Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ujuehicho ndicho unacho mtendea YESUKRISTO !


Jiulize unawatendea nini ?,  watu mbalimbali unaowajua au usio wajua hicho ndicho unamtendea MUNGU!.

Haipingiki kuwa kuna kwenda mbinguni kama umemkubali YESU au kwenda kwenye moto wa milele kama umemkataa baada ya kifo.

Imeandikwa “32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”-mathayo 25:33-46.
Anaposema nilikuwa uchi mkanivisha nilikuwa na njaa mkanilisha  na kadhalika,Hayo yote ni matendo ya upendo na Hii  inamaanisha kuwa Upendo wa kweli ndio utamfanya mtu aweze kwenda mbinguni,

Jiulize unamtendea nini  jirani yako,nduguyo,rafiki yako,hata adui wako ?,Chochote unachomtendea mtu yeyote hata uwe humfahamu ndicho hicho unamtendea YESUKRISTO.

Imeandikwa “40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”-Mathayo 25:40

Je kuna baadhi ya watu unawadharau ?, Jua unamdharau YESUKRISTO au kunabaadhi ya watu unawaona sii kitu yaani wewe uko juu yao jua unamshusha YESU.

Imeandikwa “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”- Mathayo 18:3

Waweza jiuliza inamaanisha nini ?
Watoto hawatunzi chuki,hawa hesabu mabaya ya mtu, watoto ni wepesi wa kusahau mabaya waliotendewa ,hawahesabu hata mazuri waliowatendea watu . . . .hizi ni baadhi tuu ya  tabia ambazo wanazo watoto ambazo MUNGU pia anataka tuwe nazo ilituu kuweza kumpenza YEYE.

Tunatakiwa tuwe na upendo wa kweli ,upendo wa vitendo kutoka moyoni.Imeandikwa "Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu" Wakolosai 3:14

Mbinu pekee ya kuingoja parapanda ya mbinguni / kuja kwake YESUKRISTO !!.

Unaweza kujua kabisa siku hata muda wa kufa kwako lakini hakuna atayejua siku wala muda wa kuja kwake YESUKRISTO mara ya pili .

Zaidi ametupa kujua ishara zitazotokea katika nyakati hizoo  tuu na sio muda au siku kamili ya kuja kwake duniani tena !!.

Imeandikwa “32 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.  33 Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.”- Marko 13:32-33.

YESU anatupenda sana kwa kuwa pamoja na kutotaja muda wala nyakati za ujio wake lakini ameeleza mbinu ya kufanya ili tusije aibika pindi atakapokuja mbinu yenyewe ni kukesha, kuwa macho kiroho.

Hakuna binu tofauti na hii kama wewe uu msafiri kuelekea mbinguni hii ndio pekee mbinu.

Imeandikwa “Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa”-mathayo 25:13.Unaweza kujua mambo yajayo mengi sana hata kujua siku zako kwa idadi yake ulizopewa hapa duniani lakini hakuna mtu yeyote wakujua muda au saa kamili ya kuja kwake YESU .

Siri na mbinu kuu ya kumsubiri YESUKRISTO nikukesha yaani kuwa macho kiroho masaa yote kwa kuwa hatujui saa wala muda.Imeandikwa “Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”-mathayo 24:42.

Imeandikwa “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”-ufunuo 16:15.

Sababu ya kukesha yaani kuwa macho kiroho ni kwa kuwa hatujui na hakuna anayejua muda wala saa pia atakuja kama mwivi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...