MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA


Kuna vita kubwa kuacha tabia mbaya ambazo  hazimpendezi MUNGU.Tabia mbaya ambazo zimejiwekea mazoea katika maisha yetu mpaka zinakuwa na nguvu kana kwamba ni sehemu ya maisha yetu.

Imeandikwa “ Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohon i ”-1 Wakorintho 2:14

Watu wengi wanaokoka na kuanza maisha ya wokovu huku bado zile tabia zao zamani kabla hawajaokoa zinawafuatilia na kuwasumbua sumbua.

Mfano: labda mtu alikuwa mlevi sana kabla ya kuokoka basi  baada ya kuokoka anaweza kuwa anajikuta mara kwa mara anajaribiwa kurudia ile tabia ya kulewa.

Baadhi ya tabia sugu kwa watu wengi ambazo zinamchukiza MUNGU ni
ü  Ulevi

ü  Kusema uongo
ü  Kutukana matusi
ü  Kuangalia picha za uchi
ü  Kupiga punyeto/kujichua
ü  Uzinzi
ü  Uvivu
ü  Hasira
ü  Na n.k



Hakika kuna dawa ya kuacha tabia mbaya iliyokithiri yaani “addiction” na dawa pekee inayoweza kutatua ni uwepo wa MUNGU ambao huondoa kiu ya mambo machafu na kuweka kiu ya kutafuta mambo ya Rohoni zaidi.









Unapokuta mtu ameacha kwa kujilazimisha na kujizuia kimwili labda ilikuwa ni tabia ya kuvuta sigara na akaamua kuacha kwa kujilazimisha pasipo msaada wa MUNGU huyo anawezekana 

anaonekana kimwili kama ameacha lakini kiroho bado ile tabia anayo na ndio maana  mara nyingi anaweza jikuta akilala huwa anaota anavuta sigara pia watu kama hao hawakai sana wakiwa wameziacha tabia hizo bali si muda utasikia amezirudia tena na akizirudia anakuwa na kiu kubwa zaidi ya awali.

Imeandikwa “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.” -Warumi 2:14

Ukweli ni kwamba uwepo wa MUNGU pekee ndio anaweza kukufutia kiu ya mazoea ya kutenda tabia mbaya.
Je huo udhihirisho wa MUNGU au uwepo wa MUNGU unapatikana vipi  ?.
Uwepo wa MUNGU unapatikana kwa kumuomba MUNGU mara kwa mara kwa kuwa uwepo huo huondoa kiu ya dhambi kabisa.

MAMBO YA KUFANYA ILI UONDOKANE NA TABIA MBAYA INAYOKUSUMBUA
Kila mtu anatabia fulani inayomsumbua ambayo anatamani imtoke ili azidi kuwa safi mbele za MUNGU na kuweza kumwabudu MUNGU katika roho na kweli,Yamkini  tabia ambayo wewe inakusumbua ni madawa ya kulevya,ulevi,uzinzi,pornography,kusengenya,kutukana,au kuhukumu watu.

Haya ni mambo unayotakiwa kuyafanya ili uondokane na tabia hizo :-
1.Kabla hujaitenda lazimisha kutaka uwepo wa MUNGU.
Pindi unapojisikia hamu ya kutenda ile tabia mbaya inayokusumbua labda ni kuvuta sigara,madawa ya kulevya au ni uzinzi ,

Basi wewe  jitahidi kabla ya kufanya hiyo tabia inayokusumbua  jitafutie sehemu ya siri labda ni chumbani na uombe kidogo tuu na ndipo utakapo shangaa kwa kuwa ukitoka utajikuta huna hamu tena ya kutenda ile tabia mbaya.

Mfano: Kunywa pombe, kuvuta sigara, kutumia madawa ya kulevya yaani tabia yoyote ambayo ni mbaya  badala ya kukimbilia kuitenda hiyi tabia ,Jiambie kama utani kuwa ngoja nika Sali kwanza ndipo nitakuja kifanya hiyo tabia mbaya hapo wewe nenda chumbani kwako sirini uombe MUNGU

uwepo huo unakufanya uisikie vizuri sauti ya MUNGU kupitia Roho mtakatifu.

Kila tabia mbaya yaani,uzinzi,uasherati ,tamaa mbaya,kuvuta sigara, madawa, kukasirika, kutukana, kunywa pombe, kusema uongo, 

kujichua au kupiga punyeto . . . . . . . . .tabia zote mbaya huwa zinapewa nguvu na roho za giza yaani mapepo ilizifanye kazi katika maisha yetu kwa hiyo unapokaribia uwepo wa MUNGU kwa njia ya maombi ya mara kwa mara baasi hayo mapepo yanayoleta  kiu ya kuendelea na tabia mbaya yanakimbia.

Na unapokuwa mbali na uwepo wa MUNGU basi mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukuharibu kwa kukupa kiu na hamu kubwa ya kurudia ile tabia fulani mbaya uliyoiacha.


2.Mara kwa mara unahitajika kumuomba MUNGU juu ya tabia mbaya uliyo nayo  hata kama ulishamuomba.

Imeandikwa “ombeni bila kukoma;Ukweli” 1 Wathesalonike 5:17 .




Usiogope kuomba hata mara kumi(10) kwa siku juu ya tabia ikusumbuayo kwani ukweli ni kuwa mwanzoni nguvu hiyo inakuwa inafanania na chaji katika simu  ,kwa kuwa uwepo huo wa MUNGUunweza  kupungua na unaweza ungezaka ,

Uwepo huo unapopungua sana ndipo hujikuta unatamani kufanya na kuzirudia zile tabia mbaya za zamani ,hapo  ukurudi kumuomba MUGU tena kuhusu hiyo hiyo tabia na uwepo wa MUNGU unajichaji na kuongezeka kwako kukuondolea ile kiu ya dhambi.

Hatutakiwi kuacha kuomba kwa ajili ya tabia mbaya zitusumbuazo kwa kuwa tunapoomba MUNGU hushusha wingu lake ambao ndio uwepo na kwa huo unafukuza kila pepo wanaoleta kiu za kutenda zile tabia mbaya katika maisha yako.

 “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.. .” Yakobo 5:16
3.Jitenge na mazingira yaliyo rafiki na tabia unayoikataa

Jitenge na mazingira ambayo yanaurafiki na tabia unayoipinga :Mfano labda unatumia madawa ya kulevya na umeamua  sasa unabidi uachane na kundi la marafiki wa aina hiyo kwa kutokaa karibu na mazingira yao.

Jiondoe kwenye mazungumzo na watu ambao wanakufanya ukumbuke ile tabia ambayo huipendi.Imeandikwa “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” 1 Wakorintho 15:33.

Jitahidi kukaa karibu na watu wanaokupa moyo wa kuiacha ile tabia mbaya na sio kukaa karibu na wanaokuchukia na kukucheka kwa uamuzi wako wa kuacha hiyo tabia mbaya.

4.Kiri na sema mara kwa mara kile tuu unachokipenda kitokee na sio unachokitenda.

Siku zote sema mimi nitaacha hii tabia mbaya inayonisumbua labda ya kuvuta sigara,ulevi nitaacha umalaya,nitaacha kuangalia picha za uchi(pornography),nitaacha kupiga punyeto(kujichua/ masturbation), 

kiwe chochote we sema tuu hata kama bado unaendelea na tabia hiyo tabia mbaya wewe endelea kusema tuu hata kama unasema huku ukiwa huna uhakika kama itakuwa rahisi hivyo.

Kuna nguvu kubwa katika vinywa vyetu  ingawa haionekani kwa macho.“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”-Mithali 18:21

Kuwa na hali ya kuongea kile unachotaka kitokee na sio kile unachokitenda ,kwa kuwa waweza kuwa unapenda sana uache hiyo tabia mbaya lakini unashindwa kujisemea kuwa nitaiacha kwa kuwa bado kila iitwapo leo unaitenda.

Imeandikwa  “Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila .”- Zaburi 34:13
Kwa kinywa chako kinaumba kitu katika ulimwengu wa kiroho ambao huja kutokea katika ulimwengu wa kimwili.Kwa hiyo ukiwa mara kwa mara bila kuchoka unajisemea nitaiacha tuu tabia mbaya niliyo nayo”,au kuna siku nitakuja kuacha milele hii tabia mbaya kwa msaada wa MUNGU,Kweli utashangaa siku utaacha kabisa na itakuwa shuhuda kubwa sana .imeandikwa“. . . . . . . . . . . . . . . .. . . . . . . . ; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.”-  Zaburi 45:1

“Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. “- Mithali 15:2

5.Usikate tamaa kumrudia MUNGU pale unapoanguka mara kwa mara.
Usije kata tamaa  kumuomba msamaha MUNGU mara kwa mara pale unapoanguka katika hiyo tabia mbaya.

MUNGU anapenda watu wote ila anachukia dhambi,kwa hiyo usione aibu kumwendea MUNGU kuomba msamaha kila unapoirudia ile tabia mbaya ambayo huipendi .



Kwa kuto kukata tamaa kwako  juu ya kumuomba msamaha MUNGU kila unapoitenda hiyo tabia yako mbaya,

Yeye MUNGU hutuma uwezo wake kwa neema yake ukusaidie kuacha hiyo tabia kwa kuwa anajua kuwa ukiacha hiyo tabia mbaya utaweza kumtumikia vyema na kwa ujasiri zaidi.

MUNGU hajali kuwa umeirudia ile tabia yako mbaya mara ngapi ,bali anajali umenyanyuka nakumrudia MUNGU kila ulipo itenda hiyo dhambi inayotokana na tabia yako.

Imeandikwa “ Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; . . . . . . . . . . .” Mithali 24:16.

Kitu cha muhimu ni kwamba kila unapoanguka nakuirudia tabia yako mbaya hapo hapo rudi kwake MUNGU na kutubu kwa ajili ya hicho ulichotenda naye atakusamehe na kukupa nguvu ya kuacha hiyo tabia mbaya.     




3 comments :

  1. nashukuru sana kwa mafundisho..nimejifunza mengi sana kutoka kwako kiongozi wangu Ubarikiwe...kuanzia leo nitaacha hii tabia yangu ya kupiga punyeto

    ReplyDelete

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...