menuz

MBINGUNI, KUZIMU NA HALI YA SASA YA KANISA ----Mtumishi Rodolfo Acevedo Hernandez


Mimi ni mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez.Koo langu limeathirika sasa kwa kushuhudia huu ushuhuda, lakini nitaendelea kushuhudia na kushuhudia hata kama kunaupinzani.Utukufu kwa MUNGU !,Nakwenda kutoa ushuhuda utaobadili maisha yako na maelfu kwa mamilioni ya watu wengine.

Ufunuo 1:14-15 -“14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
 15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.”

Kwa sababu sikupenda kuendelea kukaa katika hali ile ile ya kiroho nilipenda nikuwe zaidi kiroho,Ndipo nilipoamua kujifungia mwenyewe kanisani kwa siku nane.Siku nane za kufunga na kuomba, 
Kwanza hata kabla ya kuanza kufunga Bwana YESU aliniambia kupitia kwenye maono kuwa “Rodolfo, ni muda wa kujitenga mwenyewe kwa ajili yangu,” Na katika maono hayo nilipewa vazi jeupe lililo andikwa “Utakatifu mbele ya YEHOVA”.

Baada ya maono hayo dada mmoja kutoka kanisani kwetu ambaye alikuwa ni mmishionari alikutana name na kuniambia, “Rodolfo, nimekuota na katika ndoto hiyo Bwana ameniambia nikwambie ujitenge na madhabahu(kwa kuwa ulikuwa muhubiri); Bwana atakwenda kukuonyesha vitu vikubwa vitavyobadili maisha ya watu katika mataifa na dunia nzima.”
Nami nikaacha kuhubiri kwa huo muda na kuanza kujitiisha kumtafuta BWANA  kwa kuanza mfungo wa siku nane.Na ilipofika siku ya nne ya kufunga na kuomba, nilipokuwa nikiomba ghafla wakajitokeza mapepo wawili na nikawaona uso kwa uso.Mapepo haya yaliniambia “Rodolfo, hatutakuruhusu kuvuka mipaka yetu”;

Na wakapotea ghafla ,nami nikawa na hofu kubwa kutokana na jinsi nilivyowaona mapepo wale walivyotisha nao walikuwa warefu na wenye harufu mbaya ya kama sulfur kama vile wametoka moja kwa moja kutoka kuzimu.Walitumwa kunieleza kuwa hawataweza kuniruhusu kupita mipaka yao.shetani ndiye pekee mwenye kuzuia vitu,lakini YESUKRISTO alimshinda pale msalabani kalivari.Utukufu kwa MUNGU haleluya.

Nilipofika siku saba za kufunga na kuomba nilijikuta naishiwa nguvu sana nikamwambia Bwana YESU “Bwana, siwezi zaidi,mwili wangu u dhaifu sina nguvu.Bwana tafadhali nisaidie siwezi kutimiza makubaliano.Nisamehe mimi na unipe nguvu.”Ghafla, nilisikia kitu kimetoka nyuma yangu nakunisogelea mpaka kwenye sikio ikiniambia; “Rodolfo, usiache mfungo huu mpaka tutakapokuonyesha vitu unavyotakiwa kuviona”.Nilipata nguvu na kutiwa moyo kwa  sauti kwa sauti niliyoisikia.

Siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni jumapili, nilikuwa najisikia dhaifu sana asubuhi.Jioni kipindi ibada inaendelea ,kulikuwa na neno lenye nguvu sana lilohubiriwa na mwinjilisti Ruben Bells.Ibada ilipoisha niliwasalimu kaka na ada zangu.

Papo hapo nikaanza kujisikia hewa inaniishia.Nilijisikia kuishiwa pumzi na sikuwa naweza kupumua.Watu katika kanisa wakaja kunizunguka na wakaanza kuniombea.Ghafla, nilijihisi kama vile kuna sindano nyingi ninazo chomwa nazo kwenye vidole na kucha zangu.

Kuna baridi ya hali ilikuwa inaingia mwili mzima kupitia yale maumivu ambayo yalikuwa kama vile mtu ananichoma sindano na nikajisikia nakata pumzi na moyo wangu ukashindwa.
Nilidondoka kwenye sakafu na watu wakazidi kuniombea, kulikuwa na wakaka kama kumi na wawili (12) hivi.Ghafla roho yangu ikauacha mwili nanikaona kabisa ninavyouacha mwili ukiwa umelala chini.Wallioko pale hawakulijua hilo na nini kinachoendelea, nilimuona dada mmoja ambaye ni muuguzi aliwaambia wengine “Atakuwa ana tatizo la shambulizi la moyo”.Nilitaka kuwasiliana nao ,kuwaeleza kinachoendelea hata kuendea mwili wangu yote hayo nilishindwa.

Bibilia imeweka wazi kuwa mwili wa mtu una roho,nafsi na mwili wenyewe.nafsi hurudi kwa MUNGU na roho huenda sehemu iliyoandaliwa ampbapo ni mbinguni au ni kuzimu.Bibilia imeweka wazi kuwa  mwili unarudi mavumbini kwa kuwa ulitoka mavumbini.

Ghafla nikaona kama taa zimezimwa na nikaanza kupaa kwenda juu kwa kasi isiyokuwa ya kawaida.Hata hivyo kuna vitu viliingilia ile safari ikawa kama nikaanza  kurudi chini ka kasi zaidi na zaidi nilivyozidi kwenda chini nikaanza kuhisia joto kali lisilo la kawaida.

Ilikuwa kuzimu na ilikuwa ikitisha sana na hapo nilikuwa ndio naingia na nikaona joka mkubwa ambaye kichwa chake kina nyembe nyembe badala ya magamba nikaendelea mbele nikakuta kuna jela.Kipindi naingia niliona macho ya kila aina yapo kwenye ukuta yakiniangalia.Ghafla, nikaona macho mawili yakitoka kwenye ukuta na kumbe ni pepo alikuwa anashani kwenye kifua iliyosomeka Mimi ni Kisasi”.

Muda huo mapepo wengi wakaanza kunijia kutokea kwenye ule ukuta.Pepo lililoandikwa Kisasi alisema kwa sauti “Mfalme Beelzebub, tunaye mmoja wa wakubwa aliekuwa akifanya vita kinyume nasi, ufalme wa giza..” Bibilia imeandikwa,  “21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.”-2 petro 2:21.Kanisa linalomjua Bwana linapaswa kuendelea kuwa imara kwa kutambua YESUKRISTO ndiye tumaini pekee kwa ajili ya wokovu wa roho zetu.

Nilipokuwa pale ,Yule pepo aitwaye Kisasi alikuja karibu yangu na kuniambia, “Rodolfo,nataka unifukuze hapa kama mnavyowafukuza na kukemea mapepo ukiwa duniani”. Alipokuwa akisema ilijirudia rudia, ndipo akaanza kunipiga na kunitesa nikaona mapepo yapo kwenye msururu yakinifuata iliyaanze kunitesa.

Mateso yaliyopo kuzimu kwa wachungaji,wahubiri,wainjilisti….walioacha kutegemea nguvu ya MUNGU ni makubwa kuliko wengine.Hivyo kuwa imara unapotembea na Bwana,Huu ni muda wa kanisa kuwa imara.Muda ni sasa.Muda wa kanisa kucheza umefika mwisho.Tunatakiwa tuwe na ujasiri na ushujaa wa kushinda nguvu zote za kuzimukatika jina la YESUKRISTO,Yeye pekee ndiye nuru.

Yule pepo alinirushia mkuki mrefu ulioingia mpaka moyoni mwangu,Nilipatwa na maumivu makali sana yasiweza kuelezeka,Nilihisi kama mvua ya kemikali kali ipo kuzimu.Nilijisikia mwili wangu ukidondoka kutoka kwenye mifupa yangu na wadudu wakali wakitoboa mifupa yangu.

Bibilia imeandikwa “48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.”-Marko 9:48, Zaidi katika Isaya imeandikwa “11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.”-Isaya 14:11.Kuzimu ni kweli na YESUKRISTO hata agano la kale linaongelea kuzimu.

Mara nikaona kundi la mapepo wamebeba silaha, lakini zilikuwa za tofauti sana na za hapa duniani.Pepo anayeitwa Kisasi aliitoa sehemu ya chini ya mdomo wangu na akaniambia “Rodolfo,nataka sasa unikemee!,haya nguvu yako iko wapi?,Uko wapi utukufu uliokuwa nao?”
Ujumbe ninaotaka kuutoa ni huu kwa kuwa muda mwingine kwa sababu tunahubiri,na tunafikiri kuwa upako ni wetu na nguvu ya MUNGU ya kuponya,kutoa pepo ni yetu.

Bibilia inasema utukufu  watoka kwa MUNGU na huo utukufu ni wake MUNGU pekee.Kwa sababu ifananayo kuwa shetani alitupwa kutoka mbinguni kwa sababu alitaka kujitwalia utukufu wa MUNGU uwe wake.Kwa hiyo watu wengi huamini kuwa wagonjwa wanapona sababu wanaweza kutumiwa na MUNGU kuponya wagonjwa,au kufungua waliofungwa na mapepo.
Nataka nikambie kuwa hizo ni vipawa ambavyo MUNGU ametoa kwa huruma yake kwa lengo la kufungua roho zilizofungwa na kuwa huru.

Ghafla nikaona mapepo yakijificha kwa haraka na nilikuwa chini na kitu cha kwanza nilichokiona sitasahau.. ohh! utukufu kwa MUNGU!,Niliona mwanga mkuu….haleluya,niliona makovu kwenye miguu yake.

Nilimuona huyu mtu alikuwa mzuri na mkanda kwenye kiuno imeandikwa, “MFALME WA WAFALME ,na BWANA WA MABWANA,”Alikuwa na taji kubwa la dhahabu,akanyoosha mikono yake kwangu na akasema “Rodolfo,NINAITWA YESU na MIMI nitaenda kukuonyesha wewe vitu vingi huku kuzimu, mbinguni na hali ya kanisa duniani.” Alinishika mkono wangu na kuniambia “Twende sasa, Rodolfo.”

MAKAHABA NA MALAYA
Niliona sehemu kubwa ambapo alikuwepo mwanamke.YESUKRISTO akasema, “Ninakwenda kukuonyesha adhabu anbayo shetani hutoa kwa wale ambao walikuwa malaya walipokuwa duniani,Wanapokufa malaya ndipo huja katika hii sehemu .Chunguza , Rodolfo.”

Nikaangalia nikaona akiwa amefungwa, na yuleyule joka niliyemuona mwanzo.Nimuona yule joka anamuingiliasehemu za siri za mwanamke Yule;napia ukumbuke nilikwambia ngozi ya joka hili ilikuwa ina viwembe na sio magamba.Yule joka alivyokuwa akimwingilia mwanamke ,anaharibu viungo vya ndani.Yule Joka anamwingilia kwenye sehemu za siri na kwenda kutokea kwenye mdomo.

Pepo anayeongoza ukahaba na umalaya duniani anaitwa, “Metresa au Martha”,au “Domineur”.Wengi wakatoliki wanaye huyu nao humuita mtakatifu kama mwanamke ambao mwili wake umezungushwa na joka na pepo hili nao ndio wahusika katika kutesa makahaba kuzimu.
WANAOTOA MIMBA
Bwana akaniambia ni muda wa kuhama hiyo sehemu na tukaacha Yule mwanamke akilia kutokana na mateso anayoyapata kwa uchungu. “Nahitaji mtu anisaidie mimi” Alilia sana kwa uchungu.Bwana YESU aliniambia, “Rodolfo, hukumu ilishatolewa kwao,Sasa Rodolfo, sasa nakwenda kukuonyesha sehemu ambayo shetani hutesa wanawake waliokuwa wametoa mimba(ujauzito)huku duniani.

Mara nikamuona mwanamke yuko katika hali ya kuzaa na nikaona lipepo lenye kutisha ambaye mikono na miguu yake ipo kama ya punda na kulikuwa na funza wakubwa wenye pembe kali na wenye meno makali waliokuwa wakimtoboa sehemu za siri za mwanamke yule.
Mwanamke anatobolewa kwa mateso makali mpaka mwanamke anaonekana kama vile mjamzito,Ndipo mapepo yanamwambia kwa sauti “zaa sasa huyu kwa kuwa ulikataa kuzaa ulipokuwa duniani ,mapepo huzidi kusema sifu, sifu shetani huu ndio ufalme wako! ”.

Nilipomuuliza Bwana kwa nini mateso ni makubwa sana kwa mwanamke huyu,Bwana YESU akanijibu, “Rodolfo, hukumu ilishawekwa kwa huyu mwanamke !”.Bibilia inasema wauaji hawataingia ufalme wa Mbinguni.Watu wanaotoa watoto au wanaoua wakiamini wanafanya hivyo kama vile kuua mnyama, lakini wanachofanya wanaua binaadamu mwenye nafsi,roho na mwili.

Shetani aliendelea kupiga makelele kwa yule mwanamke akimwambia msifu shetani kwa sababu ni ulikuwa ni ufame wako.Hao funza walikuwa wakitoka kwenye tumbo la yule mwanamke wakiwa wameharibu kila sehemu ya ndani ya yule mwanamke na walikuwa wakitoka na vipande vya nyama nyama midomoni mwao.

SIRI YA KATUNI NA GAME ZITOKAZO KUZIMU
Unaweza hisia ni maumivu na mateso kiasi gani aliyokuwa anayapitia.Bwana akaniambia, “Tutoke kwenye hii sehemu”.

Tukaenda kufika sehemu ambako kuna vitu vyeusi, ndipo nikaona watoto wengi hapo kuzimu.Nikamuuliza Bwana YESU, Kwa nini kuna watoto huku kuzimu ?” Lakini Bwana akaniambia hawakuwa watoto, kwa kuwa ufalme wa Mbinguni kwa watoto ni wao na mtu anazaliwa tena ili kuingia katika ufalme wa mbinguni.Nikamuuliza “Bwana, sasa vipi kuhusu hawa watoto ?”,

Bwana YESU akanijibu tena “Rodolfo, hawa si watoto”, Lakini aliniambia sikiliza amri ambazo shetani anawapa.Nilipowaangalia kwa umakini na wao walipogeuka nyuma nikagundua kuwa hawakuwa watoto lakini ni mapepo nao walikuwa wakicheza gemu(game) linaloitwa Nintendo.

Nikaanza kuona kila aina ya programu za kishetani na gemu zikitoa ishara za kishetani kutoka katika mikono yao.
shetani akiwaamuru mapepo hayo akisema “Watoto wangu,nendeni mkaibe,mkaue na kuharibu.”Alikuwa sahihi kwa sababu bibilia inasema shetani amekuja ili kuua,kuiba na kuharibu, lakini YESUKRISTO amekuja ili kuleta uzima tena uzima tele( yohana 10:10).

Nikaona hao mapepo wadogo wameingia duniani na Bwana akaniambia ndiyo maana watoto wa sasa duniani wanajiua wao wenyewe hata wanasaikolojia hawaelewi kwa nini kinatokea hivyo.Miezi michache iliyopita , ilitokea tukio la mtoto wa miaka kumi na miwili(12) aliyemuua mama yake kwa kisu,na mwingine akajinyonga yeye mwenyewe,na Marekani ,mtoto wa kiume wa miaka saba(7) aliyemuua mama yake, mdogo wake wa kiume na akajiua hata yeye mwenyewe na bastola aliyekutwa nayo.

Mtoto mwingine alijirusha kutoka kwenye gorofa ya pili na kujiua mwenyewe.Ujumbe na barua zilizoachwa na watoto hawa zote huazungumzia kuwa maisha hayana maana wala thamani yoyote.Haya yote yanatokea hawa mapepo yamewaingilia miili yao na kuwa ongoza kujiua na mauaji yeyote mabaya.

Baba na mama ,wazazi na walezi wote nawaambia muwe makini na watoto wako na kile wanachokiangalia kwenye luninga.Wanachokitazama kwenye mtandao,wanachokisikiliza kwenye redio.Mapepo sasa wanawaingia kupitia luninga,muziki na komedi za kishetani.Utukufu kwa MUNGU,Haleluya, Kwa kutuamsha na kutujuza ukweli huu.

Bwana YESU aliniambia kuwa hiyo ndio sababu ndoa nyingi zimeharibiwa kwa sababu baadhi ya wazazi huwalaumu watoto nao hufikiri wao ndio  haswa kigezo cha kutalakiana, Lakini watoto si tatizo bali tatizo ni mashambulizi ya nguvu za giza zilizo kinyume na ndoa na familia kiujumla.Mwite YESU ita kanisa tuombe tuweze kuwa na nyumba huru,huru kabisa.
WAABUDU SANAMU
Tulipotoka katika hiyo sehemu tukaenda sehemu ingine nikamuona mwanamke amezingirwa na moto mkali , huyu mwanamke alikuwa akilia sana huku akisema ‘nife !,nife!,nife! Nitoe hapa’ Nilimuona huyu mwanamke akiwa na picha mkononi mwake “Picha ya Moyo mtakatifu wa kutisha wa yesu wao kutokana na tamaduni za wakatoliki(waroma),”. Bwana , huyu mwanamke ni nani ?,Bwana akaniambia “Rodolfo,huyu mwanamke ni bibi yako”.
Bibilia inasema waabudu sanamu hawataingia mbinguni.BwanaYESU akanionyesha maisha ya bibi yangu alipokuwa duniani na nikaona jinsi alivyokuwa muabudu sanamu.

Niamuomba Bwana “tafadhali naomba umsaidie”.Bwana YESU alinijibu, “Rodolfo,siwezi kufanya chochote kwa huyu ,Hukumu ilishatolewa kwake”Bwana akaniambia, “Nitakwenda kukuonyesha wewe kitachokufanya wewe upitie mateso duniani.Wengi hawataamini kile unachokwenda kukiona, lakini usihofu nitakuwa pamoja nawe.”
CELIA CRUZ YUPO KUZIMU
Ghafla nikamuona mwanamke akiwa na miguu yake ikiwa imesagwa sagwa na visu vilivyo fikia hata magotini na muda huo huo mapepo mengi yalikuwa yakiendelea kumtesa, Nilipomuangalia nikagundua kuwa alikuwa ni Celia Cruz!.Bwana YESU alinionyesha mkanda wa Celia Cruz akifanya makubaliano ya kishetani akiwa na damu alipokuwa Hollywood ,

Nilimuona akifanya vitu vingi sana vya kishetani.BWANA YESU aliniambia, “alikuwa amejiunga kwenye ushetani na kuabudu shetani.Alikuwa mchawi mwenye kutumia damu ,ili afanye miziki yake  ifahamike sana(kuwa maarufu) na kufanikiwa.Yeye pamoja na kundi lake”.

Bwana YESU alinisikilizisha nyimbo yake moja iliyokuwa ikiitwa “Yemaya”,Nyimbo ambayo ni maarufu sana ingawa imeimbwa kiihispania.Unapoimba nyimbo hiyo na kurudia rudia kutaja “Yemaya”,Bwana YESU alinifahamisha kuwa maanayake ni “mfalme shetani, njoo na unimiliki mimi” na Bwana YESU akaniambia, “hukumu ishatolewa kwa Celia Cruz.”

Duniani:Celia Cruz alikuwa ni mkyuba wa kiamerika na alikuwa mmoja ya waliofahamika na kufanikiwa sana kama muimbaji wa muziki aina ya salsa kwa karne ya 20,akiwa na tuzo 23 za ushindi wa album za dhahabu.Naye alijulikana kimataifa kuwa ndiye “malikia wa salsa” pia alifahamika kama “la guarachera de cuba”.

Muanzilishi wa Mashaidi wa YEHOVA, (Charles T Russell) YUPO Kuzimu.
Tuliendelea kutembea na Bwana YESU naye akanionyesha mtu ambaye mikono yake ilinyooshwa chakushangaza mtu huyu alikuwa na upanga mzuri katika ulimi wake na huu upanga umepitiliza mpaka kichwani pake na kutokea nje ya mwili wake.

Miguu yake ilifungwa na nyororo na mgongoni mwake kulikuwa kumejaa nyembe zimewekwa kila namna kiasi kwamba hata ajisosogeze kwa namna gani lazima akatwe.Nilipo ona yule mtu yupo katika hali ile ya mateso makali sana,

Nikamwambia Bwana YESU, “Bwana, tafadhali msaidie,mfanyie chochote Bwana YESU,Angalia maumivu makali anayoyapata mtu huyu”.Bwana akaniuliza mimi “Je wamjua mtu huyu?,” Nami nikamjibu “hapana simjui mtu huyu,Ila nimeona visu vingi katika ngozi yake na hata katika mifupa yake na jinsi ilivyojia hadi nje ya mwili wake na jinsi anavyo piga kelele kwa maumivu makali anayo yapata”.

Bwana YESU akaniambia “Hukumu ishatolewa kwa mtu huyu, Sasa nitakwenda kukufahamisha huyu ni nani.” Kwasababu ya ufunuo huu,Bwana aliniambia “Utakimbia mji mpaka mji kwa sababu haya yatakuletea mateso makubwa lakini nitakuwa nawe.”Akaendelea kusema “Rodolfo, huyu mtu anaitwa Charles T. Russell,huyu ndiye muanzilishi wa madhehhebu ya Mashahidi wa Yehova”.

Nikamwambia “Bwana YESU tafadhali naomba umsaidie” naye Bwana akaniambia “Hapana, Rodolfo”.Bwana YESU akaunyosha mkono wake,mara nikaona roho nyingi za watu zinazo anguka chini kuzimu kwa kila njia inayowezekana:walikuwa wakiangukakichwa kwanza,miguu kwanza,tumbo kwanza na n.k.

Bwana akaniambia “Rodolfo, kwa ajili ya huyu mtu aliyelaaniwa roho nyingi za watu zinaenda kuzimu.Huyu mtu anafundisha kuwa MUNGU ni tuu MUNGU wa upendo.Bibilia inasema MUNGU ni moto ulao.Huyu mtu Charles Russell ametoa neno ‘kuzimu’ kutoka kwenye bibilia neno ‘sheol’ na ‘Abadon’.

Pia wanakata uungu wa YESUKRISTO na kukataa uungu wa Roho Mtakatifu nao wameweka neno pekee Yehova katika bibilia.
Ameondoa YESU na Roho mtakatifu.Kwa ajili ya huyu mtu aliyelaaniwa roho zote hizi zina anguka na kwenda kuzimu” (ufunuo wa yohana 22:18-19).Ndipo Bwana alisema: “namlaani mtu huyu”.

Tafadhali sana ‘Mashahidi wa Yehova’ nisikilizeni sitataka kuwafanya mjisikie vibaya au kuwaumiza ninyi.Ondoka upesi na mje kwake YESU.Sikuchukii na sichukii dini yako, lakini mpo katika uongo mkubwa sana,sasa mje kwa YESU.YESUKRISTO anawasubiri kwa mikono iliyofunguka kwa wote wataobadilika.Charles Russell yupo kuzimu kwa sababu ya kuanzisha na kufundisha uongo.Msifuate uongo.

Tulipotoka pale na milago ya gereza lile ikajifunga na motomkali ukaendelea kuunguzana ye Charles Russell akalia kwa uchungu sana na kumlaani YESUKRISTO nakurudia rudia kwa sababu YESU alisema “Hukumu ishatolewa kwa mtu huyu”.

Bwana YESU akaniambia  “Rodolfo, sasa ninakwenda kukuonyesha jela nyeusi ambazo zipo huku kuzimu.Jela ambazo zinamateso zaidi,” Nami nikamwambia Bwana YESU “Hapana Bwana ,tafadhali sana Bwana !,nimeshaona vingi vya kutisha nitoe hapa Bwana”.Bwana YESU akaniambia, “Sawa,Rodolfo, sitafanya chochote usichoniruhusu mimi.Ninakwenda kukuonyesha mbinguni sasa”.

MBINGUNI
Tuliondoka kwa kasi sana natulipo kwenda kusimama tukakutana na malaika wazuri wawili katika lango walikuwa wakubwa sana.Hao malaika wawili waliniambia mimi “Rodolfo, na hizi nguo zako za dhambi huwezi ingia katika ualme wa MUNGU.” Ndipo wakanipa mimi mavazi mapya nahayo yaliandikwa UTAKATIFU.

Wachungaji, Wainjilisti, Wahubiri, Wamishioni; Tafadhali sikia hili,MUNGU hajakuita ili uhubiri wingi wa utajiri au unabii kuhusu hayo.MUNGU amekuita ili uhubiri utakatifu na utakaso, sababu bila ya utakatifu hauwezi kumuona Bwana.Chukua neno na ulisambaze neno la utakatifu na ulihubiri kwa watu wote.

Ndipo hao malaika wakaniruhusu baada ya kunipa mavazi ya utakatifu na wakaniambia YESU anakusubiri ,YESU akaniambia “Rodolfo mtoto wangu, karibu kwenye Ufalme wa MUNGU wako”.Nilipoanza kutembea kwenye mitaa niliona mitaa yenye dhahabu halisi na nikaona mto kama kioo  nan i maji haswaa.Pia nikaona mapambo ya almasi kwenye mitaa,kitu ambacho watu wanauana duniani ili kupata almasi hiso nawakati mbinguni zimejaa tele.

Bwana akanishika mkono na kuniambia “nakwenda kukuonyesha hekalu”  napo palikuwa pazuri nikaona bilauri za dhahabu,vyombo vya dhahabu na nikasikia sauti nzuri nao walikuwa watoto waliokuwa wakiimba vizuri sana.Bwana akaniambia kwamba hao watoto ni wale waliokataliwa duniani lakini wakaufikia ufalme wa MUNGU.Utukufu kwa MUNGU, haleluya !

Tukaendelea tukitembea  nikaona vazi kubwa sana na zuri sana jeupe lililopambwa na dhahabu na taji juu yake na Bwana akaniambia hiyo ni kanisa lake,Kwamba linatakiwa kuwa takatifu nakusafika.Taji ni taji ya uzima ambayo Bwana atakwenda kulipa kanisa.Tukaendelea na nikaona mstari mkubwa wa watu nao walikuwa wamevaa mavazi meupe, nikawaona malaika wakubwa wawili kwa kuangalia kwenye macho yao nikaona amani,upendo usiokuwa wakawaida.

Malaika mmoja akaniambia “Karibu kwenye ufalme wa MUNGU”.Nikawaona watu wenye furaha sana na hapo nikakumbuka kile alichokisoma katika neno la MUNGU(bibilia) kuwa shida na tabu za dunia si kitu ukilinganisha na utukufu ambao Bwana MUNGU aliotuandalia mbinguni.

Bwana akanichukua na kunionyesha meza ndefu bila ya mwisho,meza ya dhahabu,bilauri,visu, umma, viti na vyombo vine vyote vya dhahabu.Nikaonyeshwa taji kubwa na ndogo naye Bwana akaniambia zile taji kubwa ni kwa ajili ya watumishi wake, Watakapo kuja kwenye karamu ya arusi ya Mwana kondoo.
Bwana akasema “Kwa sababu karamu ya arusi ya Mwana kondoo iikaribu kuanza.Ninakuja si muda kwa ajili ya kanisa  langu.Waambie nitakuja kunyakua kanisa”.

Nikamuuliza Bwana YESU “Haya mataji adogo ni kwa ajili ya akina nani ?,” Naye YESU akanijibu “Haya mataji madogo ni kwa ajili ya wale ambao wapo ndani ya kanisa ambao wameishi maisha matakatifu, lakini hawakufanya chochote kwenye Ufalme.Hata hivo nawaambia usiridhike na taji ndogo bali wewe fanya kazi ya Bwana kwa bidii ili naye Baba akupe thawabu kubwa”.Kilichonishangaza ni kwamba kila kiti kimeandikwa jina lake nyuma ya kiti hicho na hakuna yeyote anayeweza kukaa atika kiti hicho.
HALI YA SASA YA KANISA
Bwana YESU akaniambia “Rodolfo, ninakwenda kukuonyesha hali ya kanisa sasa hivi”.Nikaona samaki mdogo anamsifu na kumuabudu YESU kwa sababu Bibilia inasema:Wenye pumzi na wamsifu Bwana !

Ndipo Bwana akanionyesha dunia kuwa nikirudi duniani natakiwa nihubiri.Bwana alinipa uelewa kuwa yeyote anayeingia mbinguni husahau kila kitu kilichotokea duniani,Na huku wale walio kuzimu hukumbuka yote waliokuwa wakiyafanya duniani,familia zao, ndugu zao.
Kwa sababu hiyo sio petro sio maria sio Stefano sio Elisha wala yohana wanaweza kuwa nakumbukumbu ya jambo lolote walilolitenda au lililotokea duniani kwa kuwa ukiwa mbinguni unakuwa na ufahamu wa mbinguni na sio wakidunia.

Hivyo petro hawezi dhani hata siku moja kuwa wakatoliki wanamtukuza au mtakatifu yeyote yulei.YESU aliniambia , “Hakuna jina chini ya mbingu liwezalo kuokoa bali YESUKRISTO,mwana wa MUNGU anayeishi,”.Maria alipokuwa katika harusi kana aliwaambia kuwa “Neno lolote atakalowaambia YESUKRISTO hilo ndilo mlifanye”.

Watu wa kwanza wanao mwabudu shetani wapo VATICAN;  wao ndio wanaoficha kila njia za dhambi watendazo mapadri/makuhani kwa kulala na masista; makuhani kufanyisha ngono watoto wadogo(uzalilishaji watoto kijinsia) na hata katika jamuhuri ya Dominika,Nicolaus Lopez de Jesus Rodrigruez ni ushetani mwingine tena, naweza hata kukuhakishia hayo kupitia maandiko,Lakini bado Wakatoliki huendelea kuamini katika uongo wao wote huo.

Bwana YESU akaanza kulia sana alipoanza kunionyesha hali ya kanisa.Nilimuona mchungaji duniani amebeba begi kubwa lililojaa fedha.Bwana YESU akaniambia, “Hawa wahubiri na wainjilisti ambao wamekuwa matajiri kutokana na sadaka kwa sababu ya kuhubiri uongo kwawatu wangu na kusababisha watu wangu kupotea”.Nawaambia wahubiri na wainjilisti, muhubirini YESU hatakama hutapata mafungu ya kumi na sadaka.Takasa kanisa.
WATUMISHI WANAOPENDA FEDHA
Ghafla !,nikaona fedha zile zilizokuwa zimejaa begi zimeyeyuka na hazikuwepo tena.Nikamuuliza Bwana YESU maana yake naye akanijibu; “Vivyo hivyo kama fedha zilivyoyeyuka ,ndivyo navyo wao watakavyo yeyuka na kuondoka na mpinga Kristo.Lakini bado nina masalia ya watu wangu ambao ni waaminifu na hawajaharibiwa na chochote.”

Naona siku hizi jinsi watumishi,manabii,wahubiri,wainjilisti,mitume,wachungaji walivyo matajiri na mamilionea.Ingawa waumini katika makanisa yao wako kwenye umasikini, ni wahitaji wa chakula na huku mchungaji yupo katika utajiri mkubwa pasipo kuwasaidia waumini wao.Ni wainjilisti wengi sana ambao ni mamilionea hata hivyo ni mabilionea wakiwa kwenye magari ya kifahari sana.

Usamaria mwema uko wapi ?,Na nikaona wachungaji wengi wakihudumu kwenye madhabahu hata nikamuona mchungaji mmoja ambaye alipomaliza kuhudumu siku hiyo hiyo akaiacha familia yake nyumbani ambako mke wake alikuwepo na akaelekea kulala na mwanamke mwingine ambaye ni muumini wa kanisa hilo pia!.

VIJANA WASIO WAAMINIFU KWA MUNGU
Baada ya hayo Bwana YESU alinionyesha kundi la vijana katika kanisa ambao wakitoka makanisani huenda katika siri kwa kuwa hudhani Bwana YESU hawaoni na wanapofika huko huanza kujichua(punyeto) na kufanya uzinzi kwa kutumia miili yao wenyewe,Na baada ya hayo huenda kusimama ili kuhudumu madhabahuni !,raisi wa vijana,kiongozi wa kanisa!.

MAKANISA YALIOJAA NYIMBO ZA KIDUNIA
Bwana YESU alinionyesha disco na kanisa naye Bwana akaniambia nichunguze kwa makini,na nilipochunguza nikaona kanisa kama disco na hakukuwa na tofauti.Kulikuwa kuna aina ya muziki kama muziki wa disko,mpangilio wa kufanana,vifaa vya kufanana,vilivyotoka katika dunia na kuingia kanisani.
Dunia inabidibadilike kuufuata ukristo na sio vyovyote vile.
Sasa tumeileta dunia ndani ya kanisa!,Na pia ninapaswa niwaambie ukweli kuwa huwezi msifu aukumuabudu MUNGU na aina ya muziki wa rege,bachaton au rock.

Na hata sasa kuna nyimbo za kikristo zinazoimbwa kwa MUNGU na kwa dunia,wakitumia maneno yale yale !, Hawataji neno MUNGU lakini wanatumia tuu neno ‘upendo’.
Na pia nimeona muziki wa RAP na PERREO ikiimbwa na imo ndani ya kanisa na hiyo haikubaliki.Bibilia inatueleza tumuabudu MUNGU kwa uzuri wa utakatifu.Sasa ni nani alieanzisha muziki aina ya ROCK ?,Naye ni Anton Lavey,naye huyo ndiye muanzilishi wa kanisa la shetani.

Ametengeneza na kuandika bibilia ya kishetani na ndiye aliyeingiza muziki wa rock ndani ya Hollywood.Kama aligundua Rock, hiyoinamaanisha ni kwa ajili ya kumtukuza shetani na sio MUNGU.Kwa maneno mengine kile anachopewa shetani nasi twataka kumpa hicho hicho MUNGU? !,Hicho hakiwezekani na hakikubaliki kwa MUNGU.Rock ni miziki ya kishetani na imegunduliwa kuzimu.

Anton szandor LaVey,born Howard Stanton Levey, naye alikuwa ni muanzilishi wa kanisa la shetani pia ni muandishi,mwanachamahuru na mwanamuziki.
Wachungaji na wainjilisti , tafadhali tokeni kwenye hiyo miziki iliyo laaniwa na itoeni kanisani.Rap iligunduliwa na mtu aitwaye Selassie.Huyu ni nani ?,Huyu ni mtu aliye jiita mwenyewe kuwa yeye ni “Mfalme wa wafalme na Bwana wa bwana”.Na kanisa linatumia aina hiyo ya miziki na huku bibilia imeandikwa kuwa pekee aliye Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme ni YESUKRISTO,Mwana wa MUNGU anaye ishi.

WAIMBAJI WA INJILI WALIOPOTOKA
Bwana alinionyesha wanamziki waliokuwa wameacha sana njia yake(Bwana).Walikuwa wakiimba kanisani kwa mkono mmoja na wakiwa wanatengeneza tenda ingine  kuimba katika migahawa kama waimbaji binafsi:  wanamsifu Bwana kanisani!, nataka niwaambie kuwa muziki na uimbaji wa namna hiyo Bwana hautaki na pia unisamehe kwa kukwambia ukweli.

Kipi ni cha Bwana ni kile ambacho ni kitakatifu nan i kile kilichotengwa tuu kwa ajili ya Bwana pekee.Na hawa waimbaji wanaimba kanisani na baada ya kuimba huondoka hatakama ni katikati ya ibada,Kwa sababu inaonekana kana kwamba ni mchezo wa kutaka mkataba wa fedha kutokana na uimbaji wao, wanajihisi hawatakiwi kuwepo katika ibada nzima nao huondoka na kuishi maisha ya umaarufu.
Na katika wakati wote, Bwana akaniambia “Kwa bahati mbaya, aina ya kanisa hili halitaingia mbinguni.”
KANISA LILILO SAFI
Baada ya hayo Bwana akanionyesha  kundi la watu,maelfu kwa maelfu ya watu wanaojilinda wenyewe kwa utakatifu.Nikaona kwa mfano dada akimwambia mwingine; “Je umekula leo ?”,nina kipande cha mkate nyumbani kwangu.”
Nikamuona mwingine amebeba viatu vingi kwa mtu asiye navyo hata kimoja.Nikaona wengine wakiwapa nguvu wale wasio na nguvu.Wengine wanajua shida za wenzao na kuaanza kuzitatua, wakiwatunza na kuwaombea kwa ajili ya mahitaji yao bila yeyote kujua.
Lakini leo katika makanisa mengi kuna umbea mwingi kwa sababu hawajui namna ya kukaa kimya kuhusu mambo ya wengine.

Tubu; Leo YESUKRISTO anataka kukupa kukufungua na hata kukuokoa.Naye anaweza kukupa kipawa na neema ya kutubu.


No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!