JIANDAE KUOLEWA/KUOA !!!!

Kama wewe ni mwanamke jiandae KUMTII mume wako.Jiandae kwa kung`ang`ania mapambo yasio haribika,yaani roho ya upole na utulivu na iliyo thamani mbele za MUNGU.
Imeandikwa “Ninyi wake, watiini waume . . . .  .”- wakolosai 3:18

 Je wewe kama mwanamke unayetarajiwa kuolewa upo tayari  kuongozwa na mume wako?
Mume /Baba ndio kichwa cha familia hata kama hana hela au hajui lolote yeye bado anakuwa kichwa cha familia maana yake maamuzi mengi yanategemewa yatoke kwake au yapitishwe kwa ridhaa yake.

Imeandikwa “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.”-mithali 21:9

Je wewe kama mwanamke unayetarajia kuolewa upo tayari kumtii mumeo kwa ajili ya mambo ambayo hujayapenda ?.
Inawezekana hujazoea kutii mtu yeyote lakini kama unahitaji uwe na ndoa yenye kudumu basi anza kujiweka vyema kumtii mume wako.

Asilimia tisini (90%) ya ndoa ambazo zimevunjika chanzo chake ni wanawake kutotii waume zao.
Utii kwa mumeo  unaweza geuza moyo wa mumeo unaweza fanya hadi mumeo abadilike kama huwa anakuwa mkali anaanza kuwa mpole,utii unaweza fanya.

Inaanza kama utani tuu mwanamke anakuwa hamtii mume wake kwa mambo madogo madogo.
Kwa wanawake wengi kutokutii waume zao kumechangia wanaume kutegeka kirahisi na wanawake ambao wanaonekana wana utii na hata kufanya wanaume hao walio oa tayari kuanza mahusiano na wanawake walio n`nje ya ndoa kwa kuwa tu wanapendezwa na utii wao.

Ukiona ndoa zinavunjika ujue sababu kubwa sio hizo wanazozitaja bali chanzo chake mwanamke alikuwa hana utii,haheshimu mumewe na hakubali aongozwe!.
Wanaume kwa asili hawawezi kuwa na furaha kukaa na mwanamke ambaye hamtii.

Kama  ndoa yako ina matatizo matatizo kama mwanamke sasa badili nia sasa na kuanza kumfanya mume wako ajisikie yeye ni kiongozi yeye ni msemaji wa mwisho wa mambo,ajisikie yeye ni mtu anaongoza na kutegemewa.

Haina maana kila anachosema ni lazima utii hapo hapo hata kama kina madhara lakini unaruhusiwa kumpa ushauri kwa upole na akaupokea vizuri.
Lakini hata kaa akubali ushauri wako endapo kila anachokisema kwako kinakuwa kibaya na unakikataa kwa kumdharau au kuonyesha hali yeyote ya kutokumtii.

Mwanamume jiandae kumpa mke wako heshima

Imeandikwa Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”-Mwanzo 2:18.

Unataka ndoa yako idumu na iwe nzuri yenye furaha na amani inabidi ukubali kuishi kama MUNGU alivyotaka kwa kuwa yeye MUNGU ndiye muanzilishi wa ndoa.

Imeandikwa “. . . . . kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”-1 petro 3:1-7

Kama wewe mwanaume unataka uwe na ndoa yenye amani na kudumu inabidi ujifunze na ujizoeshe kumheshimu mchumba wako/mkeo.

Kila kitu katika maisha kinahitaji maandalizi,na maandalizi yanaweza kutengeneza kitu kikawa kizuri au kibaya kwa hiyo basi maandalizi ni msingi wa kila kitu.Kama unataka kitu kiwe kizuri sana basi inatakiwa maandalizi yake yawe mazuri sana.

Ukiona ndoa ya watu fulani imedumu muda mrefu kwa amani na furaha ujue kila mmoja wao alijiandaa hasa katika moyo wake.
Upendo au hisia pekee hazifanyi ndoa kudumu bali maandalizi ya kitabia ndio yanafanya ndoa kuwa vizuri.

Jiulize hili na upate kujua kuwa kila mtu anapofunga ndoa hua anamapenzi ya dhati kwa mwenzi wake,huwa ana hisia kubwa sana kwa mwenzi wake lakini hushangai baada ya muda watu hao huachana!!!.

Kwa hiyo kosa sio kuwa hawapendani bali hawana tabia zinazoendana kuishi katika ndoa. Kwa hiyo tabia bora katika ndoa ni muhimu  kuliko mali/fedha,upendo ,hisia na vinginevyo.

Maandalizi yakiwa kidogo yatatoa matokeo kidogo,Maandalizi yakiwa makubwa yatatoa matokeo makubwa.
Vivyo hivyo watu wengi wanapenda kuwa na ndoa nzuri zenye furaha na amani lakini hawawi na maandalizi yanayoendana kuipata ndoa nzuri kiasi hicho.

Kwanza kabla ya kuwaza kuoa au kuolewa unatakiwa ujiandae binafsi kuwa mzuri kabla ya kuwaza unataka mtu mzuri kiasi gani.Ninaposema mzuri ninamaanisha uzuri wa moyo na sio wa sura ingawa si tatizo kama nao ukiwa nao.

Mwanzilishi wa ndoa ni MUNGU hivyo ukitaka kuishi maisha ya furaha na amani katika ndoa yako inabidi uangalie na ufuatishe kila maelekezo ya muanzilishi wa taasisi hiyo yaani ndoa.
Kujiandaa kuolewa ni kujitazama mwenyewe kwanza kama  wewe ni mke/mume mwema?

Watu wengi wanaposikia swala la kuolewa/kuoa hufikiria kujiandaa katika maswala ya kiuchumi tuu yaani awe na mali na fedha ndipo aoe au aolewe pasipo kujua kuwa ni muhimu zaidi kuwa na maandalizi katika fikra na tabia kuliko kifedha na mali.

Kwa kuwa kinachofanya ndoa nyingi zivunjike sio kukosa mali/fedha bali ni kukosa tabia njema kati ya wawili hao     
Kwa hiyo kujiandaa kitabia ni vizuri zaidi kuliko kujiandaa kifedha. Huu ndio mwenendo mzima wa kutenda,kufikiri na kusema.


Hekima zitakazokusaidia kuishi vyema katika ndoa !
Hekima ni maarifa kamiliyanayoweza kukusaidia katika mambo mbalimbali.
Sasa kuna hekima inayohitajika kujifunza na kuitumia ili kuwa na ndoa nzuri katika maisha yako yote bila kutengana,wala kuachana.Hizo hekima nazo ni pamoja na :-
                                                                                                                                         
1.Jua namna ya kuutumia ulimi wako.
ImeandikwaMpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.”-Mithali 29:11
Kuwa mwenye uwezo wa kuongea mambo ya maana na katika wakati unaofaa.Tena ni bora kunyamaza kuliko kuongea mambo yatayochochea hasira.

Imeandikwa Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo”-Mithali 11:12-13.


2.ONGEA KWA UPOLE
Haina haja yeyote ya kuongea mwenzi wako kwa ukali na si vyema kuongea kwa ukali na mwenzi wako.
Imeandikwa “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.”-mithali 15:1

Tuwe na uvumilivu kwa magumu ili kuweza kuongea kwa upole na heshima na hiyo ndio hekima kuu.

Imeandikwa “Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.”-mithali 25:15

3.Angalau Fikiri kabla hujaongea neno.

“Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye”-Mithali 29:20
Kabla ya kutoa neno ni hekima sana ukiwa una fikiri kuliko kuongea mabaya juu ya jambo lolote kwa mwezi wako.Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.”-mithali 15:28

Ongea kitu kwa namna ya kufundisha na namna ya kujenga nasio kulaumu au kukosoa ili eti uonekane uko mkamilifu sana.
“Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.”-mithali 16:23


4.Angalau sikiliza kabla ya kuongea neno/usiwe mwepesi wa kuongea.
Imeandikwa Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.”-mithali 18:13

Mabishano mengi katika mahusiano hutokea kwa kuwa tuu kuna mmoja kati yao ambaye hajamsikiliza mwenzie kwa kuongea pasipo kutaka kumsikiliza mwenzie.

 “Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”-Mithali 10:8

5.Usiongeze chumvi
Imeandikwa “Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka”- mithali 19:5
Si sawa kuwa muongo yaani mtu wa kunena uongo ni bora uongee ukweli hata kama ukweli huo unaweza kuwa unaumiza sana lakini ni bora uuseme huo kuliko uongo.

Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu.”- mithali 19:1


6.Kuwa makini na utani/jinsi unavyotania.
Utani una asilimia 50% za kujenga na pia utani una asilimia 50 % za kubomoa.Kwa hiyo upomtania mpenzi wako kuwa sana makini na utani unaoufanya kwa kuwa unaweza utani huo ukamkwaza.

Imeandikwa “Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti;
 Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?”-Mithali 26:18-19

7.Penda kutumia maneno yanayojenga katika maongezi yako
Ongea mambo yanayojenga kwa maneno ya kuvutia hata kama yeye huwa hafanyi hivyo.
Imeandikwa“Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.”-mithali 12:18

Kuna mambo ambayo mtu akiambiwa moja kwa moja anakuwa na furaha na amani. Mfano neno:nakupenda,pole,asante,samahani,nisamehe na n.k
“Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha.”-Mithali 12:25


Kuishi katika ndoa yenye amani na upendo si bahati nasibu si kamari bali ni kuamua na kupangilia kwa kujizoesha tabia njema.











Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...