UBATIZO KATIKA USAHIHI WAKE

Ubatizo ni nini ?.
Ubatizo ni tendo la imani la kuunganishwa na YESUKRISTO katika kifo chake kwa ishara ya kutumbukizwa kwenye maji na kuibuka.
Unapobatizwa jua kuwa utu wa mwanzo/wa dhambi(wa kale) unazikwa pale unapozama kwenye maji na unapotoka kwenye maji unakuwa unafufuka na utu mpya(utu wa YESUKRISTO).
Utu wa kale-  ni misingi ya mababu ya kuabudu mizimu,majinamizi,mizuka na miungu ya ajabu ajabu n.k.

Utu mpya- ni misingi mizuri ya kumpenda YESU na kuwa na agano sahihi naye YESUKRISTO.

TUNAPOENDA KUBATIZWA TUNATAKIWA TUENENDE KWA IMANI MIOYONI MWETU.
Ubatizo ni tendo na hatuokolewi kwa matendo bali kwa imani. Imeandikwa Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.”- Yakobo 2:17.

Tunapoendea kubatizwa tunatakiwa tufanye je kisahihi ?,Tunatakiwa tuende tukiamini mioyoni mwetu kuwa tunapobatizwa tunakuwa tunamkiri YESU hadharani kuwa  tumeamua kuungana naye milele.
Pia tunapobatizwa tunatakiwa tuenende huku tukiamini kuwa kwa kubatizwa tunakuwa tumeshiriki naye kwa kufa naye YESU na tunapotoka ndani ya maji tunafufuka naye kutoka katika wafu kwa ushindi wa msaada wa ROHO wake mtakatifu.

Imeandikwa “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.”-Wakolosai 2:12

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...