Watu wengi hawafahamu kuwa muziki wa kidunia una nafasi
kubwa ya kuwaletea hatari katika maisha yao ya kiroho.
Tambua kuwa mambo ambayo
yanatokea katika ulimwengu wa kimwili yanakuwa yameanza katika ulimwengu wa
kiroho ,kwa hiyo ukiweza kuudhibiti ulimwengu wa kiroho ndio umeweza
kuumeudhibiti ulimwengu wa kimwili.
Kabla ya kuainisha kansa zitokanazo na muziki wa kidunia kwanza
pata kujua athari zinazotokea kutokea kutokana na kusikiliza muziki wa kidunia.
HATARI YA MUZIKI WA KIDUNIA KATIKA MAISHA YA KIROHO
Kuna madhara mengi yanayotokea katika maisha ya kiroho pale
mtu anaposikiliza muziki wa kidunia.Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na:-
1.UKIRI MBOVU
Nyimbo zinapoimbwa baadaeKinywa kinanguvu sana na maneno
mengi katika muziki wa kidunia yanakiri madhaifu, mfano muziki unaimba unasema “sisi tu masikini sana” Sasa unapoimba nyimbo kama hiyo
inakufanya ukiri vitu ambavyo sivyema katika ulimwengu wa kiroho na kimwili pia
kwa kuwa imeandikwa “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula
matunda yake.”-Mithali 18:21.
Kwa hiyo unapoimba “sisi tu masikini sana”
unakuwa unautengeneza umasikini katika ulimwengu wa kiroho na si muda umasikini
huo utakuja kujitokeza katika masha ya kimwili.
Mtu yeyote aliye hai kiroho hawezi kukiri au kusema sema
hovyo hovyo kwa kuwa kwa kusema sema hovyo huko ndio kunapelekea hayo mambo
kutokea katika maisha yake.
Mfano:Ukikiri “kushindwa”nawe utashindwa ,ukikiri “maisha magumu” na kweli kwako wewe yatakuwa maisha
magumu hata kama yalitaka kuwa maraisi kwa kuwa shetani atashikilia
uthibitisho wa neno lako ulilolisema.
Kwa hiyo kutokana na muziki wa dunia utajikuta kwenye hatari
ya kujikuta ukiimba vitu visivyo na maana ukadhani inaishia hapo tuu,kumbe
inakwenda kuathiri ulimwengu wako wa kiroho kwa kukiri vibaya baadhi ya mambo
katika maisha yako tuu kwa sababu ya kufuatisha na kuziimba nyimbo za kidunia.
2.KUISHI KATIKA ULIMWENGU
WA KUFIKIRIKA
Muziki wa kidunia unafanya watu wengi waishi katika ulimwenu
wa kufikirika yaani ulimwenu usio halisi kwa kuwa nyimbo nyingi za kidunia huwa
haziongelei maisha ya kawaida bali maisha ya kufikirika.
Kuazia anayeimba mpaka anaye kwenda kuusikiliza muziki wa
dunia huwa wanajikuta wakiishi katika ulimwengu wa kufikirika yaani kuishi
katika ulimwengu ambao si halisi.
3.KUPATANISHWA NA KUZIMU
Mara nyingi wasanii wanaoimba muziki wa kidunia huwa
wanafanya mapatano na kuzimu ili wapewe nguvu katika kazi zao za muziki wa
kidunia ili pindi zitokapo zifanikiwe sana kwa kusikika ,kupendwa na hata
kukubalika.
Kupitia muundo wa video za miziki ya kidunia kuna baadhi ya vitendo vyao katika mkanda(scene) vinakuunganisha na ushetani .mfano katika picha chini.
Kupitia muundo wa video za miziki ya kidunia kuna baadhi ya vitendo vyao katika mkanda(scene) vinakuunganisha na ushetani .mfano katika picha chini.
Hivyo kwa kusikiliza miziki ya kidunia unaweza jikuta
ukipatanishwa na kuzimu kutokana na maagano husika juu ya miziki yao.
Pia mtu anaweza kuzidi kuungana nao hata kupitia
style(maisha binafsi) mfano ni :-
i.
Kupitia tattoo.
Imeandikwa “Msichanje chale yo yote katika nyama ya
miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi
Bwana.” Mambo ya Walawi 19:28.
Unapokuta baadhi ya
waimbaji wa muziki wa kidunia wana michoro katika miili yao maarufu kama tattoo
ni wazi kuwa wana maagano ya moja kwa moja na nguvu za giza juu ya kazi zao za
muziki .
Sasa pale mtu mwingine anapoiga ile tattoo aliyekuwa nayo muimbaji flani
wa muziki wa kidunia inamfanya naye aingie kwenye maagano ya kishetani pasipo
kujijua.
ii.
Kupitia ishara za vidole.
Kwa kusikiliza muziki
wa kidunia waweza jikuta unakutwa na hatari ya kuunganishwa na kuzimu kw sababu ya kuiga au kufuatisha wanavyofanya
waimbani wa muziki wa kidunia.
Ishara nyingi za vidole zinazotumiwa na waimbaji wengi wa muziki
wa kidunia ni za kishetani na baadhi yao waimbaji hao wanajua moja kwa moja
wanachokifanya.
Imeandikwa "Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita (666)."- -- Ufunuo wa Yohana 13:18
mfano wa chapa hii ya mnyama (damien/shetani) ni alama ya 666 ambyo inatumiwa kama ishara kwa njia ya vidole.
Imeandikwa "Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita (666)."- -- Ufunuo wa Yohana 13:18
mfano wa chapa hii ya mnyama (damien/shetani) ni alama ya 666 ambyo inatumiwa kama ishara kwa njia ya vidole.
Ishara zingine wanazozionyesha waimbaji wengi wa kidunia ni
kama mapozi bali si mapozi kwa kuwa zingine zina maana ya kumtukuza
shetani.
Ishara zingine zinakuwa ni za kumsifu shetani kwa kuwapa mashabiki
wengi ,kukubalika kwa muziki wa kidunia wanayoimba.
iii.
Maneno.
“Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye
katika Roho wa Mungu. . . . . . . . . . . . .. . . ..”1 Wakorintho 12:3
Nataka
nikuonyeshe tuu kuwa mtu yeyote anaponena anaweza kunena jambo kutokana na
kuhamasika au kuamshwa na roho ,yaweza kuwa ni roho wa MUNGU au ni roho wa
shetani.
Kama mtumishi wa MUNGU huwa kuna roho ya MUNGU husema
kupitia mumishi huyo.
Je mtu tuu ambaye ni muimbaji wa muziki wa
kidunia tuu anaimba baadhi ya nyimbo kupitia roho ya shetani,Yaani kupata awazo
ya kishetani juu ya muziki wake naye kuyatimiza ili kuweza kufanikiwa.
4.KUWAKA TAMAA
Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika
nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada
ya sanamu;” -Wakolosai 3:5
Video nyingi za muziki wa kidunia huwa na namna ambayo
huamsha watu wanao zitazama hali ya kutamani wanawake,pombe na ngono.
Video hizo
ambazo wasanii huvaa nusu uchi na kucheza kwa kuonyesha maungo yao ili tuu
kutamanisha.
Mungu hapendi sisi kama wanawe tuwake tamaa zozote bali
hupenda tuzishike sheria zae na tuzifuate. “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate
haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo
safi.” 2 Timotheo 2:22
Hivyo basi kwa kuziangalia video za muziki wa kidunia mara
nyingi unaweza kujikuta ukiwaka tamaa na kwa hiyo tamaa unakuwa umemkosea MUNGU
na unapokuwa umemkosea MUNGU hapo ndipo ulinzi wa Mungu unaondoka maishani
mwako na shetani kupata nafasi katika maisha yako.
Kwa hiyo ni bora kujiepusha kusikliza na kufuatilia muzki wa
kidunia kwa kuwa unakufanya uwake tamaa ambazo mwishowe utaangamia kwa kuwa
imeandikwa.Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya
Mungu adumu hata milele.- 1 Yohana 2:17
5.KUMSIFU SHETANI PASIPO
KUJIJUA
Unaweza kujikuta unamsifu shetani bila ya wewe mwenyewe kujijua
kama unasikiliza na kufuatilia sana muziki wa kidunia.
Nyimbo nyingi za kidunia
huonyesha majivuno,kusifu wanawake,pombe ,ngono na vinginevyo ambavyo vyote
hivyo ni kazi ya shetani.
Nyimbo huhamasisha watu kwenda kinyume na maagizo ya MUNGU
hivyo kufanya watu wengi wajikute wakimuabudu shetani pasipo wao wenyewe
kujijua na mwishowe kuangamia.
KANSA
TATU (3) ZINAZOTOKANA NA KUSIKILIZA SANA MUZIKI WA KIDUNIA
Kuna magonjwa matatu ya kiroho yanayotokana na mtu
kusikiliza sana muziki wa kidunia.
kwa kuwa mtu asikilizapo huu muziki wa
kidunia hujikuta akishindwa kwenda kanisani mara kwa mara akishindwa kusoma
bibilia mara kwa mara ,atajikuta hata akishindwa kufanya maombi yake binafsi
mara kwa mara.
Magonjwa makubwa ni :-
1.Kuwa
na mahudhurio makubwa ya disco,matamasha na nighty club kuliko kanisani.
Ugonjwa wa kwanza wa kiroho ni kujikuta una mahudhurio
makubwa ya kwenda kwenye matamasha ,kujirusha ya muziki wa kidunia kuliko
mikesha kanisani au maombi.
Utajikuta unapenda kwenda kwenye matamasha, kutokana na
i.Mavazi
Kwa kuwa mtu huyu alikuwa akisikiliza sana muziki wa kidunia
ataanza kuiga mavazi yake hivyo basi inapofika muda wa kwenda kanisani
anajikuta hana vazi lolote linaloendana na kanisani hivyo kujikuta kuendelea
kubakia kwenye utumwa wa kwenda disko na matamasha ya muziki wa kidunia.
ii.Styles
Maisha binafsi na muongozo wake unakuwa umebadilika na kuwa
anawaza miziki yenye kuharibu maisha yake.Kwa mfano style ya
nywele ya kunyoa kiduku au kama ni mwanaume ajikute amesuka,itamfanya
azidi kupata sababu ya kutokwenda kanisani kutokana na style ya nywele zake
haziendani na za wengine kanisani.
2.Kuvutiwa
kusoma habari za udaku kuliko Bibilia(Neno la MUNGU).
Tatizo lingine linalotokana na kusikiliza sana muziki wa
kidunia ni kujikuta ukifuatilia sana habari za wasanii ,yaani udaku kuliko
kusoma Neno la MUNGU.
Kwa kuwa umeshazoea kuzisikiliza sana nyimbo za kidunia na
majina yao una wajua hivyo itakufanya uwe makini kufuatilia mambo yoyote ya
maisha yao yawe mabaya au mazuri lazima uwe unayafuatilia na kukufanya kusahau
kabisa kusoma neno la MUNGU.
3.Kuweka
hazina sana kwenye ngono,wanaume,wanawake kuliko MUNGU.
Imeandikwa “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo
utakapokuwapo na moyo wako.”- Mathayo 6:21
Badala ya kuweka hazina katika kujitoa katika kazi za MUNGU
kwa fedha au hata nguvu basi kwa wanaosikiliza sana muziki wa kidunia hujikuta
wakiweka hazina zao kwa wanawake,ngono mdawa ya kulevya.
Hili ni gonjwa la
kiroho linalotokana na kusikiliza muziki wa kidunia.
Muziki
wa kidunia una athari nyingi nazo hutengenezwa kidogo kidogo kama vile ulikuwa
hujui kunywa pombe unaanza kunywa kidogo kidogo,
ulikuwa huna tamaa za wanawake
sasa waweza jikuta kutokana na video za muziki wa kidunia unaanza hamasika na
kuwa na tamaa na wanawake.
Jiulize
wewe mwenyewe kama mkristo unazo nyimbo ngapi za kidunia ,na unazo ngapi za
kumsifu MUNGU ?.
Kama una nyimbo nyingi za kidunia na chache za kumsifu MUNGU
basi wewe tambua maisha yako ya kiroho yako kwenye hatari.
No comments :
Post a Comment
Andika maoni yako hapa !! ... You may comment here !!!