Kama
wewe ni mwanamke jiandae KUMTII
mume wako.Jiandae kwa kung`ang`ania mapambo yasio haribika,yaani roho ya upole
na utulivu na iliyo thamani mbele za MUNGU.
Imeandikwa “Ninyi wake, watiini waume . . . . .”- wakolosai 3:18
Je wewe
kama mwanamke unayetarajiwa kuolewa upo tayari
kuongozwa na mume wako?
Mume
/Baba ndio kichwa cha familia hata kama hana hela au hajui lolote yeye bado
anakuwa kichwa cha familia maana yake maamuzi mengi yanategemewa yatoke kwake
au yapitishwe kwa ridhaa yake.
Imeandikwa “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,
Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.”-mithali 21:9
Je wewe kama mwanamke unayetarajia kuolewa upo
tayari kumtii mumeo kwa ajili ya mambo ambayo hujayapenda ?.
Inawezekana
hujazoea kutii mtu yeyote lakini kama unahitaji uwe na ndoa yenye kudumu basi
anza kujiweka vyema kumtii mume wako.
Asilimia
tisini (90%) ya ndoa ambazo zimevunjika chanzo chake ni wanawake kutotii waume
zao.
Utii kwa mumeo
unaweza geuza moyo wa mumeo unaweza fanya hadi mumeo abadilike kama huwa anakuwa mkali anaanza kuwa
mpole,utii unaweza fanya.
Inaanza
kama utani tuu mwanamke anakuwa hamtii mume wake kwa mambo madogo madogo.
Kwa
wanawake wengi kutokutii waume zao kumechangia wanaume kutegeka kirahisi na
wanawake ambao wanaonekana wana utii na hata kufanya wanaume hao walio oa
tayari kuanza mahusiano na wanawake walio n`nje ya ndoa kwa kuwa tu
wanapendezwa na utii wao.
Ukiona
ndoa zinavunjika ujue sababu kubwa sio hizo wanazozitaja bali chanzo chake
mwanamke alikuwa hana utii,haheshimu
mumewe na hakubali aongozwe!.
Wanaume kwa asili hawawezi kuwa na furaha kukaa
na mwanamke ambaye hamtii.
Kama ndoa yako ina matatizo matatizo kama mwanamke
sasa badili nia sasa
na kuanza kumfanya mume wako ajisikie yeye ni kiongozi yeye ni msemaji wa
mwisho wa mambo,ajisikie yeye ni mtu anaongoza na kutegemewa.
Haina maana kila anachosema ni lazima utii hapo
hapo hata kama kina madhara lakini unaruhusiwa kumpa ushauri kwa upole na
akaupokea vizuri.
Lakini
hata kaa akubali ushauri wako endapo kila anachokisema kwako kinakuwa kibaya na
unakikataa kwa kumdharau au kuonyesha hali yeyote ya kutokumtii.
Mwanamume
jiandae kumpa mke wako heshima
Imeandikwa “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake,
nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”-Mwanzo 2:18.
Unataka ndoa yako idumu na iwe nzuri yenye furaha na
amani inabidi ukubali kuishi kama MUNGU alivyotaka kwa kuwa yeye MUNGU ndiye
muanzilishi wa ndoa.
Imeandikwa “. . . . . kumpa mke heshima, kama chombo
kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu
kusizuiliwe.”-1 petro 3:1-7
Kama wewe mwanaume unataka uwe na ndoa yenye amani na
kudumu inabidi ujifunze na ujizoeshe kumheshimu mchumba wako/mkeo.
Kila kitu katika maisha kinahitaji maandalizi,na maandalizi
yanaweza kutengeneza kitu kikawa kizuri au kibaya kwa hiyo basi maandalizi ni
msingi wa kila kitu.Kama unataka kitu kiwe kizuri sana basi inatakiwa
maandalizi yake yawe mazuri sana.
Ukiona ndoa ya watu fulani imedumu muda mrefu kwa amani na
furaha ujue kila mmoja wao alijiandaa hasa katika moyo wake.
Upendo au hisia pekee hazifanyi ndoa kudumu bali maandalizi
ya kitabia ndio yanafanya ndoa kuwa vizuri.
Jiulize hili na upate kujua kuwa kila mtu anapofunga ndoa
hua anamapenzi ya dhati kwa mwenzi wake,huwa ana hisia kubwa sana kwa mwenzi
wake lakini hushangai baada ya muda watu hao huachana!!!.
Kwa hiyo kosa sio kuwa
hawapendani bali hawana tabia zinazoendana kuishi katika ndoa. Kwa hiyo tabia
bora katika ndoa ni muhimu kuliko
mali/fedha,upendo ,hisia na vinginevyo.
Maandalizi yakiwa kidogo yatatoa matokeo kidogo,Maandalizi
yakiwa makubwa yatatoa matokeo makubwa.
Vivyo hivyo watu wengi wanapenda kuwa na ndoa nzuri zenye
furaha na amani lakini hawawi na maandalizi yanayoendana kuipata ndoa nzuri
kiasi hicho.
Kwanza kabla ya kuwaza kuoa au kuolewa unatakiwa ujiandae
binafsi kuwa mzuri kabla ya kuwaza unataka mtu mzuri kiasi gani.Ninaposema
mzuri ninamaanisha uzuri wa moyo na sio wa sura ingawa si tatizo kama nao ukiwa
nao.
Mwanzilishi wa ndoa ni MUNGU hivyo ukitaka kuishi maisha ya
furaha na amani katika ndoa yako inabidi uangalie na ufuatishe kila maelekezo
ya muanzilishi wa taasisi hiyo yaani ndoa.
Kujiandaa
kuolewa ni kujitazama mwenyewe kwanza kama
wewe ni mke/mume mwema?
Watu wengi wanaposikia swala la kuolewa/kuoa hufikiria
kujiandaa katika maswala ya kiuchumi tuu yaani awe na mali na fedha ndipo aoe
au aolewe pasipo kujua kuwa ni muhimu zaidi kuwa na maandalizi katika fikra na
tabia kuliko kifedha na mali.
Kwa
kuwa kinachofanya ndoa nyingi zivunjike sio kukosa mali/fedha bali ni kukosa
tabia njema kati ya wawili hao
Kwa
hiyo kujiandaa kitabia ni vizuri zaidi kuliko kujiandaa kifedha. Huu
ndio mwenendo mzima wa kutenda,kufikiri na kusema.
Hekima zitakazokusaidia
kuishi vyema katika ndoa !
Hekima ni maarifa kamiliyanayoweza kukusaidia katika
mambo mbalimbali.
Sasa kuna hekima inayohitajika kujifunza na kuitumia
ili kuwa na ndoa nzuri katika maisha yako yote bila kutengana,wala
kuachana.Hizo hekima nazo ni pamoja na :-
1.Jua namna ya kuutumia ulimi wako.
Imeandikwa“Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote;
Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.”-Mithali 29:11
Kuwa mwenye uwezo wa
kuongea mambo ya maana na katika wakati unaofaa.Tena ni bora kunyamaza kuliko
kuongea mambo yatayochochea hasira.
Imeandikwa “Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali
mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye
roho ya uaminifu husitiri mambo”-Mithali 11:12-13.
2.ONGEA
KWA UPOLE
Haina haja yeyote ya kuongea mwenzi wako kwa ukali na
si vyema kuongea kwa ukali na mwenzi wako.
Imeandikwa “Jawabu
la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.”-mithali 15:1
Tuwe na uvumilivu kwa magumu ili kuweza kuongea kwa
upole na heshima na hiyo ndio hekima kuu.
Imeandikwa “Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na
ulimi laini huvunja mfupa.”-mithali 25:15
3.Angalau
Fikiri kabla hujaongea neno.
“Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno?
Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye”-Mithali 29:20
Kabla ya kutoa neno ni hekima sana ukiwa una fikiri
kuliko kuongea mabaya juu ya jambo lolote kwa mwezi wako.“Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi
atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.”-mithali 15:28
Ongea kitu kwa namna ya kufundisha na namna ya kujenga
nasio kulaumu au kukosoa ili eti uonekane uko mkamilifu sana.
“Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake;
Huzidisha elimu ya midomo yake.”-mithali 16:23
4.Angalau
sikiliza kabla ya kuongea neno/usiwe mwepesi wa kuongea.
Imeandikwa “Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu
kwake.”-mithali 18:13
Mabishano mengi katika mahusiano hutokea kwa kuwa tuu
kuna mmoja kati yao ambaye hajamsikiliza mwenzie kwa kuongea pasipo kutaka
kumsikiliza mwenzie.
“Aliye na akili
moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”-Mithali
10:8
5.Usiongeze
chumvi
Imeandikwa “Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala
asemaye uongo hataokoka”- mithali 19:5
Si sawa kuwa muongo yaani mtu wa kunena uongo ni bora
uongee ukweli hata kama ukweli huo unaweza kuwa unaumiza sana lakini ni bora
uuseme huo kuliko uongo.
“Afadhali
maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu.”-
mithali 19:1
6.Kuwa
makini na utani/jinsi unavyotania.
Utani una asilimia 50% za kujenga na pia utani una
asilimia 50 % za kubomoa.Kwa hiyo upomtania mpenzi wako kuwa sana makini na
utani unaoufanya kwa kuwa unaweza utani huo ukamkwaza.
Imeandikwa “Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na
mishale, na mauti;
Ndivyo alivyo
amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?”-Mithali 26:18-19
7.Penda
kutumia maneno yanayojenga katika maongezi yako
Ongea mambo yanayojenga kwa maneno ya kuvutia hata
kama yeye huwa hafanyi hivyo.
Imeandikwa“Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma
kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.”-mithali 12:18
Kuna mambo ambayo mtu akiambiwa moja kwa moja anakuwa
na furaha na amani. Mfano neno:nakupenda,pole,asante,samahani,nisamehe na n.k
“Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema
huufurahisha.”-Mithali 12:25
Kuishi katika ndoa yenye amani na upendo si bahati
nasibu si kamari bali ni kuamua na kupangilia kwa kujizoesha tabia njema.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!