ANGALIZO:
YESU haji kuchukua kila mtu aliopo kanisani
bali atakuja kumchukua kila mtu anayetenda mapenzi yake.
YESU anaheshimu na kuja kumchukua mtu anayeTENDEA kazi
neno lake.
Wanaolisikia neno la MUNGU ni wengi,wanaolijua neno la
MUNGU ni wengi lakini WANAOLITENDA neno la MUNGU ni wachache.
Saa na muda wakuokoka ni sasa na sio hapo atakapokuja YESU au
utapokufa,Muda wenye neema ya wewe kuweza kuokolewa ni sasa ,anza kumkiri YESU
kuwa BWANA na mokozi wako kwa sala hii fupi naye atakuokoa saa hii .
MPOKEE
YESU LEO naye ataokoa maisha yako kwa
kuomba sala hii fupi ya toba sasa !.
Omba kwa imani
sema “BABA MUNGU wewe uliyeniumba mimi na
vyote vya ulimwengu huu, ninakushukuru kwa neema yako ya kunikomboa siku hii ya
leo kupitia mtandao huu. Ninakuomba katika jina la YESU unirehemu na unitakase
dhambi zangu zote nilizo zifanya kwakujua ama kutojua iwe ni kwa kuwaza, kunena
au kutenda .
Leo
ninaamua kukufuata wewe YESU KRISTO,leo nimeamua kujikabidhi kwako ili niishi
kwa kadirii ya maagizo yako na sio kwa maagizo yangu,niishi kwa kadri Wewe
upendezwavyo na sio kwa jinsi nitakavyo mimi.Unisaidie nienende katika mwenendo
ukupendezao wewe BWANA MUNGU na unijalie neema ya kuutunza wokovu huu ulionipa
mpaka mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Asante YESU kwa kunipa zaidi ya
niliyoyaomba.”.
Sasa umeokolewa KAMA UMESALI SALA HIYO ,unachotakiwa
kufanya ni kuishi sawa sawa na YESU anavyopenda na kwa kujua mengi basi ungana
na kanisa lililo hai nawe utakulia
huko na kujifunza mambo makubwa zaidi jinsi ya kuwa mwaminifu hata kufa nawe
ili upokee taji ya uzima wa milele.
Hapo uliposali sala hiyo hapo juu umeokolewa na moto
wa milele na pia umeokolewa na kuonewa na shetani kwa kuwa msaada wa MUNGU uu
karibu sana nawe kuliko mwanzo.
“ENDTIME”-TUPO
KATIKA SIKU ZA MWISHO; KARIBU SANA YESU ANAKUJA.
Ni
kweli hizi ni siku za mwisho sana kwa kuwa mapema na hivi punde tuu YESU
atanakuja kulichukua kanisa lake yaani watu wanaotenda mapenzi yake.
Imeandikwa “.. ………..; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”- Mathayo 24:42.
Ni
kweli hakuna ajuaye siku wala saa ya kuja kwake lakini YESU alitoa ishara zake
tutakazo ziona kama maandalizi ya kuja kwake YESU duniani.Tunasema yesu yu
karibu kwa kuwa kila ishara aliyoisema kutokea kipindi cha kuja kwake zi mesha tokea.
1.TAIFA
MOJA KUPIGANA NA TAIFA /UFALME KUPIGANA NA UFALME.
Kweli
kumeshakuwa na vita mbali mbali kwa taifa moja kwenda kupigana na taifa jingine
hii ni ishara ambayo BWANA YESU ametupa ili tukiiona imetokea hiyo tujue kwamba
ndiyo anakuja kwa kuwa katika wakati ni kama uchungu wa mwanamke anapotaka
kujifungua.
Imeandikwa“Kwa maana taifa litaondoka
kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; . . . . . . . . . . Hayo yote
ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8
Kweli
nchi nyingi zimekuwa katika vita na wewe kama mkristo ulisha jihoji na kuona
unabidi uwe macho kiasi gani kwa kuwa YESU yu karibu kuja?.
YESU
alisema dalili ya yeye yu karibu kuja kulichukua kanisa nayo ni kuwa na njaa
kali.
Hii ni ishara ambayo inaonekana mahali mbali mbali ,nchi nyingi zimekuwa na njaa kali kitu ambacho si kawaida. Imeandikwa “. . . . . . . . . . . . . kutakuwa na njaa,…………Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8
Hii ni ishara ambayo inaonekana mahali mbali mbali ,nchi nyingi zimekuwa na njaa kali kitu ambacho si kawaida. Imeandikwa “. . . . . . . . . . . . . kutakuwa na njaa,…………Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo 24:7-8
3.KUTAKUWA
NA MATETEMEKO YA NCHI MAHALI MBALI MBALI.
Imeandikwa
“………………..na matetemeko ya nchi mahali mahali.Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”-Mathayo
24:7-8.
Matetemeko ambayo si ya kawaida kama vile tsunami na mengineyo yanaashiria YESU yu karibu kurudi kuja kuchukua watu wanaotenda mapenzi yake.
Matetemeko ambayo si ya kawaida kama vile tsunami na mengineyo yanaashiria YESU yu karibu kurudi kuja kuchukua watu wanaotenda mapenzi yake.
4.MANABII
WENGI WA UONGO WATATOKEA.
Kumekuwako
na manabii wengi wa uongo duniani ambao wamekuwa wakimpinga YESU na wengine
wakijiita wao ni YEHOVA,YESU wote manabii hao wa uongo wamekuwa wakidanganya
wengi lakini haya yote ni udhihirisho kuwa YESU anakuja mapema sana.
Imeandikwa “Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.”- Mathayo 24:11
Imeandikwa “Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.”- Mathayo 24:11
5.UPENDO WA
WENGI KUPOA NA MAASI KUONGEZEKA.
Kwa
kipindi hiki imekuwa kawaida kusikia vikundi mbali mbali vya kigaidi tena
vikijisifu kwa kuua,kulawiti,kubaka kufanya kila aina ya ubaya na
uharibifu.
Hata baada ya kufanya mabaya hayo yote badala ya kujutia wao hujisifia na kujinadi kuwa wametenda hayo.
Hata baada ya kufanya mabaya hayo yote badala ya kujutia wao hujisifia na kujinadi kuwa wametenda hayo.
Imeandikwa
“Na
kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.”-
Mathayo 24:12
Mambo
hayo yanadhihirisha ujio wake YESU upo karibu sana kwa kuwa alishasema kuwa
upendo wa wengi utapoa na maasi yataongezeka hii ndio ishara ya ujio wake.
Kama
kweli hauhitaji hukumu ya moto wa milele ndugu ni bora ung`ang`ane na YESU kwa
kuwa si muda mrefu YESU anakuja kuhukumu na ndio huo utakapo onekana mwisho wa dunia
hii.
Je siku hizo watu duniani watakuaje !?
Waweza
kujiuliza siku hizo ambazo YSU anakuja watu duniani watakuwa wanafanya nini,au
watashindwa kufnya kazi zao au ?,kutakuwa na nini? .Lakini Watu duniani watakuwa kama vile:-
1.Kama
ilivyokuwa siku za nuhu ndivyo itavyokuwa siku hizo za kuja kwake YESUKRISTO.
YESU atakapokuwa anakuja watu watakuwa wakila ,wakinywa ,wa kuoa watakuwa wakioa,wa kuolewa watakuwa wakiolewa
kama kawaida,
Imeandikwa “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika
siku zake Mwana wa Adamu.
27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile
Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.”-
Luka 17:26-27
2.Kama
ilivyokuwa siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa siku atakayokuja YESUKRISTO.
Siku ya kuja kwake YESU itakuwa kama siku za Nuhu
yaani watu wakila,wakinywa.
Imeandikwa “28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
Imeandikwa “28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
29 lakini
siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni
vikawaangamiza wote.
30 Hivyo
ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.”-
Luka 17:28-30
Kwa maana ingine
ni kwamba siku ambayo YESU “Mwana wa Adamu” atakapo kuja itakuwa siku kama
zingine hakutakuwa kuna chochote cha kushtua sana zaidi kwa wanadamu kiasi cha
kufanya kuigundua siku hiyo kwa namna yeyote ile KABLA YA UNYAKUO.
Je YESU atakuja
duniani tena kwa namna gani ?- “UNYAKUO”
Je
unadhani YESUKRISTO atakuja je duniani ?,Je unadhani dunia hii itakwisha
vipi?.Ni kweli hakuna ajuaye saa wala muda wa kuja kwake YESU lakini Je
unadhani atakuja vipi kuwachukua watu wanaotenda mapenzi yake ?.
YESU
atakuja kwa namna ya unyakuo,yaani kunyakua watu waliompendeza siku zote na
kuishi katika kutenda mapenzi yake.
Imeandikwa“16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,
na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza.”-
1 Wathesalonike 4:16
Waliokufa
katika wokovu wa YESUKRISTO watafufuliwa kwanza na kupewa nguvu mpya kumlaki
YESU mawinguni kwa muda wa haraka sana.
“17 Kisha
sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili
tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”-1 Wathesalonike 4:16-17
Ndipo
YESU atanyakuwa wale ambao walio hai na waliodumu katika kutenda matendo
yanayompendeza yeye YESU.
Imeandikwa“Angalieni,
nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,”-
1 Wakorintho 15:51.YESU atawabadilisha na kuwapa watu wake nguvu ndani yao watu wale ambao
wanatenda mapenzi yake siku hiyo ya mwisho nao watanyakuliwa na hilo tendo
linaitwa unyakuo.
Watakatifu
walioko duniani watanyakuliwa na BWANA YESU na kukutana naye mawinguni katika
muda wa kufumba na kufumbua.
Imeandikwa “19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni,
kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa
mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
20 Njoni,
watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako
ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.”-
Isaya 26:19-20
Hakuna
atayeweza kushuhudia tukio hilo la unyakuo kwa kuwa litachukua muda mdogo sana
yaani kufumbua na kufumba macho.
Imeandikwa“kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”- 1 Wakorintho 15:52
Imeandikwa“kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”- 1 Wakorintho 15:52
Hakuna
mtu atayeweza kuona hali jinsi tukio hilo litavyotokea kwa kuwa litatokea kwa
ghafla sana na kwa haraka.
Imeandikwa
“Kwa
maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo
ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”-Mathayo
24:27
ISHARA
AMBAYO WATU WOTE WALIO BAKIA DUNIANI WATAIONA IKITOKEA
Hakuna mtu ataweza kushuhudia unyakuo huo kwa makini kwa kuwa utafanyika
kwa haraka sana lakini kuna ishara ambayo watu waliobakia katika hii dunia
wataiona nayo kwa baadhi yao itawafanya wajue kuwa YESU ameshakwisha jitwalia
watu wake.Nazo ni:-
1.Watu wengi watakuwa hawapo duniani
Duniani
kote kutatangazwa kuwa na upotevu wa watu kwa kuwa watu wengi watakuwa
wamenyakuliwa hivyo dunia nzima itakuwa imeshindwa kuelewa ni nini kimetokea
mpaka watu mbali mbali hawapo.
Imeandikwa“ Luka 17:34 Nawaambia,
usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja
ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja
atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa,
mmoja ataachwa.” -Luka 17:34-36
Ndugu
ukiona au ukisikia idadi kubwa ya watu wamepotea potea ndani ya siku moja dunia
nzima wewe ujue YESU ameshachukua watu wake na wewe umebaki……. …..cha kufanya
utatakiwa usome makala inayoitwa BAADA YA UNYAKUO…………nawe utajua cha kufanya..c
Idadi kubwa ya watu watapatwa na mshtuko kutokana na
kutokuwaona ndugu au jamaa zao wakaribu kwa ghafla.
Imeandikwa
“40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja
aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa,
mmoja aachwa. ”- Mathayo 24:40-41
Wanawake wanyonyeshao na wajawazito wote watajikuta hawana watoto wao
kwa kuwa YESU atakuwa amesha wanyakua.
Hapo ndipo kutapo kuwa na kuchanga nyikiwa kwa wanawake wengi ambao ni
wenye ujauzito au watoto wadogo kwa kuwa wengi wao hawatajua ni nani aliyewaiba
au ni kitu gani kimetokea.!
DUNIA ITAKUWA KATIKA MISUKOSUKO MI KUBWA KWA MUDA KIDOGO KUTOKANA NA
WATU KUONA UPOTEVU MKUBWA WA WATU!.
-----------------------------------------------------je
nini baada ya kunyakuliwa kwa wateule wa MUNGU kitatokea ………..fuatilia blog hii
kwa makala
ingine.--------------------------------------------------------------
Lakini katika kipindi ambacho YESU hajaja bado yeye anatuonya tena sana
kuwa tuwe macho yaani tusikate tama kutenda yale mema na kudumu katika
utakatifu aliotuagiza kwa kuwa kwa
utakatifu huo tutafanikiwa kwenda mbinguni.
Imeandikwa “Kesheni basi; kwa maana hamjui
ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”- Mathayo 24:42.
Usimuache
YESU wala usikate tama kwa kuwa yu karibu sana kujia watu wake. Imeandikwa “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba,
ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa
Adamu.”- Luka 21:36
Soma post inayoelezea BAADA YA UNYAKUO ujue mambo
yatakayotokea baada ya unyakuo.
Ohhh
ReplyDelete👀
Delete