Sababu tano (5) zinazofanya usipokee kile unachomuomba MUNGU !


Imeandikwa “ . . . . . . . . . . . . . . Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu .Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.”- Yohana 16:23-24.
MUNGU anatuambia tumuombe YEYE kwa kuwa anao uwezo wakutupa yale tumuombayo.Lakini wengi wetu ,yawezekana hata wewe waweza kuwa unajiuliza “mbona nimemuomba MUNGU lakini hakunipa nilichomuomba wala kunijibu chochote !?,”.

Imeandikwa “. . . . . . . . . . . . . . . . . .; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”.-Yohana 15:16.MUNGU anatupa ruhusa yakuomba lolote ili YEYE ayatimiz juu yetu nasi tuweze furahia.
Swali linakuja  hapo kwa nini sasa wewe haupati unachokiomba kwa MUNGU ?. Hapa leo utajua kwa nini hukupata au kupokea kitu ulichomuomba MUNGU, ama kwa nini HAKUKUJIBU maombi yako.

Sababu tano(5) zinazofanya usipokee unachomuomba MUNGU !
Utagundua kuwa MUNGU ametupa uwanja mkubwa wakuongea naye na kumuelezea matatizo yetu ili atutatulie ,lakini kuna sababu ambazo zinafanya MUNGU asitupe yale tunayomuomba.Sababu zenyewe ni :-

1.KUTOSAMEHE
Maombi ya wengi hayajibiwi kwa sababu hawaja wasamehe baadhi ya watu katika maisha yao.Imeandikwa“Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”-Mathayo 6:15.

Kaa chini jifikirie na uanze kusamehe wote, waliokutenda vibaya waliokuumiza,waliokusaliti ,waliokuonea,wasamehe hata waliokukataa kabla ya kuzaliwa kwako,waliokataa kukusomesha samehe wote .Usiseme nimesamehe ila sitakaa wasahau bali wasamehe toka moyoni mwako na kuwasahau kwa yale waliyokutendea.

Watu wengi ukimuuliza kama huwa anasamehe atakujibu “mimi ninasamehe sana na nimeshasamehe wengi lakini kuna yule kaka aliyenisaliti sitakaa nimsamehe,au anasema nimemsamehe lakini sitamsahau”. MUNGU anatusamehe dhambi zetu nakuzisahau,nasi pia twatakiwa kuwasamehe na kusahau mabaya waliotutenda watu.

Ukweli hiyo si sahihi kwa kuwa MUNGU husamehe tuu wale wanao wasamehe sio baadhi ya watu bali ni wale wanaowasamehe watu wote katika maisha yao.

Waweza kukuta mtu anazunguka huku na kule kuombewa na watumishi wakubwa na wadogo hata ajiombea sana yeye mwenyewe lakini hapokei kitu anachomuomba MUNGU kwa sababu kuna baadhi ya watu hajawasamehe kiukweli.

Imeandikwa“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” Mathayo 6:14.

Jipime kama kweli umemsamehe kiukweli kwa kujiiuliza hivi,yule unayedai umemsamehe je ?,unaongea nae vizuri?,Je?, unaweza kumplekea zawadi!,Je haumkimbii au kujisikia vibaya unaposikia amefanikiwa zaidi?,au ana habari fulani njema amefanya ?,
Mpaka utapoondoa kipangamizi chochote kinacho onyesha kutosamehe ndipoi maombi yako yatajibiwa na MUNGU.

2.KUTOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUOMBA
Imeandikwa“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.“- Warumi 8:26

Wakristo wanaomba vyovyote na hata wengine wanafuta tu mkumbo ,bila hata kujua anaomba nini .Tambua kuwa pasipo kuongozwa na ROHO mtakatifu kuomba, maombi yako yanakuwa hayana nguvu mbele za MUNGU.

Jiweke huru na uruhusu Roho wa MUNGU akuongoze katika kuomba. Roho mtakatifu atakukumbusha kuwa unaomba katika jina la YESU,Roho mtakatifu atakuelekeza kumshukuru MUNGU hata kama wewe huoni jambo la kumshukuru MUNGU.

Imeandikwa “Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,”- Yuda 1:20.

3.KUTOKUMUHESHIMU MWENZI(mke/mume) WAKO.
Imeandikwa “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. “-1 Petro 3:7

Unapokwenda kumuomba MUNGU jichunguze kama mkeo au mumeo ana amani na wewe.Kama hana amani na wewe yaani kuna ugomvi au hali ya kutokuelewa ilitokea baasi rudi ukarekebishe na kusameheana naye.
Bila ya kutengeneza na mkeo au mumeo kabla ya kuomba,na ukaamua kwenda kumuomba MUNGU utakuwa unapoteza muda wako tu.

Kwa kuwa hutaweza pata majibu na kuomba kwako ukiwa una migogoro/kutokuelewana/mtafaruku na mkeo au mumeo ni bure tena ni kupoteza muda na nguvu yako.

4.KUTOKUWA NA IMANI.
Imeandikwa “6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”-Yakobo 1:6-7

Maana halisi  ya imani ni ile hali yakuwa na hakika kuwa umepata huku katika ulimwengu huu wa mwili haulioni. Uliomba MUNGU gari lakini hulioni na hujapata kwa kuwa hujaweka imani katika maombi yako.

Kuwa na hakika na vyote unavyomuomba MUNGU acha mazoea na jiondoe kwenye ile hali ya wasi wasi juu ya kile unachomuomba MUNGU kwa kujihoji wenyewe kama atafanya au hatafanya.

Tunaweza sema mtu ana imani kupitia vitu vitatu(3):-
1.Unatenda je ?
2.Unasema je ?
3.Unamtazamo upi ?

1.Unatenda je ?
Imani ina uthibitisho katika matendo yaani unatenda je?” kama umemuomba MUNGU gari basi tengeneza uzio ambao gari uliloliomba kutoka kwa MUNGU litakuja kaa.

Kama unamuomba mke au mume basi ukishamaliza kumuomba MUNGU ,nenda dukani kanunue pete yake ya uchumba na ndoa na uitunze kwa kuwa si muda utampata ili umvishe !.

2.Unasema je ?
Imani ina uthibitisho katika kusema kwetu kwa kawaida kila siku.Kama umemuomba MUNGU gari basi hutaacha kusema unapoona gari ingine lolote mtaani hata kuwaambia watu neno lolotelinaloonyesha una matarajio ya kupokea gari si muda mrefu. mfano:gari yangu itakuwa inafanana na hii” au ukiwaambia watu gari yangu itakayopewa na MUNGU itakuwa nzuri kama hii”.

Kama uliomba akoponye ugonjwa fulani utaanza watu wakikuuliza hata kama hali ni mbaya waambie “naona MUNGU ndio anaifanyia operesheni saivi kwa hiyo si muda ninapona”

3.Unamtazamo upi ?.
Imani inathibitika pia katika mtazamo tulio nao.Kama umemuomba MUNGU akupe mke au mume ,je una mtazamo upi ?.Ondoa mtazamo wa dunia kwamba haiwezekani bali weka mtazamo wa ki MUNGU “kwa kuona katika akili yako hii harusi yangu itatia foira kwa uzuri 

ingawa kweli kwa hali halisi kidunia jambo hilo linaonekana haiwezekani.Wewe endelea kuwa na mtazamo huo na MUNGU atakushangaza kwa kukuinua na kukupa jibu lako haraka sana.

Kama umemuomba MUNGU akupe afya njema basi kuwa na mtazamo utapopata afya utakuwa unafuraha kiasi gani na utamshanga vipi MUNGU.ondoa ule mtazamo wa kishetani unaokwambia wee utakaa hivi hivi maisha yako yote.

Kiukweli hatupewi kwa kuwa tumemuomba MUNGU, Bali tunapewa na MUNGU kwa kuwa tuna amini tukimuomba MUNGU anatupa yale tunayo muomba.Hivyo yatupasa tuwe na imani thabiti katika yote tunayomuomba MUNGU.

5.TAMAA ZETU WENYEWE.
Imeandikwa “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.” -Yakobo 4:3
Unapo ongozwa natamaa zako mbaya kuomba kaa ukijua hutapata unachokiomba, Mfano: unaomba MUNGU uwe na gari lakini moyoni unajua kuwa unaomba gari ili uwaringishie/wakukome hapo mtaani jinsi ulivyo juu

Unatakiwa uibadilishe hiyo hali kutoka moyoni na kusema nikiipata gari itakuwa ni vyema kwa kuwa ninavyoenda nayo kazini nikakuwa nawapa lift hawa watu njiani.

Unaomba MUNGU akupe afya njema lakini moyoni unajijua unaomba afya njema ili uufanye uzinzi vizuri., Badili  nia mbaya na kuiweka hii kwa  moyoni mwako kuwa ninapopata afya njema nitaweza kumsifu na kutukuza MUNGU vyema.

Unaomba MUNGU akupe kazi nzuri lakini moyoni unajijua kuwa unaomba hivyo ili tuu uwaonee watakao kaa chini yako na utakuwa ukipokea rushwa si mchezo, Badili hiyo nia yako kwa kuwa hutakaa upate toka kwa MUNGU unachomuomba na nia hiyo ,sasa weka nia kwamba ukiipata hiyo kazi utakuwa mtu wa haki.

Kwa kuzingatia haya mambo hutakaa uone ombi lako lolote kwa MUNGU kutojibiwa.

No comments :

Post a Comment

Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...