Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma
mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana
ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea
wakachukua ile fedha mikononi mwao.” Waamuzi
16:18
KUPENDA NI UPOFU LAKINI HAITAKIWI KUWE NI
UPOFU KWA MTU ANAYEMJUA MUNGU.
Kwa wewe ambaye unamjua MUNGU hutakiwi kuwa kipofu katika
kupenda mwanamke au mwanaume bali katika kila kitu tunatakiwa kuwa waangalifu
kwanza.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe
kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17
Hata kabla hujamuomba MUNGU kuhusu mtu anayekupenda kama
mchumba unatakiwa wewe mwenyewe upime. Je mtu huyo anaendana na viwango vya kiMUNGU au la!?,
Ndio
yawezekana ana viwango vizuri vya kidunia mfano fedha,vyeo ,mzuri lakini kama
hana viwango vya kiMUNGU hutakiwi kujihisha naye kwenye mahusiano yeyote.
Kitu
unachotakiwa kuangalia Je imani yake ni sawa na imani yangu?,kama sivyo unabidi
uachane naye hata kama unampenda kiasi gani!
Upendo wenye macho na usio na upofu ndio huu unaoangalia
imani, kwa mfano wewe dada ni mkristo na anayetaka
kukuchumbia ni mpagani/mbudha au muislamu hapo unabidi uachane naye kwa kuwa
atakusumbua popote pale siku za mbeleni.uachane naye hata kama unampenda!.
Asilimia 99.9% ya wanandoa walioana wakiwa na imani zao
tofauti mfano mwislamu ameoana na mkristo wamejikuta wakilia na kujutia maisha
yao yote kutokana na migogoro isiyokwisha vizazi hata vizazi vyao vyote.
Angalizo:Watu wengi wakiona
wamekataliwa kuchumbia kwa sababu ya imani zao mmoja wao hudai kubadilisha dini
ili tuu apate kuolewa au kuoa ,Ukweli jambo hilo husumbua wengi kwa kuwa mtu
huyo alibadilisha dini hakubadilisha akiwa anamaanisha hivyo baada ya ndoa
hurudi alipotokea yaani hurudi dini yake ya awali ambayo alikuwa nayo kabla ya
kuolewa /kuoa.
HASARA ZINAZOTOKEA KATIKA NDOA YA WATU WALIO NA
DINI TOFAUTI
Hakuna faida kabisa ya kuoa au kuolewa na mtu wa dini yaani
imani tofauti nawe hata iwe mnapendana kiasi gani kwa sababu:-
1.Mtashindwa vita zote za
kiroho kwa kuwa hamna imani yenye umoja
Kutokana na dini kwa tofauti ndani ya ndoa na
imani kuwa tofauti hakuna vita ya kiroho ambayo mtaishinda humo ndani ya
nyumba.
Mfano: “biashara yenu imetupiwa
mikosi ili isifanye vizuri,”Ninyi kama wanandoa ambao mnadini tofauti hamuwezi
kutoa hiyo mikosi hata siku moja kwa kuwa mmoja ataomba kwa jina la YESU;
mwingine ataomba kwa jina lingine ambalo si la
MUNGU kiasi kwamba hakuna kitakachojibiwa
kwa kuwa MUNGU wetu hapendi kushirikiana utukufu na miungu mingine.
Kwa hiyo mtaishi katika mikosi hiyo pasipo kuweza
kuitoa mikosi hiyo.
2.Kutokea kutafuta miungu
mipya ya kuiabudu.
Watu wengi hujikuta wakijuta na kulia huku
wakisema moyoni hawakudhani kama mpenzi wake huyo angebadilika au angekuwa
hivyo;
Na hatima yao katika kutafuta suluhu ya vita ya kiroho zinazo wakabili
hujikuta wakitafuta miungu mingine jambo ambalo huwaletea shida zaidi.
3.Usishangae kusalitiwa
muda wowote / KUTELEKEZWA .
Ukiwa kwenye mahusiano ya mtu asiye na imani au dini moja
ujue kabisa na tena ujiandae kabisa kusalitiwa muda wowote ule kwa kuwa pale
ambapo wewe utaona amekusaliti labda kwenye dini yake inaruhusiwa!!!.
Utasalitiwa kwa staili za kila namna na muda mwingine
utakuwa ukibembelezwa na kuhisi ni mapenzi kumbe unatafutiwa njia ya kusalitiwa
Imeandikwa “Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa
mgeni.”- Mithali 6:24
Delila ambaye alikuwa ni mke mwenye imani tofauti
na samsoni alimbembeleza sana Samsoni mumewe ili amtajie siri za nguvu zake
ikiwa kama njia ya kumsaliti pasipo
samsoni kujua ,Imeandikwa “Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake,
akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao
wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia,
sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?” Waamuzi 14:16
Naye samsoni alisalitiwa na delila baada ya
kumtajia siri ya nguvu zake.Hii ndiyo hasara kubwa ya kuoa au kuolewa na mtu asiye
kuwa na imani moja pamoja nawe kwa kuwa muda wowote utajikuta ukisalitiwa.
4.KUFA KABLA YA WAKATI.
Imeandikwa “..........; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe
kabla ya wakati wako? “-Mhubiri 7:17.Hasara ingine ambayo ni kubwa
kuliko kawaida kwa watu wanaoana wadini mbili tofauti ni “kufa kabla ya wakati wake”
mtu anaweza akawa amekufa ila bado anaishi kama
kopo tuu,
Kwa kuwa maono yake yamefutika ,lengo la yeye kuishi duniani
hawezi kulitimiza na kama ana watoto hawezi kuwasomesha tena wala kuwasaidia
kwa lolote lile.
5.MIGOGORO ISIYOKWISHA
KIZAZI HADI KIZAZI.
Kutokana na uhusiano wa kuwa si watu wa dini moja
au imani moja ya kueleweka hivyo ndivyo itavyokuwa migogoro kila kukicha mfano
watoto waabudu wapi anaposali baba? au anapo sali mama?Huo ni mgogoro ambao
unajitegemea.Na migogoro mingine mingine chungu mzima!.
KITU CHA KUFANYA KAMA KWELI HUTAKI
KUJUTA:
i.Kataa kuolewa na mtu asiye wa dini sawa nawe au ambaye
anabadilisha dini kwa kuwa anataka akuoe au aolewe na wewe hata kama unampenda.
Kwa msimamo wako huo MUNGU atakupa mtu ambaye atakufaa
kuliko huyo ambaye atakuletea maumivu maisha yako yote.
ii.Kama upo kwenye mahusiano na
mtu ambaye ni dini tofauti nawe na hamjafunga ndoa pia hamna mtoto,Amua
kuachana na huyo kwa kuwa kuna safari kubwa ya majuto inakuvizia kupitia huyo
mtu.
Kwako wewe mapenzi hayatakiwi yawe upofu kwako ,ili usijelia
vilio ambavyo wengine wanalia sasa hivi duniani kote.
Kuwa na msimamo kwa kuwa MUNGU wako anaweza kukutafutia mtu
ambaye ni mzuri zaidi ya huyo ambaye si wa dini yako ,
MUNGU
anachosubiri kutoka kwako ni kuona kama una imani na kama una imani utakuwa na msimamo wa
kujenga hatima ya maisha yako kwa kuachana na mwanamke/mwanaume asiye wa dini
moja nawe na kusubiria kuona MUNGU anavyokupatia wakufanana nawe!.
JE UNAONA HUNA UWEZO WA KUMUACHA
HUYU ASIYE WA IMANI YAKO?,AU JE UNADHANI HUTAPATA MWINGINE UKIMKOSA HUYO ?
Omba maombi
haya kwa imani na kumaanisha nawe utaona matokeo makubwa sana na ya ajabu
maishani mwako:
Omba sema kimoyo moyo
au kwa sauti “Baba MUNGU katika jina la
YESU ninakuomba uondoe moyo wangu kwa mtu yeyote au sehemu yeyote ulipofungwa
ambapo si sahihi kwa maisha yangu.Nakuomba ee MUNGU wangu ufungue moyo wangu
ili uwe huru .
Nawe Baba MUNGU katika jina la Yesu nakuomba unipe mume/mke wa maisha
yangu mwenye imani ya kukuamini wewe MUNGU na sio miungu mingine ,unipe huyo
mume/mke ambaye atakaa nami kwa furaha na amani sikuzote.Ninakushukuru sana
MUNGU kwa kuwa kwa maombi haya mtandaoni
unakwenda kunipa mtu wa kufanana nami na kuniunganisha naye kuwa mke/mme
wangu milele kwa utukufu wako. Asante YESU kwa kunipa ushuhuda.”
Kupitia maombi haya
moyo wako umefunguliwa nawe utakaa na kushangaa kumpata mtu sasa ambaye ni wa
imani moja nawe ambaye ndiye MUNGU amependezwa wewe kuwa naye.Utashangaaa
maajabu ya BWANA !!.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!