KWA WANADAMU NI SIRI LAKINI SI KWA MUNGU
“KUPIGA PUNYETO / PUCHU / PULI / KUJICHUA“masturbation”.
Kweli yaweza kuwa ni siri kwa wanadamu lakini haiwezi kuwa siri kwa
MUNGU kwa kuwa MUNGU anajua mambo yote hata yale yaliyositirika na kufichika.
Kitendo cha kujichua yaani masturbation kina starehe ndogo na kuwa na madhara mengi kuliko
kawaida, kujichua kuna madhara ya kimwili na kiroho pia.
Tatizo la kujichua si kwa wanaume tuu bali ni hata kwa
wanawake ,na sii kwa wasiooa na kuolewa bali hata kwa walio olewa na walio oa
baadhi yao hujikuta wakipendela kujichua pasipo kujua kuwa kuna roho za giza
ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuwasababisha waendelee kujichua tuu.
Kuna wakristo
wanawake zao lakini bado wanaona bora kujichua kuliko kulala na wake zao,Kuna
wanawake ambao wana waume zao kabisa lakini hawaoni raha ya kufanya tendo la
ndoa na waume zao kama vile wakijichua wao binafsi.
Wewe haujajiumba bali umeumba na MUNGU kwa ajili ya
kumtukuza yeye MUNGU pekee kwa kuwa mwili wako ni hekalu la ROHO mtakatifu “Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”- 1 Wakorintho 6:19
Mbaya zaidi ni kwamba shetani anazidi kuboresha utendaji wa
dhambi kwa kuwa tengenezea watu mashine za kujichua kwa kuwa anajua kwajinsi
wanadamu wanavyozidi kutenda dhambi na ndivyo yeye anaweza kutenda kazi ndani
yao.
Kujichua au kupiga puchu kumekuwa kwa staili mbali
mbali mpaka zingine zimekuwa ni za
kitaalamu sana zilizoendelezwa na
shetani ili watu wajichue kupitia mashine,midoli yaani setoyz maalumu kwa ajili
ya kujichua .Kujichua husababisha matatizo ya kisaikolojia na kuathiri mfumo wa
mwili na roho pia!.
Ukweli ni kuwa
kujichua ni chukizo mbele za MUNGU. Imeandikwa
“Hivyo
Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya
asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27
wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana
tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu
wao yaliyo haki yao.”- Warumi 1 :26-27
Hawezi
kufanya punyeto/kujichua/masturbation pasipo
kuwa na hisia za kutamani kufanya tendo la ndoa na kwa kuwa na mawazo tuu ya
kutamani kufanya ngono ni dhambi mbele za MUNGU kwa kuwa imeandikwa“lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye
mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”- Mathayo 5:28
Hivyo si mpango wa
MUNGU watu wakae katika maisha ya kujichua ,kupiga puli, kurusha ndege na kuwaka
tamaa.
Ni afadhali tena ni heri mtu aoe au aolewe kuliko kuendelea
kujichua “Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko
kuwaka tamaa”- 1 Wakorintho 7:9
Vitu
vinavyosababisha kujichua.....
Tamaa ya kufanya,uzinzi, uasherati na tamaa kubwa
ya kufanya mapenzi huchangia kujikuta unajaribiwa kufanya masturbation yaani
punyeto.Kuna vitu vinachochea kujichua vitu hivyo ni pamoja na:-
i.Kuangalia picha za kawaida zenye hisia kali au hata picha za ngono
yaani (PORNOGRAPHY).
Picha zenye unusu uchi za kwenye mitandao au
tamthilia zenye kuonyesha matamanio matamanio hupelekea mtu kuwaza kuanza
kujichua
ii.Kushawishika kumakinika na mavazi ya uchi na yenye hisia kali
kuyatazama.
Mavazi ya ajabu ajabu yenye kuwekaushawishi
kutokana na kukaa wazi kwa mwili.
iii.Mapepo na majini
Kuwa makini kwa kuwa kujichua ni moja ya kazi ambazo shetani
anapata nafasi kujiingiza katika maisha ya watu kwa kuwa kuna mapepo na majini kwa
ajili ya kuwafanya watu wasipende kuolewa wala wasioe ila wapende kujichua tuu.
Watu wengi wana mapepo na majini yanayosimamia kabisa
kuwahamasisha kujichua mara kwa mara na hata kuwafanya wasiwe na hamu na wake
zao wala wasiwe na hamu na waume zao bali wawe na hamu kubwa tuu ya kujichua.
iv.Upweke ulio na uvivu mkubwa.
Uvivu ni hali mbaya sana kwa kuwa mara nyingi mtu
anaokuwa mvivu naye shetani humtafutia kazi au jambo la kipuuzi ili ulijaribu
na hapo unapojaribu siku moja nivyo inavyo endelea siku zote kukuathiri katika
maisha yako.
Kwanini
unatakiwa uache kujichua?/Hasara za kujichua !
Kujichua kunaleta madhara kimwili na kiroho pia
yaani kujichua kwa mtu wa jinsia ya aina yeyote ile huleta madhara kattika
mwili wake pia na roho yake.
Madhara ya kimwili
yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:-
1.Kusahau sahau kusikokuwa kwa kawaida
Kujichua kukute kule kuna sababisha madhara
makubwa kisaikolojia ambayo hupelekea kushindwa kukumbuka vizuri.Sio kana
kwamba ni kusahau kwa kawaida bali ni kule kusahau kusikokuwa kwa kawaida.
2.Kunyonyoka au kuishiwa na nywele.
Kufanya sana kujichua kulikokithiri husababisha
kutokuuota kwa nywele kichwani na kwapani hasa kwa wadada.
3.Kichwa kuuma na kutapika mara
kwa mara
Mtiririko wa damu huathirika sana pindi mtu
anapojichua kwa kuwa mwili wa mtu huyo utahitaji ajifikirishe kama yupo na
mwanamke kumbe hana mwanamke.Au yupo na mwanaume kumbe hana mwanaume.
Mwishowe mfumo wa damu huleta kutokusawazika na
kuchangia maumivu makali ya kichwa(chronic head-ache)
4.Kuishiwa nguvu za mwili sana
Mtu anayejichua huishiwa na nguvu isivyo kawaida
kwa kuwa kabla anakuwa anauwezo mkubwa wa kujichua mara nyingi sana akijisikia
raha pasipo kujali nguvu zinazopotea.
5.Kutokupenda kuwa na ushirika na wengine
Mtu anayejichua huwa mara nyingi hapendi sana
kushirikiana na wengine kwa kuwa tendo hilo la kujichua hufanyika sirini pasipo
mtu yeyote.
6.Huchangia matatizo ya nguvu za kike na kiume.
Watu wengi hawajui kuwa matatizo mengi ya nguvu za kike/kiume
hutokana na kujichua.
Madhara ya kiroho
yatokanayo na kujichua / kupiga punyeto ni:-
Moja ya tatizo kubwa la kiroho litokanalo na
kujichua au kupiga punyeto ni kukosa ukaribu na MUNGU wako unakosa ushirika na
MUNGU wako.Ni mbaya kuwa kijana mzuri lakini uzuri wako hauonekani mbele ya
MUNGU kwa sababu ya kujichua.
i.Unakuwa najisi.
Imeandikwa “Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni.”- Mambo ya Walawi 15:17.Unapojichua
unafanya MUNGU akuone wewe u najisi utaona ni hasara kubwa kiasi gani kwa aliye
kuumba akuone kuwa u najisi.
ii.Unashindwa
kudumu kutokana na kukosa neema ya MUNGU…
Imeandikwa “Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake,
bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”- 1 Yohana 2:17.Duniani si makazi yetu bali tu
wapitaji kwa kuwaktu akifa atahukumiwa kwa yale aliyoyatenda kipindi alipo kuwa
hai duniani.
Kwa hiyo
kwa sababu ya dhambi ya kuwaka tamaa ya ngono inayopelekea hadi kufanya punyeto
inaweza sababisha wewe kuto enda katika makazi ya mbinguni na kukufanya uende
makazi ya motoni milele.
iii.Kujichua
ni kunaabudu sanamu pasipo kujijua…
Unapojichua unakua unaabudu sanamu pasipo kujijua,huwezi
amini bali neno la MUNGU ndivyo linavyotueleza kuwa kila afanyaye tamaa mbaya
ni sawa na anaye abudu sanamu.
Imeandikwa “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika
nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada
ya sanamu;”- Wakolosai 3:5
Ikwepe hatari hii ya kujiona kana kwamba unamwabudu MUNGU wa kweli
na kumbe MUNGU haoni kama unamwabudu yeye bali sanamu, kwa sababu ya kujichua
ambako ni sawa na kuabudu sanamu.
JINSI YA KUACHA KUJICHUA NA KUDHIBITI MADHARA YAKE KUACHANA
NA VISABABISHI NA KUUTUMIA MUDA NA WENGINE KWA UZURI
Ukiweza kuzuia tamaa ya
mwili ujue umeweza kuzuia kufanya kujichua Imeandikwa “Vita
vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa
zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?”- Yakobo 4:1.
BADILI MWENENDO WAKO KWA KUKATAA KUWA
HUNA LA KUFANYA.
Amua
leo kuacha kabisa kujichua /kupiga punyeto/kupiga puchu/kurusha ndege/ kwa kuwa
MUNGU ana mipango mizuri na mikubwa nawe ila kinacho kuchelewesha ni huku kujichua.
Kuna
vijana wengi tena ambao hawajaoa au kuolewa na bado wajitahidi na kuweza kuacha
kabisa kujichua na wanafurahia uhusiano wao na MUNGU.Nawe unaweza amua leo,amua
sasa!
Baadhi ya hatua za kuacha kujichua ni
hizi:-
1.Muda uliokuwa ukiutumia kuangalia
porno tumia muda huo huo kusikiliza na kuangalia mafundisho ya neno la MUNGU
kutoka kwa watumishi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.
2.Badala ya kuangalia video za
ngono sasa angalia video za mahubiri ya injili
3.Badala ya kusoma
magazeti yenye picha za uchi yaani zenye kuleta msisimko sasa anza kusoma
BIBILIA kusoma magazeti yenye neno la MUNGU.
4.Acha kufuatilia mitandao ya ngono
sasa anza kufuatilia mitandao ya watumishi wa MUNGU soma mafundisho yao na udownload
video zao zisikilize.
5.Tumia muda wako ule ule
uliokuwa unajichua /kupiga punyeto kuanza kuomba MUNGU.Kama ulikuwa unajichua
mara 5 kwa siku ndivyo hivyo hivyo unabidi ubadilike na uanze kuomba MUNGU mara
5 kwa siku.
6.Ulikuwa ujifunza staili
mbali mbali za kujichua sasa ziache zote na uanze kujifunza njia mbali mbali za
kumjua MUNGU,jifunze namna ya kusoma neno la MUNGU, jifunze namna ya kuomba na
kufunga kisahihi, jifunze namna ya kuombea wengine kisahihi.
7.Pendelea kufanya mazoezi ya mwili
kama vile kukimbia kila jioni na asubuhi kwa ajili ya kupunguza taratibu
madhara yaliyopata mwili kutokana na kujichua/kupiga punyeto.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru;
lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”-
Wagalatia
5:13
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuacha KUJICHUA/KUPIGA PUNYETO inawekana kabisa
badilika sasa utakuwa kijana ,mwanamke/mwanaume bora mwenye kupendeza
zaidi katika afya yako,roho yako hata
kwa MUNGU wako.
Usiishi kama wengine wanavyoishi bali ishi kwa kuwa wewe ni
wa MUNGU basi unabidi umfuate MUNGU kweli kweli
kwa kuzikimbia tamaa zote za ujanani.
Imeandikwa “Lakini zikimbie tamaa za
ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao
Bwana kwa moyo safi.”- 2 Timotheo 2:22
What is this symbol called “^”? It's a circumflex.
ReplyDeleteThose people who answered "carat" or "carrot" are misspelling
the word "caret", which you could also use, depending on your meaning.
🔥🔥🔥🤸
Delete