Mambo ya kufanya unapokabiliwa na vita
Kuna mambo
ambayo mtu anatakiwa kuyafanya anapokabiliwa na vita au magumu katika maisha yake.Nayo
hayo yatakuwa msaada katika kumaliza vita yake katika ushindi mkuu na vizuri
zaidi.
Mambo
yakufanya uanapokabiliwa na vita ni pamoja na:-
i.Kusamehe
Imeandikwa
“Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe niny i
makosa yenu.” Marko 11:26.Mtu anapopitia vita,
anapopitia mambo magumu mara nyingi watu wanaomkejeli na kumcheka ni watu wa
karibu yaani watu wa nyumbani.
Unaweza
kutendewa ubaya na watu wa karibu.Ukatendewa ubaya wa makusudi kabisa lakini
unabidi uwasamehe.Jifunze kusamehe kwa kuwa wewe pia umepokea msamaha kutoka
kwa Mungu kwa njia ya Yesukristo.
Yusufu
aliwasamehe wale ndugu zake waliotaka kumuua wakamuuza.Yusufu alimsamehe hata
mke wa mfalme aliyemsingizia kuwa amembaka “Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na
kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya
Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.” Mwanzo 47:11
Yusufu haku
muhukumu wala kuacha kumsamehe mtumwa aliyekuwa amemsahau kumtaja taja kwa
mfalme “Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje
kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii”mwanzo 40:14.
“ Lakini huyo mkuu wa
wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.” Mwanzo 40:23.Yusufu
alimsamehe hata mnyweshaji kwa kuto kumkumbuka na kumsahau kumtaja taja kwa
mfalme.
Leo kuna
watu wengi wanalalamika kwamba mdogo wangu nilimsomesha mwenyewe lakini leo
amenisahau, leo watu wanalalamika mimi mtu huyu tulianza nae maisha alikuwa
hana hata kitanda tulianza chumba kimoja tukafanikiwa, tukanunua gari tukajenga
kumbe vitu vyote alikuwa ananunua kwa jina lake leo sasa amenifukuza.
Wengine
wanalalamika kwa kuniambia mchungaji huyu kaka nilimsomesha kabisa na wakati
ule ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu, Ila nilivumilia yote nimsomeshe kwa
kuwa aliniahidi atanioa, lakini baada yakumaliza masomao yake amenikimbia na
kwenda kumuoa msichana mwingine.
Watu wanaweza kukutenda vibaya kipindi cha vita yako, wanaweza wakawa
wanakuwazia mabaya hata wanaweza kukusema vibaya.Lakini unatakiwa uwasamehe
haijalishi makosa yao au wanaukaribu na wewe kiasi gani, inabidi uwasamehe tuu.
Vita
aliyokuwa anapambana nayo Daudi ukisoma katika biblia, “Sauli akajaribu kumpiga Daudi
hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo
mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule” 1 Samweli
19:10
Ilifika
kipindi ambacho daudi anajua kuwa anawindwa na sauli ili auwawe lakini daudi
alimsamehe sauli hata pale ambapo alipata nafasi ya kumuua.
Imeandikwa “Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia
Bwana, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote
utakayoona kuwa mema.
Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.Lakini
halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake
Sauli.
Akawaambia
watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha
mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.1 samweli 24:4-6
Daudi hakutaka kulipiza kumtenda vibaya Sauli ingawa Sauli aliazimia kumuua
Daudi.Imeandikwa“Bwana atuamue, mimi na wewe, na Bwana
anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.”
1samweli 24:12
Ili usiweze kutunza uchungu wa mambo mabaya ambayo yaliyokuwekea maumivu ni
bora usamehe imeandikwa“hata kinyume cha hayo, ni
afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake
ipitayo kiasi.” 2 Wakorintho 2:7
Marko
11:25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili
na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
ii.Kumtegemea Mungu
Kumtegemea Mungu ni vyema kwa kuwa Yeye ndiye atupaye uwezo
pale ambapo tumekwama.Imeandikwa “Hata vijana watazimia na kuchoka, na
wanaume vijana wataanguka;
bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu
kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala
hawatazimia” isaya 40:30-31.
Kuna muda unafika ambapo mtu anaweza kupitia mabo
magumu,vita kubwa na asiweze kupatikana hata mmoja wa kukutia moyo wala
kukusaidia.Kama kuna watu ambao mtu anawategemea basi mtu huyo naye anaweza
kufariki muda wowote na ukakosa msaada.
Kwa hiyo katika vita yako mtegemee Mungu naye atakuokoa katika
wakati ambao haukuutarajia kabisa, Mungu anaweza kukupigania na kukuokoa
kwa kuwa tuu umemtumainia.
iii.Kukiri ushindi kabla ya
kutokea
Unapofikwa
na vita katika maisha yako, jizoeshe kukiri ushindi hata kama huoni njia ya
kutokea.Unapopitia mambo magumu hata ndugu na jamaa wanakukatisha tamaa,wewe
zidi tuu kukiri ushindi hata kama bado haujatokea.
Imeandikwa “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake.” Mithali 18:21.Maana yake mtu
akisema atashindwa na atashindwa kweli kwa kuwa kuna nguvu kubwa katika ndimi
zetu.
Kiri ushindi jinenee mema hata kama hali halisi hairuhusu
kukiri ushindi.Kiri ushindi hata kama bado hauuoni ushindi wenyewe,Hakuna neno
lolote utakalolinena ambalo Mungu halijui.Imeandikwa “Maana hamna neno ulimini mwangu
Usilolijua kabisa, Bwana.” Zaburi 139:4
Badala ya
kusema “nitakufa” wewe sema “sitakufa ili niyasimulie matendo ya Bwana”,badala
ya kusema “nitashindwa katika hii vita” wewe sema “vita ni vya Bwana hakika
nauona ushindi mkuu”.
Kuna nguvu katika kukiri au kusema kuna nguvu kubwa sana
katika ulimwengu wa roho.Daudi alikiri ushindi dhidi ya goliati hata kabla ya
ushindi wenyewe kuonekana.Imeandikwa“Ndipo Daudi
akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali
mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli
uliowatukana.
Siku
hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa
chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi
ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.”
1Samweli 17:45- 46
Shadraka, Meshaki na Abednego walikiri kuokolewa na
Mungu dhidi ya moto hata kabla hawaja uona wokovu wenyewe.Imeandikwa “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee
Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile
iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.Bali kama si hivyo, ujue,
Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo
sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha” Daniel 3:16-18
Naye Mungu aliwaokoa Shadraka, Meshaki na Abednego kwa kuwa walikiri
ushindi kwa kumtegemea Bwana,Naye Bwana akawaokoa.“Kisha Nebukadreza akaukaribia
mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na
Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo
Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.
. . . . . . . . . . . . . . . . wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto
ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea,
wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo.”
Daniel 3:26-27
Kwa hiyo siku zote pendelea kukiri ushindi katika jambo lolote lile
unalolipitia kwa kuwa utakula matunda ya ulimi wako.Kiri ushindi ukimtegemea
Bwana kuwa ndiye atakayekupigania.
kwa kuwa hakuna neno
lisilowezekana kwa Mungu.Luka 1:37
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!