Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa

Kuna uongo mwingi ambao umepandwa kwenye dini na tumezaliwa na kuupokea kama ilivyo pasipo kujua mambo hayo ni machukizo sana kwa MUNGU na yanaleta laana katika maisha yetu.

Mbaya zaidi mafundisho hayo hayatupeleki mbinguni bali motoni kwa faraja isiyo na msingi.
ImeandikwaMsifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”- Mambo ya Walawi 26:1

Kuona watu wengi wanafanya jambo fulani haimaanishi jambo hilo ndiyo sahihi. Imeandikwa   Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.”- Mathayo 7:13

Kwanza kumbuka watu wengi ndio wataoenda motoni katika siku ya hukumu ya MUNGU na ni wachache ambao wataokolewa na YESU.Imeandikwa “Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”- Mathayo 7:14.

Hivyo basi kaa macho na ujiokoe nafsi yako kwa kuwa wingi wa watu kuamini kitu flani haumaanishi kitu hicho ndiyo sahihi.

Mafundisho ya uongo yalikuwepo tokea YESU alipokuwepo ,YESU aliwatahadharisha wanafunzi wake juu ya mafundisho hayo mabaya na ya uongo. Imeandikwa “11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

12 Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.”- Mathayo 16:11-12

Kuna makanisa mengi na huduma nyingi ambazo zina mafundisho potovu juu ya MUNGU nayo mengineyo ni mafundisho ya kuabudu sanamu.Ndugu MUNGU ameniruhusu leo nikwambie ibada za kuabudu sanamu haziokoi na MUNGU hapendezwi nazo.

MAMBO AMBAYO WATU HUAMINI NI SAHIHI NA KUMBE NI POTOFU NA NI UONGO.
Inauma sana ukija kugundua kuwa ulitumia muda wako duniani ukiabudu katika dini yako, kutenda matendo mazuri na kutoa kila aina ya sadaka nzuri kwa  kudhani unatengeneza maisha yako baada ya KUFA kumbe kutokana na kuabudu kwako sanamu na kushika kwako mafundisho ya uongo, MUNGU hakusikii na wala hatakuokoa na moto wa milele !.

1.Kuomba sala kupitia mtakatifu fulani ili akuombee kwa MUNGU.
Tumepewa jina lenye nguvu kuliko majina yote nalo ni YESUKRISTO hivyo  unapo omba kupitia mtakatifu fulani ni ibada za sanamu.

 i.Mtakatifu huyo alipewa utakatifu na wanadamu na sio na MUNGU kwa kuwa wanadamu wanaweza ona mtu huyo ni mta katifu nab ado MUNGU asimuone ya kuwa ni mtakatifu.
  ii.Mtakatifu huyo ni binaadamu na siyo MUNGU hivyo hana uwezo wala mamlaka ya kukuombea toba.
 iii.MUNGU anapenda tumuombe yeye mwenyewe kupitia jina la YESU pekee.Imeandikwa Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Yohana 16:24”
Hivyo kuomba sala kupitia mtakatifu fulani si sahihi na ni matendo ya kuabudu sanamu(iwe mtakatifu huyo amekufa au yuko hai).

2.Kuomba sala kwa bikira mariamu kama mama wa MUNGU
Mariamu alitumiwa kama kipitisho tuu na sio mama wa YESU.Baadhi ya makanisa humuita Mariamu mama wa MUNGU,Huo ni uongo ambao MUNGU huchukizwa nao, Kwa kuwa YESU alikuwepo hata kabla ya kuwepo kwa dunia.

Imeandikwa “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.”- Yohana 8:58
Mungu hawezi kuwa na mama,kwa hiyo haya yote ni uongo ambao umepandwa kwenye dini na tumezaliwa na kupokea kama ilivyo pasipo kujua mambo hayo ni machukizo sana kwa MUNGU kwa kuwa utukufu wake unaibiwa na kupewa Mariam.

Mfano:Ni sawa na mchungaji aombee mtu mwenye ugonjwa na ugonjwa huo ukaondoka halafu mtu huyo akasema yeye ni mponyaji,bila kusema yeye ametumika tu lakini aliyeponya ni MUNGU.

Hivyo mariamu alitumika tuu kumzaa YESU kwa kuwa hakumjua mwanaume yeyote kabla hajamzaa YESU.Hivyo MUNGU atakuja kuhukumu wote ambao wanadhani mariamu ni mama wa MUNGU.

3.Kuamini kuwa kuna dhambi ndogo ndogo na kubwa.
Kuna uongo mwingi sana kwenye baadhi ya huduma na makanisa unao wafanya watu waamini wanaweza kufa  kama wakiwa  wenye dhambi ndogo ndogo  basi watu wakimuombea anakwenda mbinguni huo ni uongo na kujidanganya tuu wenyewe.

Imeandikwa “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; “-Waebrania 9:27
 Kwa kuwa baada ya kufa ni hukumu, nafasi ya kutubu ni sasa unapokuwa lakini ukifa tuu basi nafasi ya kutubu huna bali kuna hukumu tuu.

Ukweli ni huu kuwa kwa MUNGU hakuna dhambi ndogo wala kubwa bali dhambi zote ni sawa na ukivunja amri moja ya MUNGU ni sawa na umevunja zote.
Hivyo mafundisho yasemayo kuna dhambi kubwa au ndogo hayo ni ya uongo na kwa hayo ni ibada za sanamu ambazo hazimpendezi MUNGU.

4.Mahubiri yasemayo hakuna hukumu kuzimu wala moto wa milele.
Kuna mafundisho ya uongo mwingi ambayo yanadai tuu hakuna hukumu ya moto wa milele kwa kuwa eti MUNGU ni MUNGU wa rehema tuu.

Ndugu mafundisho hayo ni ya uongo kwa kuwa MUNGU kweli ni wa rehema lakini pia ni MUNGU wa haki naye hajipingi.
Imeandikwa “bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao”- Waebrania 10:27

5.Mafundisho ya kumjua MUNGU pasipo kumjua YESU.
YESU ndiye mpatanishi kati ya wanadamu na MUNGU hivyo hakuna namna ya kumjua MUNGU pasipo kumjua YESU. Imeandikwa Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”- Yohana 14:6
Hivyo hakuna jinsi ya kumfikia MUNGU pasipo YESU ambaye ni mpatanishi kati yetu na MUNGU.
Kwa hiyo kuamini kuwa kuna MUNGU na kutoamini habari za YESU ni matendo ya usanamu.
6.Mafundisho ya kutoku mtambua Roho mtakatifu.
Mafundisho ya uongo ambayo hayakubaliani kuwa YESU kweli alituachia msaidizi ambaye ni Roho mtakatifu ambaye ni Roho wa MUNGU mwenye awezaye kutusaidia.
Ni mafundisho ya uongo ya kutoamini nguvu ya ROHO mtakatifu aliyoiacha KRISTO ndani ya kila amwaminiye YESU.

7.Mafundisho ya mpinga KRISTO-{mohamed}
Kuna mafundisho ya uongo na potofu ambayo yamejaza watu katika misikiti na masinagogi yanayompinga YESU.
Imeandikwa Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.” -2 Yohana 1:7.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------Tubu sasa kwa MUNGU na uachane na mafundisho ya uongo ambayo hayakusaidii kwa kuwa siku ya mwisho ya hukumu hayatakuokoa.Jitenge na huduma , makanisa yenye kuhusisha kuabudu sanamu kwa namna yeyote ile.

Kama ukifa ukiwa bado ukiishi katika mafundisho hayo ya uongo unaenda MOJA KWA MOJA sehemu mbaya iitwayo KUZIMU, sehemu iliyojaa mateso ya kila aina na huku ukingojea hukumu ya MUNGU.- HAPO HAPANA NAFASI YA KUTUBU TENA.

Kama kweli ndugu unataka kuishi maisha salama yaani sasa na hata baada ya kufa kwako unabidi umfuate YESU na kuishi jinsi yeye anavyopenda na sio dini inavyo sema bali yeye YESU.

MUNGU anakupenda na hapendi uangamizwe kwa moto wa milele katika hukumu yake kwa kuwa moto huo ameandaliwa kwa ajili ya shetani na wajumbe wake, lakini mpango wa kukuokoa na moto huo ni kupitia YESUKRISTO pekee.

Naye YESU hachangamani na ibada za sanamu.Njia pekee ni kujitenga na michanganyiko ya huduma zenye misanamu na kujiunga na huduma zenye kuhubiri kweli ya YESU naye HATAKUACHA KAMWE ATAKUOKOA.

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...