Mimi ni mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez.Koo langu
limeathirika sasa kwa kushuhudia huu ushuhuda, lakini nitaendelea kushuhudia na
kushuhudia hata kama kunaupinzani.Utukufu kwa MUNGU !,Nakwenda kutoa ushuhuda
utaobadili maisha yako na maelfu kwa mamilioni ya watu wengine.
Ufunuo 1:14-15 -“14 Kichwa
chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho
yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa
sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji
mengi.”
Kwa
sababu sikupenda kuendelea kukaa katika hali ile ile ya kiroho nilipenda nikuwe
zaidi kiroho,Ndipo nilipoamua kujifungia mwenyewe kanisani kwa siku nane.Siku
nane za kufunga na kuomba,
Kwanza hata kabla ya kuanza kufunga Bwana YESU
aliniambia kupitia kwenye maono kuwa “Rodolfo, ni muda wa kujitenga mwenyewe kwa
ajili yangu,” Na katika maono hayo nilipewa vazi jeupe lililo andikwa “Utakatifu
mbele ya YEHOVA”.
Baada ya maono hayo dada mmoja kutoka kanisani kwetu
ambaye alikuwa ni mmishionari alikutana name na kuniambia, “Rodolfo, nimekuota na katika
ndoto hiyo Bwana ameniambia nikwambie ujitenge na madhabahu(kwa kuwa ulikuwa
muhubiri); Bwana atakwenda kukuonyesha vitu vikubwa vitavyobadili maisha ya
watu katika mataifa na dunia nzima.”
Nami
nikaacha kuhubiri kwa huo muda na kuanza kujitiisha kumtafuta BWANA kwa kuanza mfungo wa siku nane.Na ilipofika
siku ya nne ya kufunga na kuomba, nilipokuwa nikiomba ghafla wakajitokeza
mapepo wawili na nikawaona uso kwa uso.Mapepo haya yaliniambia “Rodolfo,
hatutakuruhusu kuvuka mipaka yetu”;
Na wakapotea ghafla ,nami nikawa na
hofu kubwa kutokana na jinsi nilivyowaona mapepo wale walivyotisha nao walikuwa
warefu na wenye harufu mbaya ya kama sulfur kama vile wametoka moja kwa moja
kutoka kuzimu.Walitumwa kunieleza kuwa hawataweza kuniruhusu kupita mipaka yao.shetani
ndiye pekee mwenye kuzuia vitu,lakini YESUKRISTO alimshinda pale msalabani
kalivari.Utukufu kwa MUNGU haleluya.
Nilipofika
siku saba za kufunga na kuomba nilijikuta naishiwa nguvu sana nikamwambia Bwana
YESU “Bwana,
siwezi zaidi,mwili wangu u dhaifu sina nguvu.Bwana tafadhali nisaidie siwezi
kutimiza makubaliano.Nisamehe mimi na unipe nguvu.”Ghafla, nilisikia
kitu kimetoka nyuma yangu nakunisogelea mpaka kwenye sikio ikiniambia; “Rodolfo,
usiache mfungo huu mpaka tutakapokuonyesha vitu unavyotakiwa kuviona”.Nilipata
nguvu na kutiwa moyo kwa sauti kwa sauti
niliyoisikia.
Siku
iliyofuata ambayo ilikuwa ni jumapili, nilikuwa najisikia dhaifu sana
asubuhi.Jioni kipindi ibada inaendelea ,kulikuwa na neno lenye nguvu sana
lilohubiriwa na mwinjilisti Ruben Bells.Ibada ilipoisha niliwasalimu kaka na
ada zangu.
Papo hapo
nikaanza kujisikia hewa inaniishia.Nilijisikia kuishiwa pumzi na sikuwa naweza
kupumua.Watu katika kanisa wakaja kunizunguka na wakaanza kuniombea.Ghafla,
nilijihisi kama vile kuna sindano nyingi ninazo chomwa nazo kwenye vidole na
kucha zangu.
Kuna baridi ya hali ilikuwa inaingia mwili mzima kupitia yale
maumivu ambayo yalikuwa kama vile mtu ananichoma sindano na nikajisikia nakata
pumzi na moyo wangu ukashindwa.
Nilidondoka
kwenye sakafu na watu wakazidi kuniombea, kulikuwa na wakaka kama kumi na
wawili (12) hivi.Ghafla roho yangu ikauacha mwili nanikaona kabisa ninavyouacha
mwili ukiwa umelala chini.Wallioko pale hawakulijua hilo na nini
kinachoendelea, nilimuona dada mmoja ambaye ni muuguzi aliwaambia wengine “Atakuwa
ana tatizo la shambulizi la moyo”.Nilitaka kuwasiliana nao ,kuwaeleza
kinachoendelea hata kuendea mwili wangu yote hayo nilishindwa.
Bibilia
imeweka wazi kuwa mwili wa mtu una roho,nafsi na mwili wenyewe.nafsi hurudi kwa
MUNGU na roho huenda sehemu iliyoandaliwa ampbapo ni mbinguni au ni
kuzimu.Bibilia imeweka wazi kuwa mwili
unarudi mavumbini kwa kuwa ulitoka mavumbini.
Ghafla nikaona kama taa zimezimwa na nikaanza kupaa kwenda
juu kwa kasi isiyokuwa ya kawaida.Hata hivyo kuna vitu viliingilia ile safari
ikawa kama nikaanza kurudi chini ka kasi
zaidi na zaidi nilivyozidi kwenda chini nikaanza kuhisia joto kali lisilo la
kawaida.
Ilikuwa kuzimu na ilikuwa ikitisha sana na hapo nilikuwa
ndio naingia na nikaona joka mkubwa ambaye kichwa chake kina nyembe nyembe
badala ya magamba nikaendelea mbele nikakuta kuna jela.Kipindi naingia niliona
macho ya kila aina yapo kwenye ukuta yakiniangalia.Ghafla, nikaona macho mawili
yakitoka kwenye ukuta na kumbe ni pepo alikuwa anashani kwenye kifua
iliyosomeka “Mimi ni Kisasi”.
Muda huo mapepo wengi wakaanza kunijia kutokea kwenye ule
ukuta.Pepo lililoandikwa Kisasi alisema
kwa sauti “Mfalme Beelzebub, tunaye mmoja
wa wakubwa aliekuwa akifanya vita kinyume nasi, ufalme wa giza..” Bibilia
imeandikwa, “21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko
kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.”-2 petro 2:21.Kanisa linalomjua Bwana linapaswa
kuendelea kuwa imara kwa kutambua YESUKRISTO ndiye tumaini pekee kwa ajili ya
wokovu wa roho zetu.
Nilipokuwa
pale ,Yule pepo aitwaye Kisasi alikuja karibu yangu na kuniambia, “Rodolfo,nataka
unifukuze hapa kama mnavyowafukuza na kukemea mapepo ukiwa duniani”.
Alipokuwa akisema ilijirudia rudia, ndipo akaanza kunipiga na kunitesa nikaona
mapepo yapo kwenye msururu yakinifuata iliyaanze kunitesa.
Mateso
yaliyopo kuzimu kwa wachungaji,wahubiri,wainjilisti….walioacha kutegemea nguvu
ya MUNGU ni makubwa kuliko wengine.Hivyo kuwa imara unapotembea na Bwana,Huu ni
muda wa kanisa kuwa imara.Muda ni sasa.Muda wa kanisa kucheza umefika
mwisho.Tunatakiwa tuwe na ujasiri na ushujaa wa kushinda nguvu zote za
kuzimukatika jina la YESUKRISTO,Yeye pekee ndiye nuru.
Yule pepo
alinirushia mkuki mrefu ulioingia mpaka moyoni mwangu,Nilipatwa na maumivu
makali sana yasiweza kuelezeka,Nilihisi kama mvua ya kemikali kali ipo
kuzimu.Nilijisikia mwili wangu ukidondoka kutoka kwenye mifupa yangu na wadudu
wakali wakitoboa mifupa yangu.
Bibilia
imeandikwa “48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.”-Marko 9:48, Zaidi
katika Isaya imeandikwa “11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na
sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.”-Isaya
14:11.Kuzimu ni kweli na YESUKRISTO hata agano la kale linaongelea
kuzimu.
Mara
nikaona kundi la mapepo wamebeba silaha, lakini zilikuwa za tofauti sana na za
hapa duniani.Pepo anayeitwa Kisasi aliitoa
sehemu ya chini ya mdomo wangu na akaniambia “Rodolfo,nataka sasa unikemee!,haya nguvu
yako iko wapi?,Uko wapi utukufu uliokuwa nao?”
Ujumbe
ninaotaka kuutoa ni huu kwa kuwa muda mwingine kwa sababu tunahubiri,na
tunafikiri kuwa upako ni wetu na nguvu ya MUNGU ya kuponya,kutoa pepo ni yetu.
Bibilia
inasema utukufu watoka kwa MUNGU na huo
utukufu ni wake MUNGU pekee.Kwa sababu ifananayo kuwa shetani alitupwa kutoka
mbinguni kwa sababu alitaka kujitwalia utukufu wa MUNGU uwe wake.Kwa hiyo watu
wengi huamini kuwa wagonjwa wanapona sababu wanaweza kutumiwa na MUNGU kuponya
wagonjwa,au kufungua waliofungwa na mapepo.
Nataka nikambie kuwa hizo ni vipawa
ambavyo MUNGU ametoa kwa huruma yake kwa lengo la kufungua roho zilizofungwa na
kuwa huru.
Ghafla
nikaona mapepo yakijificha kwa haraka na nilikuwa chini na kitu cha kwanza
nilichokiona sitasahau.. ohh! utukufu kwa MUNGU!,Niliona mwanga
mkuu….haleluya,niliona makovu kwenye miguu yake.
Nilimuona huyu mtu alikuwa
mzuri na mkanda kwenye kiuno imeandikwa, “MFALME
WA WAFALME ,na BWANA WA MABWANA,”Alikuwa
na taji kubwa la dhahabu,akanyoosha mikono yake kwangu na akasema “Rodolfo,NINAITWA
YESU na MIMI nitaenda kukuonyesha wewe vitu vingi huku kuzimu, mbinguni na hali
ya kanisa duniani.” Alinishika
mkono wangu na kuniambia “Twende sasa, Rodolfo.”
MAKAHABA
NA MALAYA
Niliona
sehemu kubwa ambapo alikuwepo mwanamke.YESUKRISTO akasema, “Ninakwenda kukuonyesha adhabu
anbayo shetani hutoa kwa wale ambao walikuwa malaya walipokuwa
duniani,Wanapokufa malaya ndipo huja katika hii sehemu .Chunguza , Rodolfo.”
Nikaangalia
nikaona akiwa amefungwa, na yuleyule joka niliyemuona mwanzo.Nimuona yule joka
anamuingiliasehemu za siri za mwanamke Yule;napia ukumbuke nilikwambia ngozi ya
joka hili ilikuwa ina viwembe na sio magamba.Yule joka alivyokuwa akimwingilia
mwanamke ,anaharibu viungo vya ndani.Yule Joka anamwingilia kwenye sehemu za
siri na kwenda kutokea kwenye mdomo.
Pepo
anayeongoza ukahaba na umalaya duniani anaitwa, “Metresa au Martha”,au
“Domineur”.Wengi wakatoliki wanaye huyu nao humuita mtakatifu kama mwanamke
ambao mwili wake umezungushwa na joka na pepo hili nao ndio wahusika katika
kutesa makahaba kuzimu.
WANAOTOA MIMBA
Bwana
akaniambia ni muda wa kuhama hiyo sehemu na tukaacha Yule mwanamke akilia
kutokana na mateso anayoyapata kwa uchungu.
“Nahitaji mtu anisaidie mimi” Alilia sana kwa uchungu.Bwana YESU aliniambia, “Rodolfo, hukumu ilishatolewa kwao,Sasa
Rodolfo, sasa nakwenda kukuonyesha sehemu ambayo shetani hutesa wanawake
waliokuwa wametoa mimba(ujauzito)huku duniani.
Mara nikamuona
mwanamke yuko katika hali ya kuzaa na nikaona lipepo lenye kutisha ambaye
mikono na miguu yake ipo kama ya punda na kulikuwa na funza wakubwa wenye pembe
kali na wenye meno makali waliokuwa wakimtoboa sehemu za siri za mwanamke yule.
Mwanamke
anatobolewa kwa mateso makali mpaka mwanamke anaonekana kama vile
mjamzito,Ndipo mapepo yanamwambia kwa sauti “zaa
sasa huyu kwa kuwa ulikataa kuzaa ulipokuwa duniani ,mapepo huzidi kusema sifu,
sifu shetani huu ndio ufalme wako! ”.
Nilipomuuliza Bwana kwa nini mateso ni
makubwa sana kwa mwanamke huyu,Bwana YESU akanijibu, “Rodolfo, hukumu ilishawekwa kwa
huyu mwanamke !”.Bibilia inasema wauaji hawataingia ufalme wa
Mbinguni.Watu wanaotoa watoto au wanaoua wakiamini wanafanya hivyo kama vile kuua
mnyama, lakini wanachofanya wanaua binaadamu mwenye nafsi,roho na mwili.
Shetani
aliendelea kupiga makelele kwa yule mwanamke akimwambia msifu shetani kwa
sababu ni ulikuwa ni ufame wako.Hao funza walikuwa wakitoka kwenye tumbo la
yule mwanamke wakiwa wameharibu kila sehemu ya ndani ya yule mwanamke na
walikuwa wakitoka na vipande vya nyama nyama midomoni mwao.
SIRI YA KATUNI NA GAME ZITOKAZO KUZIMU
Unaweza
hisia ni maumivu na mateso kiasi gani aliyokuwa anayapitia.Bwana akaniambia, “Tutoke
kwenye hii sehemu”.
Tukaenda kufika sehemu ambako kuna vitu vyeusi,
ndipo nikaona watoto wengi hapo kuzimu.Nikamuuliza Bwana YESU, “Kwa nini kuna watoto huku kuzimu ?” Lakini
Bwana akaniambia hawakuwa watoto, kwa kuwa ufalme wa Mbinguni kwa watoto ni wao
na mtu anazaliwa tena ili kuingia katika ufalme wa mbinguni.Nikamuuliza “Bwana, sasa vipi kuhusu hawa watoto ?”,
Bwana
YESU akanijibu tena “Rodolfo, hawa si watoto”, Lakini aliniambia sikiliza amri
ambazo shetani anawapa.Nilipowaangalia kwa umakini na wao walipogeuka nyuma
nikagundua kuwa hawakuwa watoto lakini ni mapepo nao walikuwa wakicheza
gemu(game) linaloitwa Nintendo.
Nikaanza kuona kila aina ya
programu za kishetani na gemu zikitoa ishara za kishetani kutoka katika mikono
yao.
shetani
akiwaamuru mapepo hayo akisema “Watoto
wangu,nendeni mkaibe,mkaue na kuharibu.”Alikuwa sahihi kwa sababu bibilia
inasema shetani amekuja ili kuua,kuiba na kuharibu, lakini YESUKRISTO amekuja
ili kuleta uzima tena uzima tele( yohana 10:10).
Nikaona
hao mapepo wadogo wameingia duniani na Bwana akaniambia ndiyo maana watoto wa
sasa duniani wanajiua wao wenyewe hata wanasaikolojia hawaelewi kwa nini
kinatokea hivyo.Miezi michache iliyopita , ilitokea tukio la mtoto wa miaka
kumi na miwili(12) aliyemuua mama yake kwa kisu,na mwingine akajinyonga yeye
mwenyewe,na Marekani ,mtoto wa kiume wa miaka saba(7) aliyemuua mama yake,
mdogo wake wa kiume na akajiua hata yeye mwenyewe na bastola aliyekutwa nayo.
Mtoto
mwingine alijirusha kutoka kwenye gorofa ya pili na kujiua mwenyewe.Ujumbe na
barua zilizoachwa na watoto hawa zote huazungumzia kuwa maisha hayana maana
wala thamani yoyote.Haya yote yanatokea hawa mapepo yamewaingilia miili yao na
kuwa ongoza kujiua na mauaji yeyote mabaya.
Baba na
mama ,wazazi na walezi wote nawaambia muwe makini na watoto wako na kile
wanachokiangalia kwenye luninga.Wanachokitazama kwenye
mtandao,wanachokisikiliza kwenye redio.Mapepo sasa wanawaingia kupitia
luninga,muziki na komedi za kishetani.Utukufu kwa MUNGU,Haleluya, Kwa kutuamsha
na kutujuza ukweli huu.
Bwana
YESU aliniambia kuwa hiyo ndio sababu ndoa nyingi zimeharibiwa kwa sababu
baadhi ya wazazi huwalaumu watoto nao hufikiri wao ndio haswa kigezo cha kutalakiana, Lakini watoto
si tatizo bali tatizo ni mashambulizi ya nguvu za giza zilizo kinyume na ndoa
na familia kiujumla.Mwite YESU ita kanisa tuombe tuweze kuwa na nyumba
huru,huru kabisa.
WAABUDU SANAMU
Tulipotoka
katika hiyo sehemu tukaenda sehemu ingine nikamuona mwanamke amezingirwa na
moto mkali , huyu mwanamke alikuwa akilia sana huku akisema ‘nife !,nife!,nife!
Nitoe hapa’ Nilimuona huyu mwanamke akiwa na picha mkononi mwake “Picha ya Moyo mtakatifu wa kutisha wa yesu wao
kutokana na tamaduni za wakatoliki(waroma),”. Bwana , huyu mwanamke ni nani ?,Bwana akaniambia “Rodolfo,huyu
mwanamke ni bibi yako”.
Bibilia inasema waabudu sanamu hawataingia
mbinguni.BwanaYESU akanionyesha maisha ya bibi yangu alipokuwa duniani na
nikaona jinsi alivyokuwa muabudu sanamu.
Niamuomba Bwana “tafadhali naomba umsaidie”.Bwana YESU alinijibu, “Rodolfo,siwezi
kufanya chochote kwa huyu ,Hukumu ilishatolewa kwake”Bwana akaniambia, “Nitakwenda
kukuonyesha wewe kitachokufanya wewe upitie mateso duniani.Wengi hawataamini
kile unachokwenda kukiona, lakini usihofu nitakuwa pamoja nawe.”
CELIA CRUZ YUPO KUZIMU
Ghafla nikamuona
mwanamke akiwa na miguu yake ikiwa imesagwa sagwa na visu vilivyo fikia hata
magotini na muda huo huo mapepo mengi yalikuwa yakiendelea kumtesa,
Nilipomuangalia nikagundua kuwa alikuwa ni Celia Cruz!.Bwana YESU alinionyesha
mkanda wa Celia Cruz akifanya makubaliano ya kishetani akiwa na damu alipokuwa Hollywood ,
Nilimuona
akifanya vitu vingi sana vya kishetani.BWANA YESU aliniambia, “alikuwa
amejiunga kwenye ushetani na kuabudu shetani.Alikuwa mchawi mwenye kutumia damu
,ili afanye miziki yake ifahamike sana(kuwa
maarufu) na kufanikiwa.Yeye pamoja na kundi lake”.
Bwana
YESU alinisikilizisha nyimbo yake moja iliyokuwa ikiitwa “Yemaya”,Nyimbo ambayo ni maarufu sana ingawa imeimbwa kiihispania.Unapoimba
nyimbo hiyo na kurudia rudia kutaja “Yemaya”,Bwana
YESU alinifahamisha kuwa maanayake ni “mfalme
shetani, njoo na unimiliki mimi” na
Bwana YESU akaniambia, “hukumu ishatolewa kwa Celia Cruz.”
Duniani:Celia
Cruz alikuwa ni mkyuba wa kiamerika na alikuwa mmoja ya waliofahamika na
kufanikiwa sana kama muimbaji wa muziki aina ya salsa kwa karne ya 20,akiwa na
tuzo 23 za ushindi wa album za dhahabu.Naye alijulikana kimataifa kuwa ndiye “malikia wa salsa” pia alifahamika
kama “la guarachera de cuba”.
Muanzilishi
wa Mashaidi wa YEHOVA, (Charles T Russell) YUPO Kuzimu.
Tuliendelea
kutembea na Bwana YESU naye akanionyesha mtu ambaye mikono yake ilinyooshwa
chakushangaza mtu huyu alikuwa na upanga mzuri katika ulimi wake na huu upanga
umepitiliza mpaka kichwani pake na kutokea nje ya mwili wake.
Miguu
yake ilifungwa na nyororo na mgongoni mwake kulikuwa kumejaa nyembe zimewekwa
kila namna kiasi kwamba hata ajisosogeze kwa namna gani lazima akatwe.Nilipo
ona yule mtu yupo katika hali ile ya mateso makali sana,
Nikamwambia
Bwana YESU, “Bwana, tafadhali msaidie,mfanyie
chochote Bwana YESU,Angalia maumivu makali anayoyapata mtu huyu”.Bwana
akaniuliza mimi “Je wamjua mtu huyu?,” Nami nikamjibu “hapana
simjui mtu huyu,Ila nimeona visu vingi katika ngozi yake na hata katika mifupa
yake na jinsi ilivyojia hadi nje ya mwili wake na jinsi anavyo piga kelele kwa
maumivu makali anayo yapata”.
Bwana
YESU akaniambia “Hukumu ishatolewa kwa mtu huyu, Sasa nitakwenda kukufahamisha huyu ni
nani.” Kwasababu ya ufunuo huu,Bwana aliniambia “Utakimbia mji mpaka mji kwa
sababu haya yatakuletea mateso makubwa lakini nitakuwa nawe.”Akaendelea
kusema “Rodolfo, huyu mtu anaitwa Charles T. Russell,huyu ndiye muanzilishi wa
madhehhebu ya Mashahidi wa Yehova”.
Nikamwambia
“Bwana YESU tafadhali naomba umsaidie” naye Bwana akaniambia “Hapana, Rodolfo”.Bwana
YESU akaunyosha mkono wake,mara nikaona roho nyingi za watu zinazo anguka chini
kuzimu kwa kila njia inayowezekana:walikuwa wakiangukakichwa kwanza,miguu
kwanza,tumbo kwanza na n.k.
Bwana
akaniambia “Rodolfo, kwa ajili ya huyu mtu aliyelaaniwa roho nyingi za watu
zinaenda kuzimu.Huyu mtu anafundisha kuwa MUNGU ni tuu MUNGU wa upendo.Bibilia
inasema MUNGU ni moto ulao.Huyu mtu Charles Russell ametoa neno ‘kuzimu’ kutoka
kwenye bibilia neno ‘sheol’ na ‘Abadon’.
Pia wanakata uungu wa YESUKRISTO na
kukataa uungu wa Roho Mtakatifu nao wameweka neno pekee Yehova katika bibilia.
Ameondoa YESU na Roho
mtakatifu.Kwa ajili ya huyu mtu aliyelaaniwa roho zote hizi zina anguka na
kwenda kuzimu” (ufunuo wa yohana 22:18-19).Ndipo Bwana
alisema: “namlaani mtu huyu”.
Tafadhali
sana ‘Mashahidi wa Yehova’ nisikilizeni sitataka kuwafanya mjisikie vibaya au
kuwaumiza ninyi.Ondoka upesi na mje kwake YESU.Sikuchukii na sichukii dini
yako, lakini mpo katika uongo mkubwa sana,sasa mje kwa YESU.YESUKRISTO anawasubiri
kwa mikono iliyofunguka kwa wote wataobadilika.Charles Russell yupo kuzimu kwa
sababu ya kuanzisha na kufundisha uongo.Msifuate uongo.
Tulipotoka
pale na milago ya gereza lile ikajifunga na motomkali ukaendelea kuunguzana ye
Charles Russell akalia kwa uchungu sana na kumlaani YESUKRISTO nakurudia rudia
kwa sababu YESU alisema “Hukumu ishatolewa kwa mtu huyu”.
Bwana
YESU akaniambia “Rodolfo, sasa ninakwenda
kukuonyesha jela nyeusi ambazo zipo huku kuzimu.Jela ambazo zinamateso zaidi,”
Nami nikamwambia Bwana YESU “Hapana Bwana
,tafadhali sana Bwana !,nimeshaona vingi vya kutisha nitoe hapa Bwana”.Bwana
YESU akaniambia, “Sawa,Rodolfo, sitafanya chochote usichoniruhusu mimi.Ninakwenda
kukuonyesha mbinguni sasa”.
MBINGUNI
Tuliondoka
kwa kasi sana natulipo kwenda kusimama tukakutana na malaika wazuri wawili
katika lango walikuwa wakubwa sana.Hao malaika wawili waliniambia mimi
“Rodolfo, na hizi nguo zako za dhambi huwezi ingia katika ualme wa MUNGU.”
Ndipo wakanipa mimi mavazi mapya nahayo yaliandikwa UTAKATIFU.
Wachungaji,
Wainjilisti, Wahubiri, Wamishioni; Tafadhali sikia hili,MUNGU hajakuita ili
uhubiri wingi wa utajiri au unabii kuhusu hayo.MUNGU amekuita ili uhubiri
utakatifu na utakaso, sababu bila ya utakatifu hauwezi kumuona Bwana.Chukua
neno na ulisambaze neno la utakatifu na ulihubiri kwa watu wote.
Ndipo hao
malaika wakaniruhusu baada ya kunipa mavazi ya utakatifu na wakaniambia YESU
anakusubiri ,YESU akaniambia “Rodolfo mtoto wangu, karibu kwenye Ufalme
wa MUNGU wako”.Nilipoanza kutembea kwenye mitaa niliona mitaa yenye
dhahabu halisi na nikaona mto kama kioo
nan i maji haswaa.Pia nikaona mapambo ya almasi kwenye mitaa,kitu
ambacho watu wanauana duniani ili kupata almasi hiso nawakati mbinguni zimejaa
tele.
Bwana
akanishika mkono na kuniambia “nakwenda kukuonyesha hekalu”
napo palikuwa pazuri nikaona
bilauri za dhahabu,vyombo vya dhahabu na nikasikia sauti nzuri nao walikuwa
watoto waliokuwa wakiimba vizuri sana.Bwana akaniambia kwamba hao watoto ni
wale waliokataliwa duniani lakini wakaufikia ufalme wa MUNGU.Utukufu kwa MUNGU,
haleluya !
Tukaendelea
tukitembea nikaona vazi kubwa sana na
zuri sana jeupe lililopambwa na dhahabu na taji juu yake na Bwana akaniambia
hiyo ni kanisa lake,Kwamba linatakiwa kuwa takatifu nakusafika.Taji ni taji ya
uzima ambayo Bwana atakwenda kulipa kanisa.Tukaendelea na nikaona mstari mkubwa
wa watu nao walikuwa wamevaa mavazi meupe, nikawaona malaika wakubwa wawili kwa
kuangalia kwenye macho yao nikaona amani,upendo usiokuwa wakawaida.
Malaika
mmoja akaniambia “Karibu kwenye ufalme wa MUNGU”.Nikawaona watu wenye furaha
sana na hapo nikakumbuka kile alichokisoma katika neno la MUNGU(bibilia) kuwa
shida na tabu za dunia si kitu ukilinganisha na utukufu ambao Bwana MUNGU
aliotuandalia mbinguni.
Bwana
akanichukua na kunionyesha meza ndefu bila ya mwisho,meza ya
dhahabu,bilauri,visu, umma, viti na vyombo vine vyote vya dhahabu.Nikaonyeshwa
taji kubwa na ndogo naye Bwana akaniambia zile taji kubwa ni kwa ajili ya
watumishi wake, Watakapo kuja kwenye karamu ya arusi ya Mwana kondoo.
Bwana
akasema “Kwa sababu karamu ya arusi ya Mwana kondoo iikaribu kuanza.Ninakuja si
muda kwa ajili ya kanisa langu.Waambie
nitakuja kunyakua kanisa”.
Nikamuuliza
Bwana YESU “Haya mataji adogo ni kwa
ajili ya akina nani ?,” Naye YESU akanijibu “Haya mataji madogo ni kwa ajili
ya wale ambao wapo ndani ya kanisa ambao wameishi maisha matakatifu, lakini
hawakufanya chochote kwenye Ufalme.Hata hivo nawaambia usiridhike na taji ndogo
bali wewe fanya kazi ya Bwana kwa bidii ili naye Baba akupe thawabu kubwa”.Kilichonishangaza
ni kwamba kila kiti kimeandikwa jina lake nyuma ya kiti hicho na hakuna yeyote
anayeweza kukaa atika kiti hicho.
HALI YA SASA YA
KANISA
Bwana
YESU akaniambia “Rodolfo, ninakwenda kukuonyesha hali ya kanisa sasa hivi”.Nikaona
samaki mdogo anamsifu na kumuabudu YESU kwa sababu Bibilia inasema:Wenye
pumzi na wamsifu Bwana !
Ndipo
Bwana akanionyesha dunia kuwa nikirudi duniani natakiwa nihubiri.Bwana alinipa
uelewa kuwa yeyote anayeingia mbinguni husahau kila kitu kilichotokea
duniani,Na huku wale walio kuzimu hukumbuka yote waliokuwa wakiyafanya
duniani,familia zao, ndugu zao.
Kwa
sababu hiyo sio petro sio maria sio Stefano sio Elisha wala yohana wanaweza
kuwa nakumbukumbu ya jambo lolote walilolitenda au lililotokea duniani kwa kuwa
ukiwa mbinguni unakuwa na ufahamu wa mbinguni na sio wakidunia.
Hivyo
petro hawezi dhani hata siku moja kuwa wakatoliki wanamtukuza au mtakatifu
yeyote yulei.YESU aliniambia , “Hakuna jina chini ya mbingu liwezalo kuokoa
bali YESUKRISTO,mwana wa MUNGU anayeishi,”.Maria alipokuwa katika
harusi kana aliwaambia kuwa “Neno lolote
atakalowaambia YESUKRISTO hilo ndilo mlifanye”.
Watu wa
kwanza wanao mwabudu shetani wapo VATICAN;
wao ndio wanaoficha kila njia za dhambi watendazo mapadri/makuhani kwa
kulala na masista; makuhani kufanyisha ngono watoto wadogo(uzalilishaji watoto
kijinsia) na hata katika jamuhuri ya Dominika,Nicolaus Lopez de Jesus
Rodrigruez ni ushetani mwingine tena, naweza hata kukuhakishia hayo kupitia
maandiko,Lakini bado Wakatoliki huendelea kuamini katika uongo wao wote huo.
Bwana
YESU akaanza kulia sana alipoanza kunionyesha hali ya kanisa.Nilimuona
mchungaji duniani amebeba begi kubwa lililojaa fedha.Bwana YESU akaniambia, “Hawa
wahubiri na wainjilisti ambao wamekuwa matajiri kutokana na sadaka kwa sababu
ya kuhubiri uongo kwawatu wangu na kusababisha watu wangu kupotea”.Nawaambia
wahubiri na wainjilisti, muhubirini YESU hatakama hutapata mafungu ya kumi na
sadaka.Takasa kanisa.
WATUMISHI WANAOPENDA FEDHA
Ghafla
!,nikaona fedha zile zilizokuwa zimejaa begi zimeyeyuka na hazikuwepo
tena.Nikamuuliza Bwana YESU maana yake naye akanijibu; “Vivyo hivyo kama fedha
zilivyoyeyuka ,ndivyo navyo wao watakavyo yeyuka na kuondoka na mpinga
Kristo.Lakini bado nina masalia ya watu wangu ambao ni waaminifu na
hawajaharibiwa na chochote.”
Naona
siku hizi jinsi watumishi,manabii,wahubiri,wainjilisti,mitume,wachungaji
walivyo matajiri na mamilionea.Ingawa waumini katika makanisa yao wako kwenye
umasikini, ni wahitaji wa chakula na huku mchungaji yupo katika utajiri mkubwa
pasipo kuwasaidia waumini wao.Ni wainjilisti wengi sana ambao ni mamilionea
hata hivyo ni mabilionea wakiwa kwenye magari ya kifahari sana.
Usamaria
mwema uko wapi ?,Na nikaona wachungaji wengi wakihudumu kwenye madhabahu hata nikamuona
mchungaji mmoja ambaye alipomaliza kuhudumu siku hiyo hiyo akaiacha familia
yake nyumbani ambako mke wake alikuwepo na akaelekea kulala na mwanamke
mwingine ambaye ni muumini wa kanisa hilo pia!.
VIJANA WASIO WAAMINIFU KWA MUNGU
Baada ya
hayo Bwana YESU alinionyesha kundi la vijana katika kanisa ambao wakitoka
makanisani huenda katika siri kwa kuwa hudhani Bwana YESU hawaoni na wanapofika
huko huanza kujichua(punyeto) na kufanya uzinzi kwa kutumia miili yao
wenyewe,Na baada ya hayo huenda kusimama ili kuhudumu madhabahuni !,raisi wa
vijana,kiongozi wa kanisa!.
MAKANISA YALIOJAA NYIMBO ZA KIDUNIA
Bwana
YESU alinionyesha disco na kanisa naye Bwana akaniambia nichunguze kwa
makini,na nilipochunguza nikaona kanisa kama disco na hakukuwa na
tofauti.Kulikuwa kuna aina ya muziki kama muziki wa disko,mpangilio wa kufanana,vifaa
vya kufanana,vilivyotoka katika dunia na kuingia kanisani.
Dunia inabidibadilike
kuufuata ukristo na sio vyovyote vile.
Sasa
tumeileta dunia ndani ya kanisa!,Na pia ninapaswa niwaambie ukweli kuwa huwezi
msifu aukumuabudu MUNGU na aina ya muziki wa rege,bachaton au rock.
Na hata sasa
kuna nyimbo za kikristo zinazoimbwa kwa MUNGU na kwa dunia,wakitumia maneno
yale yale !, Hawataji neno MUNGU lakini wanatumia tuu neno ‘upendo’.
Na pia
nimeona muziki wa RAP na PERREO ikiimbwa na imo ndani ya kanisa
na hiyo haikubaliki.Bibilia inatueleza tumuabudu MUNGU kwa uzuri wa
utakatifu.Sasa ni nani alieanzisha muziki aina ya ROCK ?,Naye ni Anton Lavey,naye
huyo ndiye muanzilishi wa kanisa la shetani.
Ametengeneza
na kuandika bibilia ya kishetani na ndiye aliyeingiza muziki wa rock ndani ya
Hollywood.Kama aligundua Rock, hiyoinamaanisha ni kwa ajili ya kumtukuza
shetani na sio MUNGU.Kwa maneno mengine kile anachopewa shetani nasi twataka
kumpa hicho hicho MUNGU? !,Hicho hakiwezekani na hakikubaliki kwa MUNGU.Rock ni
miziki ya kishetani na imegunduliwa kuzimu.
Anton szandor LaVey,born Howard Stanton
Levey, naye alikuwa ni muanzilishi wa kanisa la shetani pia ni
muandishi,mwanachamahuru na mwanamuziki.
Wachungaji
na wainjilisti , tafadhali tokeni kwenye hiyo miziki iliyo laaniwa na itoeni
kanisani.Rap iligunduliwa na mtu aitwaye Selassie.Huyu ni nani ?,Huyu ni mtu
aliye jiita mwenyewe kuwa yeye ni “Mfalme wa wafalme na Bwana wa bwana”.Na
kanisa linatumia aina hiyo ya miziki na huku bibilia imeandikwa kuwa pekee
aliye Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme ni YESUKRISTO,Mwana wa MUNGU anaye
ishi.
WAIMBAJI WA INJILI WALIOPOTOKA
Bwana
alinionyesha wanamziki waliokuwa wameacha sana njia yake(Bwana).Walikuwa
wakiimba kanisani kwa mkono mmoja na wakiwa wanatengeneza tenda ingine kuimba katika migahawa kama waimbaji
binafsi: wanamsifu Bwana kanisani!,
nataka niwaambie kuwa muziki na uimbaji wa namna hiyo Bwana hautaki na pia
unisamehe kwa kukwambia ukweli.
Kipi ni
cha Bwana ni kile ambacho ni kitakatifu nan i kile kilichotengwa tuu kwa ajili
ya Bwana pekee.Na hawa waimbaji wanaimba kanisani na baada ya kuimba huondoka
hatakama ni katikati ya ibada,Kwa sababu inaonekana kana kwamba ni mchezo wa
kutaka mkataba wa fedha kutokana na uimbaji wao, wanajihisi hawatakiwi kuwepo
katika ibada nzima nao huondoka na kuishi maisha ya umaarufu.
Na katika
wakati wote, Bwana akaniambia “Kwa bahati mbaya, aina ya kanisa hili
halitaingia mbinguni.”
KANISA LILILO SAFI
Baada ya
hayo Bwana akanionyesha kundi la
watu,maelfu kwa maelfu ya watu wanaojilinda wenyewe kwa utakatifu.Nikaona kwa
mfano dada akimwambia mwingine; “Je umekula leo ?”,nina kipande cha mkate
nyumbani kwangu.”
Nikamuona
mwingine amebeba viatu vingi kwa mtu asiye navyo hata kimoja.Nikaona wengine
wakiwapa nguvu wale wasio na nguvu.Wengine wanajua shida za wenzao na kuaanza
kuzitatua, wakiwatunza na kuwaombea kwa ajili ya mahitaji yao bila yeyote
kujua.
Lakini
leo katika makanisa mengi kuna umbea mwingi kwa sababu hawajui namna ya kukaa
kimya kuhusu mambo ya wengine.
Tubu; Leo YESUKRISTO anataka kukupa
kukufungua na hata kukuokoa.Naye anaweza kukupa kipawa na neema ya kutubu.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!